Don_tz
Social networks Influencer || Young Africans Fans 🔰 || Joker || Content creator
had a cage match in the club 😳 he had his artists and locked inside a cage while he performed.
_________________________
Rapper Kutoka Marekani Amezua Gumzo Baada Ya Kuonekana Akitumbuiza Huku Akiwa Amewafungia Wasanii Wake Pamoja Na Kwenye Banda La Chuma Huku Akiwa Juu Ya Banda Hilo Akitoa Burudani.
Wapo Wanaodai Kuwa Playboi Carti Amefanya Kitendo Hicho K**a Adhabu Kwa Wasanii wake Hao Kwa Ukosefu Wa Nidhamu Kwani Walichelewa Kufika Kwenye Tamasha La (Miami) Jumamosi. Pia wapo wanaohusisha Jambo Hilo na Imani Za Kishetani (Illuminati ) Kwani Rapa Playboi Carti Amekuwa Akihusishwa Na Tuhuma Hizo Kutokana Na Show Zake Kuwa Na Maudhui Ya Kutisha.
Rapa Playboi carti Anamiliki Record label Inayoitwa "O***m" Na Ina Wasanii Watatu (3) , Pamoja Na Kundi La
✍:
NILICHO JIFUNZA KWENYE JUA KALI KUPITIA SCENE YA LUKA
Najuwa Wengi Wenu Ni Wapenzi wa Mziki Pia Na Filamu
Na Wengi Wakahaji wa TZ wanafuatilia tamsilia ya Jua Kali
Ni Nzuri afu Kuna Mafunzo Mengi ,Afu Inagusa Sehemu Zote Za Maisha Ya Mwanadamu
, mapenzi,kuamizwa na kupendwa ,chuki ,tamaa ,fitina ,na mambo mengine
So Ila Scene Ninayo Ipenda Mimi Ni Ya Mwamba Anaye Itwa anaye Igiza humo K**a
Kwanza Nimependa ,life style ya kwao maisha moja ya chini sana ,Afu Mwamba Ana 🌟 Fulani Hivi la Kupendwa na Mademu Ila Aliye Mpenda YEYE Akamshukulia Poa Kisa Hana Cha Mfuko
Mmmh Kwenye Mahusiano yake ya kwanza nilicho penda Ni yeye Kujitowa kwa Hali yote Ili Apate Kumsaidia Mpenzi wake japo Kuwa hana Cha Zaidi ila icho Kidg Alikuwa napata alijitahidi achangie na mwenzake ila kumbe umupendae akupendi ndo njisi Mapenzi ilivyo ,
Ila muda wa mawazo na muda alio pitia akiwa hospitali
Mama yake akamtafutia mtu wa kumtolea mawazo
DEMU alitokea kumpenda sana ila mwamba alimchukulia k**a ndg wake japo kuwa demu alikuwa na mpenda na k**a tunavyo juwa kwenye mapenzi akunaga udg wala ukubwa cha muhimu, Eshima na kusikiliza au mapenzi yawe ya ukweli
Si unajuwa mjini akukosagi wale madg wapambanaji afu wanateseka kwenye mapenzi hao Yani kwenye dunia iyi wanao teswa na mapenzi ni matajiri sisi masikini ndio tuna enjoy mapenzi
K**a ni nimedanganya Mungu nisamehe
Brother akapata bonge moja la demu afu ukimuangali mwamba na demu kwenye Ali ya maisha awapo sawa ila demu alicho angali ni upendo na umuhimu wa mwanadamu kwa Ali alivyo mkuta nayo and then
Mambo yakaiva
Sasa IVI mwamba ana enjoy mapenzi Yani ukitizama scene zao kwenye iyo series utahisi mambo k**a kweli IVI
Yeah Kuna wanao pitia ayo maisha
So nilicho Jifunza ni kwamba
Unaye mpenda Kampenda mwengine, mwengine naye ana Mwengine,
Moyo sukuma damu so mashine wimbo wa
Anaandika Mange Kimambi
Huyu mtu si kuna kipindi alisema hataki kushindanishwa na wasanii wa bongo sababu yeye ni Level za kina Wizkid? Sasa mbona karudi mdogo mdogo kushindana na wasanii wa Tz? Nyie nimechekaaaaaaa mimi. Kha!!!! 🤣🤣
Kwahiyo kupambana na wanageria ndo basi tena tume give up??? 🤦🏽♀️🤦🏽♀️ . Yani mwaka 2023 bado unakomaaa na YouTube mdogo wangu? Hivi umeona wanaigeria YouTube zao jinsi hazina Issue ila ndo wanaomake $$$$$$. Wanamuziki wa maana duniani wana streams kali za spotify na Apple Music sio YouTube jamani. 😭😭
Nachompendeaga Alikiba ni hapa tu, ye huwa hapambani na mtu ila watu ndo huwa wanapambana nae. Kiba huwa anatoa hit alafu huyo anarudi zake kumtesa Amina then wasaniii wengine ndo wanaanza kuhangaika na mziki aliotoa…..
