Habari, Mikasa na Matukio.

Page hii inahusu mambo ya kitaaluma na habari mbalimbali zinazoelimisha jamii, siasa na michezo.

31/05/2024

Mwakinyo ana tatizo kubwa anahitaji msaada wa kisaikolojia.

31/05/2024

Kwamba hizi kodi tunazolipa zote hazitoshi kujenga barabara ila zinaweza kununua magari ya wabunge tu?

30/05/2024

US sanctions Uganda’s Parliament Speaker Anita Among, four other current and former ministers for alleged involvement in corruption and gross human rights violation.

29/05/2024

BODY OF KENYAN hiker Joshua Cheruiyot Kirui will remain on Mt. Everest; family says decision made after extensive consultations and careful consideration of all circumstances.

29/05/2024

IRAN vs ISRAEL - 02
Sehemu ya 2

Na Dr. Chris Cyrilo
Mapinduzi ya mwaka 1979 yaliyoondoa utawala wa Shah, na kuifanya Iran kuwa chini ya utawala wa kiislamu wa dhehebu la Shia, yalifuta ndoto ya Iran kupata silaha za kinyuklia. Utawala wa kishia, uliokuwa chini ya Ayatolla Khomeini ulijikuta ukipigana vita dhidi ya Saddam Hussein kwa miaka 8, kuanzia Septemba 22, 1980 hadi Agosti 20, 1988. Saddam Hussein alikuwa akitumia silaha kali za kikemikali, gesi za sumu pamoja na mabomu ya Scud kiasi cha kusababisha vifo kwa mamilioni ya watu wasio na hatia. Kiongozi wa Iran, Ayatollah Khomeini alikataa kutumia silaha za kikemikali kwa sababu za imani ya kidini, lakini alisikitishwa kuona dunia imekaa kimya bila kukeme vitendo vya Saddam. Baadaye, Ayatollah aligundua kuwa Saddam alikuwa akipata msaada wa kivita kutoka nchi za Magharibi, hususani Marekani na jambo hilo likabadili msimamo wake kuhusu silaha.

Mwaka 1990 baada ya kifo cha Ayatollah Khomeini Iran iliamua kurejea mpango wake wa kumiliki silaha za kinyuklia lakini sasa ikiwa na marafiki wapya, Urusi, Uchina na rafiki mwingine mkubwa aliyeitwa Abdul Qader Khan, raia wa Pakistan na mwanateknolojia mashuhuri wa silaha za nyuklia katika ukanda wa mashariki ya kati. Abdul Qader Khan ndiye aliyeua mitambo ya nguvu za kinyuklia nchini Libya, lakini Iran haikutaka kununua mitambo bali michoro na maelekezo ili iweze kujitengenezea mitambo yake yenyewe.
Wakati huu, Israel ilianza kuangalia Iran kwa jicho la uadui kwakuwa Iran tayari ilikwisha kuwa adui wa Marekani ambayo ni rafiki mkubwa wa Israel. Uadui wa Iran na Marekani ulianza baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Shah na kuanza kwa utawala wa kiislamu wa Shia, mapinduzi yalioambatana na kuwatia kizuizini wanadiplomasia 52 wa Marekani walikuwamo mjini Tehran kwa karibu miaka takriban miwili (1979 - 1981).

Baadhi ya wafanyabiashara wa Israel waliendelea kufanya biashara na Iran lakini kwa siri kubwa ili Marekani isigundue. Nahum Manbar, ofisa wa shirika la Mossad alikuwa kiungo muhimu wa biashara ya silaha baina ya Israel na Iran. Zaidi ya silaha kutoka Israel, Manbar alifika hadi Poland kununua silaha na kuiuzia Iran iliyokuwa ikijiimarisha upya baada ya kuachwa hoi na vita dhidi ya Saddam Hussein. Manbar alifika hadi china kwa ajili ya kutafuta malighafi za kutengenezea silaha za kemikali na kuiuzia Iran. Mashushushu wa kiingereza wa MI6 waligundua biashara hii kwakuwa baadhi ya mipango ilifanyika mjini London, lakini iliwawia vigumu kuamini k**a kweli Israel inafanya biashara ya silaha na utawala wa kishia wa Iran. Viongozi wa MI6 walibaki kuamini kuwa Nahum Manbar alikuwa na lengo la kuzama ndani ya jeshi la Iran ili kuchota tarifa muhimu za kiintelijensia kwa ajili ya Israel, ingawa haikuwa hivyo. Nahum Manbar alikuwa jasusi wa Mossad aliyefanya biashara na Iran kwa faida zake za kibiashara na si kiintelijensia.

Shirika la Mossad na shirika la intelijensia la ndani ya Israel, ShinBet, kwa pamoja waliamua kumfuatilia Manbar. Katika operesheni moja huko mjini Venna, Austria majasusi wawili wa Mossad wakiwa na pikipiki walikuwa wakifuatilia mienendo ya Manbar, lakini waligongwa na gari na wote wawili kufa papo hapo. Shirika Mossad liliamua kufanya uchunguzi wa tukio hilo ili kujua endapo ajali hiyo ilipangwa na intelijensia ya maadui au la, lakini haikuwahi kufahamika wazi na hakukuwa na sababu yoyote ya kumlaumu Manbar. Hata hivyo vifo vya majasusi wawili wa Mossad vilichochea hamu ya kumuadhibu Manbar kwa kufanya uchuuzi wa bidhaa za kikemikali kwa taifa adui. Mwaka 1997, Manbar alik**atwa na kufunguliwa mash*taka kwa siri kubwa bila vyombo vya habari kujua, hatimaye alihukumiwa miaka 16 jela.

