SP Mwaveyah
Nafikiri ni uamuzi mzuri kwa mtu wa kawaida kutokuwa wa kawaida-Elon Musk
Siri moja kubwa ya kufanikisha Jambo lolote ni lazima ujue kuwa wewe ni shujaa vinginevyo hutafika popote.
Huwezi kupigana vita K**a wewe mwenyewe hujui K**a una uwezo wa kupigana vita.
Kitabu cha safari ya shujaa kinaelezea uhalisia wa maisha jinsi gani shujaa alivyo na jinsi ya kukabili hatari zilizo mbele ili kupata ushindi.
Jina la Kitabu :Safari ya Shujaa
Mwandishi:Yona Jeremiah (Jeremiah Jr)
Bei halisi ya kitabu hiki ,ni Tsh 10,000 na Gharama ya ofa ni 4,999/= TU zaidi ya 50% punguzo
Gharama ya jumla ni Tsh 3,000 TU
Wekeza Tsh 4,999 tu ujipatie maarifa adimu ya kukabili chochote
Mawasiliano:
0759 76 47 98-Dar es salaam
0765 86 26 61-Morogoro
Popote ulipo kinakufikia
Your friends Your Life
Friends: Things you read,watch,think,decide, choose,hear and people you associate with.
Friends can put you in cages or freedom
Friends can kill your visions or make them happen
The best friend of your life is you,make sure you invest more in you not in things
You are the sum of all choices you have made in past, Your next life will be determined by the choices you are making right now
No one is going to make choices for you, you have brains,eyes,ears as tools
Most and best choice of all, Make GOD the number one choice, God is a living assurance of your life.
He knows the beginning and the end (Alfa and Omega), You're in the middle.
He gave you the power of will, make proper decision to make Him the first Choice. He is the SOURCE of ALL you need
Sp Mwaveyah
0759-764 798
Dar es saalam
Ukiweza kuwa mwadilifu basi ujue umewin maisha
Uadilifu kwa lugha ya kigeni ni INTEGRITY yani unachokisema ndio unachofanya na unachofanya ndio ulichokisema.
Ndani ya neno integrity kuna ethics(maadili), credibility(Uaminifu) na character (wasifu/tabia). Kuwa mwadilifu ni zaidi ya kuwa mkweli na muwazi.
Uadilifu ni kuwa mtu mmoja sio ndumi la kuwili, uadilifu ni zana kubwa ya mafanikio.
Unapopoteza uadilifu unajipoteza mwenyewe na watu wataanza kukudharau.
K**a unachosema wewe hukifanyi ujue uko nje ya uadilifu na ni mwigizaji tu. Hakuna faida kubwa K**a kufundisha kitu unachokifanya kuna nguvu kubwa sana.
Mara nyingi ninapojaribu kuwaelekeza wengine najitahidi niwe nami nafanya hicho kitu maana hata nguvu ya kukisema huwa kubwa.
Uadilifu sio kitu rahisi sana Ila kina thamani kubwa sana. Uadilifu haupatikani kwa kila mtu hivyo ni vema kuangalia hata watu wa kuwaamini.
Tupo kwenye kipindi cha uchaguzi na vyama vingi vinahitaji wagombea waadilifu ili kuja kujenga Taifa.
Bahati mbaya iliyopo ni kuwa wengi wanaosema ni waadilifu ni wanafiki na waongo wakubwa. Mtu anakuambia mkinichagua nichimba visima halafu akipata tu haonekani, huyu sio mwadilifu.
Mtu anakuja kwa upole kuomba kura,msaada,mkopo lakini wakati wa kurejesha alichosema haonekani. Wajumbe na wananchi wanaachwa kwenye mataa tu.
Hali hii imepelekea Taifa kuwa na wababaishaji wengi kupita maelezo. Ndio maana vijana wamebaki kupiga propaganda tu za hapa na pale.
Uadilifu ni CASH k**a ukiudumisha unaweza kukubeba hata sehemu uliyofikiri hutaweza kupita.
Madhara ya kupoteza uadilifu ni kukataliwa,kupoteza Undugu,urafiki, partnership.
Yupo jamaa mmoja kapoteza mamilioni ya pesa kwa sababu ya marafiki aliowaamini lakini wao hawakuwa waaminifu. Pamoja yote bado ametukanwa na kudhalilishwa hawa ndio binadamu.
Bado jamaa akajitahidi kutengeneza mazingira ya kuwasaidia vijana wenzake kibiashara kawafungulia kampuni ikawa inaingiza zaidi ya MILIONI 10+ lakini yeye hagusi hata senti Ila alichovuna bado ni matusi na dharau.
Hii ndio dunia tunayoishi hasa hapa Tz, mtu alijaribu kusaidia wengine anakuwa adui, wale watu wa karibu,marafiki wanaingiza chokochoko.
Nilisoma stori moja et motivation speaker anafundisha wenzake anawatia hamasa kuwa alianza na manyoya ya kuku na Sasa ana miliki kuku elfu moja plus.
Hii ndio jamii tuliyonayo, mimi sipigi vita motivation speaker Ila wengi ni wasanii tu, hawaishi wanachofundisha na wanafundisha wasichokijua uhalisia wake katika vitendo.