We nae embu mpe mtoto wa watu talaka aendeleee na life yake bwana. Unachofanya ni unyayasaji wa kijinsia alafu wala haikupendezi. Mambo ya kutesa wanawake na kutoheshimu wanawake ni ya huyo mwenzio wewe hizi sio zako. Either be a good husband ishi na mkeo, weka ukoo pembeni au mpe talaka binti wa watu. Hizi tabia hazikupendezi Kiba. Alafu next time usiwe mnafki kuoa wanawake wa kujistiri wakati nafasi yako inapenda wavaa vimini. Wewe size zako ni wadada wa mujini hao mabinti wa kiislaam sio zako kabisaaa.
Kwenye picha ni Diamond na kanye
Umewahi kula hii kitu 😂😂
Mwaka 2003 lilitokea tukio kubwa zaidi la ujambazi ambalo labda ndio lililotumia akili na maarifa zaidi pengine kushinda tukio lolote la ujambazi kwa miaka 50 iliyopita.. Tukio hili lilishuhudia wahusika wakitokomea na vitu vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 230 (USD 100 Millions).
Uthubutu, ubunifu, akili na maarifa yaliyotumika kutekeleza tukio hili limefanya mpaka kampuni ya utengenezaji filamu ya Paramount Pictures kununua haki za hadithi ya tukio hili ili watengeneze filamu itakayo husu mkasa mzima wa tukio hili..
TUKIO LENYEWE
Mwanzoni mwa mwaka 2000 mfanyabiashara wa madini ya almasi Leonardo Natarbartolo alifungua ofisi mpya jijini Antwerp nchini ubelgiji, mji ambao ndio kituo cha biashara ya madini ya almasi ulimwenguni.. Ofisi yake ilikuwa katikati kabisa ya kitovu cha mitaa ambayo ndio hasa biashara ya almasi hufanyika. Natarbartolo alijihusisha hasa katika manunuzi ya kiwango cha kawaida cha almasi (small deals) lakini jambo ambalo watu hawakulifahamu ni kwamba walikuwa wamemkaribisha moja kati ya manguli wa wizi wa almasi ulimwenguni.
Kutokana na kujitambulisha k**a mfanyabiashara mwenzao, Natarbartolo alipata fursa ya kuingia katika Kuba (vault) za wafanyabiashara wengine ili aweze kukagua mali kabla ya kuinunua na aliutumia fursa hii kuyasoma mazingira ya Ofisi hizo zilizo hifadhi madini na kuja kufanya uhalifu kesho yake..
Natarbatolo aliishi hivi mjini Antwerp kwa miezi kadhaa kabla hajakutana na mfanyabiashara ya almasi Myahudi ambaye kukutana kwao kulipelekea kufanikisha tukio ambalo liliushangaza ulimwengu na limeendelea kuushangaza ulimwengu mpaka leo hii..
MAANDALIZI
Mwaka mmoja baada ya Natarbatolo kuingia Antwerp, siku hiyo akiwa kwenye mgahawa akinywa kahawa alifuatwa na Mfanyabiashara wa Kiyahudi ambaye alimuomba wazungumze faragha kuhusu biashara muhimu. Baada ya kukaa nae chemba Myahudi akamueleza azma yake kuwa anataka amshirikishe katika tukio la ujambazi na alimuuliza k**a anahisi Vault ya Antwerp Diamond Center inaweza kuibiwa... Natarbartolo akamjibu kwa kifupi kuwa atamjibu swali hilo k**a yuko tayari kumlipa dola laki moja. Na Myahudi huyo akakubali.
