Gro chick farm

Wauzaji wa kuku vifaranga vya chotara aina ya Malawi,Kloiler,Sasso na Tanbro

09/08/2024

Banda simple na lenye viwango kwa wenye maeneo madogo hasa wale wa nyumba za kupanga..

26/06/2024

* MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU*

▪️Kwanza kabisa vifaranga wanahitaji Sana Mambo yafuatayo yazingatiwe.

👉Joto

👉Chakula Safi

👉Maji Safi

👉Mzunguko mzuri wa hewa

👉Idadi sahihi ya Vyombo vya chakula na Maji

👉Randa Safi ,zisizo na vumbi, kavu

👉 Biosecurity/ usalama wa viumbe.

👉 *WIKI LA KWANZA*

👆Siku ya kwanza kabisa ( Glucose/Glucovet inategemea wametoka umbali gani wanaweza kupewa masaa 3-24).

👆 *Multivitamins* Mfn! Neoxychick, Chick formula ,Tetracovit Kwa siku ya kwanza Hadi ya 3-5.

👆Siku ya 6 huwa tunashauri wapewe maji tupu,

👆Siku ya Saba ni chanjo ya kwanza ya NEWCASTLE/ KIDERI-MDONDO

👉Muda huu wote watakua wanatumia chakula cha Starter/ Broiler starter.

*WIKI LA PILI*

👆Siku ya nane Hadi siku ya 12 Wapewe vitamins zipo Aina nyingi Sana *Mfn* :Aminototo, Introvit Farmvita, Dad OCTAVIT, etc

👆Siku ya 13 wapewe maji matupu ( japo hata ukiwawekea vitamins si mbaya).

👆Siku ya 14 wapewe chanjo ya Pili ya Infections Bursal Disease / Gumboro

👉 Muda huu wote wapewe chakula cha Starter/ Broiler Starter.

*WIKI LA TATU*

👉Hapa tuna wagawa kuku kutokana na Aina

👆 *KUKU WA NYAMA/BROILERS*

👉Siku ya 14 au15 Hadi ya 22 wapewe Grower Pellets ( Kwa uzoefu wangu).

👆Hapa hawa kuku wanaweza kupewa Vitamins au Broiler Booster Mfn : Introvit A , Galvet am aUtravin broiler booster.

👆Siku ya 21 kuku Broiler wapewe chanjo moja wapo Kati ya Gumboro au KIDERI ( Hii inategemea MAZOEA ya namna ya kuchanja kuku kutokana na mkoa ulipo).

👉 *_KWA KUKU WANAOANDALIWAKUTAGA ( CHOTARA, LAYERS , KUKU WA KIENYEJI)._*

👆Wapewe chakula cha Starter Mashi inaenda mpaka wiki ya 7 au wiki ya 8 (inategemea maelezo ya chakula unachotumia na kampuni uliyo nunua chakula).

👉Siku ya 21 kuku hawa watapewa Chanjo ya pili ya Newcastle/KIDERI/MDONDO

👆Siku ya 28 kuku wanao andaliwa kutaga wapewe chanjo ya pili ya Gumboro

👆Siku ya 30-35 ni chanjo ya Ndui (Japo maeneo mengine Ndui hutokea mapema wiki ya 3).

👉Kila baada ya miezi mitatu kukuwako wapewe chanjo ya KIDERI/ Newcastle

KUMBUKA

👉 *Minyoo ni hatari Sana* Kwa maendeleo ya kuku....unapaswa kuwapa dawa za minyoo mapema Kwa mara ya kwanza wakifika miezi miwili , 👉Kisha utakua unarudia kila baada ya miezi mitatu *USIPUUZE*

👆Kwa chakula wape grower mash wiki ya nane au 9 mpaka wiki ya 18-19 ( Pale utakapo okota yai bandani).

*NB* : Kuku hawa wapewe vitamins mara Kwa mara ..sio lazima kuwapa kilasiku kupunguza Gharama

👆Kuku wako wakifikisha asilimia 3-5 za utagaji wape Layers mash moja Kwa moja Hadi pale utakapo amua kuja kuwauza

Ikumbukwe kuku hawa wanapaswa Kula Kwa kipimo maalumu kutokana na Umri

👆 *MAZOEA* YANAONESHA WATU KUFUGA KWA KUWEKA RATIBA YA DAWA K**A CHAKULA

👉 *Hii sisawa Kitaalamu* , kuku wapewe dawa pindi wanapoumwa...Uzoefu wangu haunioneshi ulazima WA kukuza kuku Kwa Dawa.

*MWISHO*

22/06/2024

📌MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA UJATUMIA CHANJO YA TATU MOJA*

👉Chanja kuku wako ili kuwakinga dhidi ya mdondo , Ndui na *mafua yanayoambukiza* kwakuweka tone moja tu katika jicho.
👉Chanja kuku wenye afya tu na usimchanje kuku wagonjwa na waliodhoofika.
👉Usiweke chanjo katika joto kali na kwenye mwanga wa jua .
👉Hii ni chanjo siyo dawa ya kutibu mdondo , ndui na mafua .
👉Usitoe chanjo hii kwenye kundi la kuku ambalo baadhi washaanza kuonesha dalili za ugonjwa .
👉Chanjo hii itumike ndani ya siku 7 tu toka kufunguliwa na ihifadhiwe kwenye jokofu baada ya kufunguliwa.
👉Chanja kila baada ya miezi minne (4) kwa kuku wa umri wowote.
👉Chanjo hii itolewe chini ya uangalizi wa mtaalamu wa mifugo.

