Soka Viwanjani

Follow page hii kwa habari za michezo za Soka.

28/09/2022

Chelsea wana kipengele cha kumnunua tena Tammy Abraham kwa Euro milioni 80 ambacho kitaanza kutumika majira ya joto. Imeelezwa Chelsea wanamtaka tena Abraham.

Lakini Tammy ana furaha akiwa Roma chini ya Jose Mourinho.

💥

28/09/2022

Lakini jamaa ameondoka akiwa staa. Nchi nzima imeimba jina lake. Alikuja Simba account yake ikiwa na followers 8,000. Kufkia leo amekuwa na followers 71.3k na idadi inazidi kuongezeka.. hii inaonyesha jamaa alikuwa anafatiliwa sana.

Kila la heri mzungu. Ila Yanga wanaweza kumchukua January 😅

💥

28/09/2022

Wilfried Zaha ameamua kuwekeza katika nchi yake kwa kununua klabu ya soka! Amenunua klabu ya Espoir Club d'Abengourou, inayocheza ligi daraja la 4.

Zaha pia ana academy ya soka nchini kwao Ivory Coast 🇨🇮

💥

28/09/2022

Mshambuliaji wa Simba, Dejan amethibitisha kwa kuvunjwa mkataba baina yake na Simba Sc. Dejan ameandika:

"Ninathibitisha kwamba mkataba wangu wa ajira umesitishwa kwa sababu za haki kutokana na ukiukwaji wa kimsingi wa mkataba na klabu.

Asanteni mashabiki kwa support na upendo mlionipa"

Mlete mzungu si mchezaji wa Simba Tena ❌

💥

28/09/2022

2002 fainali za Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Brazil iliwekwa k**ari matata sana, huku German wakijivunia golikipa wao mashuhuri kwelikweli Oliver Kahn na huku Brazil wakijivunia mshambuliaji wao hatari kabisa Ronaldo De Lima.

Ikawa ni majivuno kati ya Oliver Kahn na Ronaldo De Lima. Kahn aliapa kamwe hatafungwa na Ronaldo katika fainali ni bora afungwe na mchezaji mwingine lakini sio Ronaldo. Ronaldo nae aliapia kuwa atamfunga Kahn kuanzia mabao mawili na kuendelea na k**a atafunga bao moja Basi atatoa nyumba zake na magari yake yoote ya kifahari kwa Oliver Kahn.

Kufkia mapumziko ubao unasoma 0-0 wachezaji wa Ujerumani walipongezana kwa kumdhibiti Ronaldo. Hakupiga shuti hata moja. Kipindi cha pili kilianza mpaka kufkia dakika ya 60 hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Hapo Kahn akaanza kejeli "zimebaki dk 30 tu unipe Mali zangu" Ronaldo akajibu "Mpira unaingia wavuni kwa sekunde moja tu, nna sekunde zaidi ya 1800"

Ikawa dakika ya 67, Ronaldo akafunga bao kali. Oliver Kahn alipiga kelele kwa mabeki zake kumuachia nafasi mshambuliaji k**a Ronaldo kupiga anavyotaka. Haikutosha dakika ya 79 Ronaldo anaingia tena kambani baada ya Rivaldo kuuacha mpira umpite tobo ndani ya 18 akijua wazi utamfkia Ronaldo ambae nae bila kujiuliza aliutungua kisawasawa ukazama wavuni, ubao ukasomeka 0-2. Oliver Kahn alilala baada ya bao la pili alilia sana. Baada ya mechi kuisha alisema:

"Dunia ina wachezaji lakini Ronaldo ni Dunia nyingine". Watu wengi waliipa ushindi German kutokana na ubora wa Oliver Kahn ambae alipewa jina na kuitwa kipa wa Dunia haikua easy kumfunga. Lakini alisarenda kwa Ronaldo De Lima.

Kuna magolikipa wengine wengi tu huwa wanakataa kufungwa na flani. Gigi Buffon robo fainali ya Uefa 2017 kati ya Juventus na Monaco alisema anaheshimu uwepo wa kinda Kylian Mbappe lakini kumfunga hawezi. Dakika ya 69 Mbappe anamfunga Buffon na Buffon anaenda kumbusu Mbappe kichwani kukubali japo Monaco walitolewa kwa agg ya 4-1.

