Elimika

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Elimika, Politician, Dar es Salaam.

25/08/2021

DUMISHA AMANI.
Ni vema kuamini kuwa Elimu Ni ujuzi unaosaidia kupambana na shida za jamii K**a rushwa, umaskini, njaa, maradhi, unyonywaji, dhuluma na kupuuzwa; kuliko kuifanya elimu kuwa daraja la kupandia ngazi kuyaendea maisha mazuri haya K**a Ni kwa kuumiza wengine na kuwaacha ndugu, jamaa na jamii wakibaki na shida zao zilezile.

Tanzania tunawasomi wengi kwa sasa,hii inaonesha jinsi gani watu wameelimika kwa kiasi kikubwa sana. Taifa kuwa na wasomi wengi huwa inasaidia sana hasa katika upande wa kuleta maendeleo kweny jamii zetu. Elimu ilitumika kuikomboa jamii karne zilizopita.

Mbali na kuwa na wasomi wengi kwenye Taifa hili,wapo wasomi ambao wana influence kubwa kwenye jamii na wanatumia fursa hiyo katika kuipotosha jamii. Migogoro na kampeni nyingi zinazoendelea kwa sasa zinaongozwa na kuendeshwa na watu wachache ambao ni wasomi na wana influence kubwa kwenye jamii.

“Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii”-Mwalimu nyerere. Amani tuliyonayo Tanzania inatakiwa tuidumishe kwa nyakati zote. Nchi nyingi kwa sasa zimekosa amani hii ambayo tunayo kutokana na watu wachache wenye uchu na madaraka. Watanzani siyo walemavu wa fikra,tunajua na tutaidumisha amani yetu.
Serikali imekuwa ikihubiri suala la amani sikuzote,tutoe support kwa serikali yetu na tuache kuwafata watu ambao wapo kwa maslahi yao na uchu wa madaraka. Watanzania tunataka amani🇹🇿🇹🇿Mungu ibariki Tanzania,wabariki viongozi wake.

25/08/2021

Serikali inayojali na kuthamini watu wake, aina hii ya serikali huwa ni faraja kwa raia wake. Jamii inakumbwa na changamoto nyingi sana zinazohusu mtu mmoja mmoja lakini pia jamii kwa ujumla. Serikali pamoja na viongozi wa Dini huwa ni wafariji wakubwa kwa jamii.

Abrahamu Lincoln (Rais wa 16 wa nchi ya Marekani) aliwahi kusema "Serikali ya watu, inayowatumikia watu na iliyowekwa na watu haitapotea duniani". Sikuzote serikali inayochukua nafasi kuwa mfariji wa watu wake basi serikali ya namna hii haitoweza kupotea kamwe.

LESSONS : Serikali pamoja na viongozi wetu wanatakiwa kuwa wafariji wa wananchi wao. Matumaini ya Raia ni kwa serikali, sisi k**a wanachi tunawatizama viongozi wetu k**a kioo. M/mungu azidi kuwakumbusha viongozi wetu katika kulitumikia Taifa hili.

Photos from Elimika's post 24/08/2021

VIONGOZI WAZALENDO KATIKA HISTORIA YA TANZANIA.

Unapokumbuka juu ya viongozi wazalendo na wa kupigiwa mfano nchini lazima umtaje Sheik Abeid Amani Karume. Huyu alikubali kwa ujasiri mkubwa kuungana na Tanganyika na kuzaa Tanzania.

Busara ilimtuma mapema kabisa kujua kuwa we are stronger together.

Angekuwa na uroho wa madaraka asingekubali ku compromise sovereignty ya Zanzibar.

Mzee huyu ni k**a zege iliyotumika kujengea msingi wa taifa.

Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliitumikia nchi kwa uzalendo wa hali ya juu huku akikubali kushushwa na kupanda ndani ya Serikali ya Mwalimu. Ni mmoja wa waasisi wa taifa hili k**a tu walivyo akina John Adams Rais wa pili wa Marekani. Mzee Kawawa Ali sacrifice mengi kufanikisha ujenzi wa Tanzania.
This soft spoken hero hatosahaulika katika historia yetu.

Bibi T**i Mohamed ni mama shupavu kabisa ambaye mchango wake katika ujenzi wa taifa utakubukwa milele.

Alihatarisha sana maisha kwa kuwa Tanu active member na outspoken critic wa Waingereza. Sina hakika k**a huyu mama ameenziwa vya kutosha. Nadhani kupewa barabara tu haitoshi. Mama Maria Nyerere ana nafasi kubwa sana katika historia ya Tanzania. Tumuenzi daima mama yetu huyu.

Mzee Salim Ahmed Salim naye ni hero on his own right. Sintowasahau akina Sykes na Mzee Rupia ambaye tunaambiwa alikuwa akiichangia Tanu fedha na hivyo kugombana na wakoloni.

Ali sacrifice biashara zake and that makes him a hero.
Mzalendo maarufu mwingine ni Edward Sokoine. Alipambana na mafisadi hadi tone la mwisho. Hata alipokuwa anazungumzia mapambano dhidi ya rushwa unaona kabisa inatoka moyoni.
Mzee Augustine Mrema ni kiongozi mwenye unquestionably uzalendo. Alionesha njia akiwa Home Affairs. The rest is history.