Siku mbili baadae Natarbatolo alielekea ilipo Main Vault ya Antwerp Diamond Center (kumbuka kutokana na yeye kujitanabaisha k**a mfanyabiashara ya almasi kwa mwaka mmoja aliokaa Antwerp hivyo alifanikiwa kujisajili ili aweze kuhifadhi almasi zake katika Main Vault ya Antwerp)..
Kitu ambacho watu wote wakiwepo walinzi hawakikugundua ni kwamba katika mfuko wa pembeni wa suti yake aliweka peni ambayo inaonekana k**a peni ya kawaida lakini ilikuwa ni peni maalumu iliyokuwa na kamera ndogo ya siri.. Kamera hii ilimsaidia Notarbartolo kurekodi mandhali yote ya ndani ya vault na jinsi ulinzi ulivyo...
Kesho akakutana na yule myahudi na kumpa jibu lake kuwa ni immposible kuvunja na kuiba main vault ya Antwerp inayohifadhi almasi zote zilizopo katika mji huo.. Akampa ile peni ambayo imerekodi mandhali ya Vault pia akampa na maelezo ya mdomo kwanini haiwezekani kuiba katika ile vault na akamsisitiza zaidi juu ya matabaka ya ulinzi (security levels) ambayo yanalinda vault hiyo. Matabaka hayo yapo k**a ifuatavyo..
1) Combination dial ambayo unatakiwa uingize tarakimu nne za siri
2) Sehemu ya kuingiza funguo maalum
3) Sensor ya mitetemo (seismic sensor)
4) geti la Chuma lililo sambamba na mlango
5) sensor ya sumaku (magnetic sensor)
6) Kamera ya nje ya mlango
7) Keypad ya kuzima alarm
8 ) sensor ya mwanga (light sensor)
9) Kamera ya ndani ya vault
10) sensor ya joto na mjongeo (heat & motion sensor)
Jumlisha; walinzi na ulinzi unaozunguka jengo hilo.. Natarbartlo akamsisitizia yule myahudi "..it is immposible to rob the Antwerp diamond center vault"..
TUKIO LILIVYOTEKELEZWA
Miezi k**a mitano ikapita ndipo Notarbartolo akapokea simu kutoka kwa yule myahudi na safari hii alimuomba wakutane nje kidogo ya mji wa Antwerp... Baada ya kuonana yule myahudi alimchukua Notarbatolo mpaka kwenye nyumba moja inayofanana na ghala kubwa.. Ndani yake Notarbatolo alikuta kitu ambacho hakutegemea kabisa...
Yule myahudi alikuwa ametengeneza replica inayofanana kabisa na main vault halisi ya kuhifadhia almasi ya hapo mjini Antwerp.. Pia akamtambulisha kwa watu watatu ambao pia aliwakuta hapo.
Natarbartolo amekataa kabisa mpaka leo hii kutoa majina halisi ya watu hawa lakini anawasimulia kwa nicknames walizokuwa wanatumia, kulikuwa na The genius (huyu ni mtaalamu wa mambo ya kidigitali na eletroniki), kulikuwa na The monster ( huyu alikuwa ni mekanika na mtaalamu wa umeme) na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye walimuita The King of Keys (huyu ni mtaalamu wa kufungua vitasa na makufuli ya aina zote pamoja na kufoji funguo)..
Yule myahudi aliwaambia kazi ya ile replica ni wao wafanye mazoezi na kuitafiti na hatimae wajue namna gani wataweza kuingia ndani ya vault ya Antwerp pasipo kugundulika..
Iliwachukua miezi mitano Natarbartolo na wenzake kufanya mazoezi na kutengeneza perfect plan itakayowawezesha kuingia katika vault na kuiba pasipo kugundulika..
SIKU YA TUKIO..
Siku moja kabla ya tukio, yaani February 14 2003 Notarbartolo alienda mchana kwenye vault kana kwamba kuna almasi ameenda kuhifadhi lakini akajitahidi akae karibu na kifaa cha kuhisi joto na mjongeo (heat/motion sensor) na kwa kutumia hair spray aliyoificha ndani ya jaketi lake akapulizia juu ya kifaa hicho hivyo kukifanya kisiwe na uwezo wa kuhisi mabadiliko yoyote ya joto au movement ndani ya vault...
