Pst Janerose Khaemba Official
You may also like
Welcome to my page where you will get preachings,teachings and uplifting music
+254710 858 577
MUNGU AWABARIKI
Shout out to our newest followers! Excited to have you onboard! Everlyne Wesonga, Yobrah Yoruba, OkaPrince Mwaitege, Jacinta Nafula, Silas Wanjala, Devid Maruti, Kelvin Lutoti, Don Carlos, Amos Musombi, Rabecca Harambee, Betrona Lishindu Lishindu, Valentine Sh**ha, Naliaka Mamake Rembo
*TUNZA MAVAZI YAKO NA FUA NGUO ZAKO!*
Vazi/Nguo kiroho linawakilisha “matendo ya mtu”, maana yake kiroho mtu mwenye mavazi masafi, maana yake matendo yake ni masafi, na kinyume chake mwenye mavazi machafu maana yake matendo yake si safi (Ufunuo 19:18).
Sasa Matendo yanatunzwa, lakini pia yanafuliwa (safishwa).. k**a vile nguo inavyoweza kutunzwa lakini pia kufuliwa.
1. TUNZA MAVAZI YAKO.
Maana ya kutunza mavazi ni kuhakikisha hayaharibiki wala kuwa na kasoro yawapo mwilini. Vazi lililotoboka au kuchanika maana yake limekosa matunzo mwisho wa siku yule mtu atabaki Tupu.
Vivyo hivyo ni wajibu wetu kuyatunza Matendo yetu mema, yasiharibike.. Kwa kujiangalia mazingira tuliyopo na mambo tuyafanyayo…
Ufunuo 16:15” (Tazama, naja k**a mwivi. Heri akeshaye, NA KUYATUNZA MAVAZI YAKE, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”.
Vitu vinavyoharibu matendo yetu mazuri/tabia nzuri ni pamoja kampani tulizonazo na mazungumzo tuzungumzayo..
1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”.
Chunguza makundi uliyonayo na aina ya mazungumzo unayozungumza.
2. FUA NGUO ZAKO.
Nguo isiyofuliwa inapoteza umaridadi na unadhifu kwa mtu, hata k**a haijaharibika au kuchanika. Vile vile Matendo yasiyofuliwa yanapoteza unadhifu wa mtu kiroho.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu k**a kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Sasa mtu anafuaje Matendo yake?… Si kwa njia nyingine Zaidi ya kuomba na kusoma Neno.
Na Utajuaje matendo yako yameanza kuingia dosari?.. si kwa kusubiri uambiwe na mtu au watu, bali kwa kusoma Neno (biblia). Unaposoma Neno ndipo utakapojijua k**a una kasoro au la!, kwasababu Neno la Mungu ni kioo.. Ili ujijue k**a una uchafu mwilini, si kusubiri uambiwe, kwasababu si wote wenye ujasiri wa kukwambia kasoro zako.
Kitu pekee kitakachoweza kuutambulisha uchafu usoni mwako ni KIOO
na ni lazima usomaji wa Neno uambatane na maombi.
Hivyo Maombi ni “Maji” na Neno la Mungu ni “sabuni” kwa mambo hayo, matendo yetu yatakuwa safi daima.
Bwana atuongezee Neema yake.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
KUWA NA WIKI NJEMA
*ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.*
Shalom.
Usiishie kutafuta tu utakaso wa roho, bali tafuta pia UTAKASO WA MWILI, kwamaana vitu hivi viwili vinaenda sambamba, kwasababu vitu hivi vikichafuka vinaiharibu pia nafsi ya mtu.
2Wakorintho 7:1“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Upo usemi kuwa Mungu wetu hatazami sana Mwili, lakini anatazama Zaidi Roho ya Mtu. (Hatuna budi kuwa makini na kauli hii!!)
Kutokana na kwamba asilimia kubwa ya maombi yetu yanalenga MAHITAJI YA MWILINI, basi ni wazi kuwa Mungu anaitazama pia miili yetu. Kwasababu k**a mtu atamwomba Mungu Baba ampe fedha, au chakula, au makazi hayo yote si kwasababu ya “roho” kwasababu roho haili chakula, wala haivai nguo, wala haiishi kwa fedha.. bali mwili ndio unaohitaji hayo yote.