09/06/2024

Usiache kufuga kisa uko nyumba za kupanga hakikisha una banda simple k**a hili utakuja kunishukuru.

Photos from Gro chick farm's post 11/05/2024

*MAKALA KUHUSU UCHANJAJI KUKU NA ULISHAJI KUKU KWA MAKUNDI YOTE.*

*CHAKULA*
K**a ilivyo kwa viumbe wengine kuku nao wanahaki ya kupewa chakula bora na chakuwatosha kwa muda wote hii ni hakiyao kisheria ANIMAL WELFARE ACT.

Kwa kuzingatia hilo huu ni mwongozo wa ulishaji wa kuku wa *MAYAI, CHOTARA, WA KIENYEJI* NA aina nyingine zinazozalisha mayai

*Layer starter mash wiki 1-8 au 1-7*

*Layer grower mash 9-17 *hii inaenda mpaka kuku atakapo dondosha yai la kwanza*

*Complete layer mash* kuanzia wiki ya 18 mpaka kuku atakapo acha kutaga au utakapo amua kumuuza.

NB kuku wanatakiwa walishwe kwa kiwango wanacho stahili kulingana na aina ya kuku na umri wa kuku wenyewe

*KUKU WA NYAMA*

*BROILER*
Hawa ni kuku ambao kwa asili wanao uwezo wa kukua na kujaza nyama mapema na huweza kufikia kilo 2 ndani ya siku 42 wakilishwa chakula chenye ubora

*RATIBA YA ULISHAJI*
Broiler starter crumble siku 1-13

Broiler Grower pellets siku ya 14- 22

Broiler Finisher pellets siku ya 23-35

Hapo tunategemea utakua umeshauza kuku wote broiler bandani (japo wengine huuza broiler siku 28-32) kwa kutegemea uzito wa kuku.

*CHOTARA K**A KUKU WA NYAMA*

Broiler starter crumble siku 1-21

Broiler Grower pellets siku 22-41

Broiler finisher pellets siku 42-70...au k**a utauza ndani ya miezi mitatu utakuwa ukiwapa finisher

NB usije ukachanganya kuwalisha sterter kuku wakubwa watapungukiwa baadhi ya viinilishe ...wala usiwalishe finisher kuku wadogo watapata matatizo kwenye ukuaji

PIA unapo hama kutoka chakula cha aina moja kwenda nyingine ni vema ukawa unawachanganyia ili wazoeechakula na wasipate stress zitakazopelekea kupungua kukua MFANO starter kwenda grower unaweza changanya siku ya 11-13 kisha unaanza kuwapa grower pekee Siku ya 14.

*RATIBA ZA CHANJO*

Kuku wanaokaa muda mrefu k**a Wa MAYAI, CHOTARA, KIENYEJI

Siku ya 1 chanjo Marek's
Siku ya 7 chanjo ya Newcastle/kideli
Siku ya 14 chanjo ya gumboro
Siku ya 21 chanjo ya kideli/Newcastle
Siku ya 28 chanjo ya gumboro
Siku ya 30 chanjo ya ndui
Baada ya miezi mitatu dawa za minyoo
Rudia chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu

*KWA KUKU WA NYAMA/ BROILER*

Hawachanjwi mareks
Siku ya 7 chanjo ya Newcastle
Siku ya 14 chanjo ya gumboro
Siku ya 21 chanjo ya kideli
Wafugaji wengi wamekua wakichanja hivyo kwakua huuza kuku ndani ya siku 28-30

K**a utauza kuku baada ya siku 40 chanja chanjo ya gumboro siku ya 28.

*Kumbuka*
Chanjo zote zamaji zinatakiwa zikae ndani ya muda wa saa 1-2...baada ya hapo mwaga maji OSHA vyombo na badilisha maji ya kawaida

Zingatia usafi wa maji na vyombo kabla na baada ya chanjo

K**a utatumia maji ya mvua au usiyoamini kuwa ni masafi kwajili yachanjo yatibu kwa kidonge kinaitwa CEVAMUNE/Chlorex blue.

Nimependa tujifunze hayo kwa Leo nawatakia ufugaji mwema

Karibu kwa vifaranga bora vya chotara
Kroiler 1,700
Sasso 1,700
Malawi 2,000

Tupigie 0694021671

Photos from Gro chick farm's post 01/05/2024

*JINSI NILIVO LEA VIFARANGA WA MAYAI*

*KABLA YA MAPOKEZI*

Kwanza iliwekwa oda ya Vifaranga kutoka Kampuni ninayo iamini,

👆Nilitengeneza sehemu ya kulele vifaranga Brooder ( nakuweka Randa wiki zaidi ya 2 kabla ya kuleta vifaranga).

👆Nilisafisha vyombo vyote ( chakula na maji na kuviloweka kwenye Vrid na kuvihifadhi).

