Simulizi na Riwaya Za Saul David bril
𝐋𝐈𝐊𝐄 & 𝐅𝐎𝐋𝐋𝐎𝐖 𝐏𝐀𝐆𝐄 𝐇𝐈𝐈 𝐔𝐏𝐀𝐓𝐄 𝐒𝐈𝐌𝐔𝐋𝐈𝐙𝐈 𝐍𝐙𝐔𝐑𝐈 𝐙𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐈𝐒𝐌𝐔𝐀
MADAM PRESIDENT 05
Tulipita pale kwangu kwenda mbele kidogo Kisha tukasimama,
Tulitazama kana kwamba kila mmoja anasubiri mwenzake atoe wazo Kisha k**a tumeambizana tukashuka wote kwenye Gari na kuelekea nyumbani kwangu..
Taa zilikua zinawaka na tuliingia na kukuta milango yote ikiwa wazi na Ile piki piki ilikua pale nje,...
Hatukuwa na silaha yoyote kwahiyo tuliingia ndani moja kwa moja.
Ilikua Ni nyumba ya serikali lakini nilikabidhiwa Mimi kukaa na tayari nilishakaa zaidi ya miaka mitatu kwenye hii nyumba lakini leo nilijikuta nakuwa muoga kabisa,
Jose aliingia kwenye baadhi ya vyumba na Kisha tukatoka sebuleni K**a Tuendelee na zoezi la kupakia mizigo ama la..
Wakati tunashaurina mlango wa mbele ulifunguliwa kwa Kasi ya ajabu na mtu mmoja aliyejifunga kitambaa usoni akaruka akiwa na bastola mkononi,
Wakati tunakaa sawa mwingine akaingia akiwa na bastola na kutuweka chini ya ulinzi....
"S**t!!!!" Nilijisemea nikikubali kupiga magoti...
Jose alinitazama K**a anayeuliza maswali nami nilimuangalia K**a mtu anayesema "hiki ndio nilikua nakuambia"
"Nyie Ni Akina Nani na mnataka Nini kwangu?"
Nilisema Sasa nikifoka,
"Sisi Ni rafiki zako tumekuja kukusaidia"
"Kunisaidia?"
Niliuliza nikitweta
Mmoja alisogea na kumnong'oneza mwenzake kitu Kisha wakaangaliana tulieni hivyo hivyo na ole wake mtu ageuke...
Tulibaki tumetulia na ukimya ulitawala kwa dakika kadhaa hivi nikaamua kunyanyuka..
Hakukuwa na mtu, Jose nae alisimama na kwenda mlango ambapo hatukuona mtu, Ile piki ilibaki pale pale nje...
Ndipo Sasa wazo lilinijia
Bila shaka Hawa watu walikuja K**a wageni wa kawaida usiku ule kwangu lakini walipoona hatupo wakaamua kubaki kusubiri kwa kuvizia K**a hivi...
"Ila Sasa wanataka Nini mbwa Hawa?"
Niliwaza bila kupata jibu...
Jose alikua ananitazama K**a mtu Mwenye maswali mengi...
"Kaka hebu niambie kunani ujue Mimi Mambo ya bunduki bunduki nayaona kwenye picha tu!"
Jose aliongea..
"Jose tupakie mizigo kwanza...hii sio inshu ya dakika mbili hata hivyo itabidi tuhakikishe hakuna anayetufuata...
Familia yangu ikishakaa salama Basi nitakuambia Kaka"
Nilisema Kisha tuk**alizia mizigo iyobaki Safari ikaanza tulikwenda pole pole na kuhakikisha hakuna mtu Wala Gari linatufuata wakati mwingine tulishuka kabisa na kuangaza macho huko na huko Kisha safari ikaendelea...
Tulifika saa kumi na moja kasoro asubuhi, na kupakia mizigo
Nilitamani kumwambia mke wangu Mambo yote kuanzia mwanzo Hadi mwisho lakini niliogopa kutokana na Hali yake ya ujauzito..
Tulipanga mizigo yote ikiwemo kuweka vitu sawa ikiwemo televisheni na vitu vingine vya muhimu chumbani, tulilazimika kufanya wenyewe baadhi ya Mambo ili kuepusha watu wengi kujua ninapoishi..