Sasa k**a tutamlazimisha Mungu Baba aangalie miili yetu kwa mahitaji yetu, halafu wakati huo huo tunasema Mungu haangalii mwili, tutakuwa WANAFIKI!!.
Sasa ikiwa asilimia Zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yetu, yanalenga MIILI YETU, Basi ni wazi kuwa Mungu anaangalia Miili yetu na anajishughulisha nayo sana….
Ni lazima kulijua hili ili tusipotee na elimu ya uongo ya shetani,.. Ni lazima pia tujishughulishe kutafakari namna ya kuyafanya mapenzi ya Mungu katika miili yetu k**a tu vile tunavyojishughulisha katika kumwomba mahitaji ya mwili..
1Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU mhifadhiwe MWE KAMILI, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Katika mstari huo biblia imetaja mambo yote matatu; Nafsi, mwili na roho. (yanapaswa yawe makamilifu, bila lawama mpaka wakati wa kuja kwake Bwana YESU).
Hivyo zingatia yafuatayo:
1. NI NINI UNAFANYA KUPITIA MWILI WAKO.
Jipime ni nini unakifanya katika mwili,.. je shughuli au matendo unayoyafanya kupitia mwili wako ni kulingana na mapenzi ya Mungu??.. K**a unafanya kazi haramu (mfano ukahaba, au kazi ya kuuza vitu haramu k**a pombe, sigara, na mengineyo), basi kazi hiyo unaifanya kupitia mwili wako hivyo ibadili ili isikupeleke jehanamu ya moto.
K**a matendo unayoyafanya katika mwili ni haramu mfano uzinzi (1Wakorintho 6:18), wizi, au mauaji n.k geuka leo yasije yakawa sababu ya kukupeleka hukumuni.
2. NINI UNAKIAMBATANISHA NA MWILI WAKO
Angalia ni nini unakiambatanisha/unakishik**anisha na mwili wako.. Hapa nazungumzia aina ya mavazi na urembo na michoro (tattoo). Je mavazi uvaayo ni sawasawa na Neno la Mungu?.. Je yanaipasa jinsia yako sawasawa na Kumbukumbu 22:5.
Je mavazi unayovaa ni ya kujisitiri?, kuzuia tamaa kwa upande mwingine na kutunza heshima yako? (1Timotheo 2:9 na Mathayo 5:28)
Je michoro uichorayo na rangi yako ya asili uiondoayo ni mapenzi ya Mungu? (Walawi 19:28)
Angalia ni nini kinanin’ginia mwilini mwako.. Je hizo cheni, hereni, mikufu, bangili, vikuku n.k ni mapenzi ya Mungu?? Je si ishara ya utumwa?? (hebu soma Kutoka 21:5-6 na Kumbukumbu 15:16-17).
3. NI NINI KINAINGIA MWILINI MWAKO.
Angalia ni kitu gani unakiingiza mwilini mwako.. Je Mungu amekusudia moshi uingia katika mapafu yako ambayo yanapaswa yavute hewa safi ili kutimiza miaka uliyopewa yakuishi duniani?..
Je Mungu amekusudia uingize vilevi na madawa ya kulevya ndani ya mwili wako na kukutoa ufahamu wako kwa muda?.. Jiulize k**a si ruhusu kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa umelewa/umekunywa pombe.. vipi kuuendesha huo mwili ukiwa umelewa??.. Huoni k**a huo ni uvunjaji wa sheria kubwa Zaidi, kwasababu mwili ni bora kuliko gari au chombo kingine chochote cha usafiri.
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI. – Site title Shalom. Usiishie kutafuta tu utakaso wa roho, bali tafuta pia UTAKASO WA MWILI, kwamaana vitu hivi viwili vinaenda sambamba, kwasababu vitu hivi vikichafuk
NENO LA LEO
Matthew 6:25-26
[25]
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
[26]
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
UFAFANUZI
Ni kweli kuwa Mungu anatuthamini sisi zaidi ya viumbe vyote duniani. Kutotii kwetu ndio kunapelekea mkono wa Mungu kutofanya kazi juu yetu. Kumbuka kukaa ndani ya kristo ni kulitii neno lake. Tuonyeshe tu uaminifu katika kumwamini yeye na hayo mengine atatuzidishia hakika k**a alivyoahidi.
