Dr_Kassimu Na Afya.
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dr_Kassimu Na Afya., Medical and health, Dar es Salaam.
MATIBABU YA MIFUPA BILA UPASUAJI
Mifupa ndio inayokupa muonekano na kukusaidia kufanya shughuli zote za nguvu ikiwa inasaidiana na misuli ya nyama. Mifupa hufanya kazi kubwa wakati wa kutembea, kukaa , kusimama, kulima, na kazi mbalimbali, nk.
Kutokana na shughuli mbali mbali tunazofanya misuli hukak**aa na kusababisha kubadilisha mpangilio na muonekano halisia wa mifupa. Hii husababisha mifupa kuinda, kupishana, kusagana, kuvunjika n.k.
MAGONJWA YA MIFUPA
watu wengi nilio wahudumia huwa na matatizo yafuatayo ya viungo:-
1: Maumivu ya kichwa na shingo
2:Maumivu ya kiuno na nyonga
3: Maumivu ya magoti na miguu
4: Maumivu ya mabega, mbavu na mikono
5: Miguu kuwaka moto
6: Miguu kufa ganzi
7: Gauti
8: Arthritis
Wagonjwa baada ya vipimo vya xray, CTScan au MRI huweza kutambulika magonjwa yao na kuishiwa kupatiwa dawa za maumivu ambazo hutuliza tu maumivu bila kumaliza chanzo cha tatizo. Hii husababisha tatizo kuendelea kwa muda mrefu na baadae hulazimika kufanya upasuaji. Hata baada ya upasuaji huwa hakuna matumaini makubwa kwani madhara huwa yamefanyika kwa muda mrefu.
Tunatoa matibabu ya magonjwa ya mifupa kwa dawa nzuri zilizothibitishwa na mamlaka ya dawa na chakula Tanzania na Marekani. Dawa hizi hurekebisha tatizo na kutengeneza kinga ya kuzuia mifupa kusagana na kutengeneza gegedu, ute ute na mifupa kuwa imara. Tunaweza kukusaidia ukarudisha furaha katika maisha yako au ndugu yako unayemuhudumia.
Kwa matibabu, ushauri, maswali na maoni unaweza kuwasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim
MAUMIVU YA NYONGA YANATIBIKA
Maumivu ya nyonga yanawasumbua sana na yanaathiri ubora wa maisha. Mgonjwa hushindwa kufanya majukumu yake ya kila siku ya kujikimu k**a kuoga, kuvaa nguo, kutembea, kukaa, kusimama.nk. hii husababishwa na kuisha na kusagika kwa mifupa na ligament za maungio ya mifupa. Hii huchangiwa na kushindwa kutengenezwa kwa gegedu na mifupa hii baada ya kuumia. Mifupa pia huanza kuyeyuka kwa umri unapoanza kua mkubwa. Hii husababishwa na mwili kuacha kujijenga na kuanza kuyayusha mifupa kupata madini ya kalshiamu na kutumia sehemu nyingine ya mwili. Hivyo watu umri mkubwa wanashauriwa kupata virutubisho sahihi ili kuwezeshwa kutengeneza na kuzuia kuyeyuka kwa mifupa.
Kwa ushauri, maswali na maoni unaweza kuwasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim.......!
IJUE TOFAUTI YA KUTEGUKA NA KUVUNJIKA MGU
(JOINT DISLOCATION AND BONE FRACTURE)
Kuna tofauti kubwa kati ya kuteguka mguu na kuvunjika mguu. Kwa kifupi kuteguka na kupisha a kwa mifupa miwili ya karibu katika maungano na kuvunjika ni kukatika kwa mfupa mmoja na kutoa miwili au zaidi. unaweza kufikiri ipi ni hatari sana ukipata kuliko nyingine....! Kuteguka ni joint ni hatari zaidi kwani hupelekea watu wengi kukatwa viungo. Hii husababishwa na kuteguka maungio hupelekea mishipa ya damu kuziba na mishipa ya fahamu kutakika. Kuvunjika huwa hatari k**a mfupa uliovunjika utaenda kukata mshipa wa damu au fahamu uliokaribu. Na hii hutokea iwapo baada ya ajali majeruhi ataitumia mifupa iliyovunjika. Katika zote mbili inapotokea kwa huduma ya kwanza fanya yafuatayo.