Tulimaliza kazi saa 9 mchana tukapata chakula Kisha tukapumzika kidogo ili usiku tuanze safari ya kurudi mjini Mimi na Jose..
Kwa kawaida mwezi wa 4 Hadi wa 6 kila mwaka nakuwa na shughuli nyingi za umiseta wilaya na mkoa na taifa na wakati huu nakuwa na majukumu mengi ya kusafiri Sana pamoja na kuwa mashindano haya kwa mwaka ule yalifanyika pale pale wilayani kwangu nilitumia fursa hii kumdanganya mke wangu kuwa nitasafiri kikazi kwa mwezi mzima
"Mahitaji yote atakuwa analeta Jose, halafu Kuna Shemeji yangu mke wa rafiki mmoja nitamuomba aje akae na wewe kwa miezi hii miwili,
Hatuna haja ya kumsumbua mama safari hii"
Nilisema Kisha tukaagana Mimi na Jose tukarudi mjini...
Niliweka wastani wa mwezi mmoja nimalizane na Janet
"Jose kiuhalisia nahisi tu Kuna Mambo mabaya yanaweza kunitokea Sasa si unajua Ile nyumba yangu kule mabatini ambayo tulipeleka bomba kipindi kile?"
Niliongea Sasa nikiwa Sina utani Tena..
"Yeah nakumbuka," Jose alisema..
"Okay ikitokea chochote labda nimepotea ghafla au chochote yaani...."
Jose alinikatisha..
"Unajua we jamaa sikuelewi ulikua unasema K**a hivyo tukakuta watu kule sijui majambazi sijui usalama sijui Nini...
Mwanangu mi mtu wako bhana niambie Basi sikuelewi ujue"
Jose alinitazama
Kaka Ni stori ndefu kidogo Ila usijali kwakuwa wewe Ni mtu wangu nitakueleza kila kitu..
"Wakati nikiwa kidato Cha tano pale mombo sekondari tulikwenda tanga kwenye umiseta........."
Pamoja na kuwa Jose alikua sio ndugu yangu lakini katika harakati za maisha hususani baada ya Jacob "kupotea" katika mazingira ya kustaajabisha nilimchukulia huyu K**a rafiki yangu mwingine ...
Hivyo nilijikuta namueleza kila kitu wakati namaliza kusimulia ndio niligundua kuwa machozi yalikua yanatoka
"Kaka Pole,
Ujue kumgonga madam si mchezo ujue, Sasa nakuelewa kaka, Hawa wajinga lazima wakutafute....niambie kaka tunatokaje Sasa"
Jacob aliniuliza huku akiwa amesimamisha Gari...
"Kwasasa nitaenda kumshawishi Aida , aende kukaa na wife kwa kipindi chote, mpaka atakapojifungua.. Mimi nitaendelea kuishi K**a popo nikijigeuza geuza"
Nilisema kwa upole..
"Ulisema kuhusu kule kwenye nyumba yako mabatini kuna Nini "
Aliniuliza
"Sikiliza Jacob, ukiwa unaenda bafuni Kuna malu malu ambayo yako tofauti ukiangalia tu mwenyewe utaona zipo K**a tiles nane 8 hivi utazitoa ..
Utaona box moja la Chuma , pembeni yake Kuna chupa ya soda ambayo Ina bahasha yenye maelezo yote,
Lakini hii Ni endapo tu utakuwa umejihakikishia kuwa hutaniona Tena, lakini sambamba na Hilo Hakikisha unamtafuta Jacob Lota, ikibidi hata kwenye magazeti umkabidhi Hilo box kabla ya kulifungua, ukimkosa Jacob K**a nae atakuwa amekufa kwa bahati Basi ulifungue Hilo sanduku wewe mwenyewe"
Sasa twende zetu mjini!
Nilisema huku tukiendelea na Safari...
"Mimi nahisi Jacob yupo Tanzania na ndio atakuwa kakutumia ule ujumbe kuhusu kuvuka barabara na familia"
Jose alisema...
"Aisee Jose itakuwa kweli umenikumbusha kitu, ngoja nikaangalie Ile email Tena kesho asubuhi"
Tulifika salama kwenye majira ya saa nne usiku na sikutaka kwenda kwenye Ile nyumba Tena,
Niliagana na Jose baada ya kumpatia kiasi Cha pesa Kisha nikatafuta gesti ya karibu nikalala.