Follow: Soka Viwanjani 💥

28/09/2022

Messi akiwa Argentina mwaka huu:

vs. Venezuela ⚽️
vs. Ecuador ❌
vs. Italy ❌
vs. Estonia ⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️
vs. Honduras ⚽️⚽️
vs. Jamaica ⚽️⚽️

Mechi 6 mabao 10

💥

28/09/2022

Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni ameongezewa mkataba mpya na Shirikisho la Soka Argentina mpaka June 2026.

"Najivunia kutangaza kuwa tumefikia makubaliano na Scaloni mpaka Kombe la Dunia la 2026" Rais wa AFA, Tapia

Scaloni kaiongoza Argentina tangu 2019 kwa michezo 35 bila kupoteza.

💥

Photos from Soka Viwanjani's post 28/09/2022

Wakati mechi kati ya Brazil na Tunisia ikiendelea hapo Jana, baadhi ya mashabiki walitupa ndizi uwanjani kumwelekea Richarlson:

"Hawa watu wanapaswa kuadhibiwa sio tu kuleta bla bla" Richarlson

Brazil waliibuka na ushindi wa bao 5-1 .

💥

27/09/2022

Mnamo Septemba 2016, Roma ilifungwa 2-1 dhidi ya Sampdoria na mechi ilisimamishwa kwa saa moja kutokana na mvua kubwa. Wachezaji wote, makocha na mabenchi ya ufundi wa timu zote mbili wakakimbilia vyumbani kujilinda na mvua isipokuwa Totti ambaye aliendelea kupasha pembeni ya uwanja.

Mchezo ulirudi nyuma na Totti akarudi. Kisha akatoa pasi ya uhakika kwenye bao la kusawazisha la Roma (2-2) kabla ya dakika ya mwisho kufunga bao la ushindi la Roma ambalo walishinda 3-2 👏

Francesco Totti, kiitaliano wanaita "Franshesco" Totti leo anatimiza miaka 47.

💥

27/09/2022

Leandro Paredes juu ya uhusiano wake na Kylian Mbappé:

"Mimi sio mtu wa kuzungumza juu yake. Nilikuwa na uhusiano na wale ambao nilikuwa na uhusiano nao. Lakini wale ambao sikuwa na uhusiano nao, siwezi kukuambia juu yao ". Paredes

Fabrizio Romano

💥

27/09/2022

Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino anakaribia kuachana na Liverpool, Barcelona wakihusishwa kumsajili, Fc Porto na Juventus.

Source: Mirror

💥

26/09/2022

Beki wa Barcelona Ronald Araújo ameamua kufanyiwa upasuaji wa paja lake la mguu wa kulia na atakuwa nje kwa muda wa miezi 2-3, akikosa Kombe la Dunia.

💥

26/09/2022

Ernesto Varvelde alipoteza mechi 7 tu za ligi kuu Hispania akiwa kocha wa Barcelona. Mechi hizo 7 ni ndani ya misimu mitatu tu. Mechi 114 alipoteza 7 tu.

💥

25/09/2022

Shakira ametoa ya moyoni alivyojitoa kwa Gerald Piqué:

"Tulipoanza mapenzi yetu, ilikuwa mmoja wetu alazimike kujitolea, ama yeye angesimamisha mkataba wake na Barcelona na kuhamia Marekani kuishi na mimi ambako kazi yangu iko au ningelazimika mimi kutoka Marekani na kwenda Hispania ili kumsapoti katika kazi yake.

Kufanya hivyo niliweka maisha yangu katika gia ya pili na nilikuja Uhispania, kumuunga mkono ili aweze kucheza mpira akiwa na amani kujua kwamba mkewe nipo pamoja nae ili atulie na kushinda mataji"

Marca

💥

25/09/2022

Danieli anasema Messi na Ronaldo wangecheza kipindi cha kina Ronaldo De Lima, Ronaldinho Gaucho na Zinedine Zidane basi Messi na Ronaldo wangekuwa wachezaji wakawaida Sana. Mtazamo wake lakini.

Je, kiuhalisia mwanasoka we unaonaje? Ni kweli alichosema mzee Dani?

Zidane alikuwa ni kiungo mshambuliaji akizichezea klabu za Bordeaux, Cannes, Real Madrid na Juventus. Ngazi ya vilabu alicheza mechi 506 na kufunga mabao 95 katika mechi zake zote. Timu ya Taifa Ufaransa alicheza mechi 108 na kufunga mabao 31. Jumla mechi 614 mabao 126. Mshindi Mara moja wa Kombe la Dunia 1998. Alishinda tuzo ya FIFA mchezaji bora mara 3, tuzo ya Balon D'or mara 1 na alipewa mpira wa dhahabu baada ya fainali ya WC 2006 ambayo alitangaza kustaafu.