Ilipowadia siku ya tukio lenyewe.. February 15
Notarbartolo na wenzake waliendesha gari mpaka karibu kabisa na jengo lenye vault. Jengo lilikuwa na ulinzi mkali kwa mbele lakini nyuma ya jengo hakukuwa na ulinzi mkubwa kwani watu wa ulinzi walikuwa na imani kubwa sana na teknolojia yao inayosaidia kulinda jengo lao..
Wote wakashuka kwenye gari isipokuwa Notarbatolo alibaki kwenye gari. Baada ya kushuka wote wakazunguka nyuma ya jengo ambako walitumia ngazi ambayo The genius alikuwa ameificha hapo mchana wake wakapanda mpaka ghorofa ya pili.
Baada ya wote kupanda katika balcony ya ghorofa ya pili ilibidi wakae mbali na madirisha kwani yote yalifungwa vifaa vya kuhisi joto na movement na vikigundua tu kuwa kuna mabadiliko ya joto au movement basi alarm inalia..
Alichokifanya The genius alichukua kitambaa kirefu kilichotengenezwa kwa polyester kujifunika na kusogolea kifaa kile cha heat and motion sensor.. Kutokana na yeye kujifunika kwa nguo yenye material ya polyester hii ilipelekea kifaa kile kushindwa kudetect kilichokuwa kinatokea na alipokifikia karibu kifaa kile akakifunika kabisa na nguo ile kwahiyo korido ikawa iko salama kwa wao wote kupita.. Wakafungua madirisha wakaingia ndani na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini kwenye vault..
Baada ya kufika chini nje ya mlango wa vault ambako kulikuwa na giza kutokana na kuzimwa taa.. Wakatumia fursa hiyo kuzifunga kamera kwa mifuko meusi na kisha wakawasha taa.. Baada ya kuwasha taa ilikuwa sasa ni jaribio la kufungua mlango na hapa ndio wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wakikosea kitu kimoja tu maana yake alarm italia na mchezo utaishia hapo..
Kumbuka kuna matabaka kumi ya ulinzi wanayotakiwa wanayotakiwa kuyavuka mpaka waingie ndani.. Tabaka la kwanza ni lile la combination dial ambapo wanatakiwa waingize tarakimu nne za siri! Kabla ya siku hii ya tukio Natarbartolo alifanikiwa kumshawishi muhudumu wa vault wabadilishe mtungi wa tahadhali ya moto (fire extinguisher) jambo ambalo hawakulifahamu ni kwamba mtungi ule ulikuwa na gas ndio lakini ndani yake Natarbatolo aliweka kifaa maalumu kilichokuwa kinachukua data za kamera ya nje ya mlango wa vault! Kwa kutumia kifaa hicho Natarbartolo alinga'amua tarakimu nne za siri ambazo zilikuwa zinahizatijika kuingizwa... Kwahiyo waliingiza tarakimu nne na wakawa wamefanikiwa kwa hatua hii ya kwanza... Bado hatua tisa ili wafanikishe.!
Hatua ya pili changamoto ya pili ilikuwa ni namna gani wangeweza kudisable kifaa cha kuhisi usumaku (magnetic sensor) hii yenyewe ilitengenezwa katika katika hali ya kwamba plate moja ya sumaku iliwekwa kwenye mlango na nyingine ilifungwa kwenye ukuta pembezoni mwa mlango kwa maana ya kwamba mlango ukifungwa kunakuwa na magnetic field inatengenezwa pale katikati na kwa maana hiyo, k**a mtu ukifungua mlango unadisturb ile magnetic field na alarm inalia...
Kwahiyo alichokifanya The genius alichukua plate ndogo ya aluminium aliyoitengeneza nyumbani alafu akaifunga na tape ya gundi kali na kunasisha katika zile plate za sumaku huku na huku yaani iliyopo ukutani na mlangoni (ametumia aluminium ili asiweze kudisturb magnetic field).. Baada ya hapo akafungua screw na zile plate na kuziweke pembeni ya mlango! Kwahiyo zile plate mbili bado zilikuwa na magnetic field katikati yake lakini zilikuwa zimewekwa pembeni ya mlango..
Kwahiyo tayari matabaka matatu ya ulinzi yalikuwa yameshakuwa disabled bado matabaka saba.. Kumbuka kamera ya nje tayari ilishafungwa na mfuko mweusi.