*************
Nilifika ofisini kesho yake na wengi walinipa pole kwa kuvamiwa na kuuliza kuhusu kuibiwa chochote...
Nilienda ofisini kwangu na moja kwa moja nilifungua computer na kuingia kwenye barua Pepe yangu...
Niliangalia Tena Ile barua Pepe na kisha nikatabasamu!
Naam Ni kweli ujumbe ule ukitoka kwa Jacob, nilijilaumu Sana kutokuelewa mapema,
Kwa kawaida Jacob alikua anapenda kuchanganya Walau Herufi moja kubwa au ndogo katika jumbe zake Lau Mara kadhaa angemalizia na nukta mbili mwishoni.
Hivyo nilivyoona nukta mbili mwishoni nikajua moja kwa moja Ni Jacob alikua anataka kunionya kuhusu kinachoendelea .
Ni wakati natoka kwenda kwenye kikao Cha bajeti ya umiseta mke wangu alinipigia kuwa Kuna picha yetu kubwa ya ndoa pamoja na Cheti Cha ndoa hajaviona katika Ile mizigo yote tuliyobeba..
Nilimsihi aangalie au amuulize Stela lakini alisema alishakagua sehemu zote hakuna kitu, hivyo alinitaka kuangalia K**a nimesahau kule kwenye Ile nyumba...
"Okay nikitoka nitaenda kuangalia itakuwa tumesahau kule " nilisema huku nikienda kwenye kikao...
******************
Nilifika kwenye Ile nyumba na kukuta Ile piki piki ikiwa vile vile pamoja na ufunguo wake ukining'inia..
Niliingia ndani na kutafuta kila sehemu sikuona picha Wala Cheti hicho Cha ndoa...
Sasa nilikaa kwenye kiti pale sebuleni na kutafakari ndipo nikagundua mahali vitu hivyo vilipo...
Simulizi hii inapatikani yote mwanzo hadi mwisho kwa tsh 1000 tu njoo WhatsApp 0756862047/0788967317 k**a huna whatsp njoo inbox
MADAM PRESIDENT 04
Nilipita kwenye bustani ndogo ya maua Kisha nikaendelea mbele ambapo alitokea mlinzi mmoja akanikaribisha Kisha akachukua begi langu dogo akaniongoza njia, tulienda sehemu Nyingine ambapo tulipita kwenye ofisi Nyingine Kisha nikaambiwa nisubiri hapo,
Kwa kila namna Sasa nilianza kujisikia vibaya kukaguliwa Mara kupitishwa kwenye vidude gani nilitamani kugeuza kurudi....
Ni K**a Yale yote yalikuwa madogo..
Ni wakati nimekaa hapo nikikunja kunja vidole na kuangaza macho huko na huko akatokea mzee mmoja hivi ambaye alinisalimia kwa tabasamu Kisha akafungua mlango uliokuwa mbele yake akaniita ,
Hakuwa na maneno mengi akaniashiria nikae kwenye kiti ambacho Kiko mbele yake Kisha akafungua kabati na kutoa vifaa K**a vya kidaktari hivi....
"Aah mzee achana na Mimi aisee"
Nilijikuta Sasa uvumilivu unanishinda,
"Hahaha Tulia bhana Kijana mbona saa ulivaa? Tunamalizia tu zoezi dogo" alisema huku akichukua kidole changu na kukitoboa kidogo kwa sindano Kisha akachukua damu na kuipachika kwenye kidude K**a saa,
Alinipigisha Hadithi ambazo hazikuwa na kichwa Wala miguu nilishaelewa kuwa anasubiri vipimo vyake hivyo sikumjibu kitu na hatimaye akaacha kuongea baada ya kuona nimekasirika ...
Baada ya dakika K**a nane hivi alikichukua kile kidude na kukiingiza Tena kwenye kitu mfano wa saa ambapo alibinya binya namba fulani Kisha akatabasamu...
"Haya twende"
Alisema Kisha tukatoka Tena na kupanda ngazi ambapo aliniacha kwenye chumba kingine akaondoka zake...
Ni baada ya dakika tatu alitokea madam Janet akiwa na walinzi wawili nilisimama na tukasalimiana wale walinzi hawakunisalimia walinikodolea macho mpaka nikaishiwa pozi..
