Kijana wa kiislamu

Ukurasa huu ni kwa ajili ya kuwakumbusha na kuwahamasisha vijana wa kiislamu juu ya kuitambua dini yao.

25/08/2024

Je yafaa kumuoa mwanamke uliyezini nae?

NB: Jibu kwa mujibu wa ushahidi wa Quran na Hadith.

25/08/2024

Ni Surah gani ndani ya Quran ina jumla ya ayah 200?


Kijana wa kiislamu Kijana Wa Kiislamu Kijana wa kiislamu Maulid Bin Swaleh

25/08/2024

Je yafaa kumuoa mwanamke uliyezini nae?

NB: Jibu kwa mujibu wa ushahidi wa Quran na Hadith.


Maulid Bin Swaleh Kijana wa kiislamu Kijana wa kiislamu

04/04/2024

Asalaam alaykum warahmatullahi wabarakatuh. Ndugu yangu katika Imaan, kuelekea sikukuu ya Eid JAI MUHIMBILI imeandaa zoezi la kulisha wagonjwa chakula siku hiyo. Bajeti ni Tsh 7,0860,000/= ambapo ni chakula na vinywaji. Unaweza kutoa mchango wako kufanikisha hili kupitia namba 0676430448 jina JAI MUHIMBILI MEMBERS au kununua vitu k**a Juisi za azam embe ndogo hitajio katon 84 maji lita 1 hitajio katoni 334 nk. Tunaomba ushurikiano wako. Jazakallahu kheir

18/03/2024

Al-Ma'idah 5:91

إِنَّمَا يُرِيدُ ٱلشَّيْطَٰنُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ ٱلْعَدَٰوَةَ وَٱلْبَغْضَآءَ فِى ٱلْخَمْرِ وَٱلْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ ٱللَّهِ وَعَنِ ٱلصَّلَوٰةِۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na k**ari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?

18/03/2024

Al-Ma'idah 5:90

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْخَمْرُ وَٱلْمَيْسِرُ وَٱلْأَنصَابُ وَٱلْأَزْلَٰمُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ ٱلشَّيْطَٰنِ فَٱجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na k**ari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

12/03/2024

Usisahau kutembelea WhatsApp Channel yetu.

whatsapp.com

02/03/2024
27/01/2024

UMRI WA KUNYONYESHA MTOTO NDANI YA QURAN.

Assalam 'alaykum warahmatullahi wabarakatuh

Kila sifa njema anastahiki kupewa Mola wa viumbe wote ambaye ametupa neema ya uhai na afya.

Mwenyezi Mungu ametuambia ndani ya Quran tukufu umri wa kumyonyesha mtoto ndani ya Quran katika aya tofauti tofauti katika
Suratul Baqarah 2:233, Luqmaan 31:14, Al-Ahqaf 46:15 aya zote hizi zinatupa mazingatio makubwa sana ambayo Mwenyezi Mungu anataka tujue alichokusudia ndani ya Quran tukufu.

Madaktari na wataalamu wa afya wanawashauri wazazi/walezi wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili (2) kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika maziwa vinamsaidia kumuongezea virutubisho na kinga ndani ya mwili wa mtoto anayenyonya.

Suratul Baqarah 2:233 na Luqmaan 31:14 ametuambia umri wa kunyonya mtoto ni miaka miwili kamili na Al-Ahqaf 46:15 ametuambia kumwachisha kunyonya ni miezi thelathini (30) ni sawa sawa na miaka miwili na miezi sita.

Mwenyezi Mungu ametushushia aya hizo karne ya saba (7) hapakuwa na wataalamu na vipimo vya kujua virutubisho na kinga ndani ya maziwa ya mama.

