Ndahani N. Mwenda

Ndahani N. Mwenda

Entrepreneur, Investor, Author.

10/12/2023

Binadamu tumeumbwa kusahau, nawakumbusha tu kuwa Liverpool FC ndiyo vinara wa EPL, na watakaa hapo mpaka Mwezi Mei akiwa anakabidhiwa ndoo na wengi hamtaamini maneno yangu!

09/12/2023

Ni miaka 62 sasa tangu Tanganyika ipate uhuru. Je, kwa miaka yote hiyo Watanzania hali zao za kiuchumi zipoje? Wanatumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali hasa za kutoka sekta ya fedha?

Kufikia malengo ya kifedha na kiuchumi unapaswa kujipa muda wa kujipatia maarifa kwa kusoma vitabu, magazeti, majarida yanayohusu masuala ya fedha.

Je, malengo yako ya kifedha kwa mwaka 2023 yamefiikiwa kwa asilimia ngapi? Umejipangaje kwa mwaka 2024? Pata nakala ya vitabu vya masuala ya fedha vya JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI, HISA NA HATIFUNGANI kwa bei ya OFA ya TZS 40,000 tu badala ya TZS 50,000. Lipia kupitia namba ya simu 0714-779-627

08/12/2023
08/12/2023

Nina ndugu ambao siyo rafiki zangu na nina rafiki zangu ambao ni ndugu zangu, Daktari wa Binadamu, Bingwa wa Magonjwa ya Ndani (MD, Mmed), Ndugu yangu Dr Alex Lipendele , miaka mingi iliyopita amezaliwa leo, tangu tumejuana tukawa marafiki na sasa tumekuwa zaidi ya ndugu, mmoja ya watu wanaopenda kazi zao, Love what you do!

Naweza kumaliza kurasa elfu kumwelezea ndugu yangu huyu lakini nachoweza kusema naomba muungane nami kumtakia heri ya kuzaliwa katika siku yake hii muhimu kwenye maisha ya kila binadamu.

Na k**a ukifika Hospital ya Kitengule ukawa na shida ya moyo, ini, figo ama mapafu unaweza ulizia Ofisini lwa Dr. Alex naamini ukipata huduma yake utafurahia na kumshukuru MUNGU kwa siku hii ambayo yeye alimruhusu aje Ulimwengu kuwa msaada mkubwa kwa jamii! Happy Birthday to you Brother, Happy Birthday to Mister Liverpool!

08/12/2023

Mnamo 13 Mei 2014 baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kumiliki silaha bila kibali kutoka kwa mamlaka Rappa Radric Delantic Davis almaarufu Gucci Mane aliamua kumkabidhi mkewe pesa zake zote alizokuwa nazo.

Gucci Mane alimkabidhi Baby Mama wake Keyshia Ka'Oir kiasi cha $ 2m ili aendelee kutunza familia yao kwa kipindi chote ambacho yeye atakachokuwa gerezani akitumikia kifungo chake hicho.

Baada ya kuwa na mwenendo mzuri, mapema mwaka 2016 Gucci Mane alichiwa na Keyshia aliendesha gari umbilical mrefu kumfuata wakifanya siri ili kukwepa mapaparazi jambo ambalo hata Mwanasheria wake hakushirikishwa kwa lolote.

Lakini baada ya kufika nyumbani, Gucci Mane alikuta utajiri wa familia umeongeza mara tatu ya alichoacha, kwani mwanamke huyo aliwekeza pesa ile aliyoachiwa kwenye biashara yake ya vipodozi na nyingine kwenye biashara ya majumba (Real Estate) na kufanya utajiri wao kutoka $ 2m mpaka $ 6m jambo ambalo hata Gucci Mane hakulitarajia wakati anatoka jela.

Waswahili wanasema "Kuku anayeyaga, hachinjwi" mnamo mwaka 2017 Gucci & Keyshia walifunga ndoa ambapo kila kitu kilighamiwa na BET wambao walipata hakimiliki ya kurekodi na kuuza maudhui ya harusi (The Mane Event - TV Series 2017) hiyo.

Mpaka sasa Gucci & Keyshia ni kati ya wanandoa mastaa ambao uhusiano wao ni imara wakiwa na familia yenye watoto watatu, mtoto mdogo kabisa wakimpata mapema mwaka 2023 Mwezi Februari.

Je, wewe unaweza kumwachia mwanamke wako kiasi gani na baada ya muda akakuonesha faida aliyopata kutokana na kuwekeza kiasi ulichompatia? Pata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI Kwa bei ya OFA ya TZS 20,000 tu badala ya TZS 25,000. Lipia kupitia 0714-779-627

08/12/2023

All men lie, choose your favorite liar!

