National Housing Corporation

Government organisation, Real Estate Developer NHC is under the Ministry of Lands, Housing and Settlements Development.

The current National Housing Corporation is the outcome of the decision of the Government to dissolve the Register of building (RoB) through Act of Parliament No.2 of 1990, which vested its responsibilities with the NHC. The former NHC was established by Act of Parliament No.45 of 1962, while RoB was established by Act No.13 of 1971. The Ministry is represented by the Board of Directors which is r

15/09/2024
12/09/2024

Leo Waziri wa Fedha Mhe. Mwingulu Nchemba(MB) akiambatana na viongozi wengine ametembelea banda la NHC katika viwanja vya AICC Arusha ambapo atafunga Mkutano wa 16 wa Ununuzi wa Umma wa Afrika Mashariki. Akiwa katika banda la NHC amepata maelezo juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Shirika katika sekta ya ujenzi wa nyumba hususan miradi iliyopo sokoni kwa sasa.

11/09/2024

Jengo jipya la Wizara ya mambo ya ndani ya nchi katika mji wa kisasa wa Serikali Mtumba, Dodoma. Kwa mujibu wa msimamizi wa mradi huo Mhandisi Omari Chitawala, kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 86.5 aidha kwa mujibu wa Mhandisi Chitawala, kazi zinazoendelea usiku na mchana ni ufungaji wa mifumo ya viyoyozi na viyoyozi, kioo (rangi ya buluu) unachokiona, kupaka rangi ndani, kufunga vifaa vya maliwatoni na aluminium.
Jengo hilo ni moja ya miradi 8 ya ujenzi ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imeaminiwa na Serikali kuitekeleza katika mji wa kisasa wa Mtumba, Dodoma.

Photos from National Housing Corporation's post 11/09/2024

" NHC mmeleta huduma ama bidhaa gani katika kongamano hili la 16 la ununuzi wa umma la Afrika Mashariki"? ndivyo inavyoelekea Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa (mwenye kilemba), akimuuliza Afisa Mauzo mwandamizi wa NHC Bi. Diana Mwamba, alipofka katika banda la Maonesho la NHC katika kongamano la ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki linaloendelea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Arusha.
Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa NHC wanaoshiriki katika kongamano hilo linalowakutanisha zaidi ya washiriki 1,000.

Photos from National Housing Corporation's post 11/09/2024

Baadhi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakiwa katika banda la maonesho la NHC, wakati huu jukwaa la 16 la ununuzi wa umma la Afrika Mashariki, likiendelea katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Arusha, wakiwa ni miongoni mwa washiriki.
Aidha katika banda hilo wametembelea pia viongozi mbalimbali wanaoshirika katika jukwaa hilo la siku nne linalowakutisha watu Zaidi ya 1,000, akiwemo Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa (mwenye kilemba) pangusa 👈.

Jukwaa hilo la 16 la ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki linaenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma nchini (Nest).

Photos from National Housing Corporation's post 10/09/2024

Ujumbe kutoka Tanzania ukishiriki katika Kongamano la ushirikiano wa dunia katika masuala ya miundombinu la mwaka 2024 linalofanyika katika Jiji la Seoul, Korea Kusini. Kongamano hili linahudhuriwa na Wizara zinazohusika na miundombinu ikiwemo Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo Mhe. Degratius Ndejembi ameongoza ujumbe wa Wizara ya Ardhi. Pamoja na Waziri wa Ardhi, yupo Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Hamad Abdallah.

10/09/2024

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe. Dkt. Juma Mhina, ni miongoni mwa Viongozi wanaoshiriki kongamano la Manunuzi Afrika Mashariki linalofanyika katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Pichani akisaini kitabu cha wageni katika banda la Maonesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), lililoko AICC wakati wa kongamano hilo mahususi kuelezea bidhaa ba huduma zinazotelewa na NHC.

09/09/2024

Profesa Sufian Bukurura, mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma (PPRA), ni miongoni mwa viongozi waliofika katika banda la maonesho la Shirika la nyumba la Taifa ( NHC), katika siku ya kwanza jukwaa la 16 la ununuzi wa umma la Afrika Mashariki, linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Arusha, kuanzia Agosti 9-12, 2024.

09/09/2024

KAWE - 711
Apartments Available for Sale
Call Now! +255 736 114 433


cc

Photos from National Housing Corporation's post 09/09/2024

Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mwenyekiti wa wakala wa huduma ya ununuzi serikalini (GPSA) Bi. Dorothy Mwanyika (kushoto), akiwa katika banda la maonesho la NHC, ikiwa ni siku ya ufunguzi wa jukwaa la 16 la ununuzi wa umma la Afrika Mashariki, linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Arusha.
Aidha katika banda hilo wametembelea pia viongozi mbalimbali wa NHC, wanaoshiriki katika jukwaa hilo la siku nne linalowakutisha watu Zaidi ya 1,000.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko, amemuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi wa jukwaa hilo la 16 la ununuzi wa Umma la afrika mashariki sambamba na uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma (Nest).