Tembelea katika mitandao yetu ya kijamii ifuatayo kupata faida ndani ya Quran

Facebook: Maulid Bin Swaleh

Instagram: Maulid Bin Swaleh

Twitter: Maulid Bin Swaleh

YouTube: Maulid Bin Swaleh

20/08/2022

KULA CHAKULA KWA VIDOLE VITATU

✍️Abdillah Kitota (MMDSC)

Mpendwa msomaji wa makala zetu za uchambuzi wa ishara za kimaumbile kutoka kwa Mola wetu Mlezi Mtukufu, leo hii tunakuletea hii khabari ya kula chakula kwa kutumia mkono; lakini kwa kutumia vidole vitatu.

Katika vitabu mbalimbali vya hadithi; Riyadh As-Swalihin, Sunan Abu Dawud, Mishtak Al-Masabih, Sahih Al-Muslim n.k, zimetufikia hadithi ambazo inabainishwa kwamba, Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alikuwa anakula kwa mkono; lakini kwa kutumia vidole vitatu. Na akimaliza kula anajilamba vidole hivyo [alisema: huwezi jua ni katika sehemu gani ya chakula iliyonata kwenye vidole ina baraka].

Na ametufundisha vilevile tufanye hivyo.

K**a Mola wetu Mlezi Mtukufu alivyoahidi kutufunulia ishara zake; ambazo kimsingi zilibainishwa na Mtume wake wa mwisho Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) kupitia Qur’an na sunnah, tayari vilevile alishatufunulia sehemu ya ishara hii kupitia tiba ya sasa.

Kwamba, kuna ncha za neva [nerve endings] na vipokezi taarifa [receptors] vingi kwenye mkono. Ncha za neva zinazopokea taarifa [sensory nerve endings] zilizopo kwenye vidole zinajumuisha: Meisnner’s corpuscles [mguso hafifu, humudu haraka], Pacinian corpuscles [eneo kubwa la kupokea, linamudu haraka], ncha huru za neva [joto na maumivu], Merkel discs [ubaguzi wa mguso mwepesi wa vitu na mguso], na ncha za Ruffini [zinamudu taratibu, taarifa za nafasi za vidole].

Kwa ujumla, vipokezi hivi vinavyowezesha kuhisi mguso na ubaguzi wa maumbo, mguso, na vitu, vinahusika na hisia za joto na maumivu, na vinatoa taarifa wapi mkono na vidole vipo; katika uhusiano wake na mwili.

Hivyo, kula kwa mkono kunasaidia mmeng’enyo wa chakula kwa namna isiyo ya moja kwa moja: Kupitia kutambua haraka mguso wa chakula, umbile la chakula, joto la chakula, na kutofautisha vilivyomo kwenye chakula [contents]. Hii inachangia taarifa nyingi za awali kuhusu chakula kutumwa kwenye ubongo na ubongo kutoa mrejesho kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Zaidi, kula kwa mkono lakini kwa kutumia vidole vitatu; k**a ilivyokuja kwenye mafundisho hayo ya kiongozi wa umma huu, kunapunguza eneo la uso [surface area] wa kiganja cha mkono linaloshika chakula. Inakuwa ni sehemu ndogo ya kiganja cha mkono inayoshika chakula.

Hii inasaidia kuepusha uwezekano wa kupeleka kinywani na kwenye njia ya mmeng’enyo wa chakula vidubini ambavyo; kimsingi, vinaweza kuwa havikutolewa na maji wakati wa kunawa kabla ya kula. Vidubini hivi vinajumuisha vile ambavyo ni wakazi wa kiganja [residents], na vile ambavyo ni wapita njia [transients]; ambavyo mara nyingi, ndiyo husababisha maambukizi ya njia ya chakula.

Kiganja chote kinabeba vidubini kwa kuwa kinaamiliana na vitu au sehemu mbalimbali za mwili na nje ya mwili [kwenye mazingira]. Maeneo ambayo; kwa kawaida, husahaulika zaidi mara nyingi wakati wa kunawa kabla ya kula, au hunawisho kwa kiwango duni, ni maeneo ya baina ya vidole [baina ya kidole na kidole].