07/12/2023

Vijiweni utawasikia "Caicedo anakaba halafu Enzo anakuwa 'free' kuchezesha timu, wameisha"

Eti Blo'angu imekuwaje kuwaje tena mnafungwa mpaka na hawa wachovu??

06/12/2023

Hello December! Pata vitabu vyangu kwa bei ya OFA ya TZS 40,000 badala ya TZS 50,000 kwa vyote viwili. Kupitia vitabu hivi utajiongezea maarifa na kukupa nafasi ya kuweka mipango yako ya kifedha kwa mwaka unaofuata wa 2024. Usikose OFA hiyo!

Mafanikio ya kifedha yanapatikana ikiwa umejiwekea tabia ya kujifunza kila mara vitu vipya na kuziona fursa mbalimbali. Lipia nakala zako mbili sasa ili uanze kujifunza, mwaka mpya uanze na vitu vipya. Lipia kupitia namba 0714-779-627

06/12/2023

Let's put in this way, "I have girls that are friends"

05/12/2023

Ili uwe tajiri lazima uwe na tabia ya kuepuka matumizi yasiyo na tija, matumizi ndiyo mstari unaotenganisha kati ya matajiri na masikini, na ndiyo hufanya masikini waendelee kuwa masikini na matajiri wabaki matajiri

Wengi wasio na akili ya kitajiri kila kipato kinapoongezeka huongeza matumizi hasa kwa kujenga nyumba za kuishi hata zaidi ya tatu, magari ya kutembelea ya kuendesha kila siku gari jingine.

Nyumba ya kuishi, gari ya kutembelea si mali ambazo zinaingiza pesa bali hizi ni mali mfu (Dead Assets) hufuja pesa kwa kuzihudumia, Mike Tyson alifanya makosa haya, Richard Fuscone pia alifanya makosa haya na mwisho wa siku wote wakafilisika.

Lijendari Charlie Munger ambaye amefariki siku saba zilizopita alikuwa ni mmoja ya watu tajiri sana hapa Duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya TZS 5trl lakini ameishi kwenye nyumba yake ileile kwa miaka 70.

Vilevile rafiki yake kipenzi Warren Buffett ana utajiri wa zaidi ya TZS 200trl lakini anaishi nyumba ile ile kwa miaka 65 sasa, Buffett nyumba yake aliinunua $ 31,000 mnamo mwaka 1958 licha ya kuwa mmoja ya watu 10 ambao ni matajiri zaidi lakini ameendelea kuishi kwenye nyumba yake ileile Omaha lakini akiwa na uwezo wa kuishi popote pale Duniani.

Je, unataka kufikia malengo yako ya kifedha na kiuchumi? Wekeza kwenye maarifa, pata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI kwa bei ya OFA ya TZS 20,000 tu badala ya TZS 25,000 lipia kupitia namba 0714-779-627

04/12/2023

If you can't stand for others, you are not safe at all! What a lesson!

04/12/2023

Kwa wale wanahisa wa NICOL nawakumbusha tu kuwa ile siku muhimu imewadia ya kucheka na kufirahia uwekezaji imewadia nayo si nyingine ni leo!

Kila hisa moja ya kampuni hiyo italipwa TZS 43 tu, na NICOL imetenga TZS 2,650,297,862 kwa faida iliyopatikana mwaka wa fedha unaoishia 31 Dis 2022

Je, wewe ni mwanahisa wa kampuni gani? Wajua faida mojawapo ya kuwekeza kwenye hisa ni kupata gawio? Pata kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI ili ujifunze zaidi juu ya uwekezaji huu murua ambao kila siku maelfu ya Watanzania wamekuwa wanajiunga!

Nakala ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI inapatikana kwa bei ya OFA ya TZS 20,000 tu badala ya bei halisi ya TZS 25,000, Lipia sasa upate nakala yako, usikubali kupitwa na OFA hiyo ambayo itaishia 31 Disemba 2023. Lipia kupitia 0714-779-627

04/12/2023

Nobody don't take away your pains, Don't let anyone take away your Happiness!

02/12/2023

Baada ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Dharura wa wanahisa wa Tanga Cement PLC ulioitishwa mwanzoni mwa Novemba 2023, ambapo ajenda ilikuwa ni kuridhia kuuzwa kwa kampuni hiyo kwa washindani wake Twiga Cement ya Dar Es Salaam hatimae utekelezaji wa azimio hilo umeanza rasmi.

