Riyadh Swaliheen Kisw

Riyadh Swaliheen Kisw

"Manhaj Ya Qur-aan Na Sunnah
Kwa Ufahamu Wa Salaf Wa Ummah"

09/06/2023

:


Everyone

Send a message to learn more

07/06/2023
31/05/2023

....

26/05/2023

...

25/05/2023

Swalaa..!

24/05/2023

Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم :

{|[Hakika Mwanamke atakae kufa hali ya kuwa tumboni kwake kuna Mtoto huyo ni .]|}

04/02/2023

SOMA DUA HII UNAPOAMKA TOKA USINGIZINI (MARA MOJA)

01/01/2023

:



1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:

لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ

"Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake" Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr



2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:

((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))

"Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi". [Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy]



3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((لاَ تُنْفِقُ الْمَرْأَةُ شَيْئًا مِنْ بَيْتِهَا إِلا بِإِذْنِ زَوْجِهَا)) قالوا: "يا رسول الله! وَلا الطَّعَامَ؟ قال: ((ذَاكَ أَفْضَلُ أَمْوَالِنَا)) صحيح ابن ماجه - حديث حسن الألباني

"Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe". Wakasema: "Hata chakula ee Rasuli wa Allaah"? Akasema: "Hicho ni mali bora yetu". Hadiyth Imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.



Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe. Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:

عن همام (رضي الله عنه) قال: سمعت أبا هريرة (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا أَنْفَقَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ كَسْبِ زَوْجِهَا عَنْ غَيْرِ أَمْرِهِ فَلَهُ نِصْفُ أَجْرِهِ)) - البخاري

Kutoka kwa Hamaam (Radhwiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake". [Al-Bukhaariy]



4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).



5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Jannah (Peponi):

عن عبد الرحمن ابن عوف (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَحَفِظَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا, قِيلَ لَهَا: ادْخُلِي مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ شِئْتِ)) صحيح الترغيب

Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhwaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia Jannah (Peponi) kupitia mlango wowote autakao." Swahiyh at-Targhiyb



Hizo ni baadhi ya haki tulizojaaliwa kuzinukuu, tukitaraji kwamba pindi zikitimzwa, basi ndoa itaendelea kudumua katika usalama na amani.

01/01/2023

:

1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.



2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa). [An-Nisaa: 34]



Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu: ((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: "Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali" (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: "Ina maana mpigo usio wa nguvu".



Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:



i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.



ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.



iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali k**a alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:

عن جابر (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: أنه قال في حجة الوداع: ((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ، ولكم عليهن ألا يُوطِئْنَ فُرُشكم أحدا تكرهونه، فإن فَعَلْن فاضربوهن ضَرْبا غير مُبَرِّح، ولهن رزْقُهنَّ وكِسْوتهن بالمعروف))

Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: "Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha".[Muslim]



3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa k**a ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha hivyo:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu hawana huruma, shadidi, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. [At-Tahriym: 6]



4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.



5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. [An-Nisaa: 34]

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake" [Al-Bukhaariy na Muslim]



6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakataza kutokufanya uadillifu:



وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ

6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakataza kutokufanya uadillifu:



وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ

Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) k**a kining’inio. [An-Nisaa: 129]



Na Anasema:

فَإِنْ خِف ْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ذَلِكَ أَدْنَى أَلاَّ تَعُولُواْ

Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. [An-Nisaa: 3]



Juu ya hivyo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:



"Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu." At-Twabaraaniy

31/12/2022

Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ

Nao wake wana haki k**a ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. [Al-Baqara: 228]



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Swahaba:

((يآ أيُّهَا النَّاسُ إِنَّ لِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقاً وَلَكُمْ عَلَيْهِنَّ حَقّ)) أبو داود

"Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu," [Abu Daawuud]



Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:



1-Ukweli

Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 11]



2-Mapenzi, Huruma Na Utulivu.

Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَة ًإِنَّ فِي ذَلِكَ لَآ يَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.” [Ar-Ruwm 30: 21]



3-Amana, Uaminifu Na Kutumiza Ahadi:

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٨﴾

Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga. [Al-Muuminuwn: 8]



Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:

فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ

Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; [Al-Baqarah: 283]



4-Tabia Njema

Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa: 19]



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:



"Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake" [Al-Bukhaariy na Muslim]



5-Kuhifadhiana Siri

Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake". [Muslim]



Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلاَ تَنسَوُاْ الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). [Al-Baqarah: 237]

19/08/2022

:
Ama kipengele cha pili cha kumsomea mtu mwengine(Mgonjwa) aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri inafaa usome Aayah zifuatazo:

Mwanzo unaanza na A’udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.

Al-Faatihah (Suwrah ya kwanza).
Al-Baqarah (aayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
Suwrah Al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
Yunus (10: 81 – 82).
Twaaha (20: 69).
Al-Hajj (22: 19 – 22).
Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
An-Naml (27: 30 – 31).
Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
Al-Fath (48: 29).
Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
Al-Hashr (59: 21- 24).
Al-Jinn (72: 1 – 9,
Al-Buruuj (85).
Zilzalah (99).
Al-Humazah (104).
Al-Ikhlaasw, Al-Falaq na An-Naas.
:
Unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekevu.

"Na Allaah Anajua zaidi"

19/08/2022

:

Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) na zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.


Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni k**a zifuatazo:

Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
Al-Israa’ (17: 110 – 111).
Al-Mu’minuun (23: 115 – 118).
Al-Hashr (59: 22 – 24).
Al-Kaafiruun (109).
Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).
:
Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekevu.

03/07/2022

*Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah - 01 - 10 Dhul-Hijjah*
Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo ‘amali njema huwa na thawabu nyingi mno. Na hivi Tayari tukiwa tumeshaingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa mbele ya Allaah ambazo 'amali yoyote inayotendwa humo ni yenye kupendwa mno na Allaah:
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah k**a (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Je, hata kuliko jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]

Ee ndugu Muislamu! Usiache fursa hii kukupita kujichumia thawabu tele kutokana na uzito wa malipo katika masiku haya. Hivyo basi tunawanasihi kusoma yafuatayo kuhusu fadhila za masiku haya kumi ya Dhul-Hijjah pamoja na amali za kutenda katika masiku haya matukufu kabisa mbele ya Allaah ('Azza wa Jalla).
I-Allaah Ameziapia Siku Kumi Hizi
Kwa jinsi zilivyokuwa na umuhimu mkubwa siku hizo kumi, hadi kwamba Allaah (Subhaanah wa Ta'aalaa) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))
Kwa Jina la Allaah, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku kumi)) [Al-Fajr: 1-2]

Wanachuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni siku kumi za Dhul-Hijjah.
'Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah:

Kutokana na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali yoyote utendayo katika masiku kumi hayo, ni bora kuliko kwenda kupigana jihaad vitani. Ukizingatia kwenda kupigana jihaad ni jambo zito mtu kuliitikia, kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo kupoteza mali, khofu ya kujeruhiwa na kupoteza viungo vya mwili, kufariki, n.k. Ila hilo si zito kwa mwenye iymaan ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili mashaka hayo na kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau ‘amali yoyote hata iwe ndogo vipi itekeleze kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Al-Jawwaad (Mwingi wa Ukarimu), Al-Kariym (Mkarimu), Al-Wahhaab (Mwingi wa kutunuku, Mpaji wa yote), Al-Majiyd (Mwingi mno wa vipawa na ukarimu).
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah k**a (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Yaa Rasula-Allaah! Je hata kuliko jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]



IV-'Ibaadah Zote Zimejumuika Katika Siku Hizi
'Ibaadah zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalaah, kufunga Swiyaam, Swadaqah, Hajj, wala hazijumuiki pamoja wakati mwingine.

