Mbeya University of Science and Technology
MTC was officially launched on 1st September, 1986. LOCATION
Mbeya University of Science and Technology has two campuses. ii. iii. iv.
HISTORICAL BACKGROUND
Mbeya University of Science and Technology (MUST) is a result of the transformation of Mbeya Institute of Science and Technology (MIST) through the University Act No. 7 of 2005 and the Charter of Mbeya University of Science and Technology, 2013. The then Institute was a result of the transformation of the former Mbeya Technical College (MTC) through the National Council for T
Maonesho ya nanenane 2024 yashika kasi katika viwanja vya John Mwangale huku MUST ikiwakilishwa na wataalamu mbalimbali
MUST inashiriki katika Maonesho ya wiki ya Elimu ya Juu Zanzibar, ikiwa ni makala ya tano ya Maonesho hayo.
Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la MUST na kupata elimu juu ya Taaluma, Tafiti na Bunifu kutoka kwa watalamu wetu.
*Wafanyakazi MUST wapatiwa mafunzo ya elimu ya watu wenye mahitaji maalum.* Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo prof. Godliving Mtui amewataka wafanyakazi kuzingatia mafunzo hayo, kwani yana umuhimu mkubwa katika kuongeza utoaji huduma bora kwa wenye mahitaji maalum. Mafunzo hayo haliyotolewa kwa siku mbili ni sehemu ya utekelelezaji wa mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi, mratibu wa mradi huo katika masuala ya jinsia na elimu jumuishi, Dkt. Magreth Matonya amewataka wakufunzi wote kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kutimiza lengo la kupata elimu. Katika hatua nyingine, Dkt. Matonya amesema ni muhimu kujumuisha kozi ya elimu ya lugha za alama katika programu mbalimbali zinazofundishwa hasa zile za ufundi. Pia amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi wote kujifunza alama za msingi ili kuweza kuwasiliana na wanafunzi wenye mahitaji maalum.
MCB YAENDELEA KUNGA'RA KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA UJENZI
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kupitia kampuni yake ya ujenzi na ushauri MCB inaendelea kusimamia miradi ipasavyo. Katika kutekeleza hayo ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi yamefanyika hivi leo, Mradi wa jengo la maabara ya kisasa ya kibailojia iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Mkwawa umegharimu zaidi ya milioni mianane (800) . Katika kazi ya maandalizi ya makabidhiano (pre inspection for handing over) Prof. Zacharia Katambara kutoka chuo cha MUST, amesema licha ya changamoto walizokabiliana nazo, ikiwepo kuchelewa kupatika meza zenye uwezo wa kuhimili kemikali kutoka nje ya nchi, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi huo kwa asilimia zaidi ya 97, na makabidhiano yanatarajiwa kufanyika tarehe 22.11. 2023. Pia Prof. Zacharia Katambara ameeleza kukamilika kwa mradi huo kutaleta manufaa kwa watumiaji hao na kwa taifa kwa ujumla, kwani maabara hiyo itakuwa na vifaa vya sasa vya kugindisha na kufanya utafiti kwa maendeleo ya taifa.
NAIBU KATIBU MKUU MPANJU AIPONGEZA MUST KWA KUANZISHA NA KUSIMAMIA DAWATI LA JINSIA KWA WELEDI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Wakili Amoni Mpanju amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya[MUST] kwa hatua ya kuanzisha na kuendeleza Dawati la Jinsia Chuoni.
Wakili Mpanju amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Dawati la Jinsia Chuoni hapo ambapo amewataka Viongozi wa MUST kupanua wigo wa Dawati hilo na kuifikia Jamii inayokizunguka Chuo pia kufungua Dawati lingine la Jinsia kwenye Kampasi ya Rukwa[MRCC], huku akivitaka Vyuo vingine kufanya hivyo.