Mchakato ulianza mnamo mwaka 2021 ambapo Scancem International AD ambayo inamiliki 69% ya hisa za Twiga Cement (Tanzania Portland Cement PLC) ilipokubaliana kuuziana na Afrisam Mauritius ambayo iliyokuwa inamiliki 68.33% ya hisa za Tanga Cement lakini hata hivyo mchakato huo ulipitia vipindi vigumu baada ya mapingamizi mengi kuibuka.

Lakini hata hivyo baada ya mvutano wa muda mrefu kisheria hatimae dili hilo lilikuja kuidhinishws na mamlaka na hivyo kufanya mchakato uendelee.

Tayari uhamishaji wa hisa za Afrisam kwenda kwa Scancem umefanyika ambapo hisa hizo zipatazo 43,504,403 zenye thamani ya TZS 106.34bn, hisa hizo ni 68.3% ya hisa zote za Tanga Cement.

Hatua inayofuata ni ununuzi wa hisa za wanahisa wadogo wadogo ambao jumla wanamiliki 31.67% ya hisa zote na mchakato huo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2024 na hivyo kukamilisha mchakato mzima wa ununuzi wa hisa zote.

Hawa wanahisa wadogo wanatarajia kurejeshewa TZS 2,400 kwa kila hisa moja. Kwahiyo k**a wewe ni mwahisa wa Tanga Cement muda si mrefu unakwenda kupokea fedha zako kutokana na uwekezaji wako (na k**a ulinunua hisa chini ya bei hiyo maana yake unakwenda kutengeneza faida) kwenye kampuni hiyo kubwa ya saruji nchini.

Je, wajua hisa ni mali k**a mali zinginezo ambapo unaweza igeuza pesa muda wowote kwa kuiuza kwa mtu mwingine? Pata nakala ya kitabu cha uwekezaji cha HISA NA HATIFUNGANI kwa bei ya OFA ya TZS 20,000 tu badala ya TZS 25,000. OFA hiyo inaishia 31 Dis 2023. Lipia kupitia 0714-779-627

01/12/2023

Good memories with good people!

01/12/2023

Ikiwa zimebaki siku 30 tu kumaliza mwaka wa 2023, nawatangazia wadau wa vitabu vyangu kuwa kwanzia leo 01 Disemba 2023 kutakuwa na OFA ya bei ya vitabu vyangu. Kila kitabu utakipata kwa TZS 20,000 tu badala ya TZS 25,000 bila gharama za usafiri na ukinunua viwili utalipia TZS 40,000 pekee badala ya TZS 50,000 nje ya gharama za usafiri kukufikia ulipo.

OFA hiyo itadumu mpaka 31 Disemba 2023, Wahi sasa upate nakala zako uanze kujifunza na kujiwekea malengo ya kifedha ukiwa na uelewa mpana juu ya masuala ya fedha. Pata nakala za vitabu bora vya masuala ya fedha na uwekezaji kwa bei ya punguzo.

Mpaka sasa ni nakala ipi huna? JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI au HATIFUNGANI & HATIFUNGANI? Lipia kupitia 0714-779-627

30/11/2023

Wengi huwa wanajiuliza, nawezaje kutengeneza pesa kwenye hisa? Ni wakati gani mzuri wa kutengeneza pesa napowekeza kwenye hisa, ni wakati wa kuuza?

"Pesa nyingi hazipo kwenye wakati wa kuuza ama kununua, bali ni kwenye kusubiri" ~ Charlie Munger

Ni ukweli usiopingika ni kwamba, pesa za kwenye hisa zipo kwenye wakati wa kusubiri, ukiwa na subira basi utaweza kutengeneza pesa ikifika wakati wa kuuza.

Je, wewe una elimu yoyote ya uwekezaji wa hisa? Pata nakala ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI ili ujifunze. Lipia kupitia 0714-779627

29/11/2023

Nikitembelea Moshi mara nyingi huwa nafika eneo la Kidia - Old Moshi (eneo ambapo ndiyo yalipokuwa makao makuu ya serikali ya Utawala wa Kichaga) eneo lenye historia kubwa kwa kabila la Wachaga.

Nipo Kilimanjaro, nimepita na kutazama mazingira kidogo ya eneo hilo lenye historia tamu, hapa ndiyo umelala mwili wa Mangi Meli Mkuu (kichwa chake Wajerumani walikata na kuondoka nacho na hakijawahi kurejeshwa mpaka sasa) Mtawala wa nhi ya Wachanga aliyetawala kati ya mwaka 1891-1900 akipokea kijiti kutoka kwa Baba yake mzazi.

Mangi Mkuu Rindi Mandara alikuwa mtawala wa nchi ya Wachaga kati ya 1860-1891 alipofariki na himaya hiyo akarithi mtoto wake Mangi Meli Mkuu ambaye alitawala kwa miaka 9 tu kabla ya kunyongwa!