Ronaldo De Lima alikuwa ni mshambuliaji akizichezea klabu za Cruizero, PSV, Barcelona, Inter Milan, Real Madrid, Ac Milan na Corinthians. Ngazi ya vilabu alicheza mechi 384 na kufunga mabao 280. Timu ya Taifa ya Brazil alicheza mechi 98 na kufunga mabao 62. Jumla mechi 482 na kufunga mabao 342. Mshindi mara mbili wa Kombe la Dunia 1994 na 2002. Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA Mara 3, tuzo ya Balon D'or mara 2 nae pia alipewa mpira wa dhahabu.

Ronaldinho Gauchó alikuwa ni kiungo mshambuliaji na kuna wakati alicheza K**a winga. Akizichezea klabu za Gremio, PSG, Barcelona, Ac Milan, Flamengo, Atletico Mineiro na Fluminense. Kwa vilabu alicheza mechi 511 na kufunga mabao 205. Brazil alicheza mechi 97 na kufunga mabao 33. Jumla mechi 608 na kufunga mabao 238. Mshindi wa kombe la Dunia mara 1 fainali za 2002. Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mara mbili na Ballon D'or Mara 1.

Kiukweli katika wachezaji waliojaaliwa vipaji hawa majamaa walikua na vipaji, nguvu na akili. Kikubwa ambacho kinawatofautisha na kina Messi na Ronaldo ni kwamba wao wameshinda taji la Kombe la Dunia. Lakini pia kusema Messi na Ronaldo wangecheza enzi za hawa Basi wasingeonekana sio kweli. Kuna wakati hata hao wachezaji wa zamani wanawaelezea Cristiano na Messi kuwa ni moja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea Duniani.

Ni kwamba mambo ya soka hayajawahi kuisha. Hizi ni zama tu. Kulikuwepo na zama za kina Pelé, Maradona, Johan Cryuif, Zidane, Ronaldo, Ronaldinho. Hizo zama sio kwamba wao walikuwa wanacheza peke yao kulikuwa na wakali wenzao vilevile Sasa hao wakali wenzao hawakufkia uwezo wa hao wengine ndo mana walionekana wao ni bora kuliko wengine.

Tuje zama zetu za sasa za Messi na Ronaldo. Je wanacheza peke yao? Hakuna wakali wengine waliokuwa nao pamoja? Unataka kusema Luis Suarez, Ibrahimovic, Lewandowski, Cavani, Aguero na wengine ambao wamecheza na kina Cristiano je hawana ubora? Lakini kwanini wazungumziwe wawili tu? Ni kwasababu wao ni bora kuliko hao wengine. Hivyo ndivyo ilikuwa hata zama za kina Zidane.

Leo hawa watu wawili wanaelekea ukingoni japo hawaonyeshi dalili za kustaafu leo Wala kesho ila kadiri siku zinavyoenda wakati wao unaisha na unakuja wakati wa watu wengine. Zama za kina Haaland, Mbappe, Vini Jr ndo hizi tulizo. Leo hii Manchester City imekuwa timu bora ni zama Kuna wakati hata Derby Country ilikuwa bora pia ilikuwa Ni zama. Lakini zama za Messi na Cristiano hakuna kizazi kitafkia kwa mpaka hapa. Labda uko mbeleni. Ila kwa sasa zama za hawa majamaa ni UNTOUCHABLE.

Tuwaheshimu hawa majamaa. Usiseme wangekuwa enzi za kina Zidane wasingeonekana K**a ni hivyo ukubali pia kuwa hata Zidane, Ronaldo na Ronaldinho wangekuepo enzi za kina Pelé wasingeonekana. Yah hiyo ndo tafsiri yake. Sisi hawa tumewashuhudia bila kuambiwa hivyo si vyema kuwalinganisha na waliopita. Huwezi kumfananisha Cristiano na Haaland HAIWEZEKANI. Kuishi tu bila majeruhi mengi ni sifa ambayo Messi na Cristiano wameimudu. Ni wachezaji wasio wa hasara katika timu. Wanastahili kila heshima ✊

Follow: Soka Viwanjani

💥

24/09/2022

Richarlison anathibitisha kwamba Chelsea walitoa ofa ya kumsajili:

"Ndiyo, najua Chelsea walitoa ofa msimu wa joto... na ninaamini Arsenal waliwasiliana na Everton kuuliza kuhusu hali yangu, lakini unajua Spurs walikuja na kulipa ada? Ni rahisi k**a hivyo," aliiambia Standardsport.