******
Share huu ujumbe kwa wengine na utabarikiwa
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
JUMAPILI NJEMA.
Matthew 19:26
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
UFAFANUZI
Ukiona umejaribu njia zote zimeshindikana, madaktari wameshindwa, elimu zimegonga mwamba.
Kumbuka yuko Mungu asiyeshindwa lolote . Yaachilie tu kwake kwa imani kisha sema BWANA NIREHEMU.
Big shout-out to my newest top fans! Kassim boave, Boniface Wanyonyi, Solomon Nato, Elizabeth Simiyu, Ton Simiu Simiu, Presious Ann, Alfred Khisa, Noel Nosh, Eva Sure, Apstl William Kigame, Evania Evania, Alex Wabomba, Pstr Paul Shivachi, Collins De Wafula Mulati, Hudson Makokha, Benjamin Juma, Sammidoh Sam, Amayo Rachael, Blessed Irine, Esther Wanyonyi, Elizer Wah Nalondo, Jackline Sayia, Brotha Nthan Seme, Mike Wekesa, Christine Nyongesa, Leonard Situma Pilipili, Hosea Juma, Mercy Barasa, Willis Odhiambo, Queen Malkia, Nancy Wamalwa, Michael Malachi, Nickson Nyongesa, Kevin Asibwa, Amos Baraka, Titus Juma, Phanice Onyango, Joan Nekesa Waswa, Elizabeth Wachana, Geoffrey Avudiko, Caroline Zubeda, Brenda Nekesa, Sammy Wafula, Catherine Burudi, Sylvia Lihavi, Velimah Clarah Nakitare, Celine Cely, Nakhumicha Masungo, Bili Fao, Robai Nabututu
Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! Tariq Bhatti, Bili Fao, Msanii Bigstar, Muhgwana Liz, Clear Boset, Everlyn Lukwiso, Joy Ouma, Mdogo Wa Kale, Billy Edesh, Elizabeth Queen, Jonesy Khasiro, Anne Nekesa, Mathews Murumba Murumbaz, Jacky Wasike, Timothy Sitwaa, Erick Masinde, Kaka Wankayn Dnivisi, Mteule Izo, Protus Mwalati, Mercy Rita, Omusonge Omumakhang, Faith Imanian Kazungu, Boniface Wanyonyi, Roiny Addah, Martha Simiyu, Annet Nasimiyu, Harrison Wekhobha, Elizabeth Kisa, Lewis Wasii, Jane Jane, Martha Wanyembi, Caroline Makokha, Rehema Rose, Noel Nosh, Legress Lorez, Nancy Nyota, Wycliffe Mutoro, Ashline Lydiah, Lishy Lily, Paul Chetah, Rebecca Mutash, Seba Betty, Maximilar Fabiano, Maryjane Otanga, Robai Nabututu, Zaddies Sitati, Sammy Wakora, Velma Wasike, Shela Chebet, Laban Mutoka
*Je Adamu na Hawa waliokoka?*
Biblia haielezi moja kwa moja k**a waliokoka, au hawakuokoka, kwasababu Neno “Kuokoka”, tunalisoma kwenye agano jipya, likimaanisha kukombolewa kutoka katika uharibifu wa hukumu ya Mungu kwasababu ya dhambi kwa kupitia kifo cha Yesu Kristo mwokozi wetu.
Lakini tunaweza kufahamu watu wa agano la kale waliokolewa, kwa kutii kwao ile ahadi ya Mungu aliyoahidi ya kumletea mkombozi duniani baadaye, yaani Yesu Kristo. Hivyo wote waliotembea katika mpango huo wa Mungu, waliokoka. Na mpango wa Mungu wote ulimuakisi Yesu Kristo.