Wakati wa Utawala wa Mangi Mkuu Rindi Mandara Wajerumani walikuwa na adabu kwenye utawala wa wake, waliheshimu utawala walioukuta na hawakumsumbua kabisa Mandara na utawala wake.

Lakini baada ya Mangi Meli Mkuu kushika hatamu Wakoloni (Wajerumani) walianza kudharau na kuleta chokochoko kwa utawala wake jambo ambalo lilimkera na kuanza kupambana nao kulinda Dola yake.

Baada ya kusumbuana kwa muda mrefu, mnamo 02 Machi 1891 walimk**ata yeye na watawala wengine 8 na kuwanyonga chini ya mti ambapo mti huo bado upo mpaka leo, Watawala walionyongwa na Mangi Meli Mkuu ni pamoja na Mangi Molelia wa Kibosho, Mangi Ngalami wa Kibong'oto, Mangi Lobulu wa Meru, na watawala wengine wa Arusha!

29/11/2023

JUMANNE ya 28 Novemba 2023 Ulimwengu wa uwekezaji hasa katika masoko ya mitaji umempoteza nguli katika tasnia hiyo Charles Thomas Munger ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 99!

Charlie Munger alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Berkshire Hathaway iliyo chini ya gwiji wa masuala ya uwekezaji duniani Warren Edward Buffett. Kampuni hiyo kufikia Septemba 2023 ilikuwa na mtaji wa $ 780bn ikiwa ni moja ya kampuni kubwa Duniani.

Warren Buffett anadai kuwa mafanikio ya sasa ya BKH ni matokeo ya mchango mkubwa wa Charlie Munger ambaye amekuwepo ndani ya kampuni hiyo kwa zaidi ya kipindi cha miongo minne.

Kwa mara ya kwanza wawili hao walikutana mwaka 1959 wakawa marafiki na washirika wa kibiashara, mwaka 1978 rasmi Munger alianza kuhudumu k**a Makamu Mwenyekiti wa BKH na mshirika mkubwa wa Buffett mpaka umauti ulipomkuta huko California.

Mwaka 1948 alihitimu alihitimu kunako Shule ya Sheria ya Harvard (Magna Cum Laude) licha ya kuwa hakuwa kuhitimu Shahada ya Kwanza. Enzi za uhai wake aliwahi kujihusisha na biashara ya majengo akiwa k**a mshauri wa masuala ya kisheria kabla ya kuwekeza muda wake kwenye masoko ya hisa.

01 Jan 2024 angetimiza miaka 100, amefariki akiwa na utajiri wa $ 2.5bn huku pesa nyingi akiwa katoa msaada kwenye taasisi mbalimbali zinazosaidia jamii, Greg Abel anatajwa k**a mrithi wake ingawaje mpaka sasa Berkshire Hathaway haijasema chochote juu ya nani ataziba pengo la Charlie Munger.

Rest in Paradise, A Omaha Boy, Real Estate Attorney, Genius and Billionaire Investor Charles Thomas Munger. Je, unataka kujifunza juu ya uwekezaji wa hisa? Pata nakala yako ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI kwa TZS 25,000/- tu! Lipia kupitia namba 0714-779-627

29/11/2023

UKWELI ambao wengi hawapendi kuusikia lakini ndiyo UKWELI!

28/11/2023

Kati ya vitu ninavyojivunia basi ni kujua mapema fursa zilizopo kwenye masoko ya mitaji hasa masoko ya hisa. Uwekezaji kupitia soko la hisa unakupa nafasi ya kufurahia maisha kwa kuwa faida zake ni nyingi.

Ukiwekeza kwenye kampuni ambayo ni imara unaweza tengeneza pesa nzuri k**a ukiwa na mpango mkakati mzuri. Binafsi kila gawio nalopokea kwasasa sigusi hata senti tano, ambacho huwa nafanya ni kuirudisha ilipotoka (kufanya uwekezaji tena kwa pesa iliyopatikana kutokana na uwekezaji, Waingereza huita Re-investment) lengo ni kuhakikisha kwa kipindi hiki ambacho bado nina nguvu na akili zenye uwezo wa kufanya kazi basi pesa hizo ziendelee kuzaliana.

Faida ya kuwekeza kwenye hisa hasa kwa masoko yetu yanayokua huonekana baada ya muda mrefu, hivyo unapopanga kuwekeza huku usiwe na haraka.