HUDUMA YA KWANZA KWA MJERUHIWA
1: mlaze mgonjwa mahali salama
2: omba ruhusa ya kumhudumia mgonjwa
3: muulize sehemu alikoumia
4: baini jeraha na aina ya mvunjiko au kuteguka alikoumia mgonjwa
5: zuia damu k**a inatoka
6: funga eneo lililo vunjika au teguka kusiwe na kucheza cheza kabisa.
7: mpeleke mgonjwa hospitali kwa matibabu
Kwa maswali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nami.
Dr Kassim
0759490202
PRESHA, KISUKARI NA NGUVU ZA KIUME IJUE KINGA NA TIBA
Unaweza kutengeneza kitunguu swaumu kwa kuandaa juisi yake halisi, kuchanganya katika chakula au kutengeneza chai kwa kuchanganya na tangawizi. Kitunguu swaumu huondoa rehemu mbaya katika mishipa ya damu na kuzibua misuli hiyo na damu kusambaa vizuri.
Kwa maswali, maoni au ushauri tunaweza kuwasiliana.
Dr Kassim
0759490202
MAGONJWA YA LIGAMENTS (KANO)
0759490202
matatizo mengi ya mifupa na viungo huweza kusababishwa na kuumia kwa kano au ligaments. Hizi ni ni nyama ngumu (fibrous tissue) zinazounganisha mfupa mmoja na mwingine. Huwezesha mtu kutembea, kuinama na kufanya kazi za kila siku. Watu wa mazoezi huumiza nyama hizi na hushindwa kushiriki mazoezi tena.
MAGONJWA YA LIGAMENTS
1: Ligaments kupasuka
2:Ligament kukatika
3: Ligament kuvutika
4:Ligament kuoza
DALILI ZA MAGONJWA YA LIGAMENT
1: Maumivu makali ya maungio (joint)
2: maungio (joint) kuvimba
3: kushindwa kukunja au kunyoosha joint
4: maungio kujaa maji
Uponyaji wa ligament huchukua muda mrefu sana kuyokana na kuwa na mishipa ya damu michache. Huweza kuchukua muda wa wiki tatu mpaka wiki sita na mara nyingine huenda mpaka miezi sita.
MATIBABU YA JERAHA KATIKA LIGAMENT
1: Weka kipande cha barafu
2: chua eneo lililo athiriwa
3: funga na bandage
4: Tumia dawa za kuponesha na kutengeneza ligament imara
5: unaweza kutumia dawa za maumivu
Kwa maswali, maoni na ushauri tunaweza kuwasiliana ili kuweza kusaidia juu ya matatizo ya kiafya.
Dr Kassim
0759490202
UNAFAHAMU KUHUSU KICHOMI
kichomi ni tatizo la muda ambalo hutokea mara nyingi kwa wanamichezo au kwa mtu anayefanya kazi fulani. Kichomi ni maumivu makali ya ghafla katika nyama za eneo fulani ambayo mhanga hushindwa kukunja au kunyoosha au kutumia eneo lililo athiriwa.
SABABU ZINAZOSABABISHA KICHOMI
1: mazoezi makali
2: kutotumia kiungo fulani kwa muda mrefu
3: kukandamiza kiungo na kuzuia mawasiliano ya damu na fahamu
Kinachotokea ni hiki, mwili unategema kutengeneza nguvu (energy) kutoka katika glucose na kuichoma katika oxijeni. Endapo oxijeni itakosekana mwili huunguza glucose bila oksijeni na kutengeneza sumu inayojulikana k**a lactic acid. Kemikali hii ndio inayosababisha maumivu makali ya misuli. Kemikali hii inapoisha ndio mgonjwa nae hupata nafuu na kupona kabisa.
JINSI YA KUMSAIDIA MGONJWA
1: mlaze chini
2: piga piga eneo lililo athirika
3: maseji/chua taratibu eneo hilo
4: kunja na kunyoosha eneo hilo iwezekanapo
5: pata matibabu k**a hali si shwari
Kuna baadhi ya watu huwatokea hali hii bila kufanya shughuli yeyote ile wanakua wamekaa au wamelala. Maumivu huwa yanajirudia sana zaidi ya mara moja kwa siku. Kwa hali hii onana na daktari wako kwa uchunguzi zaidi.
Kwa ushauri, maswali na maoni unaweza wasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim..........!