Kwamfano ile safina aliyoijenga Nuhu ilikuwa ni Yesu Kristo, Ule mwamba walionywea wana wa Israeli jangwani ulikuwa ni Kristo, wote waliokataa kuunywea walimkataa Kristo, (1Wakorintho 10:4), Yule nyoka wa shamba alikuwa ni Kristo waliokataa kuitazama, walimkataa Kristo(Yohana 3:14), zile mbao mbili (Amri 10), zilikuwa ni Kristo waliozikataa kuzitii, walimkataa Kristo. Yule melkizedeki aliyemtokea Ibrahimu alikuwa ni Kristo, wale malaika wawili walioshuka sodoma kuhubiri alikuwa ni Kristo ndani yao, waliowatii walimtii Kristo. Wale wanyama waliochinjwa na damu zao kunyunyizwa katika madhabahu kwa ajili ya upatanisho wa dhambi za watu walimfunua Kristo, wote waliotii,. Walimtii Kristo ajaye.
Hivyo kila mahali walipotembea, Kristo alijidhirisha kwao kwa lugha ya maumbo na vivuli, na mifano, na maagizo, ili wamwamini yeye. Kwahiyo wote waliomtii katika nyakati zote, waliingizwa katika jopo la watu ambao Kristo atakapofunuliwa basi wataokolewa. Ndio maana baada ya Yesu kufufuka katika wafu miili mingi ya watakatifu ikatoka makaburini, wakahamishiwa peponi, rahani mwa Yesu, kwani hapo kabla watakatifu wote waliokufa walikuwa chini makaburini.
Hivyo kwa msingi huo, tutachunguza k**a Adamu na Hawa walimtii Kristo au la, baada ya anguko. Biblia inatuonyesha walipojiona wapo uchi, hawakuendelea kufurahia anguko lile, bali walijificha, kuonyesha majuto ya dhambi zao, ndipo Mungu akamchinja mnyama Yule, akawavika vazi lake. Sasa Mnyama Yule alimfunua Kristo,(Mwanzo 3:21) lakini k**a wangekataa basi wasingeweza kuokoka, ndio maana Yesu alisema..pia maneno haya haya kwetu sisi wa siku za mwisho, tuvikwe vazi lake, ili aibu yetu iondoke.
Ufunuo 3:18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona
Halikadhali, biblia inataja uzao wa mwanamke kwamba utauponda kichwa uzao wa nyoka. Kuashiria kuwa Hawa hakuwa mwana wa Adui (Mwanzo 3:15). Bali ni zao mbili tofauti kabisa.
Lakini pia watoto wao, mpaka sethi, tunaona walifundishwa njia ya kumtolea Bwana sadaka, na sadaka zile zilikuwa ni Kristo katika maumbo. Ni wazi kuwa wasingeweza kufanya vile k**a hawakupokea au kuona kwa wazazi wao.
Na sababu nyingine ya mwisho, Kristo anatajwa k**a mwana wa Adamu, hata katika vizazi vile vilivyoorodheshwa anatajwa k**a “wa Adamu” (Luka 3:23-38). Asingeitwa hivyo wa Adamu k**a angekuwa ni wa ibilisi,. Mungu hawezi anza na mguu usio sahihi. Atashinda mwanzo, vilevile atashinda mwisho.
Kwa hitimisho ni kwamba Adamu na Hawa hawakupotea, bali walimwamini Kristo, baada ya anguko.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
*Je! kufanya mazoezi kwa mkristo ni dhambi?*
Swali: Je mkristo aliyeokoka kw enda “Gym” /kunyanyua vyuma na kufanya mazoezi mengine ya viungo ni dhambi?.
Jibu: Kufanya mazoezi kwa asili si dhambi, kwasababu hata kutembea kutoka nyumbani kwenda kanisani kumwabudu Mungu au kwenda kazini tayari hayo ni mazoezi hata k**a hujarasimisha. Bwana hajatuumba kutulia sehemu moja k**a vile “MTI”, bali kujongea.
Na kujongea kuna faida katika mwili endapo kukiambatana na “Kuyafanya mapenzi ya Mungu”. Maana yake ni hii, k**a utakuwa upo sawa na MUNGU aliyekuumba kimahusiano, basi mazoezi utakayoyafanya yatakuwa na faida katika mwili wako.
Lakini k**a Mahusiano yako na Mungu ni hafifu au hayapo kabisa, basi hata mazoezi utakayofanya hatayakuletea matokeo yoyote katika mwili wako.
Lakini suala la Msingi, ni je.. Aina gani ya Mazoezi Mkristo anayopaswa kuyafanya?? Hili ndilo SWALI LA MSINGI.