Tuliongozana na madam tukipiga stori mbili tatu mpaka kwenye chumba kingine kikubwa ambacho walinzi walibaki nje ..
"Aisee siwezi kurudi Tena hapa"
Nilisema wakati nikikaa vizuri kwenye sofa
"Haha pole hata hapo bado Kuna step tumekanyaga kanuni zinasema uje hapa wiki moja kabla, "
Alisema Janet kana kwamba haikuwa Shida kubwa...
Aliniuliza habari za kazi na Mipango mingine ya maisha
Sikuwa na maneno mengi kwanza sikuwa najisikia vizuri...
"Nimekumisi Sana wewe mwanaume yaani hapa ofisini hapakaliki mpaka navurugana na mawaziri yaani sijui Hilo dudu lako likoje yaani"
Alisema Janet huku akicheka,
"Ah mzee si yupo nilimuona siku Ile ya kuapishwa"
Nilisema
"Wee bado mgeni kwenye hii nchi ndugu? Mimi Janet niwe na mzee K**a Yule na watoto hao niwapate lini?"
Hahahaa hata hivyo wapo hapa k**a utataka kuwaona! "
Janet aliongea Kish akanishika mkono...
"Sikia tunaingia kwenye chumba ambacho hatuonekani kuwa na amani mpenzi wangu"
Alisema Janet akinivuta nami nikaingia chumbani na kazi ikaanza....
Ni K**a alikua amenipania hata hivyo shughuli aliipata na mwishowe akapitiwa na usingizi nilienda bafuni kuoga Kisha nikachukua begi langu ambalo lililetwa nikavaa suti nyingine niliangalia saa yangu ilikua saa 12 jioni, njaa iliniuma Sana, nilimwamsha Janet ambaye alistuka kuniona nimevaa nguo nyingine.
"Vipi? "
Alisema akijifinyanga macho
"Madam siwez kulala hapa, halafu hapa Ni nyumbani kwako"
Nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika..
"Okay nashukuru hata hivyo nitajua namna ya kufanya najua una njaa Ila Sasa chakula Cha hapa Ni hakiivi Sasa hivi na ningependa ule chakula Cha Raisi leo"
Alisema janet Kisha akasimama vile vile na kunibusu..
Nitafanya mpango wiki mbili zijazo tuinjoy zaidi
Alivaa nguo zake Kisha akanitoa nje ambapo mlinzi mmoja alinifikisha kwenye chumba kingine ambacho nilimkuta dada mmoja ambaye alininipa begi langu Pamoja na bahasha nyingine nilitoka nje ya geti nikapiga ishara ya msalaba kutoka salama mle ndani....
"Siwezi kurudi Tena hapa kwakweli" nilijikuta nasema moyoni huku nikichanganya miguu .....
Niliangalia Ile bahasha na kukuta kiasi Cha pesa na zilikua Ni Dola za kimarekani..
Nilitafuta mgahawa mzuri nikapata chakula Kisha nikarudi zangu mlandizi,
Nikiwa kwenye Basi nilifikiri mengi Sana niliwaza mwisho wa Jambo hili utakuwaje,
Vipi Raisi akijua kuhusu familia yangu? Vipi ikijulikana natembea na Raisi?
Ni wakati natoa Simu yangu niliangusha kitambaa changu kwa bahati mbaya nikainama kukiokota wakati nanyanyua uso macho yangu yakagongana na huyu abiria mmoja aliyekaa upande wa nyuma,
Nilijaribu kumuangalia lakini kwa haraka Sana akaendelea kubonyeza Simu yake kana kwamba hakuniona,
Sikutilia maanani ingawa nilijikuta tu namuwaza na Sasa akili yangu ikakumbuka, wakati naingia pale rock mall kupata chakula alikuwa nyuma yangu na wakati nakula yeye alikua anakunywa maji
Ni wakati gani alipanda kwenye Basi sikutilia maanani...
"Au labda namfananisha" nilijisemea
Tulifika mlandizi majira ya saa tatu na robo usiku, moyoni nilikua najisikia huzuni kubwa na nilikua nikijihisi aibu kurudi nyumbani kwa mke wangu usiku ule,
Nilishuka na kuvaa begi langu Kisha nikasogea mpaka kwenye kijiwe Cha boda boda, ndipo yule jamaa nae kwa mbali niliona akiwa anashuka kwenye Basi wakati naongea na boda nilipogeuka sikumuona tena!