Ukiwa mwekezaji wa muda mrefu (Long-Term Investor) unakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kupitia uwekezaji huu. Mafanikio ya uwekezaji kwenye hisa huja polepole, hivyo ukiwa mvumilivu utaufurahia uwekezaji huu na kukufanya uwe mwenye ukwasi mkubwa endapo utakuwa na bidii ya kuwekeza!

Tayari NICOL, moja ya kampuni ambazo ninaendelea kuwekeza wameshaniomba taarifa za kibenki kwaajili ya GAWIO litakalolipwa mwanzoni mwa Disemba 2023

Je, wewe umewekeza kwenye kampuni gani? Una elimu yoyote ya uwekezaji wa hisa? Pata nakala ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI kwa TZS 25,000 ili uanze kujifunza. Lipia kupitia nambari 0714-779627

27/11/2023

Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa utajiri ni tabia na wala siyo kitu kingine, kwanini ni tabia?

Unapokuwa na tabia ya nidhamu ya pesa ndiyo unaukaribisha utajiri bila kujali unatengeneza kiasi gani, kinachokufanya uwe tajiri ama maskini hata k**a unatengeneza pesa nyingi ni matumizi yako.

Kati ya miaka ya 1980 ambapo Mike Tyson alikuwa ni moto wa kuotea mbali Ulingoni akiwachakaza mabondia wenzake alitengeneza kiasi cha $ 700m

Lakini mnamo mwaka 2003 alitangaza kufilisika na kuanza kuishi kwenye umasikini kabla ya kuanza kuigiza na biashara ya bangi ambayo kwasasa ndizo zinampa pesa lakini si k**a zile za kwenye ndondi.

Na hapo ndiyo unathirika msemo wa utajiri ni tabia, Noel Whittaker aliwahi kusema "Kuwa tajiri siyo suala la ni kiasi gani unaingiza, Wazazi wako ni akina nani au nini unafanya....Ni suala la namna gani unatunza pesa zako vema" hivyo k**a hutunzi pesa usitegemee utakuwa tajiri, hutakuwa kamwe hata k**a mshahara wako ni TZS 10m. Unajua makosa ya waliyoyafanya Mike Tyson, Richard Fuscone na wengine mpaka kuporomoka na kuwa masikini wa kutupwa?

Pata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI kwa TZS 25,000/- utajifunza zaidi. Lipia kupitia namba 0714-779-627

26/11/2023

Kwenye hafla ya uteuzi wa wania tuzo za Grammy mnamo Januari 2003, Nelly na Ashanti kwa mara ya kwanza ndiyo walikutana wakiwa bado vijana tu lakini wakiwa ni wasanii wanaowika zaidi kwa wakati huo.

Nelly alikuwa wa kwanza kuomba namba ya Ashanti na wakapiga picha kibao kwenye 'Red Carpet' na kwenye usiku wa utoaji tuzo 23 Februari 2003 pale Madson Square Jijini New York walikuwa ni moja ya watumbuzaji na wawania tuzo kwa wakati ule.

Usiku wa tuzo, Nelly alipanda jukwani na Kelly Rowland na wakaimba/wakatumbuiza wimbo wao maarufu wa Dillema ambao ulikuwa una bamba sana kwa wakati huo na hata sasa, nae Ashanti akipanda jukwani kutumbuiza wimbo wake wa Dreams.

Baada ya hapo penzi likachipua na kustawi k**a mmea ulipandwa kwenye rutabaga, penzi hilo lilidumu kwa miaka 10 tu, na katika wakati usiotarajiwa mashabiki walikuja kusikia kuwa wawili hao hawapo pamoja. Lakini nani anaijua kesho yake?

Wahenga walisema 'hawara hana talaka, ukitaka unampata' ndiyo kilichotokea Mwezi Septemba 2023 baada ya wawili hao kuanza kuonekana wakiwa pamoja kwa mara nyingi na Nelly alipohojiwa alithibitisha kuwa kwasasa wapo pamoja tena!

Kwasasa Nelly ana miaka 49 huku Ashanti akiwa na miaka 43. Je, mpenzi wako mliyeachana miaka 10 iliyopita kwasasa mnaweza kurudiaana?

25/11/2023

Faida mojawapo ya kuwekeza kwenye hisa ni kwamba wewe (mwekezaji) hujihusishi na shughuli za kampuni za kila siku. Unawekeza zako na unaendelea na shughuli zako zingine kabisa, pesa inaweza ingia wakati wowote hata ukiwa popote kule bila shida.

Pia faida nyingine ni gawio, nikiwa k**a mwekezaji wa NICOL Jumatatu ya 04 Disemba 2023 natarajia kupokea gawio langu, hilo gawio laweza nikuta mahala siyo lazima niwe Dar ama Ofisi za NICOL.