Jukumu la kudhibiti mpango wa silaha za nyuklia wa Iran lilikuwa gumu kwa Meir Dagan lakini hakutaka kushindwa kamwe ili asipate aibu kutoka kwa waziri mkuu Ariel Sharon. Wote wawili, Sharon na Dagan waliwahi kufanya kazi pamoja k**a majenerali wa jeshi la Israel. Ili kutimiza jukumu hilo, ilikuwa lazima kuiimarisha zaidi shirika la Mossad kuliko lilivyokuwa awali. Mossad na Aman (intelijensia ya jeshi la Israel) waliamua kushirikiana pamoja katika kazi hii ngumu baada ya kujiridhisha kuwa mpango wa Iran wa kutengeneza silaha za Nyuklia ulikuwa unakwenda kwa kasi, kwa kusaidiwa na wanasayansi wa ndani hasa wabadhirifu wa vyuo vikuu na wengine kutoka mataifa rafiki. Iran yenyewe ilitumia mbinu nyingi kuficha mpango huo, mojawapo ni kutumia shughuli za kijamii k**a upanuzi wa miundombinu ya umeme na viwanda vya kutengenezea dawa za binadamu na bidhaa za kilimo. Lakini intelijensia ya Israel ilijiridhisha kwamba Iran wanatengeneza silaha za Nyuklia, na kukadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2004 Iran itakuwa inamiliki angalau bomu moja la nyuklia. Waziri mkuu Sharon alimwambia Dagan itakuwa ni hatari na jambo la aibu kwa intelijensia ya Israel, serikali ya Israel na wayahudi wote endapo Iran itamiliki hata bomu moja la Nyuklia. Kwa maneno hayo, Dagan alikuwa ametumwa vitani kwa sharti moja tu la kushinda, na vita hiyo ilikuwa ya kutumia silaha yoyote iliyopo. Dagan aliamua kuanzisha vita na Iran, vita ya kisiasa, kisaikolojia na kiuchumi kwa njia za siri za kiintelijensia.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuharibu uhusiano wa kidiplomasia wa Iran na marafiki zake, pamoja na kutengeneza vikwazo vya kidiplomasia kutoka kwa jumuiya za kimataifa. Utawala wa Ayatollah ulipokea ujumbe mara kwa mara kutoka mataifa mengine ukiwalazimisha kuachana na mpango wao wa Nyuklia la sivyo hatua kali zitachukuliwa juu yao.
Hatua ya pili ilikuwa kuwashawishi washirika wa kibiashara wa Iran kuiwekea Iran vikwazo vya kiuchumi ili kudororesha uchumi wa Iran. Mashirika mengi yalikuwa ya Ulaya, ambayo yaliaminishwa kuwa mpango wa nyuklia wa Iran ni hatari kwa mataifa ya Ulaya. Matumaini ya Israel yalikuwa kwamba Iran itaamua yenyewe kuacha mpango wa Nyuklia kwakuwa vikwazo vya kiuchumi vitadhibiti biashara zake, safari za viongozi na raia, mihamara ya kifedha na manunuzi ya bidhaa kutoka nchi za nje, zikiwemo bidhaa zinazotumika katika mpango huo wa Nyuklia. Kwa imani ya Intelijensia ya Israel, isingekuwa rahisi kwa Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia huku raia wake wakitaabika, ilihali ilikuwa serikali inaongozwa kwa misingi ya dini inayohitaji kuungwa mkono na wananchi wengi.

Hatua ya tatu, ilikuwa ni kujifunza kwa undani muundo wa kijamii wa watu wa Iran pamoja na makabila yao. Nusu ya idadi ya watu wa Iran ni waajemi (Persians), na nusu nyingine inaundwa na makabila kadhaa; Waazeri, Wakurdi, Waarabu, Mabaluchi, (Balushi) na Watukimini. Watu wa makabila madogo walitazamwa k**a watu duni na kuonewa kwa namna fulani. Hapo ndipo intelijensia ya Israel ilipopata mwanya wa kuanzisha vita ya kisaikolojia kwa kuwatumia wananchi wasio na furaha na kuwatumia kuisumbua serikali ya Iran.
Kwa siri kubwa, Intelijensia ya Israel iliwanunua baadhi ya viongozi ndani ya serikali wa ya Iran na maofisa waliofanya kazi kwenye mpango wa nyuklia ambao walishiriki kufanya hujuma kwenye mradi huo na kuua wataalamu waliokuwa wakifanya kazi kwenye mitambo ya ki-nyuklia.

Utafiti uliofanywa na Intelijensia ya Israel ulibaini kuwapo viongozi wa ngazi za juu wa Iran ambao hawawezi kushawishiwa kwa maneno bali kwa vitendo ili wajue kuwa mpango wao sio tu ni hatari kwa Israel bali pia ni hatari kwao. Serikali ya Israel haikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Iran, urafiki wao wa zamani ulibadilika kuwa uadui uliowabadili kuwa mataifa hasimu yanayowasiliana kupitia vyombo vya habari tu. Kwa sababu hiyo, ilibidi Israel kutumia mataifa mengine ya Ulaya, Asia na Marekani kwa ajili ya kutuma na kupokea ujumbe. Marekani na washirika wake walikuwa wakifanya mazungumzo na Iran kila mara kishawishi nchi hiyo iachane na mpango huo, kisha taarifa kuhusu mazungumzo hayo zilifika Israel. Pamoja na hujuma zote hizo, Iran ilibaki na msimamo wake wa kutaka kumiliki silaha za Nyuklia, na kusababisha mataifa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi mwaka 2012.