"Twende misongeni kwa mzee kivu"
Nilisema nikichukua boda boda,
"Wapi Ile ya juu au kule madukani"
Boda aliuliza
"Ya juu"
Nilisema nikikaa kwenye piki piki.
Nilifika nyumbani kwangu na mke wangu alikua ananisubiri K**a ilivyokuwa kawaida yake,
Nilitoa uongo tu kuhusu kazi na bla bla ikaisha...
Hata hivyo nilijiambia Mara hii siwezi kutoka Tena na Madam President potelea pote,
"Aniue tu, K**a mbwai na iwe mbwai"
Nilijisemea huku nikipanda kitandani.
*****************
Katikati ya usiku wa manane nilihisi K**a Kuna mtu anapita sebuleni,
Halafu Tena nikahisi K**a amekuja chumbani kwetu na kusimama baadae sikukumbuka Tena kilichotokea tulikuja kuamshwa na dada wa kazi Stella saa 4 asubuhi kwa ajili ya chai!
"Mimi nilijua leo hamuendi kazini"
Alisema Stella akiwa mlangoni, nilijaribu kunyanyuka lakini mwili ulikua mzito, mke wangu pia nae alijihisi uchovu...
Ndipo fahamu zangu zilirejea
"Mama tumevamiwa, wezi bila shaka wametupulizia dawa ya usingizi"
Nilisema Sasa nikisimama kutoka kitandani
Nilipitia mpaka sebuleni ambapo Kila kitu kilikua sawa , nilirudi Tena chumbani ambako niliangalia kabati lilikua sawa Ni K**a Kila kitu kilikua sawa...
Nilichukua Simu yangu na kumpigia Mkuu wa idara kumueleza Hali yote iliyotokea na Polisi walifika muda mfupi, walijaribu kuangalia sehemu kadhaa na kutuhoji ,
Daktari alifika pia na kutupima na alithibitisha kuwa dawa Kali ya usingizi ilikuwa imepulizwa
*****************
Ni wiki moja baada ya tukio sikuwa na mawasiliano yoyote na Janet kitu ambacho niliona kizuri sana,
Nikiwa ofisini baada ya kazi kupungua niliingia kwenye akaunti ya Yahoo ili nisome baadhi ya jumbe kutoka kwa marafiki,
Lakini kipekee tu nilidhani ningepata Hata meseji moja kutoka kwa Jacob,
Maana ilishapita miezi sita hatujawasiliana,
Ni wakati nafungua nilikuta meseji ambayo ilitumwa siku kadhaa zilizopita na mtu ambaye hakutaja jina lake Wala anuani yake haikuonekana,
"Unavuka barabara na ukiwa na mke wako na watoto angalia hiyo Gari inayokuja Kasi,
Jitahidi uvuke kwa spidi au urudi nyuma"
Ujumbe uliishia hapo, nilijaribu kuelewa lakini sikuambulia chochote hatimaye niliamua kumtumia Jacob Ile ujumbe huku nikiomba msaada wake,
Hata hivyo sikuelewa Jacob Anaweza kunijibu lini...
Ghafla wazo lilinijia,
Niliona Tena sio salama kukaa mazingira yale tayari mke wangu alikua mjamzito wa mtoto wetu wa pili, na tayari alishachukua likizo ya kwenda kujifungua,
Nilitoka ofisini haraka na kuchukua boda boda mpaka kwangu,
"Dear jiandae taratibu funga mizigo yako ya muhimu taratibu, Stella atakusaidia kwenye usiku tutaondoka hapa sitaki tukae mazingira haya kwa kipindi hiki"
Nilimuelewesha Kisha nikarudi kazini,
Nilitoa Simu Yangu na kumpigia jose,
"Kaka naomba unipeleke sehemu Leo usiku "
Nilisema baada ya simu kupokelewa
"Ha Kaka usiku Tena, vipi kwema"
Jose aliongea,
Huyu alikua Ni dereva pale stendi na Mara nyingi alikua ananibebea mizigo yangu wakati wa ujenzi wa nyumba zangu...