Hatua ilifuata ilikuwa ni kudisable alarm inayo monitor seismic sensor na geti dogo la ndani. Kifaa hiki kilifungwa k**a keypad pembeni kwenye ukuta, kilichokuwa kinatakiwa ni kuingiza tarakimu nne za siri k**a pale juu kwenye mlango.. Tarakimu hizi za siri nazo walikuwa wameshazifahamu kwa kutumia kile kifaa kilichopo ndani ya fire extinguisher kwahiyo waliingiza tu tarakimu na tayari wakawa wamefanikiwa kudisable tabaka hili..
Shughuli ikabaki kwenye kufungua mlango kwa kutumia funguo.! Funguo iliyokuwa inatumika hapo sio k**a funguo hii ya kuweka mfukoni.. Ilikuwa ni funguo kubwa yenye size sawa na mguu wa binadamu!
Sasa ilikuwa ni zamu ya The king of keys kufanya miujiza yake... Kumbuka kuna kifaa chao kile kilichopo kwenye fire extinguisher kinachorekodi kila kinachoendelea kwenye vault kwahiyo kabla ya siku hii ya tukio walikuwa na Picha halisi ya funguo ya mlango ilikuwa inafananaje..
Kwahiyo alichokifanya The king of chains ni kutengeneza funguo inayofanana kabisa na ile funguo halisi.. Lakini kabla hawajaijaribu hii funguo yao ya bandia The king of keys akawaeleza kuwa kwenye zile Picha za video walizonazo aligundua kitu. Kwamba, kila mara kabla mlinzi hajafungua mlango ilikuwa lazima aende kwenye chumba kilichopo karibia na hiyo vault na The king of keys alitaka kujua walinzi wanaendaga huko kufanya nini.. The king of keys alipoenda katika chumba kili hakuamini alichokikuta, ulikuwa ni uzembe wa kiulinzi ambao hakuutegemea utokee Antwerp.. Funguo halisi ya kufungua mlango wa vault ilikuwa imewekwa pale inaning'inia.
The king of keys alichukua funguo halisi akarudi kwenye vault na kuwasisitiza wenzake kuwa angependa watumie funguo ile halisi.. Kwahiyo wakachomeka funguo na kuizungusha kisha wakazungusha ringi (usukani) wa mlango wa vault na mlango ukafunguka bila hiyana.. Kwahiyo kwa nje ya vault walikuwa wamepita vizingiti vyote na kilibakia geti la Chuma lililopo baada ya mlango.. Geti hili ni mageti fulani hivi yanayotumika kwenye vault nyingi lenyewe linakuwa lina nondo dizaini k**a madirisha yetu uswahilini ya nondo na mbao tofauti tu ni kwamba hili lilikuwa ni nondo na chuma pekee hakuna mbao.. Kwakuwa tayari walikuwa wamedisable kifaa cha kumonitor hili geti (pale ukutani unapoingiza tarakimu nne) kwahiyo hapa wakatumia nguvu tu kuliharibu na kuingia ndani..
Kwahiyo kwa walikuwa wamefanikiwa kupita matabaka yote ya ulinzi nje ya vault na wakibakiwa na matabaka machache ya ulinzi ndani ya vault ambayo ni Kamera ya ulinzi, sensor ya mwanga (light sensor) na sensor ya mjongeo na joto (heat & motion sensor)
NDANI YA VAULT..
Baada ya ya kufanikiwa kufungua mlango wa vault kwa mafanikio kabisa sasa changamoto ilibaki ndani ya vault kukabiliana na matabaka matatu ya ulinzi kabla ya kuanza kufungua visanduku vya vilivyohifadhi almasi ambavyo navyo vilihitaji funguo na namba za siri..
Kumbuka kuwa siku moja kabla Natarbartolo alikuwa amepulizia hair spray kwenge kifaa cha kuhisi joto na motion! Lakini ile spray ingesaidia labda kwa dakika tano tu k**a mtu angeingia na baada ya hapo ingeweza kuhisi kuna mabadiliko ya joto.. Kwahiyo k**a wote watatu wangeingia maana yake labda kwa dakika moja au mbili za mwanzo isingehisi kitu lakini baada ya hapo ingeling'amua kuwa kuna mabadiliko makubwa ya joto.. Hivyo bado ilikuwa inatakiwa mtu mmoja tu aingie na aweze kudisable system nzima ya zile alarm na hapo ndipo ilikuwa zamu ya The monster ambaye alikuwa ni mtaalamu wa umeme na mekanika (mechanics) kufanya miujiza yake..