Wengi maisha ni ya kuigiza sana. Huwezi kuandika kitabu cha jinsi ya kuwa milionea halafu kujimudu tu mwenyewe ni tabu, kwa nini usiwe milionea kwanza ndio uje uhamasishe wengine.
Tasnia ya HAMASA inaheshima yake na ni kubwa sana kwa wenzetu, Ila kuna raia wanaiharibu sana hasa hapa Tanzania. Yani ukitaka ugombane na watu waambie wewe ni motivation speaker utaelewa shughuli yake.
Mimi nimejitoa muhanga kuhakikisha nakuwa mtendaji kwanza ili nije niwahamasishe wengine kwa vitendo. Mafanikio yangu ndio yatakuwa utambulisho na hamasa kwa wengine, full stop nothing more nothing less
Sipendi sana kuwa mnafiki, nafurahi na kupata nguvu pale ninapofundisha ninachofanya. Ukifanikiwa watu watakupa majina wenyewe, Sasa unakuta mtu unahangaika majina mengi utendaji ni ubabaishaji.
Mwl. Spmwaveyah, Motivation Doer
0759764798
🛑 K**A NAKUFA NIFE, K**A NABAKI HAI NIBAKI HAI ILA SIWEZI KUKAA HAPA
Huu ni mtazamo wa watu wote unaowafahamu wamefanikiwa bila kujali upande waliopo aidha wa giza au nuru. Mtazamo huu ndio walioutumia wale wakoma wakati wa nabii Elisha
Ni mtazamo wa kufa na kupona(do or die). Huwezi fanikisha jambo lolote k**a hujafikia hatua ya kuwa na mtazamo huo. Ni hatari kubwa sana kuwa na mtazamo k**a huu Ila ni hatari maradufu kukosa huu mtazamo
Mtazamo wa aina hii unavuruga vitu vingi sana,ndugu,marafiki hata familia. Hivyo ukiambatana na mtazamo huu lazima uwe tayari kulipa gharama hizo.
Ni masikini pekee ndio wasioweza kuwa na akili ya mtazamo huu. Masikini ni waoga, hawataki kukosana na mtu au vitu hawako tayari kulipa gharama.
Umasikini ni mtazamo katika akili ya mtu(mindset). Utajiri mtazamo katika akili ya mtu(mindset) umasikini ni kushindwa kutumia akili katika kuunganisha vilivyopo ili kupata unavyovitaka.
Mungu hajawahi kuumba tajiri na masikini ila watu ndio wanachagua wenyewe kuwa katika kundi lipi.
Mishipa ya utajiri kwa masikini haina lishe ya kutosha ndio maana hawawezi kupambana kutoka vifungo vya umasikini. Nimeeeleza kuwa umasikini au utajiri sio vitu ni mtazamo katika akili Yako.
Tajiri anaweza kuanzisha biashara hata 10 zote zikafeli lakini hawezi kukata tamaa lakini masikini hilo zoezi haliwezi maana ni dhaifu katika Mishipa ya kujaribu jambo.
Mtazamo wa kufa na kupona sio kazi rahisi, lazima uwe umejikana kweli kweli vinginevyo haiwezekani.
Kufa na kupona ni kujitoa kafara kwa ajili ya jambo fulani inaweza kuwa biashara,huduma n.k K**a hauko tayari kutoa chochote kwa ajili ya kile unachokitaka ujue umejitoa tayari kwenye safari ya mafanikio. Lazima utoe kitu asikudanganye mtu, ukitaka watu wakusapoti anza kwanza kujisapoti, ni kweli wazo lako ni zuri lakini je wewe umefanya nini kinachowashawishi watu wengine watoe kwenye kitu chako??? K**a wewe mwenyewe hujiamini kujitoa unafikiri nani atajitoa kwa ajili yako???
Yupo mama mmoja ni tajiri sana nchini Uganda anafahamika k**a mama cheers kutokana na umaarufu wake wa juice inaitwa *cheers*. Huyu mama anahistoria ngumu sana. Alikusanya mtaji wake kwa miaka 7 ili aanze biashara lakini cha kushangaza boyfriend wake alitokomea na pesa zote lakini huyu mama hakukata tamaa aliuza nguo zote alizokuwa nazo akabaki na nguo moja yani kauka ni kuvae wanasemaga hivyo waswahili😎
Alinunua mkokoteni na kuanza Kuuza matunda na juisi mtaani, katika kuvumilia alianza kupata umaarufu wa juisi yake na hatimae akaitwa kupeleka juisi yake kwa mkemia mkuu nchini kwao ili kuipima na kuipa kibali rasmi. Juisi hiyo baada ya kibali ilipata umaarufu mara dufu na kuvuka mipaka ya kimataifa. Hadi sasa amefanikiwa sana kuanzisha biashara zingine kubwa. Kampuni yake inaitwa *DELIGHT*
Kufa na kupona ndio siri pekee ya kufanikiwa haipo nyingine. K**a umeamua kufanya kitu fulani hakikisha unajitoa 100% usijihurumie.