Je, Wewe umewekeza kwenye kampuni gani kunako Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE), Binafsi ni mwanahisa wa CRDB, NICOL, Vodacom na kampuni nyinginezo mbili. Tayari nishapokea gawio kutoka CRDB na Vodacom na sasa najiandaa kwa NICOL

K**a huna elimu juu ya hisa, pata nakala ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI kwa TZS 25,000/- tu. Lipia kupitia 0714-779-627

24/11/2023

Unajua kwanini matajiri huwa wanapigana vikumbo kuwania ama kuweka watu wao kwenye Uongozi wa hivi vilabu vikongwe hapa nchini vya Simba na Yanga?

Klabu hizi zina pesa nyingi na pia ni sehemu nzuri ya kufanyia biashara zako k**a ukiwa na akili timamu na unajua nini unataka kwenye maendeleo ya biashara zako kupitia hizi timu mbili kubwa hapa Tanzania.

Msimu uliopita klabu ya Simba SC ilidai kukataa dili la kuitangaza kampuni moja kubwa kwenye jezi zao za Klabu Bingwa Afrika (CAFCL) badala yake wakaitangaza tu Tanzania kwa kuvaa

Lakini watani zao Yanga SC waliingiza TZS 2.1bn kwa kuitangaza kampuni ya Haier. Lakini msimu huu Simba na Yanga zimeshangaza wengi, zote zimepata wadhamini kwenye jezi za Klabu Bingwa (CAFCL) ambapo michuano hiyo inaanza kutimua vumbi leo!

Simba SC kwenye jezi zao za CAFCL kifuani yupo Mo' Extra na Yanga SC mdhamini wao ni Whizmo ambapo dili zote hizi hazijatangazwa ni za kiasi gani si kwa Simba wala Yanga, dili hizi zimebaki kuwa siri mpaka sasa na hata ujio wa jezi hizo kwa timu zote hizo mbili ulikuwa ni wa kimya kimya tofauti na jezi za Ligi Kuu.

Umma unataka kujua ni utaratibu gani Simba SC walitumia kuchagua Mo' Extra awe mdhamini wa jezi za CAFCL na pia Yanga kuchagua Whizmo kuwa mdhamini wa jezi zake za CAFCL, kwanini Yanga msimu uliopita waliweka wazi kitita kilichopatikana lakini mwaka huu hawajaweka? Shida ni nini hasa?

Je, Mo' Extra hajakaa kiupendeleo kifuani mwa jezi za Simba SC? Mwenye Mo' Extra ndiyo mwekezaji wa Simba lakini huyo huyo ndiyo anateua Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, na huyohuyo anaitwa Rais wa Heshima Simba SC. Kwa mazingira haya ni kweli Simba imeingiza pesa kwenye udhamini huu wa Mo' Extra? Na k**a imengiza ni kiasi gani Mo' Extra imeipa Simba je hiko kiasi kiendana na hadhi ama ukubwa wa klabu ya Simba SC?

24/11/2023

Nasikia mwanaume kumshika mwanamke bega bila ridhaa yake ni unyanyasaji. Je, mwanaume akishikwa bega na mwanamke bila ridhaa yake nayo ni nini? Ni unyanyasaji ama ni nini hasa? Nauliza!

21/11/2023

Katika kuhakikisha Apple Inc inakuwa kampuni kubwa, Steve Jobs alimshawishi aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PepsiCo John Sculley kuja kufanya kazi nae

Lakini mnamo mwaka 1985 Steve Jobs akiwa mmoja ya waaasisi wa kampuni ya Apple alitimuliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo baada ya kupishana mtazamo kwenye uendeshaji wa kampuni hasa kwenye mauzo ya bidhaa za Lisa na Macintosh.

Bidhaa za Macintosh na Lisa hazikufanya vizuri sokoni hivyo kukawa na malumbano kwenye Bodi na mwisho wa siku Sculley aliongoza jopo la wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Apple Inc kumtimua Steve Jobs.

Lakini baada ya miaka 11 Steve Jobs alirejea Apple Inc na aliiuza kampuni yake ya NexTL kwa Apple kwa kiasi cha $ 429m baada ya hapo alifanya mapinduzi makubwa na mpaka anaaga dunia mwaka 2011 Apple ilikuwa ni kampuni kubwa Marekani na Duniani.

Sasa kilichomkuta Steve Jobs miaka 38 iliyopita, hivi karibuni ndiyo kilichomkuta CEO wa kampuni ya OpenAI ambaye alikuwa ni mmoja ya waaasisi wa kampuni Sam Altaman ambaye Bodi imemfuta kazi.