💥

24/09/2022

Baada ya kuonekana timu ya Taifa Uingereza ina ukame wa mabao, mchezaji wa timu hiyo Declan Rice amesema:

"Nimeona kwenye mazoezi, tunafunga mabao kwa kujifurahisha. Niniamini, tutakuwa wazuri tu" Rice

💥

24/09/2022

Messi kuhusu maisha yake mapya akiwa PSG:

"Najisikia vizuri, ninahisi tofauti na mwaka jana. Nilijua itakuwa hivi, niko vizuri zaidi na klabu, chumba cha kubadilishia nguo, wachezaji wenzangu. Najisikia vizuri sana na hivyo naanza kuwa na furaha tena".

💥

23/09/2022

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid ambae amejiunga na Sevilla, Fransisco Alarcon maarufu K**a Isco ameelezea namna alivyo na furaha kuwepo Sevilla:

"Sikutaka kujiuliza ni wapi niende kwa sababu ni vilabu vingi vilinihitaji lakini niliamua kubaki nyumbani. Sevilla ni klabu kubwa na nzuri. Wachezaji waana ari na hamasa ya kupambana hicho kimenivutia Sana" Isco

💥

23/09/2022

Kocha wa klabu ya Vipers SC ya Uganda, Mbrazil Robertinho Oliviera anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Zoran kuinoa timu ya Simba Sc. Olivieira ambaye amekuwa kocha bora wa mwezi kwa miezi sita kwenye ligi kuu ya Uganda anataka kuja na msaidizi wake toka Ureno.

Licha ya Simba kutopoteza katika mechi zake tatu ambazo kocha Juma Mgunda ameongoza bado klabu inataka kujiweka imara zaidi kwa kuajiri kocha mpya. Unadhani ni sahihi kutafuta kocha mpya kwa Sasa? Ikiwa aliepo ameshinda mechi zake 3 zote tena kwa cleansh*t? Tetesi huenda zikawa kweli au la.

Lakini K**a ni kweli tujiulize kwanini Tanzania hatuwezi kuwapa nafasi wazawa? Hatuwaamini kabisa Yani. Tupo tayari kumwajiri kocha toka Zambia, Kenya Ila sio Tanzania. Hatuwaamini ila mgeni akija akicheza mechi 3 akapoteza moja akashinda mbili anaaminiwa bado. Tubadilike 😅

💥

23/09/2022

Mchezaji wa zamani wa Flames Esau Kanyenda anaandika:

"Tunahitaji kuwekeza sana ikiwa tunataka kufanya vizuri zaidi katika mashindano haya ya kimataifa.

Hebu fikiria timu ambayo Nyasa Big Bullets ilikuwa ikicheza nayo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (Simba Sc) ina wadhamini zaidi ya wanane na ina wachezaji kumi na wawili wa kigeni...

Pape Sacko (Senegal)
Peter Banda (Malawi)
Chama (Zambia)
Josh Onyango (Kenya)
Enock Enonga (Kongo)
Phiri (Zambia)
Dejanorvic (Serbia)
Okwa (Nigeria)
Okra (Ghana)
Kanoute (Mali)
Outtara (Ivory Coast)
Akpan (Nigeria)

Big Bullets sio ya kushindwa, tatizo pekee ni kwamba makampuni hayako wazi katika kufadhili klabu zetu za ndani ili zifanane na baadhi ya klabu hizi za kimataifa.

Cheki pesa ambazo TNM (Wadhamini wa Ligi kuu ya Malawi) wanaingiza kwenye ligi yetu ya wasomi na ulinganishe na nchi jirani...Utapata majibu zaidi ya maswali. Kwahiyo kutolewa kwa Big Bullets asitafutwe mchawi nani, wenzetu wametuacha mbali. Ligi yao inathamani kubwa Sana kuliko yetu bado kuna Yanga, Kuna Azam timu zote hizo zina wadhamini wa maana. Tuondoke hapa tulipo tuige wenzetu" alimalizia.

💥

23/09/2022

Wachezaji 15 wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania walituma ujumbe kupitia email kwa FA ya Uhispania wakisema wanajiuzulu kwa sababu Jorge Vilda bado ni kocha.

FA ya Uhispania ilijibu kwamba haitawaruhusu wachezaji kuwashinikiza kufanya maamuzi ya ukocha na hawatawaita wale ambao hawataki kucheza. Au yule anaeona hawezi kuendelea kwasababu Jorge Vilda ni kocha basi aondoke kwenye timu.