Ukiwa na mtazamo huu hutakuwa na hofu tena ya kupoteza au kushindwa. Biashara ikifeli sio wewe umefeli ni biashara.... Unaweza kuanzisha nyingine itakayofanikiwa. Hakuna mtu anaweza kufeli mpaka aweke saini kwenye akili yake kuwa nimesarenda. Jiulize mtu anafeli mtihani wa kwanza,pili,tatu lakini wa 4 anafaulu. Je hapa tuseme mtu alikuwa anafeli au ni msomo yenyenywe yalikataa tu. Chochote unachopitia ambacho hujapata ulivyotarajia ni dalili kuwa unahitaji kufanya marekebisho na sio kukata tamaa.....endelea mpaka upate.
Zifuatazo ni zana zinazoweza kukusaidia kuwa na mtazamo chanya wa kufa au kupona.
1. Lisha akili yako kwa Maarifa ya kutosha,vitabu,semina n.k Maarifa ni chakula kikuu cha imani
2. Chukua hatua kwa uliyojifunza bila kuchoka. Matendo ni gurudumu hai la imani
3. Rudia namba 1&2
Marudio ndio kishikizi cha yote uyatendayo
Mwl. Spmwaveyah,Doer Entrepreneur
0759764798-Dar es salaam
Ukikaa na wapumbavu 9 wewe unakuwa mpumbavu wa 10.
Ukikaa na wenye akili 9 wewe unakuwa mwenye akili wa 10.
Siku zote kumbuka wewe ni jumla ya watu wote wanaokuzunguka.
Ukizungukwa na wajasiriamali lazima uwe Mjasiriamali lasivyo ujitoe kwenye mzunguko kwa sababu asilimia kubwa watakuwa wanaongelea biashara.
Ukiona umezungukwa na watu ambao hawajadili kuhusu malengo/maono makubwa,biashara,hatma zao, maendeleo n.k Basi nakushauri ondoka haraka sana hapo maana umasikini utakupata kwa kasi ya 7G
Ukiona kila siku unaona huna mtaji ujue wewe ni mpumbavu mkubwa sana na mbabaishaji unahitaji maombi ya kukufungua akili yako.
Ukiona unasema huna mtaji ujue huna sifa za kupata mtaji. Mtaji unakawaida ya kufuata thamani.
Ukiona huwezi kuanza na ulichonacho ili uanzishe biashara ujue wewe ni MBABAISHAJI. Unatakaje watu wengine waamini unachotaka kufanya wakati wewe mwenyewe umeshindwa kutoa cha kwako ili uanze biashara yako.
K**a huwezi Kukubali kuumia leo ili uitengeneze kesho yako basi endelea kulala usingizi.
Maisha yanachapa sana ukiwa mzubevu utaona K**a kila mtu hakupendi na hataki kukusaidia.
Jim Rohn aliwahi sema "If you don't learn no one can help you,if you're determined to learn no one can stop you" Yani K**a hujifunzi hakuna atakayekusaidia,K**a uko tayari kujifunza hakuna anayeweza kukuzuia.
Kujifunza na kutafuta taarifa ndio mtaji wa kwanza, hata uwe na bilioni 100 K**a huwezi kujua utafanyaje biashara yako pesa zote zitapokea.
Hatuanzi biashara kwa kutafuta pesa Bali kwa kutafuta taarifa za masoko kwanza.
Spmwaveyah,Doer Entrepreneur
0759764798-Dar es saalam
🛑 WOGA NA KUTOAMINI NI DHAMBI K**A DHAMBI ZINGINE TU(Ufunuo 21:8)
Mtu wa kwanza kulima nyanya alipelekwa mahak**ani, jina lake ni ROBERT JOHNSON(1820) wa huko New Jersey Marekani (US)
Sababu kubwa ni kuwa nyanya haikuwa inatambulika k**a chakula.
Wengi walijua ni tunda la Shetani lenye sumu.
Jamaa aliyepelekwa mahak**ani alichukua kapu la nyanya nakuanza kula ili aanze kufa yeye kwanza.
Watu wengi walizunguka mahak**ani kushuhudia jamaa atakavyokufa.
Jamaa hakufa na hapo ndipo nyanya zikaanza kulimwa huko MAREKANI miaka ya 1820
Ukitaka kufanikiwa jambo lolote lazima uwe na tabia ya kuthubutu,kujaribu,kufanya. Usiangalie nani hajafanya cha msingi wewe Fanya tu kikubwa unajua kabisa ni chema.
Woga ni kitu hatari sana, ndio maana biblia inasema waoga hawataingia *MBINGUNI* Yani woga ni dhambi k**a dhambi zingine.
Biblia imekataza sana woga, acha woga ingia mazima. Fanya kitu, acha kudimba.(Kufanya mambo kitotototo).... biblia kwangu ndio kitabu cha kwanza ninachokiamini kuliko vyote hivyo using'ae macho kuona nimekitumia sana.
Ukiwa unaomba omba kwelikweli usiogope mtu, Ukiona umeanza kunena kwa lugha usiogope nena sana. K**a unawashwa kuandika k**a Mimi andika sana maana hii ndio nafasi ya uhakika uliyopata.
Usiogope kukosea maana ili ujue k**a unajua au hujui ni lazima ujaribu kufanya. K**a ni kuimba ndugu yangu imba sana. K**a ni kukaripia karipia sana, usiogope mtu,K**a Kuhubiri hubiri sana.