Hivyo, kula chakula kwa vidole vitatu kunapunguza hatari ya maambukizi ya njia ya chakula.

Hata k**a mtu atashindwa kufuata sunnah hii ya kula kwa kutumia vidole vitatu, ni mapendekezo yangu kwamba, ale kwa kutumia vidole pekee, badala ya kutumia kiganja chote.

Haya ndiyo mafundisho ya Uislamu. Dini Tukufu iliyobainisha kila kitu; kwa namna inayomstaajabisha mwanadamu aishiye sasa.

12/05/2022

Ar-Ra'd 13:17

أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌۢ بِقَدَرِهَا فَٱحْتَمَلَ ٱلسَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًاۚ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِى ٱلنَّارِ ٱبْتِغَآءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَٰعٍ زَبَدٌ مِّثْلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْحَقَّ وَٱلْبَٰطِلَۚ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَآءًۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمْكُثُ فِى ٱلْأَرْضِۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْأَمْثَالَ

Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita k**a takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano.

01/05/2022

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi pamoja na Watendaji wake tunawatakia Waislamu wote EID MUBARAK !!!

Nasaha kwa vijana part 4-Sheikh Muhammad Issa 28/04/2022

NASAHA KWA VIJANA PART 4 - SHEIKH MUHAMMAD ISSA

https://youtu.be/8aTBLVYUIZs

Nasaha kwa vijana part 4-Sheikh Muhammad Issa

Nasaha Kwa Vijana part 3-Sheikh Muhammad Issa 28/04/2022

NASAHA KWA VIJANA PART 3 - SHEIKH MUHAMMAD ISSA

https://youtu.be/gSfD9QvBbUM

Nasaha Kwa Vijana part 3-Sheikh Muhammad Issa

Nasaha Kwa Vijana part 2-Sheikh Muhammad Issa 28/04/2022

NASAHA KWA VIJANA PART 2 - SHEIKH MUHAMMAD ISSA

https://youtu.be/my9sfbmF9sM

Nasaha Kwa Vijana part 2-Sheikh Muhammad Issa

Nasaha Kwa Vijana part 1- Sheikh Muhammad Issa 28/04/2022

NASAHA KWA VIJANA PART 1 - SHEIKH MUHAMMAD ISSA

https://youtu.be/SONuio0AAAk

Nasaha Kwa Vijana part 1- Sheikh Muhammad Issa

Photos from Kijana wa kiislamu's post 27/04/2022

JE! HAWAMTAZAMI NGAMIA JINSI ALIVYO MUUMBA?

Na….mchambuzi wako wa masuala ya kimaumbile ndani ya Qur’an na Sunna, Abdillah M***a Kitota, MMDSC., Septemba 12, 2020, saa 2 Asubuhi.

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ

Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? (Surat Al-Ghaashiya, 88:17).

1. MACHO, MAPUA NA MIDOMO

Mapua yao yenye uwazi mwembamba unaoweza kufunga [slit-like closable nostril] huwalinda kutokana na upepo uvumao na hewa ya unyevu isiingie kwenye mapafu. Wakipumulia kwa nje [exhel], unyevu wa maji unanaswa ndani ya mapua yao na unafutwa tena kurudishwa kwenye ndani ya mwili ili kuhifadhi maji.

Midomo yao ya juu yenye mpasuko [split upper lups] huwawezesha kubagua na kuk**ata kwa urahisi majani wakati wanakula. Midomo yao pia ina nyama yenye nywele-nywele inayowawezesha kutafuna miba ya miti ya jangwani.

Masikio yao madogo yaliyofunikwa na nywele nyingi yanawasaidia kuzuia mchanga unaovuma kuingia ndani ya masikio.

Kope zao ndefu huyalinda macho yao kutokana na mionzi mikali ya Jua na mchanga wa jangwani unaovuma.