*V-‘Amali Za Kutenda Katika Siku Kumi Hizi:*
1- Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo):
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Amali gani ni bora kabisa? Akasema: “Kumuamini Allaah na Rasuli Wake.” Akaulizwa: Kisha nini? Akasema: “Jihaad katika njia ya Allaah.” Akaulizwa: Kisha nini? Akasema: “Hajj Mabruwr.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
2- Kuomba Tawbah ya kweli na kujiepusha na maasi:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))

((Enyi walioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli!)) [At-Tahriym: 8]

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametupa matumaini makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao
Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

3-Kumdhukuru Mno Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
Kwa kuleta Takbiyrah kuanzia unapoandama mwezi wa dhul-Hijjah mpaka mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake. Dalili ni zifuatazo:
Ibn 'Umar na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda sokoni katika siku kumi (za Dhul-Hijjah) na kutamka Takbiyr kwa sauti na watu wakiwaigiza. [Al-Bukhaariy]

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ

Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. [Al-Baqarah: 203]

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku maalumu ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah." [Al-Qurtwubiy: 3.3]

Mdhukuru Allaah Ta'aalaa zaidi kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr: Maana yake ni: kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLLaah, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar.

Takbiyr katika masiku haya matukufu ni aina mbili:[1]
A) Takbiyr Al-Mutwlaq: Za Nyakati Zote:
Takbiyr wakati wote mchana na usiku, mahali popote ulipo, tokea unapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah) na kumalizika baada ya kuingia Magharibi.

B) Takbiyr Al-Muqayyad: Za Kuthibitika Mahali Maalumu Na Nyakati Maalumu, Za Kukadirika:

Takbiyr baada ya kila Swalaah za fardhi na huanza baada ya Swalaah ya Alfajiri Siku ya 'Arafah mpaka mpaka baada ya Swalaah ya Alasiri siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah).

Inavyopasa kufanya Takbiyr:
اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد
*Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd*
Wanaume wanatakiwa waseme kwa sauti ili kuwakumbusha wengine na wanawake waseme kimya kimya isipokuwa wakiwa na mahaarim wao.
5- Kufunga Swiyaam siku hizi khaswa siku ya 'Arafah.
Kufunga Swiyaam siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:
Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]

inamweka mtu mbali na Moto
Abuu Sa'iyd Al-Khudhwriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayefunga Swiyaam siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atauweka uso wake mbali na moto masafa ya miaka sabiini.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
🔹Na Swawm ina thawabu maradufu.
Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga Swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk.” [Muslim na Ahmad]
7🔹- Kuchinja baada ya Swalaah ya 'Iyd:
Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):
((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ))
((Basi Swali kwa ajili ya Rabb wako na uchinje)) [Al-Kawthar: 2]
kufanya mwenye kutaka kuchinja:
Baada ya kutia niyyah ya kuchinja, asikate mtu nywele wala kucha mpaka amalize kuchinja.
Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtakapoona mwezi umeandama wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake).” [Muslim na wengineo] Na katika riwaayah nyengine: "Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja."

*8- Kuhudhuria Swalaah ya 'Iyd:*
Kwenda kuswali Swalaah ya ‘Iyd ni jambo lilosisitizwa mno na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Waislaam wengi wamepuuza ‘amali hii na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza mpaka wanawake walio katika hedhi na wazee waende kusikiliza khutbah ya Swalaah. Wakati wa Swalah ukifika, wanawake hao wenye hedhi wajitenge kando hadi itakapomalizika Swalaah na kisha wajiunge na wenzao kusikiliza khutbah.
*9-‘Amali za Kutenda Siku Ya ‘Arafah Ambayo Ni Siku Ya Tisa Dhul-Hijjah*
a) Mwenye kufunga Swawm, atafutiwa madhambi ya miaka miwili!
Siku hii tukufu ni siku iliyokamilika Dini yetu. Thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili.
Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swawm ya 'Arafah, nataraji kwa Allaah kuwa afute madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]

