Urithi Arts

Urithi Arts

Sole registered company for Creative, Arts and entertainment

Urithi Arts writes and documents for Arts and artists, Artistic Consultatation, Marketing the Arts, Art Exhibitions, Branding, Art Talk, Art for Children, Training and Art Workshops, TV Program for Children, outreach and exchange programs and more.

10/06/2024

Mzazi na mlezi unaalikwa kuleta mtoto au watoto na umumtaarifu na rafiki, jirani na ndugu. SIKU YA MTOTO WA AFRIKA sisi tunaisherehekea JUMAMOSI tarehe 15 Juni 2024. Mlete mtoto ajumuike na wenzake katika mambo mbali mbali. ikiwemo Maonyesho ya michoro, warsha za uchoraji, kuimba na kucheza bila kusahau Hema la vitabu. ZAWADI KEM KEM zitatolewa kwa watakaofanya vzuri!

24/05/2024

Viongozi na wasanii wa Shirikisho la Sanaa za ufundi wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Damas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni, Sanaa na michezo na Naibu waziri Mh. Mwinjuma na viongozi wengine baada ya kusomwa kwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/25 bungeni mjini Dodoma. Aliyetuma picha hii naye yumo.

13/05/2024

Familiar faces... the ones we face in our everyday lives...again happy faces, sad faces, angry faces, and more. Is known or unknown? You can mention/name, which face is familiar to you?

Photos from Urithi Arts's post 07/01/2024
Photos from Urithi Arts's post 07/01/2024

Ukiwa JIKONI hukosi jambo la kufanya, Hatimaye nimeleta ladha hii, KWENU kwa kuanzia,. Huu ni mwanzo tu na ni mwanzo mzuri kwangu ila wewe endelea kuwa Mpenzi mtazamaji kwa kula kwa macho. Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kukuletea LADHA nitakazojaaliwa kupakua toka katika jiko hili. nataka akiwa mkubwa awe k**a WEWE.

01/01/2024

To all!

25/12/2023

Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunisimamia, nakutakia heri ya sikukuu ya kuzaliwa kwake Emanuel yaani Mungu pamoja nasi. Siku iwe ya furaha, upendo na amani kwako wewe na familia yako. MERRY CHRISTMAS!!

13/10/2023

Taking back my position.

30/09/2023

Ubunifu ni sehemu ya maisha ya kila Mwanadamu. Utumie popote ulipo. Nyumbani, kazini, ibadani, safarini nk.