GAUTI ( GOUT ) HUSABABISHA ULEMAVU
#0759490202
Magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Gauti ni moja ya magonjwa yanayosumbua watu wengi kwa Tanzania. Gauti husababishwa na mwili kushindwa kutoa kiwango cha Urea katika damu ambacho hutengeneza chumvi chumvi inayo kwenda kuhifadhiwa katika maungio ya mifupa na misuli. Chumvi hii huleta madhara ya kuumiza eneo husika na kuharibu kabisa muonekano wa eneo husika.
DALILI ZA GAUTI
1: Maumivu ya eneo lililoathiriwa
2: kutoka nundu moja au nyingi ndogondogo katika eneo husika
3: eneo husika kuwa jekundu sana na baadae kubadilika kuweka vialama vyeupe
4: Nundu kupasuka na kutengeneza vidonda ambavyo kupona ni kazi sana.
5: kushindwa kutumia sehemu iliyo athirika
NINI CHAKUFANYA
1: kupata ushauri wa daktari unapopata matatizo haya
2: kula lishe bora inayowezesha kupunguza utengenezaji wa uric acid na kuongeza utoaji wa sumu hio mwilini
3: kunywa maji mengi na mazoezi
Unaweza kuwasiliana nami kwa ushuri, elimu na maswali
#0759490202
Ahsante
AFYA YA NGOZI
1: kula vyakula vyenye ant-oxidant
2: mazoezi na kupumzika
3: kunywa maji mengi
YOUR HEALTH AND AGE ARE REFLECTED
ON YOUR SKIN.
MADHARA YA SICKE CELL KWENYE MIFUPA
Sickle cell ni ugonjwa unaosababishwa na chembe hai nyekundu za damu badala kua na umbo la donati nzuri huharibika na kujikunja na kutemgeneza k**a ndizi mbinuko hivi. Hii husababisha chembe hai hizi kushindwa kupita katika mishipa ya damu midogo na kuziba kusiba. Hii husababisha maeneo yanayopata damu kutoka kwenye mishipa hii kuanza kufa kutokana na kukosa hewa na chakula. Dalili nyingi huonekana katika mfumo wa mifupa na hewa. Mifupa inayo athirika zaidi ni ile ya miguu, kiuno, na kifua ila huweza kuathiri mifupa yote ya mwili. Maumivu ya mifupa huwaathiri watu wenye matatizo ya sikle cell mara kwa mara. Na iwapo isipopata matibabu haraka mifupa inayokosa damu huanza kufa na kuoza taratibu taratibu.
Unaweza kumsaidia mgonjwa kwa kufanya yafuatayo.
1: Kuhudhuria kiliniki ya matatizo hayo bila kukosa
2: kupata lishe bora ili kutemgeneza kiwango cha damu kufidia kile kilichoharibika.
3: kuepuka vyanzo vinavyohatarisha afya ya mgonjwa
4: kufanya kazi za kawaida, kupumzika na kunywa maji mengi na matunda mara kwa mara
5: kupata matibabu sahihi iwapo hali hio itajitokeza
Kwa maswali, ushauri na maoni wasiliana nami
0759490202
Dr Kassim.
DAWA ZA PRESHA HUPUNGUZA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA.
Moja ya madhara yatokanayo kutokana na matumizi ya dawa za presha ni kupungua kwa nguvu au uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Kwa muda dawa zinapokua kwenye mzunguko wa damu huingiliana na fiziolojia ya uume kusimama na matokea unashindwa kusimama kabisa hali yakua unatamani kufanya tendo hilo.
Unaweza kubadili dawa zinazoleta madhara hayo na kutumia dawa rafiki na afya yako ya uzazi.
Kwa maswali, ushauri na elimu unaweza kuwasiliana nami.
#0759490202
UPOFU KUTOKANA NA KISUKARI
0759490202
Kiwango kikubwa cha sukari husababisha mishipa ya damu kuziba na kupasuka na kumwaga damu kwenye majimaji ya jicho. Pia husababisha kuota kwa mishipa mingi katika retina nyuma ya jicho ambako hua ni sehemu mwanga unapokusanyika kwa ajili ya kupeleka taarifa kwenye ubongo. Uotaji wa mishipa ya damu huziba sehemu hii na miale ya mwanga kushindwa kutengeneza umbo la kitu hivyo kushindwa kupeleka taarifa katika ubongo.