*c) Du'aa bora kabisa ni Du'aa katika siku ya 'Arafah*
Inapasa kumdhukuru mno Allaah siku hii k**a alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:
“Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:
*Laa Ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. [At-Tirmidhiy]*

13/04/2022

:
Kuitidali ni kusimama wima kutoka kwenye Rukuu(kuinama),

Wakati wa kunyanyuka, Mswaliji Atanyanyua kichwa chake huku Akisema maneno haya: ”Samiallahu Liman-Hamidah”, "Mwenyezi Mungu anamsikia kila mwenye kumhimidi".

Na Atanyanyua mikono yake k**a Alivyonyanyua wakati wa Takbira ya kufunga swalah.

Baada ya kusimama sawasawa Atasema ”Rabbanaa walakal-hamdu". "Ewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako".

🔜Halafu Atasujudu.

Photos from Riyadh Swaliheen Kisw's post 13/04/2022
11/04/2022

*MASHARTI YA KUKUBALIWA TOBA*
Toba inahitajika kwa kila dhambi tunalofanya, dogo au kubwa. Allaah سبحانه وتعالى Anasema:
}}وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ{{
{{Na tubuni nyote kwa Allah, enyi Waumini ili mpate kufaulu}}
An-Nuur :24:31

Pia Amesema:
}}يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا{{
{{Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allah toba ya sawa sawa}}
At-Tahirym 66: 8 .

Toba ina masharti yake lau yatapatikana basi Allaah سبحانه وتعالى atakusamehe dhambi lolote ulilolifanya. Yakiwa maasia ni baina ya mja na Allaah سبحانه وتعالى hakuna kabisa haki ya mwanadamu basi yatakuwa na masharti matatu:
1. Kuacha hayo maasia.

2. Kujuta kwa kufanya hayo maasia.

3. Kuazimia kutorudia tena milele.

🔹Na ikiwa katika maasia yenyewe ipo haki ya mwanadamu, mfano: *kuiba Mali ya mtu*
Basi masharti yake yatakuwa manne: Matatu ya juu na sharti la nne litakuwa ni kurudisha haki ya mwenziwe na kutaka msamaha kutoka kwake.

🔹Allaah سبحانه وتعالى Ametuelezea kuwa Yeye husamehe madhambi yote maadamu mja hatakufa katika hali ya kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى au kufanya madhambi yaliyo makubwa k**a tunavyoona katika Aayah zifuatazo:
}}وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ يَلْقَ أَثَامًا{{
}} يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا{
}}إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا{{
}} وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّهِ مَتَابًا{{
{{Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi Aliyoiharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara}}

{{Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka}}.

{{Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}}.

{{Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Allaah}}
Al-Furqaan 25: 68 – 71 .

Na Amesema tena:

}}قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ{{
{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Allaah . Hakika Allaah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}}
Az-Zumar 39: 53 .

Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم anatuelezea hayo pia:

((اتق الله حيث ما كنت , واتبع السيئة الحسنة تمحها))
((Mche Allah popote ulipo na ufuatishe jambo baya kwa zuri, litalifuta (hilo baya))) (at-Tirmidhy, Pia imenukuliwa na Ahmad na ad-Daarimi kutoka kwa Abu Dharr na Mu‘adh))

Na amesema tena:
((إن الله يقبل توبة العبد ما لم يغرغر)) الترمذي و أحمد وإبن ماجه وصححه إبن حبان
))Hakika Allah Aliyetukuka hukubali toba ya mja maadam roho haijafika kooni (hayuko katika kukata roho)( (at-Tirmidhy, Ahmad na ibn Maajah na ameisahihisha Ibn Hibbaan).