👆Nilinunua chakula, Mkaa, Vyungu, Vitamins, siku 4 kabla vifaranga hawajaja

🐓🐓 *SIKU YA KULETA VIFARANGA* 🐓🐓
👉Nilihakikisha Brooder imekamilika kila kitu, na kumpa maelekezo kijana vitu vichache vya kufanya nikiwa nimeenda kufata Vifaranga

👆Nilifuata Vifaranga SAA 3 usiku, nikampigia kijana simu akoleze Majiko Moto na kuyaweka Bandani ( _masaa 4 kabla sijaja na Vifaranga)._

👆Nilichukua Vifaranga Mbezi Beach, na Kuanza safari kwenda karibu na Mlandizi PWANI.

👉 *Tukifika shambani SAA SITA na nusu Usiku, Cha Kustaabisha*
👆Tulikuta Joto kwenye Brooder halipo , Nidogo kiwango kisichoruhusu kuweka vifaranga.

👆 *Ilibidi Kwa haraka sana nipunguze Size ya Brooder Kwa Turubai, na kukoleza Moto haraka Sana ,mpaka joto lilipo ongezeka*

👆Majira ya Saa Saba na nusu Usiku Ndipo tulipo Anza kuingiza vifaranga kwenye Brooder.

*WAKATI WA KUWEKA VIFARANGA*
👆Kwanza Brooder ilikua imetandikwa Magazeti na vyombo vya chakula vilikua vimesambazwa tayali

👆Tuliweka maji , nilitumia Glucose na Tetracovit ( multivitamin).

👆Kisha tukaanza kuingiza vifaranga ( *vifaranga wote walihesabiwa na idadi kuandikwa kwenye kitabu Cha kumbukumbu* ).

👆Tuliendelea kuwahudumia vifaranga mpaka asubuhi bila *Kulala hata dakika moja*

👆Asubuhi SAA 3 tulibadilisha maji , tukaweka maji Yasiyo na Glucose na kuweka *Tetracolivit multivitamin pekee*

👆Tuliendelea kuzingatia *joto* hasa usiku, Mchana joto Tulitumia Kwa siku *4* na Usiku tuliweka mpaka siku ya *10* Vifaranga wakawa wameshazoea joto la mazingira.

👆Zoezi likabaki Kuongeza chakula na kubadilisha maji asubuhi na jioni ( Tunaosha vyombo).
*NB: NILILALA BANDANI MWENYEWE KWA SIKU SITA MFULULIZO*

👉Mpaka sasa wamefikisha siku 39 wamekufa vifaranga 14 *Kati ya 2039 tuliowaweka siku ya Kwanza* Wengi wamekufa Kwa uzembe ( *Watano waliungua kwenye Vyungu, wanne walifunikwa na vyombo vya chakula, mmoja alikanyagwa, Mmoja aliangukiwa na taa kubwa ya Sola)*

🐓🐓VITU TUNAVYOFANYA KWA SASA🐓🐓
👆Kupima chakula kila siku asbh sa 12-1 wanakua wameshakula na Jioni SAA 9-10 wanakua wamewekewa chakula.

👆Kuwa karibu nao kuwaangalia Kwa karibu na kujaza kitabu cha kumbukumbu Kwa kila kinachofanyika Kwa siku husika.

*CHANJO NILIZO WAPA*
👉Nilitafuta taarifa Kwa *madaktari* kadha wa kadha tukashuariana Kuchanja k**a ifutavyo hasa Kwa Kupambana na *Gumboro*

🐓Siku ya NNE ( Gumboro) Maji
🐓Siku ya Saba Newcastle + IB ( *Matone kwenye jicho)*
🐓Siku ya 14 Gumboro ( maji)
🐓Siku ya 21 Newcastle (maji).
🐓Siku ya 26 Gumboro ( maji)
🐓Siku ya 30 Ndui (Bawa)

*VITAMINS NILIZO WAPA*
👆 Tetracolivit siku 1-5
👆 Amintoto siku 7-13
👆Amintoto siku 15-20
👆 Amintoto siku 22-25
👆Introvit A+ siku 27 Hadi sasa ( siku ya 40) kuna siku nawapumzisha bila vitamins.

*CHAKULA NILICHOWAPA*
👉Broiler starter crumble ( siku 18 za mwanzo).
👉Layers Strarter Crumble siku ya 19 mpaka SASA tutaacha wiki ya SITA
🐓🐓 *NB Broiler starter hatukuwapimia, Ila Layers starter tulianza kuwalisha Kwa gramu walipo Anza siku ya 21.*

CONCLUSION
👉Mungu Mwema kuku wanakua vizuri
👉Hatujapata ugonjwa
👉Hatujapata shida ya mafua
👉Hatujapata shida ya Upungufu WA vitamin A Wala E

Tunaendelea Kuwaangalia Kwa karibu Sana ili k**a kutakua na dalili ya Ugonjwa tudhibiti mapema *MPAKA SASA HATUJANUNUA DAWA YOYOTE
Acknowledge (Kahise)

22/04/2024

Gro chick farm 7 Days chicks👍

27/03/2024

⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️

MAISHA HAYANA FORMULA LAKINI YANA SIRI NYINGI! CHUKUA HIZI 11, K**A ZITAKUFAA

1. SIRI YA KWANZA

Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake!