Viongozi wa kisiasa wa Israel walishawishi Mossad kuanzisha vita halisi dhidi ya Iran, kwa kulipua maeneo yote ambayo mradi wa nyuklia ulikuwa ukiendelea, lakini maofisa wa Mossad walisita. "Mradi wa nyuklia wa Iran haukuwa hatari kwa Israel pekee bali kwa dunia nzima", ni kauli iliyotolewa na wanasiasa wakubwa wa Israel tangu wakati wa waziri mkuu Arier Sharon kisha Ehud Omert na baadaye Benyamin Netanyahu, lego likiwa ni kuishawishi mataifa mengi ya dunia kuichukia Iran na kuacha kushirikiana nayo. Hata hivyo, mbinu hiyo ilifanikiwa kirahisi kwa wanasiasa na watu wa kawaida, lakini sio kwa vyombo vya kiintelijensia vya mataifa mengine ambavyo vilijua fika kuwa Israel ndio ilikuwa hatarini na sio dunia yote. Ilikuwa ni kazi ngumu kushawishi jumuia yote ya intelijensia ya dunia kuwa Iran ni nchi hatari kwani mwaka 2007, Rais wa Marekani George W. Bush alipokea taarifa kutoka Intelijensia ya Marekani kuwa Iran iliachana na mpango wake wa nyuklia tangu mwaka 2003 kwa hofu iliyotokana na uvamizi wa Marekani nchini Iraq. Kwa mujibu wa intelijensia ya Marekani, ni kwamba Iran iliogopa isije kuvamiwa na Mataifa ya magharibi kwa sababu Iraq ilivamiwa kwa vigezo vlivyotolewa na Marekani kuwa ni kumiliki silaha za maangamizi.

Kwanini dunia iamini kuwa taarifa za Israel ni sahihi kuliko za Marekani?

Itaendelea...

29/05/2024

ISRAEL vs IRAN -01
Kufuatia ahadi yangu ya kumchambua Ebrahim Raisi, nimeona bora kwanza tuanza na mahusiano ya Iran na Israel.

Sehemu ya I
Ndani ya jengo la makao makuu ya shirika la kijasusi la Mossad, ghorofa ya tatu ni rahisi kuona kibao kilichoandikwa Ramsad, neno ambalo ni kifupi cha maneno ya kiebrania - Rosh ha Mossad, yaani 'Mkuu wa Mossad'. Chini ya kibao hicho kuna mlango wa kuingia ndani ya ofisi ya mkuu wa Mossad, ofisi ambayo kuta zake zilipambwa na picha kadhaa zenye ujumbe maalumu kwa Meir Dagan aliyeongoza shirika la Mossad kuanzia mwaka 2002 hadi 2010. Picha moja kati ya chache zilizopo ndani ya chumba hiko, iliibua kumbukumbu na hisia za kutisha kila ilipotazamwa. Picha hiyo ilimuonesha mzee wa kiyahudi akiwa amepiga magoti, mkononi ameshika kitambaa maalum cha kufanyia ibada za kiyahudi kiitwacho Talllit, huku amezungukwa na askari wa chama cha N**i cha Ujerumani.

Mzee huyo wa kiyahudi alikuwa babu mzaa mama wa Meir Dagan, aliyeitwa Ber Ehrlich Sloshny na picha hiyo ilipigwa katika mjini mdogo wa Lokov, nchini Ukraine muda mchache kabla ya mzee huyo na maelfu ya wayahudi wengine kuuawa mikononi mwa askari wa N**i. Ni kwa namna gani aliipata picha hii! Dagan anahadithia namna baba yake alivyosafiri hadi mjini Lokov ili kuwatafuta ndugu wa kiyahudi waliosalia, lakini hakukuwa na myahudi aliyebaki hai katika mji huo. Isipokuwa, mtu mmoja asiye myahudi alibaki kwa kazi ya kuzika miili ya wayahudi, amri aliyopewa na askari wa N**i. Mtu huyo, alikuwa na picha za wayahudi wengi ambazo pia alizichukua kwa amri ya askari wa N**i, mojawapo ikiwa ni picha ya mzee Sloshny. Baba yake Dagan alichukua picha hizo na kurudi nazo Israel.

Dagan aliibeba picha hii kila alipohama ofisi, na sasa akiwa Mkuu wa Mossad ameitundika ukutani na kuitazama kila siku. Ilikuwa ni kumbukumbu ya namna jamii ya kiyahudi lilivyoponea chupuchupu kutoweka juu ya uso wa dunia kutokana na mateso na mauaji dhidi ya wayahudi yaliyopamba moto huko Ulaya wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Picha hiyo pia ilitoa funzo mujarabu, ya kwamba binadamu anaweza kugeuka kirahisi na kuwa mnyama katili dhidi ya binadamu wengine, na hilo laweza kutokea kwa kila mtu.

Meir Dagan, akiwa Mkuu wa Mossad aliamini kuwa jukumu la kuhakikisha usalama, ustawi na uwepo jamii ya kiyahudi duniani upo mikononi mwake.
Moja kati ya majukumu makubwa aliyokuwa nayo, ni kudhibiti maadui wa Israel, hasa Majirani zake kumiliki silaha za maangamizi, kwa namna yoyote inayowezekana. Mwaka 2004, miaka miwili baada ya kubeba cheo cha ukuu wa Mossad, Meir Dagan aliamua kwamba jukumu namba moja ni kupambana na Iran ambayo ilidhamiria kwa dhati kumiliki silaha za kinyuklia, chini ya uongozi wa kishia wa Ayatollah Ruhollah Khomeini.

Dhamira ya kumiliki silaha za kinyuklia nchini Iran ilikuwapo tangu miaka ya 1950 wakati wa utawala wa Shah Mohammad Reza Pahlavi, aliyewekwa madarakani kwa nguvu za CIA na kufanywa kuwa kiranja wa eneo la mashariki ya kati. Wakati huo Iran iliweza kununua vinu vya kuzalishia nguvu za kinyuklia kutoka Marekani, kwa ajili ya kuzalisha umeme, kufanyia tafiti za kitabibu lakini pia, utawala wa Iran haukuficha dhamira yake ya kutumia teknolojia hiyo kwa manufaa ya kijeshi, jambo ambalo lingeongeza ushawishi zaidi kwa Majirani, maadui na marafiki wa mbali.