09/09/2024

Viongozi wa NHC Makao Makuu wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wa ujenzi wa Mkoa wa Arusha eneo la Kibla ambapo maduka ya biashara yanaanza kujengwa.

Photos from National Housing Corporation's post 09/09/2024

Meneja miradi ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi. Elizabeth Maro, akiongoza jopo la NHC katika mkutano baina yao na Kampuni 5 zilizofuzu kupata ubia na Shirika, kufuatia upembuzi yakinifu.
Muktadha wa kikao baina ya pande hizo mbili ni NHC kuhakiki na kujiridhisha nyaraka muhimu za wabia hao kabla ya kuanza kutekeleza miradi husika.
Miongoni mwa nyaraka hizo ni pamoja na vibali kutoka Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), uwezo wa kifedha, michoro ya majengo yatakayojengwa, vibali vya ujenzi na kujiridhisha juu ya wakandarasi na washauri.

Photos from National Housing Corporation's post 09/09/2024

Washiriki wa Mkutano wa 16 wa Afrika Mashariki ulioandaliwa wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma wakiwa tayari kumpokea Mgeni Rasmi Dkt Mashaka Dotto Biteko kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC.

Photos from National Housing Corporation's post 07/09/2024

Meya wa Jiji la Dodoma Profesa David Mwamfupe, akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Makazi Afrika Adiss Ababa, Ethiopia uliofanyika September 4 - 6, 2024

Photos from National Housing Corporation's post 07/09/2024

**Tanzania Yashiriki kwa Mafanikio Mkutano wa Makazi Afrika Addis Ababa**

Katika mkutano wa Makazi Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Septemba 4 hadi 6, 2024, ujumbe wa Tanzania umeshiriki vyema na kuonyesha jitihada za nchi katika kuboresha hali ya makazi na mipango ya miji, ikiwa ni pamoja na mipango ya viwanja vya makazi, maendeleo endelevu ya miji, na ushirikiano wa kimataifa.
Mkutano huu umeongeza nafasi kwa Tanzania kuimarisha uhusiano na nchi nyingine za Afrika, kubadilishana mawazo kuhusu changamoto za makazi, na kuonyesha hatua za maendeleo zilizofikiwa katika sekta ya makazi na mipango ya miji.

Ujumbe wa Tanzania umeeleza kuridhishwa na matokeo ya mkutano na kutangaza nia ya kuendelea kuboresha sera na mikakati ya makazi kwa lengo la kutoa majibu bora kwa changamoto za urbanization.

Photos from National Housing Corporation's post 07/09/2024

Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa Makazi Afrika Addiss Ababa, Ethiopia uliofanyika September 4 - 6, 2024

Photos from National Housing Corporation's post 04/09/2024

MENEJIMENTI YA NHC YAPIGWA MSASA Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Neema Kilembe, akitoa mada kuhusu masuala ya Tathmini na Ufuatiliaji kwa Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) k**a sehemu ya mafunzo ya wiki nzima yanayotolewa kwa watendaji na menejimenti ya shirika hilo. Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuimarisha utendaji wa Serikali na taasisi zake.

Katika mafunzo hayo, Bi. Kilembe amesisitiza umuhimu wa ufuatiliaji na tathmini katika kuboresha utendaji na kuhakikisha kuwa malengo ya serikali yanafikiwa kwa ufanisi. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo watendaji na Menejimenti ya NHC ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu zaidi.

Mpango huu wa mafunzo unafanyika k**a sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha utendaji wa taasisi za umma. Serikali ilifanya uamuzi muhimu wa kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Bunge na Uratibu. Idara hii ina jukumu la kushirikiana na Wizara, Wakala za Serikali, Idara za Serikali Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa zote katika kuhakikisha kuwa shughuli za serikali zinafanywa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.

Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha utendaji wa taasisi za umma na kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa za kiwango cha juu zaidi.