2. SIRI YA PILI

Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako!, K**a hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa

3. .SIRI YA TATU

Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji 3.bidii yenye akili!, Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana?

4. .SIRI YA NNE:
Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.

5. SIRI YA TANO
Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matundo ndo unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka!, Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona.

6. SIRI YA SITA

Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute K**a kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?

7.SIRI YA SABA

Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako hovyo!

8.SIRI YA NANE

Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako alichagua kuyaficha! K**a unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako.

9. SIRI YA TISA

Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli.

10.SIRI YA KUMI

Hata k**a umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike

11. SIRI YA KUMI NA MOJA

Haijalishi umri umekwenda kiasi gani k**a una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee ni hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu
UWE NA WAKATI MWEMA BARAKA ZA MUNGU ZIKAWE NASI SOTE KWA KADRI YA FADHILA NA NEEMA ZAKE

18/03/2024

🐓Tunauza vifaranga pure vya Malawi weusi (Black australorp).
✍️Sifa yao kubwa kwenye kutaga na wavumilivu wa magonjwa kuliko mbegu nyingine yeyote.

Kifaranga cha siku 2,000 (Order)

Vimepatiwa chanjo zote za awali ✅
Tupo Dar es salaam Yombo na mbezi
☎️+255 694 021 671
☎️+255 654326908

18/03/2024

⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️
SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

Ukiamua kufuga. katika banda kuna njia mbalimbali utatakiwa kujenga banda lenye sifa zitakazokidhi mahitaji ya msingi ya kuku. Banda bora la kuku linatakiwa kuwa k**a ifuatavyo:

LIWE JENGO IMARA
• Pasiwe na sehemu zilizo wazi kwenye msingi na kati ya ukuta na paa.

• Banda lijengwe na vifaa vinavyopatikana katika mazingira yako ili liwe na gharama utakayoweza kumudu.

• Unaweza kutumia matofali ya udongo, udongo, miti, fito,n.k. Ukitumia fito au mabanzi ondoa maganda ili kuthibiti mchwa.

• Jengo mara litazuia maadui k**a panya, vicheche, paka, nyoka na wezi kuingia ndani ya banda na kuwadhuru au kuwaiba kuku.

LIWE RAHISI KUSAFISHA
• Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa ili kurahisisha kusafisha.

• Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha katika nyufa k**a papasi, viroboto n.k.

• Sakafu ya banda lazima iwekewe matandazo k**a pumba ya mpunga au maranda ya mbao au mabaki ya mazao au nyasi kavu kutegemeana na kinachopatikana kwa urahisi katika mazingira yako.

• Matandazo haya husaidia kunyonya unyevu unaotokana na kinyesi cha kuku au maji yanayomwagika katika banda.

• Banda hubakia kavu bila kuwa na harufu mbaya na wadudu k**a inzi hata vimelea vya magonjwa hudhibitiwa.
Eneo la nje kuzunguka banda kuwe na usafi wa kudumu
Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu k**a siafu au mchwa na wanyama k**a panya na paka mwitu wakose maficho. Nje ya banda ndani ya uzio kuwe na miti midogo na mimea mingine midogo kwa ajili ya kivuli.

BANDA liwe na nafasi ya kutosha kwa kuku waliopo:
Kwa kawaida eneo la mita mraba moja hutosha kuku wanne wanaotaga au kuku 8 wa nyama. Nafasi ya mita mraba 1 inatosha vifaranga 16 hadi kufikia umri wa majuma manne.

Liweze kuingiza hewa na mwanga wa kutosha:
Banda linaloweza kuingiza hewa safi na kutoka ndani yake hubaki kavu. Harufu mbaya hutoka na kuku huweza kupumua hewa safi. Hii husaidia pia kudhibiti kuzaliana kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa,hivyo hudhibiti magonjwa.

Lisiwe na joto sana au baridi sana:
Panda miti ya kuzunguka banda lako ili eneo liwe na kivuli cha kutosha na pia lisiwe na upepo mkali.K**a hali halisi ya eneo la kufugia ina joto kubwa kwa vipindi virefu paa la banda wakati wa ujenzi liinuliwe juu zaidi kuruhusu mzunguko zaidi wa hewa na joto la paa ( k**a ni la bati) liwe mbali juu ya kuku.
Joto kwenye banda linaweza kusababishwa na msongamano wa kuku, hivyo mfugaji aangalie aweke idadi ya kuku inayowiana na ukubwa wa banda lake.

PAA
Liwe imara na lisilovuja. Waweza kutumia mabati, nyasi, madebe, makuti n.k. kutegemeana na upatikanaji wa vifaa vya kuezekea. Wakati wa kuezeka paa lisiishie karibu sana na ukuta bali liwe na sehemu kubwa iliyozidi ukuta kuzuia mvua kuingia ndani k**a ni ya upepo

VIFAA
vinavyohitajika katika banda la kuku
Kuku wakifugwa kwa mtindo wa nusu ndani na nusu nje wanahitaji huduma mbalimbali ndani ya banda na ndani ya wigo. Ili kutoa huduma hizi vifaa.

vifuatavyo ni muhimu viwe katika banda:

VYOMBO VYA MAJI.