Wakati Iran ikinufaika kwa Teknolojia hiyo ya Marekani, Israel nayo ilitamani kupata chochote kutoka Iran, na hivyo kuunga urafiki wa karibu. Ingawa Israel ilikuwa ikipambana mara kwa mara na mataifa ya kiarabu, Iran iliyokuwa chini ya uongozaji wa ukoo wa Shah ilibaki kuwa rafiki wa Israel na kuhatarisha mahusiano yake na nchi za kiarabu, Saudia na Misri. Katika mashirikiano hayo, Intelijensia ya Israel iliweza kutoa mafunzo kwa kikosi cha siri ndani ya jeshi la polisi la Iran kilichoitwa Savack, na kwa upande wa Israel ilinufaika kwa kupata upendeleo wa kutumia ardhi ya Iran kwa shuguli zake za kiintelijensia dhidi ya mataifa mengine ya karibu, hususani Iraq. Ndani ya Iran, Intelijensia ya Israel iliweza kupanga mipango yake, kutekeleza misheni zake na kuwasajili mawakala wapya wa ushushushu wa kwenda kuiba taarifa katika nchi za kiarabu. Serikali ya Iran iliyoa hata nyaraka zake rasmi kwa ajili ya kusaidia shughuli za Irael. Kwa upande wa biashara Iran iliiuzia mafuta Israel na Israel iliiuzia Iran silaha, zaidi wakati Iran ikipigana vita dhidi ya Iraq.

Mradi wa pamoja wa nyuklia uliopewa jina la siri la 'Flower' ulilenga kuzipatia Iran Israel silaha za Nyuklia, huku Israel ikitoa msaada wa kiteknolojia na kuishawishi Iran itumie urafiki wake na Marekani kwa ajili ya kupata nyenzo zaidi ili zisaidie mradi huo. Lakini utawala wa Shah wa Iran ulikataa mpango huo, na endapo mradi huo ungekubalika basi leo hii Israel na Iran wangekuwa marafiki wakubwa au maadui wakubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Utawala wa Iran ulitamani kuwa na silaha za kinyuklia lakini haukuhitaji msaada kutoka Israel, kwakuwa Iran ilikuwa na marafiki wenye nguvu na teknolojia kubwa zaidi; Marekani, Ufaransa na Uingereza. Kwa hiyo, kwa Iran ilikuwa ni suala la muda tu kuweza kupata silaha za nyuklia. Israel, baada ya kukataliwa mpango huo iliamua kufanya operesheni yake binafsi kuelekea umiliki wa silaha za kinyuklia.

Inaendelea...

29/05/2024

MACHACHE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NCHINI AFRIKA.

Siku ya leo Jumatano ya 29 May, Taifa la Afrika Kusini limeanza rasmi kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kuchagua viongozi mbalimbali watakalolingoza Taifa hilo akiwemo rais kwa safari ya miaka 5 ijayo.

Huu unakuwa uchaguzi wa saba(7) kufanyika tangu 1994, ulipofanyika uchaguzi wa kwanza ulimuweka madarakani Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha ANC aliyepata 62.5% ya viti 400 vya ubunge.

Baada ya miaka 30 ya utawala wa Chama Cha African National Congress(ANC) mwaka huu inategemewa kukabiliwa na upinzani mkali zaidi katika historia, ili kupata asilimia 50%, ili iweze kutawala bunge ambapo mpaka sasa kabla ya kuanza uchaguzi ilionyesha kukubalika kwa 43% tu.

Mfumo wa kumpata rais nchini Africa Kusini hauruhusu wananchi moja kwa moja kumchagua rais bali, wanashiriki kufanya uchaguzi wa Wawakilishi wa viti 400, ambapo Chama kitakachopata viti 201 ambapo itakuwa ni zaidi ya 50% ya viti vyote kitakuwa kimeshinda uchaguzi na kumpata rais ili kuliongoza Taifa hilo

Africa Kusini ina jumla ya watu milioni 62, huku wapiga kura milioni 27.79 wakijiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi huo kulingana na tume ya uchaguzi ya Africa Kusini(IEC) na mtu mzima mwenye umri wa miaka 18 tu ndiye anayeruhusiwa kupiga kura.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika kwenye jumla ya majimbo 9 yanayounda Taifa hilo, huku kukiwa na takribani manispaa 257, jumla ya vituo vya kupigia kura 23,292, na rais atakayechaguliwa atahudumu kwa takribani miaka mitano.

Baadhi ya viongozi wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi huo ni pamoja na:

Cyril Ramaphosa(miaka 71) ANC

Kulingana na kura za maoni zilizoendeshwa na chombo cha habari cha eNCA, Ramaphosa ambaye ndiye rais aliyeko madarakani akiwakilisha Chama tawala cha ANC anaonekana kukubalika kwa 43.4% huku akitarajiwa kushinda majimbo 7 kati ya 9 nchini humo.

Kwenye uchaguzi uliopita mwaka 2019 ANC ilikuwa na uwakilishi wa viti 230 bungeni sawa na 57.5%

John Steenhuisen(miaka 48) DA

Anashika nafasi ya pili akiwa na 18.6% za kukubalika akiongoza Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance(DA).

Mpaka sasa DA inaonekana kwenda kulitwaa jimbo la Western Cape, ambako linapatikana jiji la Cape Town, ambapo mwaka 2019, DA ilishinda 55.45% ikishinda uchaguzi ndani ya jimbo hilo na walifanikiwa kuwa na ushindi wa viti 84 vya uwakilishi bungeni sawa na 21%.