Mazoezi Mkristo anayopaswa kuyafanya ni yale yasiyo na NIA YA KIDUNIA, wala YASIYOJIFUNGAMANISHA NA MIFUMO YA KIDUNIA. Tuangalie moja baada ya nyingine.
1. MAZOEZI YENYE NIA YA KIDUNIA NI YAPI?
Mfano wa mazoezi yaliyobeba Nia ya kidua ni yale yote yanayochochea tamaa za kimwili..mfano wa hayo ni yale ya kunyanyua vyuma ili kutanua misuli kwa lengo la kutazamwa na watu, au kuvutia jinsia nyingine…mazoezi ya namna hii ni haramu kwa mkristo.
Lakini k**a mkristo atafanya mazoezi ya kutanua misuli aidha kwasababu kazi yake ya mikono aifanyayo itahitaji ukak**avu, hiyo sio kosa.
Mfano mwingine wa mazoezi haramu ni yale ya kupunguza mwili kwa lengo la kutumia mwili huo k**a kivutio cha matangazo ya urembo au mitindo.(Maarufu k**a Umiss, au Umodel), mazoezi ya namna hii mkristo hapaswi kufanya..
Lakini k**a lengo lake si hilo, bali anafanya tu mazoezi ya kupunguza mwili kwa lengo la kujiongeza wepesi katika viungo vyake afanyapo kazi au aendeleapo na majukumu yake ya kila hapo afanyi kosa.
2. MAZOEZI YALIYOJIFUNGAMANISHA NA MIFUMO YA KIDUNIA.
Mazoezi yaliyojifungamanisha na mifumo ya kidunia ni yale yote yaliyobeba tamaduni za kidunia kuendesha/kuongoza mazoezi hayo…(Mazoezi ya dizaini hii haijalishi yana NIA nzuri, lakini maadamu tu tayari yamejifungamanisha na mifumo ya kidunia, basi yanakuwa Najisi kwa mkristo).
Mfano wa mazoezi haya ni yale ambayo Mtu atakimbia barabarani huku kavaa nguo ya kubana au nguo ya ndani tu peke yake!!…kwasababu tu ndio mfumo wa ukimbiaji ulioidhinishwa au ulio katika wakati. Mkristo kwa vyovyote vile hapaswi kufanya mazoezi kwa mtindo huo… haijalishi nia yake ni kupunguza mwili ili awe mwepesi katika kazi au kuongeza ili imsaidia katika kazi zake.
Maana yake k**a wewe ni mkristo na unataka kufanya mazoezi ya kukimbia ili kupunguza mwili, na kujifanya mwepesi, vaa nguo zako za kujisitiri, (Uwe mwanamke au mwanaume) na fanya mazoezi yako kwa staha.. na tena si sehemu za kujionyesha onyesha..
Mfano mwingine wa mazoezi yaliyochanganyikana na udunia ni yale yanayofanyika katika majumba maalumu almaarufu k**a “Gym”. Majumba ya Gym hayana tofauti na DISKO, kwani k**a vile disko kulivyo na kule kumo vivyo hivyo, Disko utakuta watu wamevaa nusu uchi, na GYM ni hivyo hivyo.
Disko utakuta watu (wakike na wakiume) wanaserebuka na midundo ya miziki, na Gym ni hivyo hivyo, utakuta wamepanga mistari na wanafanya mazoezi huku wanaongozwa na ile midundo wakiwa nusu uchi, na hata wakati mwingine kupapasana kana kwamba wanaelekezana au kusaidiana kanuni za mazoezi n.k
Sasa mazoezi k**a hayo, Mkristo hapaswi kushiriki wala kufanya kwasababu yamejifungamanisha na mifumo ya kidunia. (1Yohana 2:15)
K**a mkristo ni lazima kuenenda tofuati na dunia siku zote. Kwasababu mambo yanayofanyika duniani karibu yote maudhui yake ni ya kishetani.
Lakini jambo la mwisho la kuzingatia ni kwamba, hata k**a umeokoka usitie kipaumbele sana kufikiri kutengeneza mwili, lakini ni heri kufikiri kutafuta afya ya rohoni, kwani ukiipata hiyo hata hiyo ya mwilini itajiweka tu katika uwiano..
1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”.
Bwana akubariki
Usifanye lolote kwa kushindana wala kwa majivuno.