Kuna njia nyingi za kutengeneza vyombo vya kuwekea maji ya kuku ya kunywa.

• Aina ya mojawapo unayoweza kutumia ndoo au debe la lita kumi au ishirini ya plastiki. Kata ndoo hiyo pande nne kutoa nafasi ya kuku ya kunywea k**a kielelezo kinavyoonyesha. Tengeneza idadi ya vyombo hivi inayowiana na wingi wa kuku ulionao.

• Au waweza kutumia sufuria au beseni pana kiasi. Hii huwekewa tofali au jiwe safi pana baada ya kuwekewa maji ya kunywa ili kuzuia kuku wadogo wasizame na maji yasichafiliwe kirahisi.

• Vifaa maalum vya kunyweshea kuku vinapatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo.

VYOMBO VYA CHAKULA.

Vyombo hivi ni muhimu viwe vimetengenezwa vizuri ili visiwe chanzo cha upoteaji wa chakula. Unapotengeneza kilishio cha kuku kumbuka kuwa kuku wana tabia ya kuchakura. Husambaza au kupekua chakula kwa miguu hata kwa midomo ili kupata chakula cha chini.
Tabia hii husababisha kumwagwa kwa chakula kingi chini na kusababisha hasara. Unaweza kudhibiti tatizo hili kwa kutengeneza vyombo visivyoruhusu kuku kuchakura k**a inavyoonyeshwa kwenye kielelezo hapa chini.
Unaweza kutengeneza kilishio hiki wewe mwenyewe au fundi seremala waliopo katika eneo unaloishi. Inafaa kilishio kiwe chembamba ili kuku wasiweze kuingia. Pia kinatakiwa kiwe kirefu ili kuku waweze kula bila kusongamana.

VIOTA

Zipo aina tofauti za viota ambazo hutumika kwa ajili ya kutagia. Ipo aina ya ambayo ni ya kutagia kuku mmoja mmoja. Vipimo vinavyopendekezwa kwa kila kiota ni upana wa sentimita 30, urefu sentimita 30 na kina sentimita 35. Upande wa mbele uachwe wazi ila sentimita 10 za kwanza kutoka chini zizibwe na ubao ( angalia kielelezo). Weka idadi ya viota inayotosheleza kuku ulio nao.

Pia ipo aina nyingine inayoweza kutumiwa na kuku zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ni k**a kiota kimoja kilichogawanywa katika vyumba kadhaa. Ila kila chumba kina vipimo k**a vya kiota kimoja( angalia picha hapa chini).Aina hii ya kiota ina upana wa sentimita 30 na kina sentimeta 35 na urefu wake unategemea idadi ya viota.

VIOTA
VIOTA vinatakiwa kuwa na giza ili kuku wasiogope kuingia kutaga ndani yake. Pia giza husaidia kupunguza tabia ya kuku kula mayai na kudonoana. Kiota kinafaa kuwekwa mahali ambako ni rahisi kuku kuingia na kutoka. Vile vile iwe ni sehemu itakayorahisisha usafishaji wa kiota chenyewe.

KICHANJA

Kuku wana asili ya kupenda kulala au kupumzika sehemu iliyoinuka. Hivyo ndani ya banda weka vichanja vitakavyotosheleza idadi ya kuku waliopo

ULISHAJI:

Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.

BANDA:
Kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa k**a vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.

MAJI YA KUNYWA:

Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.

CHANJO kwa mifugo ni lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni k**a vile Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.

Uwekaji wa kumbukumbu: Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.

Mwanzoni unahitaji nini?
Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku.
Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.

Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako.
K**a unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.

• Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima ukamilishwe.

• Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika

18/03/2024

Gro chick farm mission and vission.

✍Welcome to Gro chick farm, a newly developing poultry farm on the path to establishing a prominent presence in the industry.Currently we have operation spanning across yombo abiola district. Abiola serves as our primary hub where the majority of our operation takes place.whereby specialized in selling Day old chicks and Monthly chicks.

At Gro chick farm, Our currently focus lies on Black australorp (Malawi weusi) ,Kroiler and sasso. These breeds are known for their exceptional qualities that they have. We believe that this breeds offers excellent potential for our farm’s success. With carefully consideration and extensive research we have chosen the black australorp and Kroiler to be centerpiece of our enterprise.

By the end of this year 2024 we aim to have flourishing main farm area which will accommodating a minimum of 500 birds layers parent stock. We aim to establish wide range of Gro chick sales branch across Tanzania in Dar es salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza. Although journey ahead may present with a-lot of challenges. We are fueled by hope and determination with an wavering commitment and relentless efforts, we are confident in our ability to overcome obstacles and achieve our goals.

When you think of chicken and eggs we want you to think of us! Gro chick farm is dedicated to delivering high quality poultry products and services that meet and exceed your expectation. We strives to establish ourselves as reputable and reliable source for all your chicken related needs.

Join us together on this exciting venture as we work towards creating a thriving poultry farm that sets new standards in the industry. Together let’s build a brighter future for Gro chick farm where quality,innovation and customers satisfaction are paramount.