Jacob Zuma(miaka 82) MK

Rais wa zamani wa Africa Kusini na kiongozi wa zamani wa ANC, amerudi kwa mara nyingine na Chama chake kipya cha uMkhonto we Sizwe(MK) ikiwa na maana ya "Mkuki wa Taifa" huku akionekana kukubalika kwa 14.1%

Mpaka sasa anaonekana kukubakika zaidi katika jimbo la Kwazulu Natal.

Julius Malema(miaka 43) EFF

Anak**alisha top 4 akionekana kukubalika kwa 11.4% kupitia Chama chake Cha Economic Freedom Fighters(EFF) ambapo uchaguzi uliopita alikuwa na viti 44 vya uwakilishi bungeni sawa na 11%.

Mshirika wa zamani wa Jacob Zuma ambaye alifukuzwa na Chama Cha ANC mwaka 2012 baada ya kutofautiana na Zuma na kuamua kuanzisha Chama chake cha EFF mwaka 2013.

18/11/2023

Mahak**a ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahak**a Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili (Sylvester Nyegu na Daniel Mbura) waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela

Mahak**a imesema imejiridhisha kwa ushahidi usioacha mashaka kuwa wajibu Rufaa (Sabaya na Wenzake) hawakuthibitika kutenda kosa la Unyang'anyi wa kutumia Silaha au Makundi bali walikuwa katika majukumu halali ya kufuatilia Makosa ya Uhujumu Uchumi

Awali, DPP alikata rufaa katika Mahak**a hiyo akipinga uamuzi uliowaachia huru Watuhumiwa akidai walihusika na uhalifu wa Kutumia Silaha na Kuendesha Genge la Uporaji

09/11/2023

NG'OMBE 806, KONDOO 420 NA MBUZI 100 ZAPIGWA MNADA HUKO SERENGETI, WAFUGAJI WALIA NA TANAPA.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kuwa suala linalohusisha Ng'ombe 806, Kondoo 420 na Mbuzi 100 waliok**atwa Serengeti na kupigwa mnada baada ya Mahak**a ya Musoma kutoa hukumu, limeshahitimishwa Kimahak**a baada ya taratibu zote kukamilika.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 9,2023 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Ole Shangai aliyeilalamikia Serikali kuhusu mifugo hiyo iliyok**atwa na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika eneo la Mugumu Serengeti na kupelekwa Mahak**ani kisha kupigwa mnada.

“Ni suala ambalo limehitimishwa Mahak**ani kupitia kesi ya jinai namba 10 ya mwaka 2023 kwa kuingiza mifugo hifadhini isivyo halali na tayari hukumu ilitolewa, na tarehe 1 Novemba 2023 ilielekezwa dalali wa mahak**a ateuliwe kwa ajili ya kupiga mnada wa hadhara kwa kufuata taratibu k**a ambavyo sheria yetu ya Wanyamapori ya mwaka 2009 lakini vilevile sheria yetu zinazosimamia Hifadhi za Taifa zinavyoelekeza ” Mhe. Kairuki amesisitiza.

Amesema, kufuatia mnada huo kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahak**a Kuu ya Musoma zilipatikana fedha kiasi cha shilingi milioni 169,264.

Aidha, ameongeza kuwa lengo la Serikali kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria ambazo zimewekwa ni kuendelea kulinda hifadhi za Taifa pamoja, maliasili na uoto wa asili uliomo ikiwa ni pamoja na wanyama na viumbe vingine vilivyoko katika maeneo yaliyohifadhiwa

Kufuatia ufafanuzi huo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameipa Serikali muda wa kuliangalia upya suala hilo.

19/10/2023

Mwanaume mmoja nchini Rwanda anayefahamika kwa jina la Callitxe Nzamwita mwenye umri wa miaka 71 amejitenga kwa kujifungia ndani kwa miaka 55 akidai kuwa sababu ni kuogopa wanawake.

Inaelezwa kuwa Nzamwita alipokuwa na miaka 16 ndipo alipata tatizo hilo la kuwa na hofu pindi awaonapo wanawake na kuamua kuchukua uamuzi wa kujitenga mbali kidogo na kijiji ambapo alijenga uzio wa miti futi 15 uliozunguka nyumba yake huku ikielezwa kuwa toka aingie katika uzio huo hajawahi kutoka nje.

Nenda kasome zaidi

19/10/2023

Uamuzi wa Serikali kuifanyia marekebisho Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika mwaka 2017 na kanuni zake ni chanzo cha Serikali kulipa Sh75 bilioni kwa mwekezaji Winshear Gold iliyemfutia leseni.

Fedha hizo zingeweza kutumika kuboresha sekta kadhaa za maendeleo, lakini zimeishia mikononi mwa mwekezaji kutokana na uamuzi uliofanywa na Serikali miaka michache iliyopita.

Fedha zilizolipwa kwa kampuni hiyo zingeweza kujenga zahanati 267 na vituo vya afya 68.

Kwa upande wa magari ya kubebea wagonjwa, yangeweza kununuliwa 250, moja likigharimu Sh300 milioni na kila mkoa ungeweza kupatiwa magari tisa.

Bado kukiwa na upungufu wa madarasa na madawati nchini, kiasi hicho cha fedha kingeweza kujenga madarasa 3,750 kwa gharama ya Sh20 milioni kila moja au kununua madawati 2.5 milioni kwa gharama ya Sh30,000 kwa kila moja.

Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

(Imeandikwa na Herieth Makwetta)

19/10/2023

(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐍𝐞𝐞𝐦𝐚 𝐄𝐦𝐦𝐚𝐧𝐮𝐞𝐥)

BAADA ya gazeti hili kuripoti zahanati mbili zilizojengwa kwa nguvu za wananchi kushindwa kutoa huduma licha ya kukamilika kwa zaidi ya miaka minne, huko wilayani Maswa mkoani Simiyu, kituo cha afya kingine kimebainika kuanza kubomoka kabla ya kuanza kutumika.