Pia wana vigubiko vitatu vya macho [eyelids]: vya juu viwili, na cha tatu cha chini [cha ndani] kinachoitwa nictitating membrane. Hivyo viwili vya juu vina kope zinazozuia uchafu na mchanga uvumao usiingie machoni

Hicho cha tatu cha ndani ni chembamba, kina weupe, na kinapitisha mwanga. Wakati mwingine wanaweza wasivifunike hivyo viwili vya juu, wakakifunika hicho kingine cha tatu, huku wakiendelea kutembea.

Unaweza kudhani wanatembea kwenye vumbi huku wamefumba macho na hawaoni, lakini kutokana na wembemba wa hicho kifuniko cha 3, huwa wanaona. Kazi zingine zinazofanywa na kigubiko hiki cha tatu ni kuboresha uoni wao k**a miwani ya lenzi, kuzalisha na kueneza machozi, na kuzalisha dutu za ulinzi, immunoglobulins.

Muhimu zaidi siyo kuyajua maumbile haya pekee, bali muhimu zaidi ni kutafakari uhusiano wake na mazingira ya jangwani wanapoishi. Uhusiano huu unaonesha kwamba, maumbile haya yanawiana moja kwa moja na mazingira ya jangwani wanapoishi.

Hali ambayo vilevile inaonesha kwamba, uhusiano huu usingeliweza kutokea kwa bahati nasibu, bali Yupo Muumbaji aliyewaumba na akawakadiria maumbile haya maalumu kabisa kwa ajili ya maisha ya jangwani.

Kimsingi, kinachobainishwa kwenye aya hii ni hakika ambayo katika Biolojia tunaita adaptations; isomwayo kote duniani katika shule na vyuo vinavyotoa kozi za Biolojia.

Yaani, maumbile ya kianatomia na kifiziolojia ambayo yanamwezesha kiumbe hai husika kumudu kuishi kwenye mazingira anayoishi.

Kila kiumbe hai ameumbwa kwa maumbile maalumu yanayomwezesha kuishi kwenye mazingira yake.

Hii inatuonesha kwamba, mifumo hii maalumu kwa kila kiumbe haijatokea kwa bahati nasibu, bali kuna Muumba Aliyewaumba viumbe hai na kuwawekea mifumo hii.

Tukipanua tafakari yetu zaidi, aya hii inatubainishia kwamba, tunapaswa kuzifahamu hizi adaptations za viumbe tunaoishi nao kwenye mazingira yetu.

Na kuzijua kwetu iwe ni asbab ya kupata mazingatio ya kuwepo, ukubwa na utukufu wa Mola wetu Mlezi (Subhaanahu wata'alah).

26/04/2022

MAZINGATIO YA UDHU [KUTAWADHA]: ISHARA KATIKA TIBA YA SASA

✍️Abdillah Kitota (MMEDSC)

Uislamu ni dini ya kimaumbile. Tumeumbwa kwa mfumo wa Kiislamu. Sharia zote zimewekwa juu ya misingi ya kimaumbile. Zinayasimamia maumbile. Zote zinatoa faida mbili: za kimaumbile [za kiafya] na kiimani. Katika makala ya sasa, zinabainishwa faida za kiafya pekee.

Ishara [tafiti] katika tiba ya sasa zinaonesha kwamba, ngozi inabeba mabilioni ya vidubini [bakteria, virusi, fangasi n.k]. Mathalan, katika kila skwea mita 1 ya ngozi kuna bakteria salama takriban bilioni 11. Ngozi inaweza pia kuwa na vidubini vinavyopita njia [transient microbes]. Kupe na chawa pia wameripotiwa kuwepo.

Mikono, pua, kinywa, uso, sikio na miguu vinaweza kuwa na vidubini vinavyopita njia kwa wingi kwa sababu ni sehemu za ngozi zinazoamiliana sana na mazingira; ambavyo baadhi viwanaweza kusababisha magonjwa ya maambukizi, hususan kwa watu wenye kingamwili dhaifu. Ngozi za sehemu hizi vilevile zinabeba vidubini salama vingi ambavyo vikihamishwa kupelekwa kwenye maeneo mengine ya mwili vinaweza kusababisha maambukizi, hususan kwa watu wenye kingamwili dhaifu.