Tulikubaliana Kisha nikampigia gogo aliyekuwepo huko misufini ambako nilitegemea kumpeleka mke wangu,
Haikuwa mbali Sana na mjini lakini ilikua Ni sehemu nzuri sana kwa kutulia ama kujificha K**a nilivyowaza,
**************
Saa mbili usiku tulianza safari na ndani ya masaa matatu na nusu tulishafika na kushusha mizigo,
Nyumba ilikua kubwa na nzuri Sana,..
Tulishusha mizigo kwa kusaidiana na Yule kijana ambaye nilimuacha k**a mlinzi, Mimi na Jose tulirudi Tena kumalizia mizigo iliyobaki...
"Kaka usiniambie ule mjengo Ni wako"
Nilitabasamu tu Kisha nikamwambia Jose kwa msisitizo..
"Jose wewe Ni Rafiki yangu, nimekuchagua kwenye hii kazi kwakuwa nakuamini,
Siku sio nyingi pengine Kuna Mambo mabaya yanaweza kunipata, naomba mtu yoyote asijue kuwa mke wangu anakaa katika Ile nyumba ndio maana tumehamia usiku,
Jose alisimamisha Gari ghafla na kutoka nje..
"We jamaa unaumwa? Mbona unongea ujinga hivi?" Eti Nini?
Jose alihamaki akitweta...
"Jose sikiliza bhana sijasema nitakufa! Nimesema naweza kupatwa na jambo baya kwa tahadhari tu sitaki mke wangu aguswe tutaongea zaidi hebu tumalize kazi kwanza tukachukue mizigo iliyobaki....
Ilikua Ni K**a saa Saba usiku na tulikuwa tunakaribia kufika kwangu ndipo kwa mbali nikaona piki piki imeegeshwa nje kwangu,
"Jose ona kule!"
Nilisema nikinyoosha kidole
"Aisee huyu fala anaweza kuegesha kabisa piki piki nje kwa mtu saa hizi?"
Jose alisema akiongeza Mwendo..
"Sikiliza usipaki pale home fanya K**a unapita hiyo nyumba tumsome kwanza huyo boya" nilisema
Simulizi hii inapatikani yote mwanzo hadi mwisho kwa tsh 1000 tu njoo WhatsApp 0756862047/0788967317 k**a huna whatsp njoo inbox
MADAM PRESIDENT 03
Wiki moja iliisha na tulipitia shule chache tu Kisha nikarudi ofisini kuendelea na kazi,
Nilijisikia vibaya moyoni kwa yote niliofanya na Janet lakini sikuwa na ujasiri wa kumueleza mke wangu chochote,
Janet aliendelea kunitumia pesa nyingi ambapo nilinunua eneo kibaha Kisha nikajenga nyumba kimya kimya bila kumwambia mke wangu,
Mke wangu nilimhamishia hospitali ya mlandizi ambako ilikua karibu na sehemu tuliyoishi,
********************
Mwaka 2010
Nilikua nimetoka kazini mapema ili kujiandaa kumpokea mdogo wake mke wangu ambaye alikua anakwenda chuo Cha uuguzi muhimbili,
Tuliona Ni Busara apitie kwetu walau tumuongezee mahitaji kidogo .
Ilikuwa Ni mwezi wa sita ambapo chama tawala Tanzania ilikua Ni siku yao ya kupitisha jina moja la mgombea uraisi kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,
Kwa miaka miwili mfulululizo hatukuwahi kuonana na Janet zaidi ya kuwasiliana tu kwenye simu na kwa njia ya mtandao,
Bila kuelewa chochote nilishindwa kumueleza Janet kuwa nimeoa
Nakumbuka nilimshirikisha rafiki yangu Jacob ambaye kwa kipindi hicho alikua katika chuo Cha jeshi Monduli katika maongezi yetu aliniambia
Nihakikishe nimeshajipanga vizuri kiuchumi ikiwemo kuwa na miradi ya Siri, Kisha nimwambie Janet wazi wazi kuwa nimeoa na Mambo mengine yatajitengeneza yenyewe.....
Kwa miaka miwili hii nilihakikisha najenga nyumba tatu ambazo zote nilipangisha ,
Kisha nikamfungulia mke wangu duka kubwa la dawa kibaha mjini, hakika maisha yalikwenda vizuri...