DALILI ZA KUANZA UPOFU
1: kuona giza giza
2: kushindwa kuona rangi za kitu
3: kushindwa kuona usiku
4: jicho kubadili rangi
5: kushindwa kuona vitu vya pembeni na kuona katikati tu
Unaweza kuepuka matatizo haya kwa kufanya yafuatayo
1: kutumia dawa sahihi za kisukari
2: kupima macho mara kwa mara
3: kutumia mboga mboga zenye vitamin A
Dr Kassim
0759490202
KULALA KUNAONGEZA UREFU
0759490202
Unapoamka pingili za mgongo hua zime pumzika na kuachana kidogo hivyo huongeza urefu wako kidogo. Unapoanza kutembea urefu hupungua kutokana na pingili kujishindilia tena chini na hiyo husababisha mtu kurudia katika urefu wake wa kila siku.
Unaweza kulike, kushare au kucomment.
Maswali maoni na ushauri
#0759490202
UTE UTE WA MAGOTI (SYNOVIAL FLUID)
Tunza viungo vyako unapokua kijana ili ukifika uzeeni viweze kukutunza vizuri. Ute ute wa viungo ni muhimu sana kwa inapunguza kuharibika kwa magoti. Kula karanga, bamia, almond, bamia na maji mengi ili kuongeza utengenezaji aa ute ute huu kwa wingi.
Dr Kassim
0759490202
EPUKA ULEMAVU WA MIGUU
Magoti ni muhimu kwa afya ya miguu. Watu wengi wanateseka na maumivu ya magoti na wengine hua makali kushindwa hata kufurahia maisha. Jali afya ya magoti kwa kula vyakula sahihi, virutubisho sahihi na mazoezi yanayotakiwa.
Dr Kassim
0759490202
Epuka kuwa mlemavu wa miguu
Maoni maswali
#0759490202
JONGOO HAPANDI MTUNGI ( IMPOTENCE )
0759490202
Maisha ya kisasa tuliochagua yanatuathiri sana kiafya. Vyakula tunavyokula na kiwango cha mazoezi tunachofanya kinaelezea hali ya kiafya tutakayokua nayo. Wanaume wengi kwa sasa wana athiriwa na tatizo la nguvu za kiume.
Ukosefu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kusimamisha uume au kusimamisha na kufika kileleni chini ya dakika 1 na kushindwa kusimamisha kabisa. Wengi niliowahudumia hua na hamu ya kuendelea na tendo na wako na wake zao wanaowapenda lakini hali hii huwatokea.
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
1: magonjwa ya presha na utumiaji wa dawa zake
2: magonjwa ya kisukari na dawa zake
3: utumiaji wa baadhi ya dawa za magonjwa kwa muda mrefu
4: uzito uliopitiliza
5: magonjwa ya mafuta katika mishipa ya damu
6: magonjwa ya moyo
7: msongo wa mawazo
8: lishe duni/ isio na tija
9: ukosefu wa mazoezi
10: umri
Afya bora itasaidia kuboresha mfumo wa uzazi na kutengeneza mbegu bora kabisa. Unahitaji kujali afya yako ili kufurahia ndoa yako. Watu wengi nimeweza kuwasaidia na kupona tatizo hili kabisa.
Kwa mawasiliano ushauri, maoni na maswali tunaweza kuwasiliana kwa namba hapa chini.
#0759490202
MIGUU MPANTI ( MATEGE - RICKETS )
Call #0759490202
Dr. Kassim
Matatizo ya matege huathiri kuanzia utotoni na madhara huendelwa mpaka ukubwani. Hii husababishwa na ukosefu wa virutubisho muhimu katika ukuaji wa mtoto hasa madini ya calcium na vitamin D. Ukosefu huathiri uimara wa mifupa na matokeo yake ni kuwa na mifupa laini inayopinda au kuvunjika rahisi na mtoto kuwa mlemavu. Madhara haya yanaweza kuzuilika iwapo mtoto atapata matibabu sahihi utotoni kabla tatizo halijakomaa
Kwa maswali, ushauri na kuelimishana piga.