Kituo cha Afya cha Miswaki, kilichopo Kata ya Mwasubuya, wilayani Bariadi mkoani hapa kilichogharimu zaidi ya Sh. milioni 500, kinadaiwa kujengwa chini ya kiwango huku baadhi ya maeneo yakianza kubomoka kabla ya kuanza kutumika. /https://www.ippmedia.com/sw/habari/mbunge-ashtushwa-kituo-cha-afya-kuanza-kubomoka-kabla-hakijatumika

23/08/2023

Wananchi wa Zimbabwe wanapiga kura kuchagua Rais na Wabunge baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi zilizotawaliwa na suala la mfumuko wa bei.
Siku ya uchaguzi imefanywa kuwa ya mapumziko ili kuruhusu wananchi milioni 6.62 waliojiandikisha kupiga kura.
Rais Emmerson Mnangagwa anakabiliana na wagombea wengine 10 akiwemo Nelson Chamisa wa chama kikuu cha upinzani cha Citizens Coalition for Challenge (CCC).
Mgombea urais anahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kutangazwa mshindi.
Ikiwa hakuna mshindi wa moja kwa moja duru ya pili itafanyika.
Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kufariki dunia kwa Robert Mugabe ambaye alitawala siasa za Zimbabwe kwa miongo mingi. (BBC)

22/08/2023

CHEYO: UCHAGUZI WETU TANGU VYAMA VINGI NI MNADA. ANAYETOA FEDHA KUBWA NDIO MSHINDI
-
Mwazilishi wa TCD na Mwanasiasa Mkongwe, John Cheyo amesema tatizo moja kubwa lililopo katika Mfumo wa Vyama vingi na katika jambo la Demokrasia ni fedha. Amesisitiza kuwa Fedha sasa ni adui yetu namba moja Tanzania
-
Ameongeza "Labda na mimi nijilaumu kidogo, nilisema nikiwa Rais nitawajaza mapesa kibao. Ila sio kuwa na nia ya kuwajaza mapesa ili mapesa hayo yatumike kununua vyeo. Uchaguzi wetu tangu Vyama vingi ni mnada"
-
Amesema leo k**a mtu huna pesa usijaribu kuwa Mbunge wala kugombea Uwenyekiti wa Kitongoji kwani watu wanahonga hadi Ng'ombe

Influential Muslim religious leader Yusuf al-Qaradawi dies 26/09/2022

Influential Muslim religious leader Yusuf al-Qaradawi dies Qatar-based Egyptian scholar Qaradawi, who was in his nineties, was well-known across the Muslim world.

18/09/2022

KUNA WATOTO WA AINA MBILI AMBAO BAADAE HUFANYA MAMBO MAKUBWA DUNIANI:

(1) Waliopata malezi mazuri toka kwa wazazi wao AMBAO waliwekeza elimu kubwa kwao na wakalelewa katika maadili na elimu ya kiMungu. Na mara nyingi wazazi wao huishi miaka mingi ili waje Kula matunda ya watoto wao....na hufanikiwa kuwaona hadi wajukuu pengine na vitukuu kabisa.

(2) Watoto wa baba aliyetelekeza familia.....Mara nyingi hawa walilelewa na mama.

Sijui k**a kina baba wa tabia hii wanaelewa hii?
Kwamba unapomkataa mtoto au mimba ya mtoto wako au kumtelekeza na mamae hauwakomoi Ila unajimaliza wewe.....siku zote Mungu ni baba wa wasio na baba duniani (Baba wa yatima) ukitelekeza mtoto/watoto na uko hai, inahesabika umekufa....

Mungu anasearch jina lako na anachomoa mafanikio ya ndoto yako aliyokuwa amekuandikia anampa mwanao na mama yake,na wewe utaishia kupata hela ya mboga Tu...Na yenyewe pia utaitafuta Kwa tochi.

Wanaume wengi wako kila mahali wakitafuta kuombewa wapate kazi Ila watumishi hawawaambii ukweli huu.....wanatakiwa wakazitafute watoto wao wa huko nje hata k**a sasa hivi Wana familia mpya.

Kabla mtu sijaanza kumwombea habari za kupata kazi au biashara zinapoyumba, namwuliza kwanza habari za familia yake anawajibikaje?

Kawasababu kuitwa baba sio jinsia, Baba ni majukumu....ikiwa baba hakuwajibika Kwa lolote Kwa mtoto akiwa mdogo, na huyo mtoto akakua na kulelewa Kwa namna ingine,na sasa hivi baba anakijionyesha hadharani k**a ndiye Baba wa mtoto, huyo si Baba Ila ni mwanaume k**a wanaume wengine Tu na ukimkataa Hakuna laana yoyote.

Watu wengi hawafanyi research,nakuruhusu kafanye utafiti Leo....watoto wa nje waliotelekezwa na kufichwafichwa na wakakua....huwanyeshea mvua ya vipaji,anawapa talents zenye ujazo mkubwa za kuwasaidia kuishi huku duniani maana Mungu ndiye baba wa walioachwa......sasa ili awatunze walioachwa hawapi hela kuzidondosha toka juu, ball huwatunuku vipaji hata k**a hawajaokoka ili kutimiza neno Hilo;

“maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” Mathayo 5:45

Nasema hivi;
HAKUNA MWENYE MAISHA MAZURI NA MAREFU YA MTU ALIYETELEKEZA FAMILIA YAKE...NA HATA AKIISHI MIAKA MINGI HUWA NI YA TABU SANA! Wengi wanaishia kufukiwa na vifusi huko machimboni, ukiwafuatilia Sana umakuta wameacha familia zao zaidi ya miaka 15-20 na wamejipatia vimada huko huko.