Sikuona umuhimu wa Janet Sasa katika maisha yangu Tena, hata wakati mwingine anapiga Simu Ningeweza kupokea kwa kujisikia ..
Niliyawaza hayo nikiwa sebuleni kwangu wakati nawasha tv yangu..
"Na chama Tawala Tanzania kimemteua Bi Janet Abraham Shayo kuwa mgombea uraisi mwaka huu 2010, ukumbukwe hii Ni nafasi kubwa kabisa ya kwanza kwa mwanamke kuwahi kushika tangu nchi hiyo kupata Uhuru,..."
Alikua mtangazi wa KTN akiongea katika taarifa hiyo fupi ...
"Ohooooooo"
Nilijisemea nikitetemeka
Janet alipitishwa kuwa mgombea Uraisi na hatimaye akapita kwa kura zaidi ya asilimia 70 na akatangazwa kuwa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Binafsi nilifurahi kwakuwa nilijua Sasa mahusiano yetu yamefikia mwisho,
Wakati anaapishwa Janet alifika uwanjani akiwa na mwanaume ambaye alisadikika ndie mume wake pamoja na watoto wawili,
Kwa muda wote niliokaa na Janet sikuwahi kumuona akiwasiliana na mume wake huyo,
Hata hivyo nilifurahi tu kwakuwa Sasa ningeweza kuwa huru na maisha yangu,
Nilishazoea kazi yangu pale halmashauri na tayari nilishazoeana na marafiki pale ofisini...
Ilipita wiki moja ambapo siku hiyo nakumbuka ilikua ijumaa Jacob alinipigia Simu kuwa ameacha kazi jeshini!
Nilipigwa na butwaa Sana kwani Jacob ninayemjua alipenda kazi ya Jeshi kuliko hata kula, kila Mara alipotoka kwenye mpira wa kikapu aliwaza jeshi,
Eti leo hii anaacha kazi kwa hiari yake nilishangaa Sana,
Hata hivyo mwishoni mwa mazungumzo yake niligundua Kuna ujumbe alikua ananitumia nakumbuka tukiwa shule tulipenda kuongea kwa mafumbo hususani katika Mambo yaliyohusu wasichana,
"Ndio hivyo kaka, hata ukisoma mhubiri 3 kwenye Biblia utaona kila Jambo na wakati wake, naamini muda wangu Jeshini umeisha
Kumbuka Sana haya maneno"
Alimalizia Jacob
Niliwaza hayo maneno Kisha nikachukua Bibilia na kuangalia huo mstari ..
kila Jambo na wakati wake na kusudi lake chini ya mbingu
Nilijikuta natabasamu baada ya kuona Hilo neno chini ya mbingu..
Siku moja tukiwa tumekaa na Jacob aliniambia kuwa unapofanya kazi jeshini unafanya kazi chini ya mbingu,
Siku zote amri na mamlaka zote jeshini zinatoka juu kwenye mbingu kwahiyo kazi yao Ni kutii mbingu!
"Kaka tuko chini ya mbingu"
Hivyo bila shaka Jacob alikua haachi kazi Ila labda alikua anabadili kitengo,
K**a nilivyohisi Jacob aliniambia anasafiri nje ya nchi kwenda kutafuta maisha ughaibuni,
"Unajua kaka sisi ukishaacha kazi ukiendelea kubaki mtaani mtaa wa pili mtu akiiba kuku unaambiwa Ni wewe"
Jacob alikua anasema wakati tunapata chakula nyumbani kwangu baada ya yeye kuja kuniaga.
**********
Baada ya mwezi mmoja Sasa nilichokihofia kilianza kutokea,
Wakati natoka ofisini kwangu natembea kuelekea ilipo stendi ghafla alijitokeza mtu mmoja kana kwamba Alikua ananisubiri..
"Oya Broo subiri kidogo"
Alisema nikageuka bila kujali Sana akanitolea Simu yake kana kwamba Kuna kitu ananionyesha,
Nilipoichukua alinionyeshea ishara niweke sikioni,
"Ndio Allan mpenzi Mimi Janet , utapewa mzigo wako na hao vijana na maelezo mengine jumapili tuonane"
Simu ikakatika.