Photos from National Housing Corporation's post 03/09/2024

Ofisa Mwandamizi Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ritha Patrick akifuatilia majadiliano yanayoendelea kwenye vikundi vya Watendaji na machampioni wa ufuatiliaji, tathmini na Utendaji kwenye mafunzo yanayoendelea kwa wiki nzima.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali Katika kuimarisha Utendaji wa Serikali na Taasisi zake, ilifanya uamuzi muhimu ya kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali Iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Bunge na Uratibu. Idara hiyo inafanya shughuli zake kwa kushirikiana na Wizara, Wakala za Serikali, Idara za Serikali Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa zote

Photos from National Housing Corporation's post 02/09/2024

Mradi wa Samia Housing Scheme, Kawe, Dar Es Salaam unavyoonekana usiku huu ambapo inaonyesha ni kazi kazi hakuna kulala na hadi kufikia sasa ujenzi umefikia asilimia 76. Mradi huu wa nyumba 5,000 unaotekelezwa kwa awamu, utagharimu takriban shilingi bilioni 466 sawa na Dola za Kimarekani milioni 200. Katika kuendeleza mradi huu, maandalizi ya ujenzi wa Mradi wa Samia Housing Scheme wenye nyumba 100 Jijini Dodoma, nyumba 560 eneo la Kawe na nyumba 400 eneo la Mtoni kijichi Dar es Salaam yanaendelea kukamilishwa

02/09/2024

Hongera sana Bw. Eliud Betri Sanga

Photos from National Housing Corporation's post 02/09/2024

Ofisa Mwandamizi Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Ritha Patrick akitoa maada kwa Watendaji na machampioni wa ufuatiliaji, tathmini na Utendaji kwenye mafunzo hayo ya wiki nzima.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali Katika kuimarisha Utendaji wa Serikali na Taasisi zake, ilifanya uamuzi muhimu ya kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wake Iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Bunge na Uratibu. Idara hiyo inafanya shughuli zake kwa kushirikisha Wizara, Wakala za Serikali, Idara za Serikali Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa zote.

Photos from National Housing Corporation's post 02/09/2024

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa Serikali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Rehema Kerefu akitoa maada kwa Watendaji na machampioni wa ufuatiliaji, tathmini na Utendaji wa NHC muda mfupi baada ya mafunzo hayo ya wiki nzima kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Utafiti, Vihatarishi na Maendeleo, Amos Zephania Kulwa.

Photos from National Housing Corporation's post 30/08/2024

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah, akipokea tuzo ya utambuzi wa udhamini wa kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma, kilichoanza Agosti 27 mpak 30, 2024, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC).
Anayekabidhi tuzo hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Daktari Moses Kusiluka, ambaye ndiye aliyefunga kikao kazi hicho kilichofunguliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Agosti 28, 2024.

30/08/2024

NHC Wachangamkia fursa katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma

Photos from National Housing Corporation's post 30/08/2024

Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Takwimu Afrika Mashariki (Eastern Africa Statistics Training Centre) Dkt. Tumaini Katunzi, akiwa katika banda la maonesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), kunakofanyika kikao kazi cha Wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma 2024.

Dkt. Katunzi ni mmoja kati ya watendaji wakuu wa taasisi za Umma, wanaoshiriki katika kikao kazi hicho waliochangamkia uwepo wa banda la NHC katika kikao hicho na kujaza fomu ya maombi ya ununuzi wa nyumba.

Photos from National Housing Corporation's post 28/08/2024

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi. Irene Isaka, akiwa katika banda la maonesho la Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC), lililoko katika viwanja vya kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha (AICC), kunakoendelea kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma nchini.

Bi. Isaka, ni miongoni mwa wenyeviti na maafisa watendaji wakuu wa taasisi za umma, wanaoshiriki kikao kazi hicho cha siku 3 kilichofunguliwa rasmi na Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan, Agosti 28, 2024.

Photos from National Housing Corporation's post 28/08/2024

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah, akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (kulia) alipotembelea banda la maonesho la NHC, pembeni mwa kikao kazi cha siku 4 cha Wenyeviti na Watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini, kilichofunguliwa mapema leo na Rais wa JMT Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Arusha.

NHC ni mojwapo ya wadhamini wa kikao kazi hicho hivyo k**a wadhamini wengine imepata fursa ya kunadi bidhaa na huduma mbele ya viongoz mbalimbali wanaofika katika banda hilo.

Photos from National Housing Corporation's post 28/08/2024

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Mhandisi Anthony Sanga, akiwa na Makatibu wakuu wenzake akifuatilia kwa makini kinachoendelea katika kikao kazi cha Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma mwaka 2024 jijini Arusha.
Kikao kazi hicho cha pili cha mwaka, kinachotarajiwa kufunguliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan asubuhi hii, kinawakutanisha takribani wakuu hao 600 kikibeba maono ya Mhe. Rais, kutaka Taasisi na Mashirika ya Umma nchini kuwekeza nje ya mipaka ya nchi.