The monster alitembea hatua kumi na moja mpaka katikati ya vault k**a ambavyo alikuwa amefanya mazoezi kwa takribani miezi mitano kwenye replica waliyokuwa nayo nyumbani.. Baada ya kufika katikati ya vault aliinua mikono juu kugusa dari la vault ambalo hapo juu kulikuwa na kiboksi cha umeme ambacho chenyewe ndicho kilikuwa kinakusanya electric pulse kutoka kwenye vifaa vyote vya ulinzi ndani ya vault na kupeleka kwenye system ya alarm.. Yaani kwa mfano k**a light sensor ikihisi kuna mwanga kwenye vault basi itatuma electric pulse mpaka kwenye kifaa hiki na chenyewe kitatuma taarifa juu kwenye system ya alarm na alarm italia..
Kwahiyo alichokifanya The monster ni kufungua mfuniko wa kifaa hiki kisha akazichuna plastiki ya juu inayofunika nyaya na hatimae zile nyaya zikawa wazi, kisha akachukua kipande cha nyaya alichokuja nacho na kufunga kwa ustadi kuunganisha nyaya hizo na kutengeneza 'bridge' ya umeme (alikuwa anafanya re-route) naamini watu wa umeme na fizikia watelewa vizuri..
Kwahiyo baada ya kufanya hii reroute ilimaanisha kwamba umeme uliokuwa unatoka kwenye alarm system unaishia hapo kwenye 'bridge' na kurudi nyuma na umeme uliokuwa unatoka kwenye vifaa vya ulinzi ulikuwa hauvuki hiyo bridge!!
Kwa kifupi ni kwamba mawasiliano kati ya alarm system na vifaa vya ulinzi yalikuwa hayapo hivyo haikujalisha nini kilikuwa kinatokea ndani ya vault, alarm system isingeweza kudetect..
Baada ya hapo wote wakaingia ndani na kuanza kazi ya kufungua visanduku vidogo vilivyopo ukutani vilivyokuwa na almasi.. Walitumia drill ambayo ilitengenezwa na The king of keys nyumbani.! Kwa kila kisanduku walitumia k**a dakika tatu kukidrill mpaka kufunguka hivyo mpaka mida ya saa kumi na moja alfajiri walifanikiwa kufungua visanduku 109 kati ya 120 vilivyopo ndani ya ile vault.. Ili kuogopa kukutwa na watu maana kitongoji cha Antwerp kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu mitaa inaanza kufurika watu! Kwahiyo wakajiridhisha kuwa wana mali ya kutosha wakabeba mzigo wao wakatokomea..
WIKI CHACHE BAADE..
Natarbatolo alik**atwa wiki chache baadae kwa kuhusika na tukio hili!
Kuk**atwa kwake kulikuwa ni kwa kizembe mno, walitupa taka taka za vifaa vyao vya maandalizi nje kidogo ya mji wa Antwerp na walipuuzia kuzichoma moto wakiamini hakuna mtu atakayeziona.. Katika takataka hizo pia kulikwa na kipande cha Sandwich ambacho Natarbartolo alikibakisha alipokuwa anakula.. Polisi walitumia kipande hicho cha sandwich kupima DNA na kukuta inamatch na DNA ya Natarbartlo..
MAMBO YENYE UTATA MPAKA LEO HII
Kuna vitu kadhaa ambavyo mpaka leo havijapata majibu sahihi..
i) yule myahudi aliyempa dili Notarbartolo ni nani?? Kuna watu wanadai kuwa Natarbartolo anajificha identity ya huyu mtu kwasababu inawezekana ni mpwa wake Benedetto Capizzi ambaye mwaka 2003 aliteuliwa kuwa Capo dei capi, ambacho ni cheo cha juu kabisa katika mtandao wa kihalifu wa Sicilian Mafia..
Natarbartolo anakataa kabisa mpwa wake kuhusika katika tukio hili..
ii) Natarbartolo anadai kuwa wao wenyewe waliingizwa mkenge na yule myahudi kwasababu anahisi kuwa yule myahudi na wenzake walitengeneza insurance scum ili kikundi fulani cha wafanyabiashara ya almasi ambao walikuwa wanahifadhi mali zao hapo waweze kujipatia fedha kutoka kwenye kampuni ya Bima baada ya tukio hilo la mali zao kuibiwa.