Pia wakati akifungua Mafunzo ya Jinsia kwa Viongozi wa Vyuo Mkoani Mbeya,amewataka Viongozi wa vyuo hivyo watakaopata Mafunzo kuhakikisha wanaanzisha Madawati ya Jinsia kwenye Taasisi zao ili kupambana na changamoto za Ukatili wa Kijinsia kwenye Vyuo hivyo
Aidha,amewataka Wajumbe wa Dawati la Jinsia kwenye Taasisi za Elimu kutoa Elimu kwa Wakufumzi na Wadau wengine namna ya kubaini viashiria vya Wanafunzi walioathirika na Vitendo vya kikatili ili kuwapa Msaada stahiki ili kuongeza ufanisi na tija kwenye Jamii yao
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa MUST Prof. Aloys Mvuma amesema kuwa Chuo kimeweka njia rafiki na rahisi za kupata taarifa za ukatili ikiwa ni pamoja na kuweka Sanduku la Maonikatika maeneo mbalimbali ya Chuo na sehemu maalumu ambapo Watu wanapata nafasi ya kupeleka hoja na Malalamiko yao kwa uhuru.
Prof.Mvuma ameongeza kuwa Lengo la kuanzishwa kwa Dawati Hilo ni kuunga mkono juhudi za wizara na Serikali kwa ujumla za kupinga Vitendo vya Ukatili wa aina zote katika jamii na hasa katika maeneo ya kutolea huduma muhimu k**a elimu ya juu na elimu ya kati.
Dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya lililozinduliwa leo lina jumla ya wajumbe saba ambao wawili kati yao ni wanafunzi na hufanya kazi k**a timu moja ili kuhakikisha wanayafikia makundi yote ndani ya Chuo.
Welcome all
WAWAKILISHI BENKI KUU YA DUNIA, WIZARA YA ELIMU WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MRADI WA HEET MUST.
Timu ya Wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Dunia na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wamefanya ziara katika eneo la ujenzi wa Majengo matatu, ambayo ni Jengo la kitaaluma, Jengo la Karakana na Jengo la Kituo cha Ubunifu na Uhaulishaji Teknolojia.
Akiwa katika eneo hilo Mwakilishi ya Benki kuu ya Dunia kutoka nchini Marekani Bi. Roberta Bassett amesema kuwa wameridhishwa na hatua za awali za ujenzi wa Majengo hayo nakusisitiza kuwa Mkandarasi aendelee na kasi hiyo hiyo ya ujenzi ili aweze kukamilisha kazi kwa wakati uliowekwa katika mkataba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dr. Keneth Hosea amekipongeza Chuo cha MUST kwa utekelezaji wa mradi wa HEET kwenye ujenzi na maeneo mengine ya mradi huo.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Prof. Aloys Mvuma amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia na Wawakilishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Kuridhishwa na Maendeleo ya Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya juu kwa maendeleo ya Kiuchumi [HEET ]unaoendelea Chuoni.
Akiwakaribisha Wawakilishi hao, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anaesimamia Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Godliving Mtui amesema kuwa Chuo cha MUST kimejipanga kukamilisha mradi wa ujenzi kwa wakati na kukamilisha miradi mingine inayofadhiliwa na mradi wa HEET.
Mradi wa HEET katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya unahusisha ujenzi wa Jengo la Kitaaluma, Jengo la Karakana pamoja na jengo la Kituo cha ubunifu na uhaulishaji Teknolojia.
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA MBEYA LAKAGUA MIUNDOMBINU MUST.
Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Mbeya limefanya ukaguzi wa Miundombinu mbalimbali hapa Chuoni ikiwemo Madarasa,Ofisi, Migahawa, Kumbi, Mabweni na Karakana zote kwa lengo la kuangalia Usalama wa maeneo hayo endapo janga la moto linaweza kutokea.
Katika Ukaguzi huo Jeshi limekagua Milango ya kuingilia na kutokea hasa katika Majengo yanayotumiwa na watu wengi na uwepo wa vifaa muhimu vya kujihami endapo janga la moto litatokea katika Majengo hayo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa muhula mpya wa masomo 2023/2024.
Akiongea wakati wa zoezi hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, Kamanda Malumbo Ngata amesema kuwa, hali ya miundo mbinu ni nzuri na inauwezo wa kutumiwa na idadi kubwa ya watu licha ya kuwepo kwa changamoto chache ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi, amebainisha changamoto hizo ni pamoja na kutokuwepo na alama za tahadhari katika baadhi ya maeneo, kutofungwa vifaa vya kuzimia moto katika baadhi ya maeneo.