K**a ni kufanya biashara Fanya kwelikweli usiogope mtu.
Waoga hawataenda mbinguni. Acha woga aise....unafikiri Thomas Edison ilikuwaje???...jamaa alijitokeza akawaambia watu kuwa yeye anataka kutengeneza bulb ya umeme.
Kweli jamaa hakuogopa alijaribu mara 10,000 mara ya 10001 jamaa kafaulu ndio taa ya umeme unayoiona hiyo.
Ni kweli kila mtu ana mdomo na kuongea ni rahisi kuliko vitendo Ila ujue kabisa kuongea ni hatua ya kwanza ya uumbaji. Mithali 18:21
Usiogope kusema unachotaka kufanya Mungu alikuwa anajua kabisa Yesu atazaliwa na ametangaza sana kupitia manabii K**a Isaya licha ya kuwa alijua kuwa Herode atasababisha maafa ili amue Yesu.
Usiache kusema, kusema ni Hatua ya kwanza kabisa ya uumbaji Kisha unafanya au hujaona Mungu alivyokuwa anafanya.
Soma Mwanzo utaona maneno haya *akasema tumfanye mtu, akasema akafanya* Mwanzo 1:3 Mungu akasema iwe nuru ikawa nuru.... Kwa hiyo usiogope kusema..... Ni kweli maadui wapo na hila zipo Ila hawawezi kuzuia lililosemwa, vikwazo ni sehemu ya mafanikio usiogope et mbona Yusufu walimfanyizia ndugu zake, ishu iko pale pale u
Ilitakiwa aseme tu ili ndoto itimie, ....
Angalia kitabu cha Habakuki 2:1-3 anavyosema(.......Iandike njozi ukaifanye wazi sana katika VIBAO ili aisomaye apate kuisoma K**a maji. Maana njozi hii ni kwa wakati ulioamriwa inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake wala haitasema uongo,ijapokawia ingojee kwa kuwa haina budi kuja HAITAKAWIA. .......Acha woga acha woga
Kwenye kufanya mambo mapya utapoteza vitu vingi wakiwemo hata ndugu,marafiki n.k wote hao wasikuzuie ndugu, maisha ni yako peke yako utahojiwa peke yako ulifanya nini duniani.
_WATU WOTE WALIOFANIKIWA DUNIANI NDIO WALIOWAHI KUSHINDWA MARA NYINGI KULIKO MTU YEYOTE YULE_
Acha kujifanya mstaarabu et hutaki kuonekana unakosea, hakuna ustarabu kwenye mambo ya msingi.
Hivi unafikiri Mungu alikuwa chizi anapotumia damu za ndama wakati alikuwa anajua kabisa yupo Yesu atakuja kufa kwa ajili ya wanadamu???.si angeweza kusubiria....Sasa kwa nini alianza na vitu dhaifu??...wewe ndama wako ni yupi wa kuanza nae?? Au hujasoma pale anasema _mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia_ Ufunuo 13:8... Tokea hapo damu ya YESU ndio imekuwa funga kazi hakuna mbadala tena, Usiache kujaribu hadi upate suluhisho la kudumu.
Kwani wewe unapata somo gani hapo??? Inamaana huoni kuwa unafundishwa kuanza hata k**a hujafikia kule unakotaka,?? Cha msingi anza ukiwa unaona picha kubwa ya mbele.
Mungu alikuwa na uwezo wa kusubiri tu. Lakini alijaribu damu za mafahali zinasafisha dhambi kwa mwaka tu kisha inarudiwa tena.
Usiache kujaribu kisa unaogopa watu. Njia sahihi zipo mbele lakini huwezi kuzipata k**a hujaanza kufanya ndugu.
Damu ya Yesu imekuja kufanya Kazi baada ya Mungu kutumia mibadala mingi sana. Wewe ni nani unataka ukifanya mara moja tu ufanikiwe.
Yesu mwenyewe alianguka sana na msalaba kabla hajafika goligotha licha ya kuwa msalaba ulikuwa mzito.
Mungu alikuwa anatuonyesha kuwa katika safari ya maisha ili ufanikiwe lazima ujaribu sana na kushika lililo jema au hujaona hili andiko??? *_JARIBUNI MAMBO YOTE LISHIKENI LILILOJEMA_* 1Wathesalonike 5:21
Acha woga acha woga wewe, acha woga acha woga ndugu, maisha yanachapa sana, ukiendelea kuwa mwoga maisha yatakunyosha hadi uiteke abee.😎
Usiogope kufanya eti kwa sababu huoni matokeo sasa, kumbuka mianzi ya kichina inachukua miaka mitano(5) kuota toka ipandwe yaani unapanda Leo na kila siku unamwagilia maji,unapalilia kitu usichokiona, mwaka wa 5 wote unamwagilia tu .....sio rahisi lakini ndio iko hivyo. Wiki ya tano ya mwaka wa 5 mianzi hii huota kwa kasi ya ajabu sana na kuwa mirefu sana futi 90+
Kuna watu unaona wanafanya biashara lakini hawaonyeshi matokeo, sikia iko siku ghafla tu mambo yatajibu usifikiri itakuwa ni bahati....hapana ndugu ni imani yenye matendo tu bila kukoma.... _Imani ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo bayana ya mambo yasiyoonekana.