For quickly service:
Call +255 694021671
WhatsApp +255 654326908

05/03/2024

Je! Uneshaona hii.. Kuku mwenye sehemu mbili za haja kubw

Photos from Gro chick farm's post 27/02/2024

✅Vifaranga wa Mwezi Wanapatikana
✅Aina ya sasso na kroiler
✅Bei 6,000
✅Vifaranga Wanachanjo Zote Za Awali

☎️ +255 694021671
Dsm Yombo Abiola

25/02/2024

⚠️Yajayo yana furahisha…
Napokea order ya vifaranga vya Malawi weusi (Black australorp)

Kifaranga cha siku 2,500
Kifaranga cha mwezi 6,500 (Kwa order)

Marek’s✅
Tupo Dar es salaam Yombo na mbezi
☎️+255 694 021 671
+255 654326908
fans Highlights

Photos from Gro chick farm's post 23/02/2024

⚠️Swali kutoka kwa member wa group

Q.Kwa nini unapenda kulisha pellets kuku zako? Jibu: Ulishaji wa pellets kwa kuku hutoa faida nyingi, kuhakikisha wanapata lishe kamili na kukuza tabia bora za ulishaji.

✍️Lishe Kamili: Pellets hutoa lishe bora yenye virutubisho muhimu, vitamini, na madini muhimu kwa ukuaji na afya.
✍️Upotevu wa Malisho Uliopunguzwa: Ukubwa wa sare za pellets huhimiza ulishaji bora, kupunguza umwagikaji na upotevu wa malisho.
✍️Umeng’enyo Ulioboreshwa: Uchakataji wa Pellets huboresha usagaji chakula, hivyo kusababisha ubadilishaji bora wa mlisho na utendaji wa ukuaji. ✍️Urahisi: Pellets hurahisisha kulisha, kuokoa muda na bidii, haswa kwa shughuli za kiwango kikubwa.
✍️Kuzuia Magonjwa: Pellets hupitia matibabu ya joto, kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa na kuhakikisha ubora thabiti.

✍️Hitimisho: Kulisha kuku huboresha afya zao, utendaji wao, na mazoea ya kulisha, na kufaidisha kundi na ufugaji. Endelea kufuatilia makala zijazo uendelee kujifunza vitu tofaut tofauti..

Gro chick Farm

Photos from Gro chick farm's post 23/02/2024

⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️
CHUKUA HII KWA KIPINDI HIKI CHA JOTO ITAKUSAIDI

Hivi sasa katika nchi za Afrika Mashariki hasa Kwetu Tanzania hali ya joto ya mchana lifaikia hadi nyuzi 34°C na itaendelea kwa muda. Hii inaweza kuwa hatari kwa ufugaji wa kuku na inaweza kusababisha kiharusi cha joto katika na kusababisha vifo vingi vya kuku wako ndani ya banda. Ili kuzuia hili unaweza kufanya mambo yafuatayo:

✍️Lisha kuku wako asubuhi na jioni (kabla jua halijawa kali na jioni jua linapopungua)

✍️Walishe asilimia 70% ya mgawo wa kila siku asubuhi na 30% alasiri au jioni.

✍️Wape maji baridi Ikiwezekana ni pamoja na vipande vidogo vya barafu hasa wakati hali ya joto ni zaidi ya kawaida.

✍️Wape ndege wako nafasi ya kutosha. Epuka kuwajaza kupita kiasi. dalili za wingi wa joto kwa kuku k**a vile kuongezeka kwa unywaji wa maji, kupungua kwa ulaji wa malisho, kuinama sakafuni na mbawa zilizolegea, kuhema kwa kasi kuliko kawaida na kuongezeka kwa vifo kutokana na kushindwa kupumua kwa moyo.

✍️Epuka kuwasumbua au kuwapa stress kuku wako kwa kelele, kuwashtua, kuwatisha.

✍️Toa antistress/multivitamins zenye electrolytes ili kuzuia upotevu wa electrolytes kupitia upotevu wa maji mwilini.Vitamin C pia hufanya maajabu mwilini kwa kuwaongezea nguvu ya kuoambana na hali ya joto

✍️Unaweza kutengeneza banda la kuku kwa kutumia pampu ya maji iliyoboteshea kwa kiwango cha ukungu yaani matone madogo madogo. Ikiwa unaweza kumudu kufunga foggers katika banda lako lako la kuku basi fanya hivyo.

Imeandaliwa na
Gro chick Farm
+255 694021671

Photos from Gro chick farm's post 23/02/2024

⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️⚠️
CHUKUA HII KWA KIPINDI HIKI CHA JOTO ITAKUSAIDI.

Hivi sasa katika nchi za Afrika Mashariki hasa Kwetu Tanzania hali ya joto ya mchana lifaikia hadi nyuzi 34°C na itaendelea kwa muda. Hii inaweza kuwa hatari kwa ufugaji wa kuku na inaweza kusababisha kiharusi cha joto katika na kusababisha vifo vingi vya kuku wako ndani ya banda. Ili kuzuia hili unaweza kufanya mambo yafuatayo:

✍️Lisha kuku wako asubuhi na jioni (kabla jua halijawa kali na jioni jua linapopungua)

✍️Walishe asilimia 70% ya mgawo wa kila siku asubuhi na 30% alasiri au jioni.

✍️Wape maji baridi Ikiwezekana ni pamoja na vipande vidogo vya barafu hasa wakati hali ya joto ni zaidi ya kawaida.