Na kuna walokole baadhi AMBAO kabla hawajaokoka walizaazaa hovyo huko nje, akishaokoka eti "aaah Kwanza niliwapata kwenye uzinzi Tu saivi nakomaa na familia yangu ya ndoa tu"
Nakwambia utaishia kunena Kwa lugha Tu na maandiko yako...Ila kufanikiwa kimaisha sahau.

Mbali na kwamba macho ya Bwana Mungu yako duniani kuwaelekea wamchao, lakini pia jicho la Mungu liko kuwatafuta walioachwa,

Waliotelekezwa,

Waliokataliwa,

Waliotengwa,

Walioitwa watoto wa haramu....

Mungu anachofanya ni kuwapa vipawa ili vitumike kuwaletea riziki.

Fuatilia watu wengi walio na vipawa duniani vilivyotukuka, utakuta waliishi na kulelewa na mama zao katika hali duni sana.

Steven Kanumba,Naseeb Abdul,Omary (Ommy), hata wanasoka wakubwa duniani walilelewa na mama zao tu.



Staa aliyewahi kuchezea vilabu vya Manchester United na timu ya taifa ya Chile, Barcelona na Arsenal aliwahi kusema baba yake aliitelekeza familia yao wakati huo yeye akiwa na umri wa miaka mitano tu na hivyo mama yake kubeba majukumu yote ya kumlea.

Amesema mambo yalikuwa magumu sana kiasi cha kushindwa hata kumudu kununua viatu vya kuchezea mpira na hivyo alikuwa akiazima tu kutoka kwa marafiki zake.

Viatu vyake vya kwanza vya mpira alipewa na meya wa Tocopila baada ya kufunga mabao manane katika mechi moja ya chini ya umri wa miaka U-14.



Ni mwanasoka aliyewahi kucheza soka lake katika kikosi cha Bayern Munich na Juventus kwa mafanikio makubwa sana, alikuzwa na mama yake, Jacqueline Pardo katika maisha ya kimasikini sana.

Baba yake Vidal, Erasmo Vidal alitengana na mkewe...kutengana na mke sio tiketi ya wewe kukimbia majukumu yako Sawa?

Maisha ya Vidal na mama yake yalikuwa magumu na Vidal akajikuta akibeba majukumu ya kuwa baba mwenye nyumba ili kumsaidia mama yake akiwa bado mdogo sana.

Mama yake alikuwa akifanya kazi ya ufagiaji. Tangu wakati huo, Vidal hakukata tamaa na kuendelea kupambana na maisha hadi kufikia sasa akiwa mchezaji mwenye pesa ya kutosha na kutoa mchango mkubwa katika maisha ya sasa ya mama yake mzazi.



Straika aliyewahi kuchezea vilabu vikubwa ulaya Ajax,Liverpool na Barcelona na Timu ya Taifa ya Uruguay hakuna ubishi ni mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa kwenye soka la dunia waliowahi kutokea na anamiliki pesa nyingi sana.

Staa huyo alikuzwa na mama yake pekee

Suarez hakukuzwa kwenye familia yenye wazazi wote wawili, baba na mama.

Wazazi wake walitengana wakati Suarez akiwa na umri wa miaka tisa na hivyo majukumu yote aliachiwa mama yake katika kumkuza hadi kufikia sasa akiwa mshambuliaji mahiri kabisa duniani aliyewahiwahi kukipiga vilabu vikubwa k**a Liverpool, Barcelona na timu ya taifa ya Uruguay.



Aliwahi kutoa huduma yake kwenye kikosi cha Olympique Lyon huko Ufaransa...Manchester United n.k

Ni mmoja kati ya wachezaji waliokuzwa kwa malezi ya mama.

Baba yake Memphis aliachana na familia yake tangu mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka minne tu.

Staa huyo aliwahi kusema hataki kuchapisha jina la ‘Depay’ kwenye jezi yake kwa sababu hayupo tayari kumtambua baba yake kwa sababu hakuwa na mchango wowote katika maisha yake.

Memphis alisema hayo ni mambo binafsi na hayahusiani na mpira, lakini huo ndio ukweli hataki kumtambua baba yake kwa sababu alimwacha tangu mdogo sana na kukuzwa na mama yake pekee.



Supastaa wa Manchester United na Ureno, Cristiano Ronaldo hakuna asiyemjua duniani.

Ni mtu ambaye anaongoza kwa kuwa na followers milioni 103 katika Twitter na Instagram ana wafuasi milioni 475 na Facebook ana wafuasi 153

Pia naye amelelewa na mama yake tu, Maria Dolores dos Santos Aveiro kwa sababu baba yake alikuwa mlevi na hakuwa na mchango wowote katika maisha yake.

Lakini miaka ya karibuni, mama yake Ronaldo aliwahi kukiri kuwa ilibaki kidogo tu atoe ujauzito uliokuwa wa Ronaldo kabla ya kubadili mawazo na kubaki na mimba hiyo hadi kuja kujifungua mwanasoka huyo bora mara tano duniani.

Ronaldo alisema baba yake alikuwa mlevi kupindukia na alikuwa akipiga pombe mboo! Ronaldo kwa sasa ni staa mkubwa kabisa duniani na kuwa msaada mkubwa kwa mama yake ambaye kwa sasa anaishi kwa raha tu.

Hao ni miongoni mwa walio wengi waliokosa malezi ya baba zao.

Mungu si k**a mwanadamu anavyotazama.....

Unaweza kuzaliwa nje ya ndoa na waislamu wakakuita mtoto haramu k**a wamwonavyo nguruwe, ila Mungu anaondoa aibu kwako na kukuchipushia talent yako na dunia ikakujua.