NENO LA LEO.
1 Corinthians 1:26-27
[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
*SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.*
Ufunuo 3:11 “Naja upesi. SHIKA SANA ULICHO NACHO, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Hapo anasema “..Asije mtu.” na si “..Asije shetani”. Maana yake anayeitwaa taji ya mtu ni MTU, kwasababu shetani yeye taji lako au langu halimsaidii kitu, kwasababu haendi kulivaa.. lakini mwingine akilichukua litaenda kumfaa anakokwenda!.
Labda tuzidi kuliweka hili vizuri..
Aliyelichukua Taji la “Yuda Iskariote” ni mtu aliyeitwa “Mathiya”… baada ya Yuda kushindwa kushikilia alichopewa…
Matendo 1:24 “Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,
25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe.
26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja”.
Vile vile aliyeichukua Taji ya “ESAU” ni ndugu yake “YAKOBO”…Baada ya kuidharau ile haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa tamaa ya chakula kimoja tu.
Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, k**a Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi”
Umeona unapoacha kuthamini kile ulichopewa, basi mwingine atakichukua,..unapoacha kuthamini nafasi yako mwingine ataichukua.. Unapoacha kuthamini huduma yako uliyopewa na Mungu, mwingine ataichukua na utapoteza thawabu zako.
> Umepewa huduma ya Uinjilisti, usiipuuzie na kuifanya kilegevu.. Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine atakayeifanya vizuri na kwa ushujaa.
> Umepewa huduma ya maombezi, fanya hayo kwa bidii, usipuuze kwani Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine ikiwa utaipuuza.. na thawabu yako (Taji yako) utakuwa umeipoteza.
> Umepewa huduma ya kukirimu (kwamba kupitia ulivyopewa unahudumia watumishi na kazi ya Mungu) basi usidharau neema hiyo kwasababu Bwana anaweza kuiondoa kwako na kumpa mwingine na hivyo Taji yako ikaondoka, fanya uliyojaliwa na BWANA kwa bidii sana..(Na huduma nyingine zote ni hivyo hivyo).
SHIKA SANA ULICHO NACHO!!.. SHIKA SANA ULICHO NACHO!!!… SHIKA SANA ULICHO NACHO!! Kwasababu kina thamani kubwa!.. Hakikisha unakizalia matunda.
Na majira haya, shoka lipo kwenye mashina ya miti kukata kila tawi lisilozaa,
Luka 3:9 “Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.
Bwana atusaidie tusikatwe. Lakini Neno ni moja tu kwetu. TUSHIKE SANA TULIYO NAYO!!!
Bwana akubariki.
Nipe matokeo ya Mti usiozaa matunda.
NENO LA LEO
1 John 2:9-10
[9]Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
[10]Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.......******........
Tujichunguze je tupo nuruni?
MUNGU
NI
MWEMA
Hadi Rais Ruto akacheza.
Nyimbo ina nguvu
Glory be to God
Happy madaraka day
Big shout-out to my newest top fans! Wepu Mabonga, Petro Luarpyen Tow Mk, Ton Simiu Simiu, Noel Nosh, Patrick Mwanzi, Alex Wabomba, Pstr Paul Shivachi, Benjamin Juma, Sammidoh Sam, Mos Liza, Blessed Irine, Mike Wekesa, Sabbastian Alex, Kevin Kulundu Makawa Kevin, Michael Malachi, Peter Lubonga, Nickson Nyongesa, Phanice Onyango, Sarah Lukorito, Elizabeth Wachana, Sammy Wafula, Celine Cely, Nakhumicha Masungo, Dennison Wawire, Mamake Junior, Faithnelly Fayum, Emmah Bash, Hellen Sikuku, Esther Ivy, Leah Khasandi, Diorlizer Dashel, Shemlov Shem, Hellen Nasimiyu, Salome Busibo Galigado Galigado
Two more days to go
Permanent Presidential Music Commission
State House Kenya
Honoured to feature in this years Madaraka day celebrations theme song courtesy of .house.kenya
Psalms 12:7
Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele.