*Hizi aya na Hadithi ni dalili tosha ya kwamba toba inakubaliwa kwa madhambi yote maadamu mja atafuata masharti yake*
🔹lakini tujue ya kwamba toba haikubaliwi kwa hali hii Aliyoitaja Allaah سبحانه وتعالى : Anasema :
}}وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّى إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الآنَ وَلاَ الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ أُوْلَـئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا{{
{{ Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu}
An-Nisaa 4: 18

Kwa ajili hiyo Allaah سبحانه وتعالى Aliikataa toba ya Firauni pale alipokuwa anaghariki katika bahari
}}وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا حَتَّى إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لا إِلِـهَ إِلاَّ الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَاْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ{{
{{Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Fir'awn na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Fir'awn alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!}} (Yunus: 90)

Allaah سبحانه وتعالى Akamuuliza Fir'awn wakati anatapatapa na kuomba na kudai kuwa kaamini:
}}آلآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ{{
{{Alaa! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!}}
(Yunus: 91)

Kisha Akaikataa Tawbah yake katika hali hii:
}}فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ{{
{{Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu}}
(Yunus: 92)

*Aya hizi kuna mazingatio makubwa kwa Waumini hasa na wanaadamu kwa ujumla*
Wa Allaahu A'alam...!

10/04/2022

*Swalah Na Du’aa Za Kusoma Unapotaka Kutubu*
Hivyo, jambo la kwanza linalokupasa ni kumshukuru Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa) kwa Kukuzindua ukatambua kuwa uko makosani kabla ya adhabu Yake au mauti kukufika. Yote hayo ni neema kutoka kwa Mola wako unapasa umshukuru sana kila wakati.

*Kuomba Maghfirah unaweza kuswali Rakaa mbili tu kwa nia moyoni ya kuomba Tawbah kwa Mola wako*
Ama du’aa, ziko mbali mbali ambazo hata Mitume waliomba walipokuwa wakifanya makosa au katika kawaida ya kumdhukuru Allaah, pamoja na adhkaar mbali mbali alizotufunza Mtume (Swallah Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)



Du’aa ifuatayo ambayo inaitwa ‘Sayyidul-Istighfaar’ (Bwana wa Kuomba Maghfirah) inapasa uisome kila mara na katika usimulizi Swahiyh ni kwamba pindi ukiisoma asubuhi ikawa ni ajali yako kuondoka duniani basi utaingia Peponi. Na pindi ukiisoma jioni ikawa usiku huo ni siku ya kuondoka duniani basi utaingia Peponi. Hivyo inampasa kila Muislamu awe anaidumisha du’aa hii kila siku asubuhi na jioni:



اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك ، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت ، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت ، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .

‘Allaahumma Anta Rabiiy laa Ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘Abduka wa ana ‘alaa ‘Ahdika wa Wa’dika mastatwa’tu, A’uudhu Bika min sharri maa Swana’tu, abu-u Laka Bini’matika ‘alayya wa abu-u bidhanbiy, Faghfir-liy fainnahu laa yaghfirudh-dhunuuba illa Anta’
*Tafsir*
Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, Umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa Kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba Unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe”

Vile vile:
Du’aa ya kusoma baada ya Tashahhud na kabla ya kutoa Salaam katika Swalah:

اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت ، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني، إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم

Allaahuuma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman-kathiyran wa laa yaghfirudh-dhunuuba illa Anta. Faghfir-liy maghfiratam-min ‘Indika War-Hamniy, Innaka Antal-Ghafuurur-Rahiym.
*Tafsir*
‘Ee Allaah hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka Kwako, na Unirehemu, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu’

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

#KILA_NAFSI_IJIULIZE_JAMBO_HILI....
SOMA DUA HII UNAPOAMKA TOKA USINGIZINI (MARA MOJA)
#Ramadhaan_1442_AH#Nguvu_Ya_Utashi Na Sheikh Kombo Ally Fundi  #RiyaadhSwalheenkisw
Allah Tujaalie Furaha Ya Kweli Inshaallah..!

Address

Arusha