Makatibu wakuu wa wizara, ndiyo watendaji wakuu wa taasisi na Mashirika ya Umma yaliyo chini ya wizara mama husika.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Our Story

The current National Housing Corporation is the outcome of the decision of the Government to dissolve the Register of building (RoB) through Act of Parliament No.2 of 1990, which vested its responsibilities with the NHC. The former NHC was established by Act of Parliament No.45 of 1962, while RoB was established by Act No.13 of 1971.
NHC is under the Ministry of Lands, Housing and Settlements Development. The Ministry is represented by the Board of Directors which is responsible for the corporate policies and strategies. The day to day management of NHC's business is overseen by the Director General who is responsible to the Board of Directors. Effective from July, 1994, the Corporation's portfolios have been divided into profit centers which are income generating and self-sustaining directorates and cost centers which play a supportive role. This role mandates the NHC to undertake an array of business.
- Construction of houses for sale.
- Construction of buildings as part of approved scheme.
- Provision of facilitating the provision of building materials, components, concrete article and other related articles.
- Business of building contractors, planners or consultants.
- Renting out and managing houses or properties built by the corporation and those acquired by the government.
- Carrying out other activities related to construction of houses or other building built or acquired by the corporation.

Videos (show all)

KAWE - 711 Apartments Available for Sale Call Now! +255 736 114 433#tunajengataifaletu cc @nhctanzaniaupdates
NHC  Wachangamkia fursa katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma
NMB yasema toka kuanza ushirika na #NHC hii ya #Samia Housing Scheme, haijawahi kutokea.
Hatua za kufuata kununua nyumba za NHC kupitia Benki ya NMB popote pale Tanzania.
Mnafanya kazi #nzuri Msisahau #malengo ya kuanzishwa #NHC - Ndejembi.
#Repost @wizara_ya_madini_tanzania ——*“Nichukue fursa hii kwanza kabisa kuwapongeza Shirika la Nyumba la Taifa [NHC] amb...
Shughuli iliyopo uwanjani leo siyo ya kitoto, mtoto hatumwi dukani mpaka dakika 30 ya kipindi cha kwanza, timu ya makao ...
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya NHC Makao makuu na wenzao wa kombaini ya Mikoa ya Dsm, wakipiga jaramba muda mcha...
Sijaja na torati, naendeleza alipoishia Silaa.
Kawe 711 Residency...here we go!!
Hivi ndiyo ilivyokuwa...!!

Telephone

Address

P. O Box 2977
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:30 - 16:00
Tuesday 08:30 - 16:00
Wednesday 08:30 - 16:00
Thursday 08:30 - 16:00
Friday 08:30 - 16:00

Other Government Organizations in Dar es Salaam (show all)
U.S. Embassy Tanzania U.S. Embassy Tanzania
686 Old Bagamoyo Road, Msasani
Dar Es Salaam

The U.S. Mission to the United Republic of Tanzania. Terms of Use: https://www.state.gov/tou

dcea_tz dcea_tz
8 Kivukoni Road
Dar Es Salaam, S.L.P80327

The Drug Control and Enforcement Authority (DCEA) has the functions of define, promote, coordinate, and implement all measures geared towards control of drugs, drug abuse and traff...

NemcTanzania NemcTanzania
Regent Street
Dar Es Salaam, 00000

Karibu katika ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Pamoja tulinde na kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.

Juma fund kupauwa Juma fund kupauwa
Buza Dar Es Salaam
Dar Es Salaam, [email protected]

business

Algerian Embassy in Dar es Salaam Algerian Embassy in Dar es Salaam
Dar Es Salaam, 2963

EMBASSY OF THE PEOPLE'S DEMOCRATIC REPUBLIC OF ALGERIA DAR ES SALAAM TANZANIA سفارة الجزا?

Ubungo Manispaa Page Ubungo Manispaa Page
55068
Dar Es Salaam, LUGURUNI

Ukurasa rasmi wa Manispaa ya Ubungo (Page)

Tanzania people's Defense Force -TPDF Tanzania people's Defense Force -TPDF
Upanga
Dar Es Salaam

To provide Truely Information.

NSSF Tanzania e-Services NSSF Tanzania e-Services
P. O. Box 1322, Azikiwe Street
Dar Es Salaam, 0255

The National Social Security Fund is a fully funded scheme running under defined benefit principles.

Shemaya tz wcb tweens Shemaya tz wcb tweens
Dar Es Salaam

Shemaya

MBOWE Chadema MBOWE Chadema
Dar Es Salaam, 134

Mwenyekiti wa chama cha chadema.

Tanzania Commission for Universities Tanzania Commission for Universities
Magogoni Street
Dar Es Salaam, 11000

Promoting accessible, equitable, harmonised and quality university education systems in Tanzania

ThinkX GSM security ThinkX GSM security
Pugu Kajiungeni
Dar Es Salaam