#0759490202
MADHARA YA KISUKARI NA KUKATWA MIGUU
Kisukari ni gonjwa hatari sana kwani hushambulia na kuleta madhara kila mfumo wa mwili ambako damu hufika k**a ubongo, moyo, figo, uzazi n.k. sukari huziba mishipa midogo ya damu (capillary) na kuzuia damu kufika katika maeneo inakohitajika kwa chakula, hewa ya oksijeni na kuondoa taka mwili. Mfano katika mfumo wa mifupa na misuli damu husaidia kupeleka mahitaji muhimu katika maeneo haya. Kuziba kwa mishipa ya damu k**a matokeo ya kuchomwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu hukosesha eneo husika kukosa damu.
DALILI ZA KUZIBA MISHIPA YA DAMU
1: eneo lililoathiriwa kuwa kavu, baridi, na kusinyaa
2: kukata kwa mawasiliano ya fahamu katoka eneo husika
3: kupinda kwa eneo la mwishoni k**a vidole
4: kubadilika rangi kwa eneo husika
5: kutoka vidonda
6: kumeguka kwa nyama au viungo k**a vidole
Na matokeo yake ni kuanza kupata vijidonda vidogo vidogo katika maeneo hayo ambavyo baadae huongezeka na kuwa vikubwa. Vidonda hupata maambukizi ya bakteria na hugoma kupona kwani dawa wala kinga ya mwili haiwezi kufika maeneo hayo kushambulia vijidudu na kuponesha kidonda. Baada ya muda maambukizi haya hufika katika mfupa au hua kidonda ndugu na hivyo matibabu yake huwa na kukata eneo husika ili kuzuia kidonda hicho kumtesa mgonjwa na kusambaa zaidi.
MATIBABU NA NINI CHAKUFANYA
1: Hakikisha una daktari anayefatilia afya yako kwa karibu na anakushauri juu ya ugonjwa huu.
2: fata mlo unaoshauriwa na daktari wako
3: kunywa dawa zako k**a unavyoshauriwa na mtaalamu wako wa afya
4: fanya mazoezi sahihi kutokana na tatizo lako
5: jielimishe kila siku juu ya tatizo lako
The vision is to shift health sector from curative medicine to preventive medicine.
Dr Kassim #0759490202
MAGONJWA YA MAGOTI
Magonjwa ya magoti yanazidi kuongezeka nchi zinazoendelea na hii husababishwa na yafuatayo.a
1: uzito mkubwa
2: magonjwa ya sukari
3: mazoezi yasiyo na ushauri wa mtaalam
4: vyakula vya kileo
5: magonjwa ya kurithi
DALILI
1: Maumivu ya magoti na miguu
2: vichomi katika magoti
3: kuvimba magoti
4: kushindwa kukunja magoti
5: kushindwa kutembea
Madhara ya maradhi haya kwa muda mrefu husababisha magoti kupata shida zifuatazo
1: kumalizika kwa uteute katika magoti
2: kusagika kwa gegedu
3: kuchanika kwa tendon
4: kusuguana kwa mifupa ya goti
Wahi kupata matibabu kwa daktari wako kabla hali haijawa mbaya kwani madhara yakishakua makubwa hulazimika kufanya matibabu ya upasuaji ambayo ni ghali sana na huchukua muda mrefu kupona.
MATIBABU YA NYONGA
Nyonga ni muunganiko wa mifupa mbalimbali inayolinda mfumo wa uzazi, mmen'genyo wa chakula na mkojo. Mifupa hii ni muhimu sana kwa ulinzi wa ogani zinazopatikana maeneo hayo.
Mfupa wa paja unaungana na mfupa wa tako na kutengeneza maungano ya nyonga. Kutokana na mazingira mbalimbali hupelekea maungano haya kusagika au kutanuka na kusababisha kushindwa kupata damu ya kutosha katika kichwa cha mfupa wa paja. Hii husababisha kichwa cha paja na mfuniko wa nyonga kuanza kufa na kupoteza ute ute na gegedu zinazolinda mifupa hii. Madhara yake na kufa na kuungana kwa mifupa hii miwili.
WALIO HATARINI KUATHIRIKA
1: Kisukari
2: wajawazito
3: siko seli
4: uzito mkubwa
DALILI ZA MAGONJWA YA NYONGA
1: Maumivu makali ya nyonga na mfupa wa paja
2: upande ulio athirika mguu kuwa mfupi
3: mguu ulioathirika kushindwa kukunja katika maungio.