Aidha, katika kuchukuwa udhu [kutawadha] kwa Waislmu, Sheria ya Kiislamu imeamrisha miguu, mikono, kinywa, uso na pua vioshwe kwa maji, na kichwa na pua vifutwe kwa maji. Mola wetu Mlezi Mtukufu ameamrisha kwamba:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru (Qur’an, 5:6).

Ni Uislamu pekee ndiyo wenye utaratibu huu unaokwenda sambamba na maumbile tuliyoumbiwa. Ufafanuzi wake wa kina tunaupata katika sunnah.

Kitiba, kuoshwa kwa miguu, mikono, kinywa, uso na pua kunapunguza vidubini salama na vidubini vinavyopita njia; ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi. Katika sunnah imefundishwa kwamba kuosha pua ni kwa mtindo wa kupandisha maji puani na kuyapenga. Hii inasaidia kuondoa/kupunguza vidubini salama, vidubini vinavyopita njia na vumbi lililonaswa kwenye k**asi/utelezi wa puani. Ina mchango mkubwa vilevile kwenye kupunguza/kuondoa virus vya COVID-2019 katika hatua zake za awali za maambukizi.

Katika sunnah imefundishwa kuwa kuosha kinywa ni kwa mtindo wa kusukutua [na kwa matumizi ya mis-wak/siwak]. Hapa kuna mazingatio maalumu. Zaidi ya bakteria bilioni 6 wanaishi kinywani: mate pekee yana bakteria takriban bilioni 9, jino moja linaweza kuwa na bakteria 1000-100,000 kwa mtu anayesafisha meno mara kwa mara, na bakteria takriban bilioni 1 kwa mtu asiyesafisha kinywa mara kwa mara. Huu ni mfano mmoja tu; hatujazungumzia kwa vidubini vingine k**a fangasi n.k.

Hivyo, kuosha kinywa [zaidi 5 au zaidi kwa siku] kwa mtindo huo uliokuja katika sunnah kunapunguza kiwango hicho cha bakteria [na vidubini vingine]; ambao wakiachwa wakazaliana zaidi ni sababu ya maradhi ya kinywa ambayo; kwa mujibu wa WHO TECHNICAL INFORMATION NOTE ya 2017, yanaathiri takriban nusu ya watu duniani.

Kufutwa kwa kichwa kunaondoa vumbi, uchafu n.k. Kufutwa kwa masikio nako kuna umaalumu wake; kwa mujibu wa hadithi. Kwenye sikio la nje kuna uchafu unaotokana na seli za sikio zinazokoboka [zinazo kufa na kutoka], na mafuta na dutu zingine zinazoweka hali ya uasidi ya kuua vidubini vinavyopita njia [bakteria, fangasi n.k]. Kwa pamoja, chembe hizi za seli zinazokoboka na vumbi inayoingia sikioni huunda k**a utelezi ndani ya sikio la nje. Utelezi huo hautakiwi kutolewa wote kwa sababu una dutu zinazoua vidubini vinavyopita njia. Badala yake, unatakiwa kupunguzwa tu; ili kutoa vumbi lililonata juu yake na vidubini vilivyouliwa.

Kiujumla, kila sehemu ambayo Waislamu wameamrishwa kuiosha au kuifuta wakati wa kuchukua udhu ni katika sehemu za mwili; ambazo kitiba, zinaitwa portal of entries; sehemu vinapoweza kuingia vidubini vya magonjwa. Hivyo, kuoshwa au kufutwa [mara tano au zaidi kwa siku] kunaondoa hatari [risk] ya kupata maambukizi ya aina mbalimbali.

Zaidi, aya hiyo imetaja pia kuoga janaba ikiwa mtu alishiriki tendo la ndoa.