Tofauti na Steve Jobs, Altman yeye kapata watetezi ambao ni wafanyakazi wa OpenAI wapatao 738 kati ya 770 ambao wamesaini azimio linaloshinikiza Bodi kujiuzulu ama kumrejesha Sam Altman kazini.

Wafanyakazi hao wanadai Bodi imekosa uhalali kwasasabu kumwondoa Altman ni kufanya Dira na Dhumuni la kampuni hiyo kutofikiwa kwa wakati.

Je, Ni Bodi ama Sam Altman atakayeibuka kidedea kwenye huu mvutano?

21/11/2023

Siku chache zilizopita nyota wa zamani wa Nigeria na Chelsea FC Mikel John Obi aliibua mjadala mzito sana!

Nguli huyo akiwa kwenye Podcast moja hivi karibu alidai kuwa Afrika ukishaanza kutengeneza pesa basi hizo si zako ni za familia. Huna uhuru nazo kabisa!

Yaani kwanzia Dada zako, kaka zako, binamu, rafiki zako, wajomba, mashangazi wote watakutazama wewe tu kwa kila kitu kwasasabu una kipato kikubwa.

Dada zako wanaweza olewa na wanaume ambao hata hawawapendi ila wao wanapenda kwasasabu ni ndugu zako na wanajua utawapa pesa!

Watazaa watoto wengi kwa kuwa wanajua utawasomesha, na ukiwauliza wanasema wewe si upo! Na ukianza kusitisha misaada basi wataanza kukuona mbaya watakutishia maisha ama kukutangaza kwenye vyombo vya habari.

Baada ya Podcast ya Obi wengi wameonekana kumnanga na kumwona k**a mtu mbinafsi na mchoyo na kusema mbona Sadio Mane anasaidia mpaka majirani kijijini kwao na halalamiki?

Lakini Je, ni mchezaji ama mtu gani hasaidii kwao akifanikiwa? Ukweli ni kwamba watu wengi wakifanikiwa hukumbuka kusaidia kwao lakini watu wetu wengi hawaridhiki, leo utamtumia TZS 500,000 kesho akiomba laki ukasema huna ni kesi kana kwamba alikupa pesa umshikie, inatia hasira.

Ushauri wangu ni kwamba, fanikiwa ufanikiwavyo lakini weka utaratibu wa kusaidia ndugu zako, kumbuka matatizo hayaishi, na binadamu hawaridhiki.

Usipokuwa makini kwenye misaada ya nduguzo unaweza jikuta unarudi kule kule kwenye umasikini na ukishakuwa masikini hao hao watakucheka! Elewa tu kuwa utajiri ni tabia na si vinginevyo!

21/11/2023

Kila Mwaka Mwezi Novemba, Tanzania huadhimisha WIKI YA FEDHA Kitaifa, Mwaka huu Wiki hiyo inadhamishwa Jijini Arusha ambapo 22 Novemba 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa (MB) atazindua rasmi.

Kauli mbiu ya Mwaka huu 'ELIMU YA FEDHA KWA MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA' kampuni na taasisi zote zinazojihusisha na masuala ya fedha k**a vile Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE), Benki, Kampuni za Udalali Katika DSE, Kampuni za Bima, Kampuni za Uwekezaji, Kampuni za Ushauri wa Masuala ya Fedha.

Lengo la Kuanzisha wiki hii ni kuwapa fursa wananchi kujifunza juu ya huduma za kifedha zinazotolewa na kampuni hizi kwani huduma na fursa zinazopatikana kwenye taasisi za fedha nyingi watu wengi hawazijui na zimebaki kuwa za watu wachache mno siku zote.

Elimu ya fedha ikiwafikia wengi, itaimarisha uelewa wa watu wengi katika kuhakikisha wanafikia uhuru wa kifedha na kiuchumi na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, na uchumi wa mtu mmoja mmoja unapokuwa imara ndiyo uchumi wa taifa huimarika.

Je, una elimu ya fedha ambayo imekuwa msaada kwako katika kufikia malengo yako ya kiuchumi kwa maisha yako ya baadae? Pata nakala za vitabu vya HISA NA HATIFUNGANI pamoja na JINSI YA KUJENGA UCHUMI BINAFSI kwa TZS 50,000 tu uweze kuongeza uelewa juu ya masuala ya kifedha na uwekezaji. Lipia kupitia namba 0714-779-627

20/11/2023

Tangu mwaka 2005 wakati UTT-AMIS inaanzishwa imekuwa ni mkombozi kwa Watanzania wengi ambao wanatafuta mahala salama pakuwekeza mitaji yao.