Au hujifunzi kutoka kwa ELON MUSK , kati ya watu ninaowakubali kwenye kujihatarisha ni huyu jamaa. Ni zaidi ya risk taker lakini Sasa hivi ni top 10 ya mabilionea duniani Yani jamaa kaibuka ghafla tu lakini alianza mbali Huyu jamaa walimuuliza kwa nini hakati tamaa baada ya kupoteza pesa nyingi kwenye mradi wa kampuni yake ya SPACE X aliwajibu kuwa hajui maana ya kukata tamaa ndio maana huwa anaendelea kufanya anayoamini. Kwa Sasa kampuni zake zinafanya vizuri sana mfano TESLA(Magari ya umeme), SOLAR CITY(Umeme wa jua) NA SPACE X(Mambo ya anga)
Hata k**a huoni matokeo fanya ndugu, usiangalie watu watakuonaje, hawakulishi hao, hawajui changamoto unazopitia. Wewe ndio unajua ukweli wote hivyo pambana hadi tone la mwisho.
Kuna huyu bilionea wajuzi hapa bwana Laizer watu wanafikiri ni bahati .....hahaaaa sio kweli huyu mzee kachoma sana pesa halafu sio mchimbaji mdogo k**a raia wanavyotafsiri huyu mzee kila siku alikuwa anachoma pesa tsh. *LAKI 6* kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji madini. Amefanya kwa miaka 17+ ....unaona eeeh??? Sio bahati hiyo
Bahati ni pale Fursa inapokutana na maandalizi. Hivyo usikae tu kujifurahisha eti siku moja utalala na kuamka tajiri. Sahau kabisa sahau ndugu acha ujinga fanya Kazi. Kutegemea miujiza ni k**a kucheza k**ari(betting).
Maisha yanachapa sana, Fanya bidiii vinginevyo utapata umasikini wa kukutosha.
Kuna mtu Leo nilikuwa naongea nae. Sasa kuna shughuli nazifanya za kilimo nikawa namuuliza tathmini ikoje. Tukaaongea mengi sana baadae akanitolea ushuhuda kuwa kuna mtu kapata miloni miamoja plus, kupitia kilimo cha vitunguu huko Mbeya kila gunia alikuwa anauza tsh. LAKI TATU NA NUSU. Sasa sikia iko hivi huyu mtu kwa miaka mitatu mfululizo alikuwa akilima vitunguu kwa hasara sana ila anasema hakushawishika kukata tamaa alijua ipo siku atapata.
Katika hizi milioni 100+ plus alizopata yeye alijua atapata milioni 30 tu. Lakini Mungu si athumani maandalizi yanekutana na Fursa katoboa tayari. Miaka mitatu tu ya uvumilivu ameshatoboa(hii ni kanuni ya uvumilivu) lakini kuna mtu yupo kwenye ajira miaka 20 anavumilia kimshahara cha laki 5 huku ni kufungwa aise......tuzinduke.
Nikiwa chuo nilisoma sehemu moja hivi ilikuwa inaelezea kuhusu ajira na mishahara(Kitabu cha Rich Dad Poor Dad,Four Quadrants na Why *A* students work for *C* students and *B* for government---Roberty Kiyosaki).Alisema mara nyingi mshahara ni asilimia 10 au 20 ya kile unachozalisha.
Kwa mfano ukilipwa milioni 1 maana yake wewe unazalisha milioni 10 kwa mwezi hivyo boss anakula milioni 9 wewe moja tu. ...... HUU NI UNYONYAJI tokea hapa akili yangu ilivurugwa hadi leo sijafikiria kuajiriwa nilianza kujifunza biashara,kusoma vitabu vya biashara, kuhudhuria semina za biashara,kusikiliza vipindi vinavyohusu biashara na ujasiriamali hadi leo ndio tabia yangu....mimi ukinipitisha sehemu wanakouza vitabu unaweza kuta nabaki mtupu K**a pesa ipo maana ndio ulevi wangu.
Hata hivyo kusoma soma vitabu ni tabia ya muda mrefu toka nikiwa shule ya msingi nilikuwa nanunua vitabu vya shuleni hata kwa pesa zangu.....ndio nilikuwa navijibiashara fulani hivi na kufuga kuku.
Mimi nilishawaambia kuwa nitakuwa bilionea baada ya miaka 10 hivyo wekeni kumbukumbu. Nitakuwa mtu wa kwanza kwenye familia k**a sio ukoo mzima au kijijini kwetu. Nafanya k**a Thomas Edison au k**a Yesu ilivyokuwa akiwambia wayahudi na wanafunzi wake kuwa atakufa na siku ya 3 atafufuka. Mimi naamini kabisa lazima niwe bilionea....kwa sababu maisha yangu ninayoishi ni ziada tu ningekuwa nimeshakufa sasa k**a niliponea chupuchupu lazima nifanye jambo, kuna sababu ya mimi kuwa hai mpaka Leo najua kabisa lazima niwe mkubwa k**a Mungu alivyoahidi. Najua kabisa naweza(Wafilipi 4:13).
