JuHas food product service

JuHas food product service

You may also like

Shari
Shari

pata huduma ya vyakula lakini pia ushauri mbalimbali juu ya vyakula na mche ya matunda na elimu juu ya chakula unachokula na tiba yake katika mwili hapa juhas

15/10/2022

Kula vizuri

27/07/2022

Ishi ukweli wako. Onyesha upendo wako. Shiriki shauku yako. Chukua hatua kuelekea ndoto zako. Tembea mazungumzo yako. Ngoma na imba kwa muziki wako. Pokea baraka zako. Ifanye siku ya leo ikumbukwe.-

20/01/2022
31/07/2021

DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:

Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri haraka zaidi. Sasa usinywe zote wakati mmoja, moja tumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni. Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari.

1. UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu k**a tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula k**a vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.

2. KABEJI

Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

*Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

*Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

*Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

3. NDIZI

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.

Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

4. N**I

N**i ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. N**i huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la n**i na maji ya n**i (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la n**i au maji ya n**i kila siku. Pia unaweza kuitafuana n**i yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.

Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya n**i asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.

5. UWATU

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika k**a utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.

Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.

Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa k**a vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

6. ASALI MBICHI

Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. K**a ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho k**a ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

7. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye k**a Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 1 kwa wiki 2 au 3

8. MKAA WA KIFUU CHA N**I

Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya n**i. Chukua vifuu vya n**i vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

9. MAFUTA YA HABBAT SODA

Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

Share page yetu kwa kupata taarifa zaidi za afya.

Want your business to be the top-listed Business in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address

Ubungo
Dar Es Salaam
-KIBAMBA

Opening Hours

Monday 09:00 - 23:00
Tuesday 09:00 - 23:00
Wednesday 08:00 - 23:00
Thursday 08:00 - 23:00
Friday 08:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 23:00
Other Business Services in Dar es Salaam (show all)
Marie fashion tz Marie fashion tz
Kariakoo
Dar Es Salaam, 27255

Ally Mchana Ally Mchana
Ally
Dar Es Salaam

Mafuruka event decoration Mafuruka event decoration
Dar Es Salaam

MAFURUKA decoration events

Delivery ya mashuka na nguo  popote ulipo Delivery ya mashuka na nguo popote ulipo
Dar Es Salaam

Pata nguo bomba na mashuka ya kisasa

Taishan Technology Mabati Taishan Technology Mabati
Buguruni
Dar Es Salaam, 255

The MOGUL The MOGUL
Dar Es Salaam

suarez_outfit_store suarez_outfit_store
Dar Es Salaam

Usedphones from Dubai,UK. Brand New phones � 0785126380

Dstv Tz Dstv Tz
Dar Es Salaam

Bongo_Flavour Stories Bongo_Flavour Stories
Banana
Dar Es Salaam

Taishan Mabati Limited Tz Taishan Mabati Limited Tz
Buguruni
Dar Es Salaam, 255

Fahad Khami Fahad Khami
Dar Es Salaam

Kilimo cha kisasa1 Kilimo cha kisasa1
Victoria
Dar Es Salaam

https://chat.whatsapp.com/GVfIuP91JTs2HnXIJe1P2O