4: kushindwa kutembea
5: kushindwa kushiriki tendo la ndoa vizuri
MATIBABU HOSPITALI
1: kubadilisha nyonga yote na kuweka ya bandia ambayo matibabu yake ni ghali sana
2: kuishi na matatizo yako kwa dawa za maumivu
TIBA NA KINGA MBADALA
Unaweza kuijali afya ya nyonga yako na kula na kufanya mazoezi sahihi yenye tija na kuokoa nyonga yake.
Unaweza kutumia tiba lishe ili kuongeza utengenezaji wa uteute na gegedu na kuilinda nyonga yako
KUSAGIKA KWA MIFUPA WANAWAKE
wanawake wengi kipindi cha uzee huathiriwa na maumivu makali ya mifupa hasa uti wa mgongo, nyonga, miguu na mikono. Hii husababishwa na kuachwa kuzalishwa kwa homoni ya estrogen katika ovari na tishu za uzazi. Homoni hii husaidia kulinda mifupa isiweze mon'gonyoka. Kukosekana kwake mifupa huyeyuka na kuacha kuboreshwa hivyo hua laini na huvunjika kwa urahisi.
Wagonjwa wengi huanza kupata dalili zifuatazo homoni hii inapoachwa kuzalishwa.
DALILI ZA UPUNGUFU WA ESTROGEN
1: Maumivu makali ya mifupa kushindwa kutembea na kufanya shughuli za kawaida
2: kushindwa kuchuchumaa au kusimama
3: kuvunjika mifupa kwa urahisi zaidi
4: mwili kuwaka moto
5: maungio kupwita kwa uvuguvugu
Wagonjwa wengi hulazimika kufanyiwa upasuaji kutokana na kuvunjika ila kwa sababu ya umri wao, hua ni ngumu kuhimili upasuaji kwani dawa za usingizi kwao ni kali hawataamka na kinga iko chini pia jeraha halitaweza kupona kwa haraka.
MATIBABU
1: kupatiwa homoni
2: dawa za kuongeza uimara wa mifupa
3: dawa za kuboresha gegedu na uteute wa maungio.
YOUR HEALTH FOR YOUR WEALTH
TIBA YA MGONGO BILA UPASUAJI
Dr. Kassim
0759490202
Mazingira ya kiafrika katika shughuli za kila siku za utafutaji eidha kulima, kufuga, cherehani, ualimu, kukaa muda mrefu ofisini au michezo hupelekea presha ya muda mrefu katika uti wa mgongo. Presha hii husababisha nyama kuvutana na pingili za mgongo kukaribiana. Matokeo yake ni kuisha kwa ute wa mgongo na kusagika kwa gegedu za uti wa mgongo.
DALILI ZA KUSAGIKA PINGILI ZA MGONGO
1: Maumivu makali ya mgongo yanayozunguka kiouno hushuka mpaka kwenye mapaja.
2: kushindwa kutembea na kukaa kwa muda mrefu
3: Kushindwa kutembea
4: kushindwa kushiriki tendo la ndoa
5: ganzi na vichomi miguuni kuanzia katika unyayo
6: kushindwa kulala vizuri na kugeuka unapolala
Wagonjwa wengi hupuuza dalili za awali ambazo hua ni
1: kuhisi mgongo umefunga mzigo unaogasi muda wote
2: maumivu madogo ya mgongo
Wagonjwa wengi huanza matibabu wanapokua na maymivu makali na kushindwa kufanya majukumu yao ya kila siku. Na wengi huanza mazoezi ili kush*tua misuli na kurekebisha mifupa ila hua ni ngumu kuponya tatizo. Wengi hufanya upasuaji ili kuzuia uharibifu zaidi wa uti wa mgongo na kupunguza msuguano ila matokeo hua si ya kuridhisha kwa wengi na kuishia kupata ulemavu.
Unaweza kuanza kuulinda na kuboresha afya yako ya mifupa na kuanza kutumia tiba lisha zinazo saidia kulinda kusagika kwa pingili za mgongo. Nimeweza kuwasaidia wengi, karibu nikusaidie.