Mwalimu wangu(sio wa shuleni, wa mtaani) aliwahi kuniambia kuwa siku zote ukiwa na mawazo ya elfu moja moja hata ukiambiwa mshahara elfu tisini utaona inakutosha. Siku zote huwezi kupata zaidi ya pale unapowaza. Mithali 23:7 _aonavyo mtu nafsini ndivyo alivyo.
Mawazo yako yananguvu kubwa sana ya kuamua utakuwa nani maishani.
Usitgemee kuwa milionea,bilionea k**a wanaokuzunguka hata mawazo ya kulima karoti tu hayapo. Watu wanaokuzunguka,vitabu unavyosoma,video unazotazama,kurasa unazofatilia mtandaoni fb, Instagram,semina unazohudhuria zina madhara makubwa sana kwenye maisha yako.
Amini usiamini unachokitamka kinatokea kwenye maisha. Siku moja mtu mmoja aliniambia nitakuwa masikini nilimkatalia kata kata nikamjibu siku moja wewe ndio utakuja kununua ndala dukani kwangu, Leo hii ilishatimia kitambo sana duka lipo na raia wanashangaa tu imekuwaje.
Unachokisema kina matokeo makubwa sana. Maneno ya watu yananguvu k**a ukiyaruhusu yaingie moyoni mwako.
Hata watu milioni waseme huwezi lakini wewe ukikataa hayawezi kukudhuru,lakini k**a wewe mwenyewe umesema huwezi hata watu bilioni waseme unaweza hutaweza.
Jamaa mmoja aliwahi kuniambia kuwa kwa kuwa nimechagua kusoma sayansi basi kila siku niwe nakunywa maziwa fresh ili nifaulu, sikukubaliana na vitisho vyake. Nilisoma sayansi na nikafaulu licha ya kuwa ni shule changa tena kayumba(sisi tulikuwa ndio awamu ya 3 kumaliza form four). Yule jamaa yeye alithibitisha kuwa dunia ni duara🌍(alikula bonge moja la ZERO).
Usikubali maneno na maoni ya watu kukuambia kuwa huwezi. Pambana uwathibitishie kuwa wewe sio wao.
Mimi sijaandika haya kujisifu ila nakupa picha tu ujue kuwa inawezekana kufanya maajabu ukiamua hakuna wa kukuzuia.
Jim Rohn alisema K**a hujifunzi vitu vipya hakuna atakae kusaidia Ila ukijitambua na kujifunza na kufanyia kazi uliyojifunza hakuna wa kukuzuia.
Sisi ni uzao wa kifalme. Shauku yangu ni kuona tunakuwa na mawazo makubwa na kuleta mapinduzi ulimwenguni.
Mentor wangu wa muda wote YESU alisema kuwa siombi kuwa uwatoe katika ulimwengu Bali uwalinde na yule mwovu(Yohana 17:15). Mimi Mungu wangu ni tajiri hivyo lazima kabla sijaondoka duniani lazima niwe tajiri Kumbukumbu 8:18....Maana kila mtu anachagua mwenyewe Kumbukumbu 30:19,11:26
Utajiri na heshima, naam utajiri udumuo upo kwangu Mithali 8:17,Hagai 2:8
YOTE YAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE MARKO 9:23
Mwl.Spmwaveyah, Doer Entrepreneur
0759764798
Dar es saalam
🛑 MAFANIKIO SIO AJALI WALA BAHATI. MAFANIKIO YANAONGOZWA NA KANUNI
Maana ya mafanikio inategemea na jinsi mtu anavyoielezea au kuitafsiri.
Wengine maana ya mafanikio ni kuwa na pesa,wengine kuwa na familia bora,wengine kuwa na Mali nyingi, wengine kuwa maarufu sana,wengine kuwa na Nguvu za Mungu maradufu, n.k
Sasa iko hivi haijalishi wewe unaelezeaje au unatafsiri vipi maana ya mafanikio ila ujue kuwa kuna kanuni zinazoongoza ili kufanikiwa.
Kanuni hizi haziangalii wewe ni nani au unaamini nini, ukizifuata zinakufanikisha usipofuata hutafanikiwa kwenye chochote.
1️⃣ UVUMILIVU
Mafanikio yoyote Yale yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana. Hakuna njia ya mkato ili ufanikiwe lazima ulipe gharama. K**a huelewi vizuri kamuulize yule mjane na kabaila luka 18:1. Hakuna namna ya kufanikiwa K**a huna uvumilivu. Vikwazo lazima viwepo kukupima K**a uko serious kweli au MBABAISHAJI TU.
2️⃣ SIO KILA MTU ATAFURAHIA UNACHOFANYA
Hata uwe nani k**a unasubiri kila mtu akubaliane na wewe ndio ufanye basi ujue unajidanganya. Dunia imekaa vibaya sana. Lolote unalofanya lenye kuleta matokeo chanya ujue vikwazo havizuiliki. Ukibisha kamuulize Yesu. Kamuulize Magufuli, Kamuulize Elon Mask, Kawaulize wote waliofanikiwa watakupa majibu mazuri.