Baada ya tendo la ndoa, mwili unaweza kuwa na jasho [kwapani na sehemu zingine za mwili], na ute [unaoteleza] kwenye uke na uume. Kimsingi, ute huu unakuwa umetoka ukeni.

Kwa kawaida, ute huu hauna harufu wala rangi. Ukiwa na harufu na rangi [hata k**a ni rangi nyeupe], basi hiyo ni ishara ya maambukizi ukeni.

Vilevile, kemikali za kibiolojia zenye harufu [pheromones]; zinazoathiri tabia na fiziolojia za wote mwanaume na mwanamke wakati wa tendo la ndoa, zinaweza kuwemo kwenye majimaji [secretions] ya aina zote yanayotoka mwilini wakati wa tendo la ndoa. Lakini, tafiti zimejikita zaidi kwenye jasho. Mathalan, jasho la kwapa linaweza kuwa na aina 16 ya kemikali za androstenes. Miongoni mwa hizi, androstadienone inapatikana kwa wingi kwenye jasho la mwanaume, na humvutia mwanamke.

Kwa hiyo, kuoga janaba kwanza kabla ya kuchukua udhu ni ili kuondoa ute na jasho lililosheheni kemikali hizo za kibiolojia zenye harufu. Imeripotiwa katika hadithi kwamba, Mtume Swalla Llaahu ‘alayhi wasallam alikuwa akioga janaba anajimwagia maji mwili mzima: anapitisha vidole vyake kwenye nyewele mpaka ahakikishe maji yamefika kwenye ngozi, kwenye mizizi ya nywele.

Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wenye nyoyo zenye mazingatio.

25/04/2022

TEKNOLOJIA NDANI YA QUR’AN

✍️Abdillah Kitota (MMEDSC)

Teknolojia ni matumizi ya ujuzi wa sayansi; kwa kutumia zana/vitu mbalimbali k**a vile mwanadamu mwenyewe, taarifa, vitu [matirio], mashine, nishati, mtaji na muda, ili kutatua matatizo fulani ya jamii kwa manufaa ya hapa duniani na akhera [tafsiri yangu kwa mujibu wa tafsiri mbalimbali].

Kwa tafsiri hiyo, misingi ya teknolojia ni miwili: ujuzi wa sayansi na kuwepo kwa zana/vitu/malighafi mbalimbali, ambayo yanaweza kutumiwa kupitia ujuzi wa sayansi, ili kupata mahitaji ya maisha yetu.

Ndani ya Qur’an zipo aya za makundi mawili zilizoibainisha teknolojia.

Kundi la kwanza ni zile aya zinazobainisha teknolojia mbalimbali.

Hizi zinajumuisha zile zinazosimulia teknolojia mbalimbali walizopewa umma zilizopita; ikiwemo mitume na waja wema wengine [Qur’an, 7:74, 15:82, 18:93-96, 26:149, 34:10-12, 89:7 & 9 etc.]; ikiwemo ile aya inayobainisha kuteremshwa kwa madini ya chuma [Qur’an, 57:25]; ambayo kimsingi inabainisha pia kuteremshwa kwa madini mengine mazito kutoka kwenye mbingu ya chini [Ulimwenguni].

Kundi la pili ni zile aya zilizoweka msingi na kuonesha mwelekeo wa dunia katika masuala ya kiteknolojia.

Hizi zinajumuisha zile zilizotumia neno la Kiarabu sakhkhara lenye maana ya kukifanya [kukiumba] kwa namna au mfumo ambao kinaweza kutumika kwa mahitaji ya kimaisha baada ya kuchakatwa au kunyumbuliwa [Qur’an, 22:65 & 45:13].