Mzee Sitta alionesha uzalendo wa hali ya juu alipokuwa akiongoza Bunge kati ya mwaka 2005 na 2010 na baadae Bunge la Katiba mwaka 2014. Ni mmoja wa wazee walioipenda nchi yetu kwa dhati kabisa.

Bila shaka mzalendo namba moja atabaki kuwa Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE. RIP.

Photos from Elimika's post 24/08/2021

FIKRA.

“Ni bora kuishi na fikra hai kuliko kuishi na fikra zilizokufa"-Mwalimu Nyerere. Hamna utajiri wenye thamani k**a utajiri wa Fikra na hamna umasikini wenye kutisha k**a umasikini wa Fikra. Ni vyema kwa sasa Tuliombee Taifa ili liwe na watu wenye fikra zilizo Hai.

Viongozi wetu ndiyo kioo cha maendeleo yetu. Wanapokuwa na Fikra zilizokufa,basi Taifa hili haliwezi kuendelea.Lakini Taifa hili likiwa na viongozi wenye Fikra zilizohai,tutafanikiwa kwa kaisi kikubwa sana.

Tuwaombee viongozi wetu ili wawe na Fikra zilizo Hai🇹🇿🇹🇿🙏

24/08/2021

PROPAGANDA.

Maranyingi nimekuwa mpenzi wa nukuu mbalimbali za watu mashuhuri na viongozi waliopita. Kutokana na Taifa kuwa katika hali ya kupambana juu ya ugonjwa wa COVID_19 basi yatupasa kusaidiana na viongozi wetu katika kupambana na janga hili.

Kwenye jambo la wengi huwa kuna mengi pia. Kutofautiana kimawazo huwa ni jambo la kawaida sana “ different Ideology “. Lakini inapofikia hatua viongozi kutofautiana kimtazamo na kupeleka tofauti zao kwenye media na social network, watakuwa hawapo sahihi.

“Itakuwa ni kosa na haina umuhimu kudhani kuwa ni lazima tusubiri hadi viongozi wafariki kabla ya kuanza kuwakosoa”-Mwalimu Nyerere. Moja ya kazi za kiongozi ni kuleta matumaini juu ya wanachi wake lakini kwa sasa hii imekuwa tofauti, viongozi wetu wamekuwa ndiyo chanzo cha kuleta hofu na mtazamo hasi kwenye jamii.

SOLUTION: viongozi waache kuonesha tofauti zao kwenye media na social network. Zipo k**ati mbalimbali ambazo hutumika katika kuboresha maadili ya viongozi wetu, zitumike k**ati hizo. Kutofautiana na kuhitilafiana ni jambo la kawaida ,zipo sehemu maalumu za kwenda kusemea mambo haya.

Mungu ibariki Tanzania na pia wabariki viongozi wake🇹🇿.

23/08/2021

“Unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda fulani na baadhi ya watu wakati wote ila huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote"-Nelson Mandela.

TANZANIA; Taifa lililokuwa na Amani miongoni mwa mataifa machache yaliyokuwa na amani Duniani. Katika vitu siwezi kujutia ni kuwa Mtanzania. Kila nikiangalia namna ambavyo mataifa mengine yanavyohangaika juu ya Demokrasia yao, nabakia kushukuru kuwa Mtanzania na mzalendo wa nchi yangu.

Watanzania tunaheshimu na kuthamini katiba ya nchi yetu ambayo imetoa mamlaka katika uundwaji wa Serikali yetu. Sera na mikakati ya chama tawala ndiyo iliyotufikisha hapa kwa miaka yote hiyo toka mwaka 1961. Pongezi nyingi kwa viongozi wetu wa CCM pamoja na serikali kwa ujumla.

Mbali na kutoa sifa kwa chama tawala na serikali kwa ujumla, lakini pia ni muhimu kuonesha wapi k**a taifa tunatakiwa kuwa napo makini. Kitu pekee kitakachoweza kufikisha malengo yaliyowekwa toka uhuru wa nchi hii mpaka sasa ni UONGOZI BORA & IMARA.

Uongozi bora na imara ndiyo chachu ya maendeleo ya Taifa hili. Hatuwezi kusonga mbele bila kupata viongozi watakaojali maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.Serikali inahitaji kuwa na viongozi wenye maono na mikakati katika kutatua kero na kuleta maendeleo ndani ya Taifa hili.

WITO; siku zote wito wangu ni kwa viongozi wenye dhamana ya kulisimamia Taifa hili. Tunawaamini kwa 100% katika kutufikisha pale ambapo tunapahitaji. Matarajio yetu sisi k**a wananchi ni kuona viongozi tuliowapa dhamana wanatekeleza kile ambacho kitaleta faida kwa Taifa la Tanzania.

Photos from Elimika's post 23/08/2021

“Kutokana na umri mkubwa wa chama chetu cha CCM, watu wengi wenye kasoro wamejiingiza kwenye chama hichi. Sasa kimekuwa k**a dodoki ambalo linabeba vitu visafi na vichafu. Sasa tumekuwa na watu wa ajabu sana ndani ya chama chetu”-Mwalimu Nyerere.