3️⃣ K**A HUNA MWELEKEO UTAISHIA SEHEMU ISIYO SAHIHI
Lazima uishi kwa malengo na ujue unaelekea wapi. Usitafute mchawi kabla ya kuangalia k**a unamwelekeo unaoeleweka. Kuwa na malengo makubwa,kuwa na mikakati makini. Usipojua unaelekea wapi kila mtu atakutumia tu maana hujielewi.
4️⃣ CHUKUA MAJUKUMU YOTE KUHUSU HATMA YAKO.
Watu wote waliofanikiwa hawakuwahi kulaumu mtu, walipambana sana bila kuchoka. Huwezi kufanikiwa k**a huwajibiki,huwezi kufanikiwa k**a unalaumu serikali,familia,Kiongozi wako, n.k
5️⃣ SHUKRANI
Ili kufanikiwa huna budi kushukuru vile ulivyo na ulivyonavyo huku ukipambana kuvitafuta unavyotaka. Watu waliofanikiwa ni watu wa shukrani sana. Uhai ulionao kuna watu wanautamani Ila hawana, wewe ni mzima Ila umejaa lawama kila siku et huna mtaji, acha ukichaa aise fanya kitu.
6️⃣ KUJIFUNZA KILA SIKU NA KUFANYIA KAZI ULIYOJIFUNZA
Unapoacha kujifunza unaanza kufa. Wanaojifunza na kufanyia kazi wote lazima wafanikiwe haijalishi ni lini ila mafanikio yao huwa makubwa sana.
Ukiwa unakwepa vitabu,semina basi ujue wewe ni masikini mzuri tu.
7️⃣ KUSHINDWA NI HITAJI MUHIMU LA KUFIKIA MAFANIKIO
K**a unaogopa kushindwa basi sahau kabisa kufanikiwa. Kuendelea kusubiri kila kitu kikae sawa ni ujinga maana hakuna siku kila kitu kitakuwa sawa. Anzia hapo hapo mengine yatajipanga mbele ya safari. Watu waliofanikiwa ndio wanaongoza kwa kushindwa mara nyingi kuliko kundi lolote la watu katika jamii tunayoishi. Thomas Edison mgunduzi wa bulb ya umeme alijaribu mara ELFU KUMI kabla ya kufanikisha uvumbuzi. Mara ya 10001 bulb ikawaka
8️⃣ KUJITOA ASILIMIA 100%
Wote waliofanikiwa watu wakubwa walikuwa tayari hata kufa kwa kile wanachofanya.
K**a unafanya nusunusu bora uache tu maana unadimbadimba tu, k**a ukoserious fanya kweli acha maigizo.
9️⃣ MAMBO YA NYUMA HAYANA NGUVU KULIKO YALIYOMBELE YAKO
Kuendelea kujutia kwa nini ulikosea haikufanya kuwa sahihi kwa yaliyombele. Unachotakiwa kufanya ni kupambana kuhakikisha mwisho wako unakuwa bora zaidi.
1️⃣0️⃣ UKIAMUA KUFANYA UNAWEZA KUPATA
Hakuna linaloshindikana ukiamua. Maisha tunayoishi ni uchaguzi mtu anaofanya. Ndoto Yako inawezekana tu pale ukiwa unachukua hatua madhubuti kila siku bila kuchoka.
1️⃣1️⃣ FUATA NJIA YAKO UNAYOIAMINI.
Dunia imejaa kelele nyingi sana. Miluzi mingi ndio hupoteza mbwa. Fahamu kuwa hakuna anaejua unataka nini zaidi ya wewe mwenyewe.
1️⃣2️⃣ ISHI MAISHA YAKO HALISI
Ili kufanikiwa lazima ujue kuishi ukweli wako. Usifanye mambo ya maigizo ili kuwafurahisha watu, kila mtu anamaisha yake. Kununua vitu vya gharama ili watu wakuone ni ujinga100%😎.
Kufanikiwa sio maonyesho ni maboresho.
1️⃣3️⃣ USITAFUTE PESA ACHA ZIKUTAFUTE WEWE
Wengi hawaelewi hapa, wanatafuta pesa lakini hawajui kuwa pesa ukiitafuta inakimbia. Pesa utaratibu wake ni kuwa inafuata thamani. Jinsi ya kutengeneza thamani lazima ujue au kutambua kusudi lako na kulifanyia kazi.Wenye thamani siku zote ndio wanaotafutwa.
1️⃣4️⃣ TABIA INAJENGA AU KUBOMOA
Chochote unachofanya ni uwekezaji unafanya. Hivyo kila unachofanya kinachangia tabia yako. Tabia zako za ulaji, matumizi ya pesa,unasikiliza nini,unatazama nini vyote hivi ni uwekezaji na utavuna. Mafanikio ya kweli yanahitaji nidhamu ya hali ya juu.
1️⃣5️⃣ HAKUNA CHENYE THAMANI KISICHO NA GHARAMA
Kila unachotaka kufanikiwa lazima ujue kuna gharama za kulipia. Huwezi kuamka tu ghafla unataka muujiza wakati hujafanya chochote. lazima upambane sana. Vitu vya thamani vinahitaji bidii,vinahitaji kujitoa.
1️⃣6️⃣ MATOKEO YA MWISHO NI MUHIMU ZAIDI
Chochote unachofanya usiweke mategemeo ya papohapo angalia faida kubwa ya baadae. Endelea kufanyia kazi malengo yako. Usitishwe na wanaopata haraka maana hujui waliwekeza kwa muda gani au wametumia njia gani.