Big thanks to Noel Nosh, Pius Wanjala, Sarah Jay, Nekesa Masinde, Mukabwa Esther for being top engagers! Congrats for your streaks on my engagement list! 🎉
Nitajuaje k**a ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
JIBU: Maarifa yanayohusiana na ndoto ni mapana kidogo, lakini kwa ufupi, zipo ndoto za aina tatu,
1) Ndoto zinazotokana na shughuli (Mhubiri 5:3): hizi ndio mara nyingi zinamjia mtu, kwamfano mtu alikuwa anafanya shughuli fulani siku nzima na usiku anapolala bado anaota anaifanya ile shughuli au anaota mambo yanayoendana na jambo ambalo amekuwa akijishughulisha nalo mara kwa mara. Sasa Kutokana na shughuli ile kuchukua sehemu kubwa ya siku yake au maisha yake, inapelekea pia kuchukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa ndoto zake. Ndoto hizi ni mwili ndio unaozitengeneza, hazitokani na Mungu wala shetani.
2) Ndoto zinazotokana na yule mwovu. Hizi zinatengenezwa na yule mwovu na kutumwa ndani ya mtu, Hizi ni ndoto zote zenye maudhui ya kumfanya mtu aikane au aiache IMANI, au zinampelekea mtu aende mbali na mpango wa Mungu, au kutenda dhambi na huwa zinaambatana na ushawishi fulani mkubwa sana mara baada ya kuamka.
kwamfano mtu anaota kaachana na mume/mke wake na kupata mke/mume mwingine ambaye ni mzuri kuliko yule aliyekuwa naye, na anapoamka asubuhi anajikuta anaanza kuona kero ya kuishi na mke wake au mume wake k**a ilivyokuwa hapo mwanzo. Au anashawishika kuamua kumwacha mumewe au mkewe.
Au mtu anaota mzazi wake mmoja ni mchawi na hamtakii mema, na ile ndoto inamtaka ajitenge na huyo mzazi, au amchukie awe naye mbali. Au mwingine anaota anafanya uzinzi/uasherati na mtu asiyemjua au anayemfahamu, na anajikuta akiamka asubuhi ile roho ya tamaa bado inakuwa ndani yake kwa nguvu zaidi, tofauti na alivyokuwa jana.
Au mtu anaota kapata utajiri kwa kumwibia mwajiri wake, au kwa kucheza k**ari , na baada ya kuamka anajisikia msukumo ndani yake wa kwenda kufanya jambo lile na wakati mwingine mazingira aliyoyaona kwenye ndoto ndio hayo hayo anayaona akiwa nje ya ndoto kana kwamba ni unabii unatimia.. Au wakati mwingine mtu anaota ndoto ameenda kwa mganga, akafanikiwa na anapoamka anashawishika kufanya mambo yale, au mtu anajikuta anaota kuna sanamu mahali fulani au kuna mti mahali fulani umebeba mafanikio yake (pengine uani kwake) na kwenye ndoto anaona ameukata ule mti na mambo yote yakaharibika, na anapoamka anajikuta anaogopa kuukata ule mti akijua ndio mafanikio yake yapo pale.
Au wakati mwingine mtu anaota, ametenda dhambi na amejaribu kumwomba Mungu, na Mungu hataki kumsamehe, na anapoamka asubuhi anashawishika kuamini kuwa Mungu hataki kumsamehe na anamchukia. Au ndoto nyingine mtu anaota amekufa baada ya kujaribu kuwa mkristo au kumpa Kristo maisha yake. N,k…
Sasa ndoto zote k**a hizi zinatoka kwa yule mwovu kwasababu zina maudhui ya kumlazimisha mtu asilitii Neno la Mungu au aende kinyume na maagizo ya Mungu, zinampeleka mtu katika kutenda dhambi zaidi kuliko kumfanya kuwa mtakatifu, nyingine zinamfanya mtu awe mwoga zaidi na kumchukia Mungu kuliko kumpenda! N.k
Namna ya kuzidhibiti hizi ndoto ni kuamua kuishi maisha masafi yampendezayo Mungu na kujifunza kwa kina Neno la Mungu ili shetani anapoleta mawimbi yake k**a bahari uwe na uwezo wa kuyadhibiti, Kadhalika na kudumu katika maombi. kwamfano mtu anayeoota kafanya kosa na hasamehewi, hiyo ni mishale ya shetani kutaka kukuvunja moyo usitake kuendelea kumtafuta Mungu, kwahiyo k**a Neno halipo ndani yako linalosema
“1Yohana 1: 9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. ” hutaweza kumshinda shetani.