Kutokana na serikali ya Tanzania kuwa imara na yenye kuendeleza mengi mazuri chini ya sera na ilani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ). Bado zipo changamoto kadhaa ambazo zinaleta dosari juu ya chama hichi kikongwe Afrika.

CCM ni chama imara na chenye nguvu kubwa ya ushawishi kutokana na misingi iliyojiwekea toka 1995.Watanzania bado wanaimani kubwa juu ya maendeleo yao kupitia chama hichi.

CHANGAMOTO: Kitu pekee kinachopelekea Taaisis yeyote Duniani kuanguka au kupata mafanikio huwa ni “uongozi”. Tunapokuwa na viongozi wenye msimamo na wanafanya kazi k**a “Team work” matokeo yake huwa ni makubwa sana juu ya maendeleo ya wananchi.

Tunapokuwa na viongozi ambao wanashindwa kuziibua changamoto za wananchi katika jamii na kisha kuzitatua,hapa lazima kuwe na itilafu. Tunapokuwa na Viongozi ambao wanashindwa kuelewa jamii inataka nini kwa wakati stahiki,lazima tufeli. Tunapowapa dhamana watu wanaoshindwa kuleta tumaini juu ya wanachi bali wao wanakuwa ndiyo sababu ya kwanza ya kuondoa tumaini na kuleta hofu kwa Raia,lazima tufeli.

SOLUTION: viongozi wafanye kazi Kwa kushirikiana kwa pamoja k**a team. Kuondoa tofauti baina ya viongozi ni muhimu sana. Waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi basi wafanye kwa umoja na mshik**ano. Viongozi wanatakiwa kukaa mbali na media na social network kwa sasa. Viongozi wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi. Lakini pia, ukipewa majukumu ya kuteuliwa au nafasi ya uongozi na ukaona hautoiweza basi ni vizuri kuwa muwazi ili nafasi hiyo apatiwe yule ambaye anaiweza kuifanya.

Tumsaidie Mama katika Ujenzi wa Taifa hili.

23/08/2021

"Siasa Hazikuja kwa lengo la Kuleta Uhasama bali kukuza demokrasia katika nchi"

Rais Mstaafu wa awamu ya 2 Mzee Ally Hassani Mwinyi katika mahojiano maalumu na TBC 2016 kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania.
SIASA siyo vita wala mchezo mchafu bali siasa ni maisha ambapo jamii hunufaika nayo. Mchakato wa kupambana ili kuwapata viongozi ambao watakuwa ndiyo chachu ya maendeleo ya Taifa huamuliwa na Wananchi, wakati wa upigaji kura.
Mchakato wa kupiga kura unapoisha na wananchi kuamua ni aina gani ya viongozi wanaowahitaji, kinachobakia ni kupewa mamlaka wale walioshinda au kuchaguliwa ili waongoze jamii. Kutoa support na ushirikiano kwa viongozi wateule ni haki na wajibu wa kila Mtanzania.

TUJIPIME: siasa siyo vita wala ugomvi na kuwa mpinzani siyo kupinga kila kitu, tusiufanye mwamvuli wa upinzani kupinga juhudi na jitihada za serikali yetu katika ujenzi wa Taifa na Maendeleo ya Wananchi.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Dar Es Salaam
Other Politicians in Dar es Salaam (show all)
Faustine Ndugulile Faustine Ndugulile
Dar Es Salaam

My thoughts. My views. My ideas

Demokrasia ya Kweli Demokrasia ya Kweli
Magole
Dar Es Salaam, KKKKKK

Ukweli na Uwazi

Ulinzi na usalama Ulinzi na usalama
Dar Es Salaam

Mshauri Serikali Mshauri Serikali
Lumumba
Dar Es Salaam, 11108

Sio Akaunti Rasmi ya Serikali ya Tanzania. TikTok | Insta & YouTube @MshauriSerikali

UVCCM TAWI La Airport UVCCM TAWI La Airport
JNA Airport
Dar Es Salaam

Vijana ni walinzi wa chama, jukumu letu kutetea maslai ya chama chetu, kidumu chama cha mapinduzi

Samia Suluhu Hassan page Samia Suluhu Hassan page
State House
Dar Es Salaam

Samia Suluhu Hassan (born 27 January 1960) is a Tanzanian politician and the designated President Of

Dedan Chacha Wangwe Dedan Chacha Wangwe
Segerea, Ilala
Dar Es Salaam, 011

A Jurist + Political & Human rights Activist + Founder: @MTCAssociation + CHASO-DSM City Co-ordinator

Omary Adamu Omary Adamu
Boko
Dar Es Salaam

Ommy mbishi!

Goodluck Kapyela Goodluck Kapyela
Dar Es Salaam, 0255

This page describes workshops, trainings undertaken by Goodluck Kapyela in achieving millenium natio

DEe Pompy DEe Pompy
Dar Es Salaam

Alanus Bitesigirwe Alanus Bitesigirwe
Dar Es Salaam

#Tanzania for#ever