Kwa upande wake Mkurugeanzi wa Milki hapa Chuoni Dkt. Hieronimi Mboya amesema kuwa Chuo kimeashanunua vifaa vya kuzimia moto kwa ajili ya maeneo yote ya Chuo.
“Tumeshafunga vifaa vya kuzima moto katika jengo la Utawala na maeneo mengine yote, kwa sasa tunaendelea na kazi ya kukamilisha maeneo machache yaliyobakia, lengo ni kuhakikisha tunakamilisha ndani ya wiki hii”. Dkt. Mboya ameeleza.
Kuhusu alama muhimu za tahadhari Dkt. Mboya amesisitiza kuwa alama zinaendelea kuwekwa, mpaka sasa wameshakamilisha kuweka alama katika Jengo la Utawala na wanaendelea kuweka katika maeneo machache yaliyosalia
Hata hivyo ametoa wito kwa wanafunzi na watumishi kuhakikisha kuwa wanaendelea kujifunza alama hizo na namna ya kuchukua tahadhari juu ya majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza Chuoni hapo.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha Mipango na Utawala Dkt. John P. John ametanabahisha kuwa Chuo kimeweka mpango wa kutoa elimu ya Zimamoto na Uokoaji kwa Wanafunzi na Watumishi ambapo elimu hiyo itatolewa kila juma la pili la mwezi Novemba kuanzia mwaka huu wa masomo 2023/2024.
Zoezi la Ukaguzi wa Miundombinu ya kujikinga na Majanga k**a moto hufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa mwaka wa Masomo ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hutuma wataalamu wake Chuoni kukagua Miundo mbinu hiyo.
Call for application 2nd round
TANZIA
Salamu za pongezi
MUST YAN'GARA NANE NANE KITAIFA 2022
Karibuni katika Maonyesho ya kilimo ya nane nane 2022 katika viwanja vya John Mwakangale Mbeya, mtembelee banda la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya lililopo mkabala na banda la ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya.
Kauli mbiu, "Ajenda 10-30 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi".
Hongera sana Mhe. Meghji
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, utafiti na ushauri wa kitaalamu Prof. Godliving Mtui akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea vifaa tiba kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara.
MUST YAPOKEA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 70 KUTOKA TAASISI YA AFYA YA IFAKARA.
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 70 vitakavyosaidia katika kufundishia wanafunzi wa kozi ya Uhandisi wa Vifaa tiba (biomedical engineering) Chuoni hapo, pamoja na watoa huduma katika Vituo vya Afya na Hospitali kwa kanda ya nyanda za juu kusini.
MUST yaunda ndege za kilimo.
Call for applications 2022/2023 Bachelor Programmes at MUST Rukwa Campus College
Call for applications:2022/2023 Bachelor Programmes
Tunawatakia Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla Sikukuu njema ya Eid al adha, "msherekee kwa amani na utulivu".
Sasa tunapatikana Twitter mbeya university of science and technology, karibu utufollow, mwambie rafiki amwambie rafiki
Tunawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Sikukuu ya Sabasaba 2022.
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimetiliana Saini mkataba wa kuzalisha mita maalumu za maji na wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA),tarehe 21Juni 2022, ambapo MUST watakuwa wazalishaji wa mita za maji ambazo zitatumia teknolojia ya kisasa inayomuwezesha mteja kulipia huduma hiyo kabla ya kuitumia (pre paid).
Pia mita hii itaruhusu mteja kulipia kiasi cha maji anachokihitaji, kwa kuanzia na shilingi mia mbili (200).
Katika mkataba huo kwa hatua za awali MUST itatakiwa kuzalisha kiasi cha mita 100 ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya majaribio ( Pilot Study) kwa kipindi cha miezi sita.
Mita hii imebuniwa na wataalam (Wakufunzi na wanafunzi) kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Sensa kwa Maendeleo, jiandae kuhesabiwa.