Usijidharau,
Ile tu kwamba Mungu ameruhusu uzaliwe duniani maana yake anao mpango na wewe....angeweza kukuua k**a alivyomuua mtoto wa Saudi Kwa Bathsheba.

Sisi watu wa kristo hatumtupi aliyezaliwa nje ya NDOA maana tunaamini iko damu ya Yesu inayoweza kumtakasa na akawa sawa na wengine walivyo.

Waislamu wanasema mtoto wa nje ya NDOA hawezi kutithi mali za babaye huku wakimshabikia Ismail kwamba ana haki ya kuwa na urithi pale kwa mtoto wa agano isaak.

Sijui k**a watu wanajua Mungu ni mwenye rehema sana?

Hajiri msichana wa kazi za ndani ya nyumba ya Abraham alipofukuzwa na Sarah mwanamke wa ndoa.....Macho ya Bwana yakamtafuta alikokuwa anateseka akiwa na kiu ya maji pamoja na mtoto....

Mwanzo 21
¹⁷ Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
¹⁸ Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
¹⁹ Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
²⁰ Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
²¹ Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

Hiyo rehemu Mungu aliyokuwa ameiachilia juu ya mtoto yule wa nje ya ndoa, ndiyo rehema anayoiachilia kwa watoto wa nje ya ndoa waliotelekezwa....Nawaombea waokokage tu maana Mungu ni wa rehema na atawapokea.

Wacha nimalize kwa kusema,
Hatuhalalishi watoto wa nje ya ndoa ila pia hatuwapuuzi. K**a wewe ni baba una mtoto nje ya ndoa....kwanza usimfiche mke, mwambie ukweli ili uwe huru kumtunza...Na k**a wewe ni mwanamke unajua mumeo ana mtoto nje, usiendeleze chuki juu yake....k**a una akili mhimize mumeo kumtunza,bajeti ya mshahara wake iwekwe na ya mtoto yulee.

Usimzuilie asimtunze mwanaye, k**a ukiwa hivyo huyo mtoto atakuja kuwa nyotq kuliko wanao wa ndoa.
Kuna vitu vikishatokea huwezi kuzuia visiwepo kabisa k**a mtoto/watoto.

Watoto wa nje wasitupwe, wana nguvu sana hao watu.

Siku moja daudi alisikika akitunga wimbo na akaanza kuuimba na kinanda chake....waliokuwa karibu nse walimsikia akilia huku akiimba kwa kuomba akisema;

“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.”— Zab 51:5

Daudi hakuwa mtoto wa ndoa ila nje ya....

Alikuwa akitengwa na baba yake yesse na alifanywa k**a kijana wa kuchunga mifugo tu,ingawa wayahudi hawakatai watoto ndio maana wanabarikiwa.

Wakati wa sensa mzee yesse alikuwa anapata shida sana kwa utambulisho wa daudi..Nabii samwell alimwambia yese niitie watoto wako wote hapa kuna jambo Mungu amenituma nilifanye

Akawaita watoto wa ndoa tu.....

Yule daudi alipuuzwa alionekana mtoto haramu.....
Mzee yese aliwaleta watoto wote wa ndoa mbele ya samweli kuamzia wa Kwanza hadi wa Saba.

alipomaliza kuwakagua ikiwa yupo mtoto mkusudiwa,akamwambia Hakuna mtoto aliyechaguliwa na Bwana hapa.....

“Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.”
— 1Sam 16:11

Mungu akamchagua uyo huyo apakwe mafuta ya kuongoza taifa lake pendwa Israel. Daudi alikuwa akiimba watu wanajazwa Roho alikuwa yuko talented hujaona!

Kwa kusema haya,haimaanishi watoto waliotokana na uzinzi wako salama kabisa kiroho, na si kila mtoto hufanikiwa....kuna Mambo ya kufanya ili wapokee ukombozi na kutengwa na roho za zinaa zinazoweza kufuatilia vizazi vyake.

K**a umedaka points achia comment yako

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Dar Es Salaam
Other Public Figures in Dar es Salaam (show all)
Akhenaton Family Akhenaton Family
P. O. Box, KGN, Dsm
Dar Es Salaam, 36402

...the new breed!

MUSTAFA HASSANALI MUSTAFA HASSANALI
Dar Es Salaam

Pan African Designer, Mustafa Hassanali has showcased in 33 cities in 23 Countries & named One of Af

Ramsey's official tz Othman Ramsey's official tz Othman
Kauli Moja 1 Camp
Dar Es Salaam, 0000

Blog

ipende_ngozi_yako ipende_ngozi_yako
Dar Es Salaam

Tunauza vipodozi asili za ngozi na nywele

Michael Clement Michael Clement
Dar Es Salaam

#never give up never surrender

CayteAkaro Talents Owner CayteAkaro Talents Owner
Ilala
Dar Es Salaam, 0000

Her Own🎂 31.12. LL.B Jurist ⚖️👩‍⚖️🇹🇿 #HairBraiding #Massage #HennaTattoos #ApplicationForVisa #InNungwi-Zanzibar #GoodPrice

Sady King Sady King
Dar Es Salaam

Dee Ommy Dee Ommy
Dar Es Salaam

Dee ommy

Mo Dewiji Mo Dewiji
Posta
Dar Es Salaam, 255

Oficial Man Plate Oficial Man Plate
Dar Es Salaam

Emerging entrepreneur from Tabora Tanzania @Power brand Shop ||Chief Executive Officer (CEO) .

Fatty_the_killer Fatty_the_killer
Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

mtu anaekupenda kwa dhati lazima akuhurumie maana mapenzi ya dhati na HURUMA huishi pamoja

Pst Brian Mwimba Pst Brian Mwimba
Dar Es Salaam, 828282