Yaani iko hivi, polisi wanadai kuwa almasi iliyoibiwa zilikuwa na thamani ya dola milioni 100 lakini Natarbartolo anadai kuwa viboksi vingi walivyovifungua ndani vault vilikuwa havina kitu kana kwamba watu waliambiwa kabla wasiweke alamsi zao siku hiyo.. Natarbartolo anadai kuwa almasi walizozikuta zilikuwa na thamani isiyozidi dola milioni 20.!! Natarbatolo anahisi kuwa yule myahudi alipanga dili na wenzake wamshawishi aende akaibe lakini siku moja kabla yule myahudi na wenzake wengi wakatoa almasi kwenye vault, kwahiyo baada ya tukio lile la wizi watu wote wenye visanduku kwenye vault wataenda kulipwa fidia na kampuni ya bima lakini huku almasi zao zikiwa ziko nyumbani wamezificha kwani walizitoa siku moja kabla ya tukio! Kwahiyo wanakuwa wamepata hela ya bima na almasi zao wanazo.. sijui naeleweka.?
iii) Hizi almasi zilizoibiwa hazijapatikana mpaka leo, na hazijulikani ziko wapi licha ya Natarbattolo kuk**atwa..
Natarbartolo alik**atwa na kushtakiwa kwa wizi huu uliotokea! Kutokana na kukosekana ushahidi wa moja kwa moja (almasi zenyewe) ikabidi mahak**a itumie ushahidi wa kimazingira (circumstantial evidence) ili kumtia hatiani na alihukumiwa miaka kumi jela.. Mpaka hivi tunavyoongea Natarbartolo ameshamaliza kutumikia adhabu yake na yuko uraiani na ameingia mkataba na Paramount Pictures ili kutengeneza filamu kuhusu tukio hili na filamu itatengenezwa na Director nguli J. J. Abrams huyu ndiye aliyetengeneza filamu za Lost (series), Armageddon, Star Trek, Star Wars: Force Awaken pamoja na filamu ya Mission Impossible III.
Share, Like, Comment
HABIBU B. ANGA
0759 181 457
Insta: habibu_anga
Twittet: habibu_anga
'BLACK MAMBA' KATIKA HISTORIA YA TANZANIA
Wakati wa vita ya Kagera, Brigedia namba 207 ambayo ndiyo hasa ilikuwa ya kwanza kuusogelea mstari wa adui iliongozwa na Meja Jenerali Walden. Kwa Usiku mitatu, Walden alipita katika maji na matope ambayo yalikuwa ni hatari kabisa kwa kuwa kulikuwa na mamba wengi. Baada ya kufanikiwa kupenya, wanajeshi wengine walishambulia Mamba hao na kumfikia. Hapo alipata jina Black Mamba kwa Ujasiri wake!
Katika eneo la Masaka, vita vilikuwa vikali sana kiasi kwamba, Idi Amin alimtuma Luteni Kanali Abdu Kisuule kutuliza ‘mambo’, Lakini haikufaa kitu, Wakapata msaada wa wanajeshi elfu moja toka Libya lakini Jeshi la Tanzania lilikuwa imara chini ya Black Mamba. Black Mamba alikuwa ni Bingwa wa shabaha, alikuwa na mbinu imara za kupigana kwenye hali ngumu na misituni. Baada ya Mapambano hayo, Luteni Kanali Kisuule alikuja kukiri kwamba mapambano ya eneo la Masaka ndio hasa yalidhoofisha jeshi la Uganda, ‘K**a ni kushindwa vita tulishindwa pale Masaka’. Baadae ‘Black Mamba’ aliongoza jeshi la Tanzania kuvamia makazi ya Nduli Idd Amin jijini Kampala.
Black Mamba ni nani?
Ni ngumu kabisa kizazi cha vijana wa sasa kujua Black Mamba ni nani, kutokuijua Historia yetu ni moja ya sababu kubwa kushuka kwa hali ya uzalendo, Taifa lisilowajua mashujaa wake ni Taifa la kitumwa!