Matumizi ya neno hilo kwenye muktadha wa aya hizo yanatubainishia kwamba, Mola wetu Mlezi Mtukufu ameumba mali asili [natural resources] na mali zilizoundwa na mwanadamu [man-made/artificial resources] katika muundo au mfumo ambao unatuwezesha Sisi kuzichakata au kuzinyambua; kulingana na makadirio ya ujuzi wa sayansi aliyotupa kwa wakati husika, na kupata mahitaji yetu ya maisha ya hapa duniani na akhera.

Kwa hiyo, Qur’an imeweka misingi na imeonesha mwelekeo wa kila jambo; ikiwemo teknolojia mbalimbali tunazoziona au tunazotumia leo hii duniani. Ni juu yetu kujipanga na kuisoma Qur’an kwa vitendo.

Aidha, wazazi wanakumbushwa kuwasomesha Watoto wao masomo haya ya sayansi na teknolojia kwa sababu ni sehemu ya dini. Wala mwanafunzi/mwanachuo asiwe ni mwenye kuacha/kupuuza msomo haya ya sayansi na teknolojia; k**a Mola wetu Mlezi Mtukufu amempa kipawa cha masomo haya, kwa madai kwamba siyo sehemu ya dini.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

An-Nahl 16:15#Itambuediniyako#kijanawakiislamu@followers Kijana wa kiislamuMaulid Bin Swaleh
Al-Ghashiyah 88:17#Itambuediniyako#kijanawakiislamu@followers Maulid Bin Swaleh
Karibu kwenye ukrasa huu tukuhabarishe yanayohusiana na dini ya uislamu.#Itambuediniyako#kijanawakiislamu @followers Mau...

Telephone

Address


Arusha
Other Nonprofit Organizations in Arusha (show all)
School of St Jude School of St Jude
PO Box 11875
Arusha

St Jude's is a charity funded school in Tanzania, EA providing free education to poor bright students

LivLife LivLife
Meserani
Arusha

LivLife supports KCEM - an adult education centre, pre-school and safe, supportive space in Tanzania

Ombeni Nnyari Ombeni Nnyari
Arusha, 1222

Karibu kwenye Ukurasa huu kwajili ya Kujifunza NENO la MUNGU, na kushaurina mambo mbalimbali kuhusu kumtumikia MUNGU.

Ramat Tanzania Ramat Tanzania
Ngaramtoni Ya Chini, Matevesi, Bajuta House
Arusha

UNITE ALL SOCIAL AND ENVIRONMENTAL CONSCIOUS PEOPLE OF TANZANIA

ICMDA World Congress Arusha 2023 ICMDA World Congress Arusha 2023
Arusha International Conference Centre
Arusha

The home of the 17th ICMDA World Congress. Held in Arusha, Tanzania 20-25 June 2023.

Women,youth & Children Org-Woeychisu Women,youth & Children Org-Woeychisu
SANAWARI
Arusha

woychisu-org

Daisies Family Foundation Daisies Family Foundation
Arusha

We are a non-profit organisation that encourages sharing of resources in helping the underprivileged to improve the standard of living in the community.

Drive Change Foundation Drive Change Foundation
Ambureni Street, Sekei Ward P. O. Box 1 Duluti
Arusha

Drive Change Foundation is a non-governmental organization created to help vulnerable children.

Gospel Alive Ministries - Africa Gospel Alive Ministries - Africa
Arusha

The aim of Gospel Alive Ministries is to do just what it says, "Bring the Gospel, the Good News of Jesus Christ ALIVE to people!"

HIHA  Children's  HOME HIHA Children's HOME
Makuyuni/Monduli
Arusha

Hiha Children's home and school is a school which help children from humble/poor background,the orphans, vulnerable, normadic societies, Support us Bank name CRDB Account name H...

Athlantia Football Organization Athlantia Football Organization
Simeon Road
Arusha

Supporting the youth in underprivileged areas in Tanzania & Peru to have the opportunity to fulfill their ultimate dream with a football at their feet.

Tabasamu Africa Tabasamu Africa
Arusha, 14239

Tabasamu Africa is an African Non-governmental organization which provides various social help in Ed