✍️Wape ndege wako nafasi ya kutosha. Epuka kuwajaza kupita kiasi. dalili za wingi wa joto kwa kuku k**a vile kuongezeka kwa unywaji wa maji, kupungua kwa ulaji wa malisho, kuinama sakafuni na mbawa zilizolegea, kuhema kwa kasi kuliko kawaida na kuongezeka kwa vifo kutokana na kushindwa kupumua kwa moyo.

✍️Epuka kuwasumbua au kuwapa stress kuku wako kwa kelele, kuwashtua, kuwatisha.

✍️Toa antistress/multivitamins zenye electrolytes ili kuzuia upotevu wa electrolytes kupitia upotevu wa maji mwilini.Vitamin C pia hufanya maajabu mwilini kwa kuwaongezea nguvu ya kuoambana na hali ya joto

✍️Unaweza kutengeneza banda la kuku kwa kutumia pampu ya maji iliyoboteshea kwa kiwango cha ukungu yaani matone madogo madogo. Ikiwa unaweza kumudu kufunga foggers katika banda lako lako la kuku basi fanya hivyo.

Imeandaliwa na
Gro chick Farm
+255 694021671

14/02/2024

📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌
JE! Umejitathmini Mwaka ndo umeanza na sasa ni mwezi wa pili.

1)Unauchukuliaje mradi wako? Ni k**a Ajira au part time job??

2)Vipi unautegemea ukuongezee kipato au ni hobby tu??

3)Au unafuga ili iwe nini?? Unafata nyayo za walezi wako au kwasababu flani anafuga??

4)Tuambie ukweli umewahi kuupa muda mradi wako kwa kukaa chini na kutathmini maendeleo na matarajio yako??

Kabisa yani kabisa ,umewahi kukaa kitako kudiscuss na vijana wako wa shamba wakupe changamoto zao na changamoto za mradi??

Vipi kuhusu mtaalam anayesimamia shamba lako, mmewahi kupata muda kutathimini mradi wenu ??

Ebu subiri huenda hata mtaalamu wa shambani huna,unatumia uzoefu wa enzi za mwalimu 🤔
Au wewe kazi yako tu ni KUFUGA KWA REMOTE??! 🤣🤣🤣

📞 “vipi huko wamekula??
📞”vipi huyo daktari alikuja kweli eti??
📞”mlishawauza hao kuku?? Wekeni pesa bank
📞”walianza kutaga kwani ?? Mbona hamkusema??

JIPE MUDA NA MRADI WAKO ILI KUYAONA MATOKEO CHANYA

GRO CHICK FARM
Tupo Dsm-Yombo na Mbezi
0694021671

14/02/2024

📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌JIFUNZE MBINU ZA KUPAMBANA NA MINYOO

MAKALA KUHUSU MINYOO KWA KUKU
👉Minyoo ni viumbe hai ambao huishi kwa kutegemea uwepo wa kiumbe mwingine kwa malazi na chakula
👉Kwa kuku minyoo ipo ya aina nyingi, ipo ile ya duara, ipo ile inayokua mirefu sana ambayo ikiwapata kuku kupotea huchukua muda mrefu

CHANZO CHA MINYOO
👉Kuku kula chakula kichafu hasa kilicho changanyika na kinyesi...hapa hasa k**a unachanganya kuku wakubwa na wadogo madhara huwa endelevu bandani usipokinga

👉Kuku wanao zunguka nje, kunywa maji yaliyotuama au maji yaliyokaa kwa muda mrefu pia kuparua mabaki yenye mazalia au mayai ya minyoo

👉Kwa kawaida minyoo huwa na mzunguko wao kunzia *YAI, LAVA, PUPA ,NA MNYOO* mnyoo mkubwa...hivyo minyoo ikiingia kwa kuku huvhukua muda wa wiki zaidi ya mbili kukua kufikia mnyoo kamili

👉Kuku akishapata minyoo wakubwa...hapa ndipo tatizo huanzia kwani mahai hutagwa kwa wingi na hutolewa kwa njia ya kinyesi na kuwafikia kuku wengine hivyo k**a hatua za maksudi hazitachukuliwa ndani ya muda wa wiki 4 tangu minyoo kuingia bandani asilimia kubwa ya kuku watakua na minyoo

KUZUIA

👉Hakikisha mazingira yako ni salama na safi muda wote yasiyo na maji yenye kutuama kwa wala matope yanayo kuwepo kwa muda wote kuzunguka mahali kuku wanapoishi

TIBA

👉Kitaalamu zipo dawa nyingi za minyoo ambazo kwa ratiba iliyo zoeleka hutakiwa kutolewa na kurudiwa kila baada ya miezi mitatu
👉Tatizo limekuja ni upi wakati sahihi wa kuanza dozi ya minyoo kwa kuuliza madaktari bobezi wa kuku wanashauri dawa za awali za minyoo zitolewe baada ya miezi miwili