John Walden alizaliwa Tunduru, Kusini mwa Tanzania mwaka 1939. Baba yake alikuwa ni Mwingereza na Mkuu wa wilaya ya Tunduru kwa wakati huo Bwana Stanley Arthur Walden, Mama yake alikuwa ni mtanzania Bi. Violet Nambela. Akiwa na miaka mitatu tu, John na Bibi yake upande wa Mama walihamia Mbeya. Wakati vita vya pili vilipomalizika mwaka 1945, John aliungana na baba yake mzee Stanley Walden ambaye alikuwa amehamishiwa Njombe, Iringa. John Walden alisoma shule ya Msingi ya bweni TosaMaganga, alihitimu darasa la kumi mwaka 1956. Mwaka ulifuatia yaani 1957 alijiunga na jeshi la kikoloni The King’s African Rifles (KAR). Ndani ya Jeshi, alikuwa kijana mchangamfu na ambaye alikuwa mwepesi kujifunza. Alikuwa ni mtunza ‘stoo’, mpiganaji, mara nyingine karani na hata ukalimani pale ilipohitajika.
Baada ya uhuru, John Walden alikutana na vikwazo vingi kwani alikuwa wa uzao wa ‘baba mzungu’. Kwa wakati huo, wazungu wote hata wale ‘machotara’ walionekana wakoloni tu. Alivumilia ubaguzi wote jeshini, alikuwa mtu mcheshi na mara nyingi wanajeshi wengine ‘weusi’ walisahau kuwa Walden alikuwa ‘Mweupe’. Uwezo wake wa kulenga shabaha, kugundua aina ya silaha kwa sauti na mbinu za kivita zilimfanya akubalike Zaidi. Kati ya mwaka 1962 na 1963 alihudhuria mafunzo maalumu katika shule ya kijeshi ya Aldershot, Uingereza. Mwaka 1963, Mwalimu Nyerere alimwapisha kuwa luteni, pamoja na luteni mwingine mzawa ‘Elisha Kavana’.
Baadae aliteuliwa kuwa mkuu wa kambi ya JKT Mafinga, kwenye miaka ya 1970 aliongoza operesheni za kijeshi kusini mwa Afrika, Kusaidia kuzikomboa nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Angola. Vita vya kagera, Walden au Black Mamba alikuwa kati ya makomandoo wachache walioteuliwa kufanya jaribio la kuiteka Kampala. Walden aliongoza kikosi kilichovamia makazi ya Iddi Amin. Na walifanikiwa kupata tuzo na nyaraka kadhaa ndani ya chumba alichokuwa analala Idd Amin.
Baada ya vita vya Kagera, wengi waliamini angeteuliwa kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Lakini haikuwa hivyo! Siha yake ya uchangamfu iliendelea k**a kawaida, alikuwa ni mtu mzalendo, aliyejitoa kwa ajili ya nchi sio vyeo na sifa. Aliitwa miaka ya 1989 kuongoza operasheni maalumu dhidi majangili waliokuwa wakishambulia wanyama hasa Tembo, Kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi mkubwa. Iliitwa operesheni UHAI, nyakati za usiku alitembea nyikani kwa ujasiri na kikundi cha askari wanyama pori. Kazi hiyo ilipunguza mno matukio ya kuuliwa kwa tembo.
Meja jenerali John Butler Walden au Black Mamba alifariki Julai 7, 2002. Na kuzikwa Mbeya. Huyu ndio ‘Black Mamba’, Komandoo hodari wa operasheni za misituni na mlenga shabaha ambaye hajapata kutokea katika Historia ya Jeshi letu imara la Tanzania.
Share
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
Tegeta Nyuki, Nyuki House Office No 22
Dar Es Salaam
Karibu kwenye page yetu kwa ajili ya kujifunza Jinsi ya kufanya BIASHARA yako MTANDAONI.
Earth
Dar Es Salaam
TechGuru💻|Motivation&Inspiration❤️|Entrepreneurship💰|Lifestyle💃|Gaming🎮|Health 🩺|VideoCreator🎬
Dar Es Salaam
Pan Africanist�| Heritage Manager & Concerned Citizen of the United Republic of Tanzania ��
MBEZI
Dar Es Salaam
This page is subjected to all my digital works.Most of them are portraits and panoramic with different styles.I do wedding, Graduation, modeling and all other photography.
Dar Es Salaam, 15115
Huu ni Ukurasa Rasmi wa Baraka Mafole ambaye ni Mjasiriamali ,Mbunifu na Muhamasishaji kupitia Mitandao ya kijamii