Au ndoto inapokuja umegombana na mke wako na umeachana naye na kupata mwingine bora kuliko huyo, utajua imetoka kwa yule mwovu kwasababu Neno la Mungu limekaa ndani yako linalosema
“Luka 16:18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini. ”
Hivyo unajua ni ndoto iliyotoka kwa yule mwovu kukutaka wewe kutoka nje ya kusudi la Mungu na kutenda dhambi. Au unapoota umebeti na umekuwa tajiri ghafla, utajua kabisa ni ndoto kutoka kwa yule mwovu kwasababu Neno la Mungu limekaa ndani yako linalosema “11 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. (Mithali 13:11)” Kwahiyo utajua ni yule mwovu anataka kukupeleka kwenye kazi iliyolaaniwa.
Kadhalika na ndoto nyingine zote zinazofanana na hizo utazipima kwa Neno la Mungu tu! na utaweza kuzishinda na kuzifahamu k**a Neno la Mungu linakaa ndani yako. Na pia kusali kabla ya kulala ni muhimu sana..Hiyo itasaidia kufunga mipenyo yote ya yule mwovu anayoweza kuitumia kukujaribu katika ndoto.
3)Aina ya tatu ya ndoto ni ndoto zinazotoka kwa Mungu. Hizi ni zile zinazomjia mtu kutoka kwa Mungu kwa maudhui ya kumwonya mtu au kumuimarisha katika imani, na hizi haziwi kwa wingi k**a zile zinazotokana na shughuli nyingi. Mfano wa ndoto hizi ni pale mtu anapoota kakutana na mtu/muhubiri kamshuhudia na kumwonya juu ya maisha yake maovu na anapoamka asubuhi anajikuta anahukumiwa na maisha ya dhambi anayoishi na kushawishika kutubu. Na mfano mwingine wa hizi ndoto ni pale mtu anaota unyakuo umepita na kaachwa, na anapoamka asubuhi anashawishika kujikagua maisha yake, nyingine mtu anaota kafa na kaenda kuzimu na anapoamka asubuhi anagundua ilikuwa ni ndoto tu.
Nyingine ni zile mtu anaota kafanyiwa jambo baya sana la kumuumiza, na anapaamka asubuhi anajikuta yeye ndiye kamtendea mtu hilo jambo, hivyo anashawishika kujirekebisha na kutubu, Nyingine unakuta mtu anaota kabeti, au kaenda kwa waganga, au kufanya uasherati, au kaiba, au kamtukana mtu, au kachukua mke au mume wa mtu, au kamsengenya mtu, au kaua na baada ya kufanya hivyo mambo yake yote yakaharibika, akajikuta kafilisika, au kafungwa, au kahukumiwa kufa, na anapoamka asubuhi anashawishika kutokufanya moja wapo ya mambo hayo ili yasimpate hayo mabaya. Hizo ni ndoto kutoka kwa Mungu, zinalenga kumuonya mtu Na nyingine unakuta mtu anaota yupo shuleni anasoma, na kumbe alishamaliza muda mrefu sana, na anajiona anapambana kusoma na bado anafeli, ndoto ya namna hii unajua kabisa ni kutoka kwa Mungu kwasababu inayokuonyesha aina ya maisha unayoishi kwamba mwendo wako ni wa taratibu katika kumtafuta Mungu na bado upo nyuma ya wakati.
Kwahiyo kwa ufupi ndoto zote zinazotokana na Mungu utazijua pia k**a Neno la Mungu linalo kaa ndani yako, ndoto yoyote inayokupeleka kumtafuta Mungu zaidi, kutubu, au kukuonya tabia uliyonayo ambayo sio nzuri unajua kabisa ndoto hiyo inatoka kwa Mungu , au uichukie imani au ujitenge na kweli basi hiyo utajua moja kwa moja ni ya shetani.
Ayubu 33:14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
Ubarikiwe sana.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Videos (show all)
Category
Telephone
Address
Kitale
Kitale
African Pride Boy,From Zero To Hero The Boy With Vision In Mission Call Me Platah √√√