Mwaka 2005 UTT-AMIS ilikuwa na mfuko mmoja tu wa UMOJA FUND, lakini kufikia mwaka 2019 ilikuwa tayari ina mifuko sita ambayo mpaka mwisho wa mwaka 2022 thamani ya mifuko yote ilikuwa ni zaidi ya Shillingi za Kitanzania (TZS) 1,000,000,000,000 tu

Kwenye masoko ya mitaji, kati ya sehemu salama ya kuwekeza ni pamoja na kwenye Uwekezaji wa Pamoja (CIS) na Tanzania ina taasisi zaidi ya mbili za uwekezaji UTT-AMIS pamoja na FAIDA FUND.

Je, unaijua mifuko yote inayosimamia na UTT-AMIS ambapo mwekezaji anaruhusiwa kununua kwanzia vipande 10 tu na kuendelea katika mfuko wowote na akaanza safari yake ya uwekezaji? Pata nakala ya kitabu cha HISA NA HATIFUNGANI kwa TZS 25,000 ujifunze zaidi juu ya uwekezaji huo wa pamoja.

PICHANI, Ni wawekezaji wa mifuko ya UTT-AMIS wakiwa katika AGMs inayoendelea pale JNICC-Dar Es Salaam kwanzia tarehe 18-20 Novemba 2023!

Kupata nakala yako ya kitabu, Lipia kupitia namba ya simu 0714-779-627

19/11/2023

IKIWA dunia inaadhimisha SIKU YA KIMATAIFA YA WANAUME, Nitumie nafasi hiyo pia kuwapongeza WANAUME wote Duniani ambao wanapambana kuhakikisha familia zao/wapendwa wao wanafanikiwa/wanaishi maisha mazuri yenye furaha.

Uanaume siyo tu kuwa na jinsia ya kiume (kwasababu hata mashoga nao wana jinsia ya kiume lakini wameshapoteza sifa ya uanaume) kwasababu uanaume siyo jinsia tu bali ni kuwa na haiba ya kiume, kuwajibika k**a mwanaume hasa pale unapozungukwa na watu ambao wewe ni Kiongozi wao na hatima ya maisha yao ipo mikononi mwako.

Kumzalisha mwanamke na kisha kumtelekeza siyo Uanaume, kupiga na kuumiza mwenza kwasababu yoyote ile siyo uanaume, kumdhalilisha mwenza kwa matusi ama kuweka mambo yenu ya zamani hadharani wakati mkiwa pamoja siyo uanaume, yoyote anayofanya haya anakuwa kapoteza sifa ya uanaume!

Mwanaume sifa yake kuu ni kuwa mwenye busara, mkak**avu hata wakati wa nyakati ngumu, mwenye kuhudumia familia yake kwa kila namna kuhakikisha familia hiyo inakuwa bora ili kujenga taifa imara!

Yoooo' Happy International Men's Day Buddies ALL over the World!

18/11/2023

Zawadi ya maisha, Zawadi yenye kuambatana na Upendo!

18/11/2023

Ayeeeh! Wanasema Usiku wa Deni haukawii kucha, ni Leo pale Machinga Complex. Unakosaje kwamfano?

Kwa yoyote ambaye hajawahi kununua vitabu vyangu, akija kuchangia damu anapata nakala mbili za vitabu vyangu kwa TZS 35,000/- tu badala ya TZS 50,000/-

Tukutane Saa 3 Asubuhi nami nitakuwepo kwenye zoezi hilo!

17/11/2023

Call him Golden man! Pia nae ATAKUWEPO pale Machinga Complex, Dodoma hapo Kesho, Jumamosi!

Unakosaje kwamfano?

17/11/2023

Nasemaje!!! Dodoma tumeingia kwenye Mji wenu, yule Daktari mwenye akili mingi nae ATAKUWEPO. Je, unakosaje kufika pale viwanja vya Machinga Complex?

Ungana nasi kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wanaofariki kwa kukosa damu hasa pale wanapopungukiwa!

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Let's put in this way, "I have girls that are friends" #DiplomaticWay #Intelligence #PGTA #AskMwenda
If you can't stand for others, you are not safe at all! What a lesson! #PGTA #CriticalThinking #AskMwenda
UKWELI ambao wengi hawapendi kuusikia lakini ndiyo UKWELI! #PGTA #UtajiriVsMshahara #AskMwenda
Biashara imahitaji vitu viwili, AKILI na ELIMU lakini inahitaji zaidi matumizi ya AKILI kwasababu ELIMU ina ukomo kuliko...
#CRDBHQ
#HisaNaHatifungani
#Migombani
#GhanaMps
#BarrackObama
#AkiliKubwa
#Entrepreneurship
#ProfitableBank

Category

Website

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00