*_JIPATIE SULUHISHO_*
*TEZI DUME ( BPH )*
*~~_0759490202_~~*
*DALILI ZA UVIMBE WA TEZIDUME*
Tezi dume hupatikana katika mfumo wa uzazi wa kiume pekee chini ya mlango wa kibofu likiunganisha njia ya mkojo na njia ya kupitisha mbegu za uzazi kwa mwanaume. Lenyewe likitengeneza uteute mweupe ( Semen ) muhimu kwa ulinzi na chakula kwa mbegu za uzazi. Tezi dume hua dogo sana utotoni na hukua kulingana mtu anavyokua. Hivyo basi kufikia umri wa miaka 40 na kuendelea hukua na kuanza kuziba njia ya mkojo na uzazi.
Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:-
1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara
2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
3.Kushindwa kuanzisha kukojoa hali ya kua una mkojo mwingi na kushindwa kumaliza kukojoa hali ya kua mkojo umeisha.
4.Mchirizi/nguvu ya kurusha mkojo mbali kuwa dhaifu
5.Mkojo kukatakata unapofika karibu au mwisho
6.Kujichafua wakati wa kukojoa
7.Damu kwenye mkojo
8.Kushindwa kukojoa kabisa.
9.Kupata mkojo mchache sana
Ni zipi athari za tezi dume k**a haitawahi kutibiwa?
Tezi dume ni k**a maradhi mengine, inatibika bila wasi. Hata hivyo endapo matibabu yatachelewa athari zifuatazo zinaweza kupatikana:-
1.Kushindwa kabisa kukojoa
2.Kupatwa na maambukizi ya UTI
3.Kupatwa na vijiwe kwenye kibofu
4.Uharibifu wa njia ya mkojo toka ktk figo (ureter )
5.Figo kuharibika
6.Kifo
*~~_0759490202_~~*
🔴🟠🟡🔵🟢🟣🔴🟠🟡🔵
**KWA MATIBABU NA USHAURI*
*Dr. KASSIM**
*_*PIGA: 0759490202_**
_*WASAP: 0759490202*_
0629194363
SULUHISHO
1: Uvimbe via k**e vya uzazi,
2: Uvimbe wa tezidume,
3: Uvimbe/Kinyama cha bawasiri.
*UJUE MFUMO K**E WA UZAZI*
Via vya mwanamke vina sehemu kuu nne. Nazo ni:-
1: O***y (kiwanda cha mayai)
2: Fallopian tube (mirija ya mayai)
3: Uterus (Nyumba ya uzazi)
4: Birth canal ( Njia ya kuzalia)
Katika sehemu zote hizo zinaweza kupata vimbe ni kusababisha dalili sawa au tofauti kulingana na chanzo cha uvimbe huo. Dalili za hatari za ujumla zinaweza kujumuisha zifuatazo.
*DALILI ZA UVIMBE KATIKA VIA K**E VYA UZAZI*
➡️Kutokwa Na Damu Nyingi Sana Isiyokauka Katika Hedhi,Hii Inaweza Kusababisha Hali Ya Kupungukiwa Damu(Anaemia)
➡️Kuhisi Kuna Kitu Kigumu Kwa Ndani Chini Ya Kitovu Hata Ukigusa Kwa nje,Inaweza Kusababisha Kuhisi Kukojoa kila saa Au Maumivu wakati wa Kukojoa Na Haja Kubwa
➡️Kutokwa na Maji Maji au uchafu wenye harufu mbaya au ambao hauna harufu mwingi na mweupe, njano, ugolo au kahawia
➡️Kupata Maumivu Makali Ukikaribia Siku Zako Za Hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe
➡️Kupata Hedhi nyepesi Sana Au Hedhi Nzito Sana Yenye Mabonge Ambayo Huwa na rangi Ya brown Au Nyeusi
➡️Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Na Ukifanya Unapata Maumivu Makali Sana Hata Baada Ya Kumaliza
➡️Hedhi zisizokuwa na mpangilio Maalum,Kila Mwezi Tarehe Zinabadilika Sana Wakati Mwingine Unapata Hedhi Mbili Ndani Ya mwezi Mmoja Au Inapita Miezi kadhaa bila Kuona Hedhi
➡️Kutopata Ujauzito, Kupata Maumivu Makali Sana Ya Nyonga,Kiuno Na Chini Ya Kitovu(Inaweza Kuwa Upande Mmoja Au Pande Zote.