INASHAURIWA KWA SEHEMU ZENYE MAJI YASIYO SALAMA SANA
👉Na mfumo wa utoaji dawa za minyoo kwa Mara ya kwanza unatakiwa uwe wa kurudia kila baada ya wiki 2 rudia Mara tatu
KWA NINI IRUDIWE UNAPOANZA DOZI
👉Dawa za minyoo hushambulia hatua mbili za ukuaji wa minyoo..ambazo ni minyoo wakubwa na wale wanaofuata kwa ukubwa ilaa haziathiri hatua za mayai na LAVA...hivyo ukiwapa dawa kwa kurudia kila baada ya wiki mbili Mara 3 mfululizo hii itapelekea hata yale mayai yatakua yamegeuka na kuwa minyoo wakubwa hivyo dawa itawaua na kupunguza tatizo kwa 75-85%
👉Ila ukiwa unasubiri kuwapa kila baada ya miezi mitatu bila kufanya hizo hatua nilizolekeza utakua unapunguza idadi ya minyoo na wakati mwingine minyoo itazidi na haitasikia dawa Zipo dawa aina nyingi za minyoo k**a Ant worms ...Piperezine...,Levamisole, Leva,Askarex , Fenhbendazole .zipo nyingi sana madukani

KWA URAHISI

👉Awamu ya kwanza ya kuwapa dawa
👉Baada ya miezi miwili....dozi siku 1-2
👉Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2
👉Rudia baada ya wiki 2 dozi siku 1-2

Ukimaliza hapo sasa wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu kuku wako watakua salama na huru dhidi ya minyoo

ZINGATIA
👉Maji safi
👉Chakula safi
👉Banda safi
👉Fuata ratiba sahihi ya dawa hasa kila baada ya miezi mitatu zingatia usipitishe na uzipuuze

Karibu ufuge na Gro chick Farm
Tupo Dsm-Yombo na Mbezi
0694021671

Want your restaurant to be the top-listed Restaurant in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Chicks
🐓Tunauza vifaranga  pure vya Malawi weusi (Black australorp). ✍️Sifa yao kubwa kwenye kutaga na wavumilivu wa magonjwa k...
🍃BLACK AUSTRALORP🍃          (Malawi weusi)                 🫵🏽Asili ya jamii hii ya kuku ni Australia  kutoka Black Orpin...
⚠️Yajayo yana furahisha…Napokea order ya vifaranga vya Malawi weusi (Black australorp)Kifaranga cha siku 2,500Kifaranga ...
📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌JE! Umejitathmini Mwaka ndo umeanza na sasa ni mwezi wa pili.1)Unauchukuliaje mradi wako? Ni kama Ajira a...
✅Habari Njema Kwa Wafugaji Wote!!!!Sasa vifaranga wa Mwezi Wanapatikana(MALAWI WEUSI, SASSO NA KLOILER)Vifaranga Wanacha...

Category

Address


Yombo Dovya
Dar Es Salaam
Other Chicken Joints in Dar es Salaam (show all)
kuku_chapchap kuku_chapchap
Tegeta Nyaishozi
Dar Es Salaam, 0000

Farm | Chicks Production | Chicken Farm Management | Poultryhouse Booking : [email protected]

thechicks_tz thechicks_tz
Buza
Dar Es Salaam, 255

We sell and supply local chicken � � at retail and wholesale. �Dar es salaam. Countywide delivery. � 0765777889

Fugakuku Fugakuku
Fugakuku
Dar Es Salaam

Wauzaji wa Vifaranga vya kuku aina mbali mbali, Broiler, Layers, Chotara na Kienyeji. Tunauza Vifaa mbali mbali vya Kuku..Drinker,Feeder, Incubator N.K

Ghjj Ghjj
Kitunda, Buza, Pwani 301
Dar Es Salaam

Interchick Shambani Interchick Shambani
New Bagamoyo Road, Jogoo/Mbezi Industrial Area, P. O. Box 5774
Dar Es Salaam

� Tunawekeza ubora kwenye kila yai tunalototolesha, kila kuku tunaefuga na kila chakula tunachotengeneza.

TCBIZ TCBIZ
Dar Es Salaam, 10201

Classified Farms Classified Farms
Dar Es Salaam

Supplier of Organic Chicken meat and eggs

The New Genesis Tanzania Ltd The New Genesis Tanzania Ltd
Magomeni, Usalama
Dar Es Salaam, 34523

TNGT use the best poultry breeds because our customer's satisfaction comes first hence serving our clients by offering better product timely and effectively.

The_bestkuku_tz The_bestkuku_tz
Dar Es Salaam

Tunauza kuku wakienyeji kutoka singida kwa bei nafuu/dagaa/samaki.....Tunapatikana Kawe(Dar es salaam)tunafanya delivery maeneo yote ya Dar es salaam kwa gharama za mteja...karibun...

Manok Time Manok Time
Namanga Msasani
Dar Es Salaam, 14111

We are a fast food restaurant offering the "crunchiest" - "juiciest", and the "crispiest" chicken on the planet.

VifarangaKuku Project VifarangaKuku Project
Boko Magengeni
Dar Es Salaam, BOX708813

Uzalishaji na Uuzaji wa vifaranga wa aina zote Utunzaji wa kuku and Ushauri wa kitaalamu Usambazaji

urbans.chicken urbans.chicken
Koba 7
Dar Es Salaam

Kwa mawasiliano piga 0758230211 Na follow instagram: @urbans.chicken