💥

22/09/2022

De Bryune amechoka kucheza na Wales😅:

"Nadhani nusu ya mechi zangu nimecheza dhidi yao. Mechi 12 karibia nimecheza dhidi ya Wales. Sipendi hii hali kukutana na timu ile ile kila wakati" Kelvin De Bryune, leo.

💥

22/09/2022

Borussia Dortmund sasa wameongeza thamani ya mchezaji wao Jude Bellingham kutoka Euro milioni 35 mpaka Euro milioni 150.

Wiki iliyopita baada ya mchezo kati ya Borussia Dortmund na Manchester City, Pep Guradiola alisema Jude ni mchezaji mzuri ana uwezo mkubwa kwa sasa kuliko wachezaji wengine wa Dortmund.

Huenda kauli ya Pep ndo imewafanya Borussia Dortmund kujiongeza na kuona kauli ya Pep k**a kocha mkubwa Duniani inafaa waitumie k**a fursa 😅. Walimuuza Haaland kwa Pound 58 milioni tu. Hivyo kwa Jude hawataki kucheza na pesa.

Via The Athletic

💥

22/09/2022

Beki wa zamani wa Juventus, Chiellin amemkingia kifua beki mwenzake anaekipiga Manchester United Hary Maguire:

"Nina huzuni kwa hali ya Maguire kwa sababu ni mchezaji mzuri. Wanahitaji mengi mno kwake. Kwa sababu tu walimnunua kwa Pauni 80M Basi ndo lazima awe bora zaidi ulimwenguni kila mechi? Sio sawa" Chiellin

Via ESPN UK

💥

21/09/2022

Messi ametoa asisti 5 kwa Mbappé na asisti 3 kwa Neymar msimu huu.

Neymar ametoa asisti 3 kwa Mbappé na asisti 2 kwa Messi msimu huu.

Mbappé ametoa asisti 0 kwa Neymar na asisti 0 kwa Messi msimu huu.

💥

21/09/2022

Kocha wa Mexico Tata Martino amethibitisha Chicharito na Carlos Vela hawatashiriki Kombe la Dunia.

Vela hapo awali alijiondoa, na kocha anaenda na ‘washambuliaji wengine’ badala ya Chicharito 🇲🇽

💥

20/09/2022

RASMI: Urusi haitashiriki mechi za kufuzu kwa Euro 2024 huku taifa hilo likipigwa marufuku kushiriki mashindano ya UEFA kufuatia uvamizi wake wa kijeshi nchini Ukraine.

💥

20/09/2022

RASMI! Miezi 4 tu baada ya kurejea Uruguay, Luis Suarez tayari ataondoka klabu yake ya Nacional! 🇺🇾

Anaweza kurudi Ulaya baada ya Kombe la Dunia 🔥

💥

20/09/2022

Admin wa Augusburg 😅

💥

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

😅 haya ndiyo yanayokuwa yakiendelea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Watizame Pep Guardiola na Jóse Mourinho wakiwa ...

Category

Website

Address


Zambezi
Dar Es Salaam
Other Sports in Dar es Salaam (show all)
Msukuma Msukuma
0753875919
Dar Es Salaam, MUME

Daud Obogo Platform Daud Obogo Platform
Ilala
Dar Es Salaam, 765432

Simba sport big team

Mbogella sport Mbogella sport
Kyela
Dar Es Salaam

Habari za michezo ya aina zote na breaking news ndani na nje ya Tanzania �

Kgkhblbjhk Kgkhblbjhk
BOZ 3455
Dar Es Salaam, 54432

ijnkljm

FRÆÑK Øffïçīãl FJr7 FRÆÑK Øffïçīãl FJr7
Dar Es Salaam

Welcome Home Of Champions

SokaLetu Tz SokaLetu Tz
Ubungo
Dar Es Salaam

Soka

Lydia_bodied Lydia_bodied
Kimweri Road Msasani
Dar Es Salaam

I provide advise and best home workouts and Meal guide to help you keep fit.

Shaday twaha Shaday twaha
Shaday Twaha
Dar Es Salaam, 0717030115

Pavard JR Pavard JR
Dar Es Salaam

Sport for Refreshment

Ally Juma Ally Juma
Kinondoni
Dar Es Salaam

football movie

Hamisi Charles Kamuga Kayanda Hamisi Charles Kamuga Kayanda
Dar Es Salaam

Masengwa

Sports global News Sports global News
Kigamboni
Dar Es Salaam

HOME OF SPORTS TANZANIA, EVERY BODY YOUR INVITED