Uvimbe Usipotibiwa Huwa Unaongezeka Kila Siku Na Madhara Yake Ni Makubwa sana K**a Kutopata Ujauzito,hata kifo
*~~_0629194363_~~*
🟣🟢🔵🟡🟠🔴🟣🟢🔵🟡
*DALILI ZA UVIMBE WA TEZIDUME*
Tezi dume hupatikana katika mfumo wa uzazi wa kiume pekee chini ya mlango wa kibofu likiunganisha njia ya mkojo na njia ya kupitisha mbegu za uzazi kwa mwanaume. Lenyewe likitengeneza uteute mweupe ( Semen ) muhimu kwa ulinzi na chakula kwa mbegu za uzazi. Tezi dume hua dogo sana utotoni na hukua kulingana mtu anavyokua. Hivyo basi kufikia umri wa miaka 40 na kuendelea hukua na kuanza kuziba njia ya mkojo na uzazi.
Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:-
1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara
2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
3.Kushindwa kuanzisha kukojoa hali ya kua una mkojo mwingi na kushindwa kumaliza kukojoa hali ya kua mkojo umeisha.
4.Mchirizi/nguvu ya kurusha mkojo mbali kuwa dhaifu
5.Mkojo kukatakata unapofika karibu au mwisho
6.Kujichafua wakati wa kukojoa
7.Damu kwenye mkojo
8.Kushindwa kukojoa kabisa.
9.Kupata mkojo mchache sana
Ni zipi athari za tezi dume k**a haitawahi kutibiwa?
Tezi dume ni k**a maradhi mengine, inatibika bila wasi. Hata hivyo endapo matibabu yatachelewa athari zifuatazo zinaweza kupatikana:-
1.Kushindwa kabisa kukojoa
2.Kupatwa na maambukizi ya UTI
3.Kupatwa na vijiwe kwenye kibofu
4.Uharibifu wa njia ya mkojo toka ktk figo (ureter )
5.Figo kuharibika
6.Kifo
*~~_0629194363_~~*
🔴🟠🟡🔵🟢🟣🔴🟠🟡🔵
*DALILI ZA UVIMBE/KINYAMA CHA BAWASIRI*
Ishara na dalili za bawasiri kawaida hutegemea aina ya Bawasiri
*BAWASIRI YA NJE.*
Hizi ziko chini na nje ya ngozi karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa. Ishara na dalili zinaweza kujumuisha:
1. Kuwasha katika maeneo yaliyozunguka sehemu ya haja kubwa
2. Maumivu au usumbufu
3. Kuvimba kuzunguka sehemu ya kutolea haja kubwa
4. Mara nyingine yaweza Kuvujadamu au k**a michubuko
5. Kutokwa na kinyama baada ya kwenda haja.
*BAWASIRI YA NDANI* .
Bawasiri ya ndani iko ndani ya sehemu ya kutolea haja. Kawaida huwezi kuziona au kuzihisi, na mara chache husababisha usumbufu. Lakini kukaza au kuwasha wakati wa kupitisha kinyesi kunaweza kusababisha:
1. Kutoa haja/kinyesi chenye damu na maumivu yasiyo makali. Unaweza kuona kiasi kidogo cha damu nyekundu kwenye haja yako.
2. Maumivu na muwasho sehemu ya haja.
**KWA MATIBABU NA USHAURI*
*Dr KASSIM**
*_*PIGA: 0629194363**
_*WASAP: +255629194363*_
Live health Live wealth
Click here to claim your Sponsored Listing.
Videos (show all)
Category
Website
Address
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
EMANUELY MSHAURI WA AFYA NA MTOA HUDUMA WA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA AFYA;!?MFANO TEZ DUME BILA UPASUAJI BAWASIRI UTI PID 0672518275
Kijitonyama (Near Sinza Maalum School)
Dar Es Salaam
We connect student with internationally accredited university, we deal with medical tourism and High
Mliman City Dar-es-salaam, Kinondoni, @Afya_kavishe
Dar Es Salaam
Tiba kwa matatizo ya UTI,PID,SUKARI,VIDONDA VYA TUMBO,UZAZI,TEZI DUME,NGUVU ZA KIUME,UVIMBE, n.k
Muhimbili
Dar Es Salaam
Tunawasaidia watu kuboresha afya ya uzazi, kupunguza uzito na kitambi, kuboresha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ngozi. Tuma ujumbe neno afya kwenda WhatsApp 0659414711 au piga s...
Charambe Magengeni, Mbagala Rangi Tatu
Dar Es Salaam
We're working with Internal Medicine Specialist, Gynecologist, Pediatrician and Medical Directors.