28/04/2022

Mtihani wa Mwisho
Acrylic on Canvas

23/04/2022

Same but different
Acrylic on canvas
26x20cm

Photos from Urithi Arts's post 28/03/2022

HAPO KATIKATI YA KAPIRIMPOSHI NA DAR ES SALAAM KUNA NINI?
Imeandikwa na Fred Halla
Safari ni Safari, haijalishi unatembea kwa miguu, unatumia baiskeli, motokaa, jahazi, ndege au gari moshi la msingi ni kuwasili kule uendako. Kuna wakati unaweza fika salama lakini njiani kukawa na misuko suko ya hapa na pale mfano dhoruba, hitilafu, maradhi na rabsha kadha wa kadha.
Ukiachana na Safari pamoja na njia mbali mbali za kufanikisha safari, kuna huyu msafiri ambaye anatoka eneo moja na kuelekea eneo lingine kwa kutumia njia mojawapo ya usafiri uliotajwa hapo juu.
Mara nyingi safari huja na simulizi kadha wa kadha, zenye kufurahisha, kupendeza, kusikitisha na pengine za kutisha. Leo hii ningependa kuongelea kwa kifupi tu juu ya safari ya msanii Klaus Hartmann kutoka Ujerumani ambaye alisafiri toka Zambia kuja Tanzania, akitokea Kapirimposhi kuja Dar Es Salaam, hakuja tu kutembea bali ni kwa mualiko maalum kutoka taasisi ya Sanaa inayoongoza nchini Tanzania, Nafasi Art Space ili atushirikishe akijuacho naye kujifunza asichokijua.
Kila mwaka Nafasi Art Space hutoa nafasi kwa wasanii mbali mbali kutoka ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kutumia muda wa mwezi mmoja au Zaidi kwa msanii kufanya kazi ya Sanaa na hatimaye kuionyesha kwa hadhira.
K**a nilivyoelezea hapo mwanzo kuwa kila safari ina hadithi yake, basi ndivyo ilivyo kwa Bwana Klaus ambaye katika safari yake alitumia usafiri wa Gari Moshi kwa reli ya TAZARA (ushirikiano wa usafiri wa reli kati ya Tanzania na Zambia) alikuwa na jambo la kutusimulia. K**a ilivyo kwa wengi tunaposafiri njiani kuna mambo na vitu mbali mbali ambavyo hatutilii maanani na kuvichukulia ni vitu vya kawaida. Lakini kwa Klaus Hartmann vitu hivyo vya kawaida kwake yeye ni hadithi nzuri ambayo ameweza kuisimulia vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu kupitia michoro ya rangi.
K**a wewe ni msafiri wa kutumia Gari moshi (Treni) au basi utakuwa shahidi kuwa kuna vitu au mambo yanayotokea ukiwa safarini, na unaona vitu vingi vya kuvutia na vingine visikuvutie, Klaus katika safari yake ameweza kutukusanyia taarifa mbali mbali k**a vile aina za nyumba za wenyeji, nyumba zilizo katika miundo na mpangilio tofauti wa kuvutia, nazo zimejengwa pembezoni kufuata njia ya reli.
Katika baadhi ya maeneo Bw. Klaus amevutiwa na shughuli za kiuchumi na jinsi wenyeji wanavychangamkia fursa ya uwepo wa Reli ya TAZARA. Biashara k**a vile Vyakula, vikapu na Matunda ya aina mbali mbali. “Haikuwa rahisi kwangu kupata kila picha niliyoitaka kwa kuwa treni ilikuwa iko katika mwendo, alisema Klaus, “…Lakini kila iliposimama niliweza kupata nafasi ya kukusanya taarifa zilizonisaidia katika kazi yangu”, aliongeza.
Ukitazama kwa jicho la kawaida jambo alilofanya Bw. Klaus unaweza kuona ni la kawaida lakini ukitazama na kutafakari ni jambo kubwa na muhimu kwa leo n ahata kwa siku zijazo kwa kuwa michoro yake itadumu kwa miaka mingi ambapo mabadiliko haya ya kasi yanayoendelea baadhi ya taswira hazitakuwepo lakini kwa kupitia Klaus zitakuwepo.
Klaus Hartmann ni msanii kutoka Ujerumani aliyekuja mpango wasanii waalikwa kutoka nje ya Tanzania unaoendesha na kuratibiwa na kituo cha Sanaa cha Nafasi Art Space. Hii si mara ya kwanza kuzuru Afrika Mashariki, na ameandika na kuchapa vitabu kadhaa vyenye majengo na mandhari mazuri ya vijiji kutoka nchi za Tanzania, Rwanda na Zambia.

09/03/2022

TUWALINDE Project
Aiming at reminding local and International community to protect the wild animals and their habitants.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Telephone

Website

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
Other Dar es Salaam gyms & sports facilities (show all)
Oyster Bay Football Club Oyster Bay Football Club
Dar Es Salaam

OFC

Digitouch ltd Digitouch ltd
Dar Es Salaam

Digitouch Ltd is the perfect choice for all your supply of sporting goods; from Sportswear to Gym equipment.

cadttraining.org cadttraining.org
Conerstone Centre
Dar Es Salaam, H100

BRINGING DEVELOPMENT TO AFRICA THROUGH HUMAN RESOURCE TRAINING AND DEVELOPMENT

BestGoals BestGoals
Dar Es Salaam

Mutensa kabombo Mutensa kabombo
Mutensa Kabombo
Dar Es Salaam

Shaibu Shaibu
Sadas
Dar Es Salaam, SHAIBU

Nguvu za kiume wellness Nguvu za kiume wellness
Makumbusho
Dar Es Salaam, 255

TUNAKUSAIDIA KUONDOKANA NA MATATIZO YA AFYA YA UZAZI KWA KUTUMIA VIRUTUBISHO VYA ASIRI KARIBU SANA

Msukuma Msukuma
0753875919
Dar Es Salaam, MUME

Mavado_ d laz Mavado_ d laz
L
Dar Es Salaam

Young Afric VS Simba Sport Club Young Afric VS Simba Sport Club
Kaliakoo
Dar Es Salaam

Habari Kamili Na  Michezo Habari Kamili Na Michezo
0747883565
Dar Es Salaam

THE PLUG FOR YOUR FS, CONTACT ADMIN FOR ANY INFO BEFORE PURCHASE. REFUND IS ALLOWED IF

Yanga sports club Yanga sports club
Bunju
Dar Es Salaam, BUNJU

Hii ni kwa ajili ya mashabiki wa yanga Africans kwa group la WhatsApp nicheki 0696222100