1️⃣7️⃣ UNAWEZA KUBADILI HALI YAKO YA SASA KUWA VILE UNAVYOTAKA
Hakuna wakuja kubadilisha hali yako K**a wewe hutaki,huichukii hiyo hali. Hakuna namna nyingine zaidi ya kuchukua hatua za uhakika. Wewe ndio kiongozi wa maisha yako. Mwaka au mwezi wa mafanikio yako inategemea umefanikiwa kwa kiwango gani katika siku. Kumbuka hakuna mwaka mzuri bila siku au wiki nzuri. Hivyo usifariji utabadilika mwakani anza Sasa K**a sio Sasa hivi.
1️⃣8️⃣ HUJACHELEWA KUWA YULE MTU MKUU UNAETAKA KUWA
Bado unayonafasi ya kufanya. Kunguru aliyetumwa na Nuhu hakufanya vizuri K**a alivyoagizwa. Lakini Mungu hakukata tamaa nae bado alimtuma kumpelekea mkate Elia. Acha kujiona mdogo bado nafasi ipo Usikate tamaa.
1️⃣9️⃣ HAKUNA ATAKAE KUAMINI K**A HUJIAMINI KWANZA MWENYEWE
Siku zote binadamu hupenda kufanya kazi na watu wanaaojiamini. K**a huna mpango wa kujenga tabia ya kujiamini sahau mafanikio. Utahisi wengine wanaupendeleo fulani kumbe hakuna ni wewe tu ndio unazingua.
2️⃣0️⃣ HOFU NI UONGO UNAOJIFANYA UHALISIA
Mara zote kinachokutisha huwa hakipo,ukiamua kuchukua hatua tu mambo yanaenda. Mtu wa ndani yako ananguvu kubwa. Kale kasauti kanakosema huwezi kapige teke. Wewe unaweza amini hivyo.
YOTE YAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE
Mwl. Spmwaveyah, Doer Entrepreneur
0759764798
Dar es saalam
Wewe unachagua nini?
Mimi Nashauri Chagua kupigania ndoto zako
_Chagua kutokata tamaa_
Chagua kuwa mbunifu
_Chagua kuwa na MAONO na malengo makubwa_
Chagua kuwa mfano wa kuigwa na kuzungukwa na watu wenye mtazamo chanya na akili kubwa
_Chagua kuacha mabaki(Legacy) vizazi na vizazi_
Chagua kuwa mshindi hata vikwazo viinuke kiasi gani
Chagua kuzifanyia kazi fursa ulizonazo na unazozipata kwa wakati
Chagua kutunza muda,Chagua kuwa na ratiba
_Chagua kuwa mkweli,mwaminifu na Mtakatifu_
Chagua kuwa na Imani nzito bila kusitasita
Chagua kuwajibika asilimia 100%
CHAGUA KUFUNGUA MASIKIO ZAIDI KULIKO MDOMO
Chagua kutojihurumia,chagua kuchukua hatua hata k**a mazingira yanaonyesha haiwezekani
Chagua kugusa maisha ya watu wengine
Chagua kujifunza zaidi,Chagua maarifa,soma vitabu k**a biblia,hamasa, biashara,uongozi,mauzo, n.k hudhuria semina,mikutano,Chagua kuwa mdadisi(kuuliza si ujinga)
CHAGUA KUANZA BIASHARA YAKO
Chagua kuweka akiba na kuwekeza, Chagua kuwa na vyanzo vingi vya mapato
Chagua kuheshimu na kushukuru kwa kile ulichonacho,chagua unyenyekevu
Chagua kutunza kumbukumbu katika notebook
Chagua kuwa na nidhamu(Uwezo wa kufanya jambo bila kushurutishwa au kusimamiwa na mtu yeyote),Chagua kuacha nidhamu ya woga
Chagua kutumia pesa vizuri kwa mahitaji yaliyolazima tu
_Kumbuka kuwa tunaishi mara moja tu hivyo usipoteze muda na watu wanaosema bado,siwezi,nitaanza kesho,pesa haileti furaha, wasio na malengo wala mipango,wenye manung'uniko,wabishi,wanafiki_
PATRICK, Entrepreneur
0759764798
Usighairishe malengo yako fanya namna yatimie
Usikose kukusanyika katika kumwabudu Mungu. Ebrania 10:25
🛑 If you're not willing to learn no one can help you. If you're determined to learn no one can stop you--Zig Ziglar
K**a hauko tayari kujifunza hakuna atakayekusaidia, K**a unajitambua na kujifunza hakuna anayeweza kukuzuia.
Learning= Earning
Kujifunza=Kupata(money).
Hakikisha unajifunza kila siku ili changamoto zisikuzuie
SP Mwaveyah
Entrepreneur
0759764798
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Address
0000
Opening Hours
Monday | 09:00 - 12:00 |
Tuesday | 09:00 - 12:00 |
Wednesday | 09:00 - 12:00 |
Thursday | 09:00 - 12:00 |
Friday | 09:00 - 12:00 |
Saturday | 09:00 - 12:00 |
Sunday | 09:00 - 12:00 |