Nilibaki nimeduwaa Yule jamaa akanielekeza sehemu ya kupita ambapo tulifika na kutokea kwenye Gari lililokua na vioo vyeusi, akanitolea begi moja na bahasha ndogo ya kaki Kisha wakasepa zao...
Nilibaki na Lile begi na bahasha nikiwa nimeduwaa ...
Niliiweka Ile bahasha kwenye begi upande wa juu tu Kisha nikazunguuka kutokea stendi Kisha nikaenda upande wa kwenye vyoo vya wasafiri ,
Nililipa shilingi 100 Kisha nikaingia chooni,.
Nilifungua begi na kukuta suti mbili nzuri mmoja nyeusi na Nyingine rangi ya kijani,
Pamoja na saa ya mkononi na Simu moja Aina ya Sony Erikson nzuri Sana,
Nilitabasamu Kisha nikatoa Ile bahasha ambapo nilikuta Dola za kimarekani kadhaa, pamoja na ujumbe mfupi kwenye kikaratasi..
vaa upendeze dear
_Njoo jumatatu ikulu
Ukifika waonyeshe hiyo saa
Niliiweka kile kimeseji mfukoni Kisha nikaangalia Ile saa Tena,
"Ah watajua wenyewe!"
Nilijisemea nikitoka pale chooni,
Sikutaka kwenda na Ile mizigo nyumbani hivyo kwa dakika kadhaa nikawaza niupeleke wapi ule mzigo....
"Aaah Aida"
Niliwaza haraka kisha nikatoa Simu yangu...
"Ndio Shemeji yake"
Nilisema baada ya simu kupokelewa...
"Haya wewe mzungu leo kunipigia Simu mchana!"
Alisema huku akicheka...
"Ah nakuja aisee Nina hamu Sana na wali N**i"
Nilisema huku nikimkonyeza boda boda mmoja..
"Hahaha karibu Sana K**a umeotea vile ndio napika hivyoo"
Nilikata Simu na kupanda piki piki kuelekea kwa Aida ilikua Ni Mwendo wa dakika tano tu ....
Aida nilifahamiana nae wakati natafuta kiwanja alikua Ana mgahawa wake mkubwa pale mjini kabla hajabomolewa kupisha barabara,
Wakati natafuta eneo la kujenga nilimtumia na hata nilipoanza ujenzi kimya kimya nilimuachia baadhi ya pesa kulipa mafundi....
Aida hakuwa na mume Ila alikua na watoto wawili, hakuna ajuae baba wa watoto wake isipokuwa Aida mwenyewe, wapo waliosema Raisi mstaafu , wengine walisema sijui jaji Mkuu, ili mradi wabongo tu hawakukosa la kusema,
Nilichompendea Aida ilikua Ni usiri wake,
Nilishafanya dili nyingi Sana na Aida,
Nilifika kwake na kumkuta kweli anakuna N**i...
"Haha Shemeji yake kumbe kweli kitu N**i kabisa!"
Nilisema nikiingia ndani,....
"Karibu bosi wangu hivi nimekuona najua leo lazima Nile kuku"
Alisema akinisimama,
"Sasa sikia, sikai ujue nimetoka job Sasa kuna huu mzigo nitaupitia jmos jioni au jumapili asubuhi Sana , naona Soo kwenda nao home si unajua Tena"
Sikia kula huyo huku bhana ngoja niwahi"
Nilisema nikitoa elfu 10 na kumpa Kisha nikarudi kwenye piki piki kurudi kwangu,
****************
Jumapili saa 5 asubuhi nilikua kwenye geti la kwanza ikulu,
Sikuwa na hofu yoyote nilishaingia mtegoni sikua na namna ya kujinasua....
Nilijitambulisha K**a mgeni wa madam,
Na kutokana na suti niliyovaa hata mke wangu angeweza kupishana na Mimi!
Kwa haraka ungeweza kudhani Ni muwekezaji hivi,
Nilipita geti la pili na la tatu hatimaye nikafika geti kuu ..kulikua na mlinzi mmoja tu...
Hakuongea zaidi ya kuninyooshea mkono K**a anayetaka kitu....
Haraka nilivua saa na kumkabidhi..
Aliichukua na kuichomeka mahali Kisha akanionyesha sehemu ya kusimama nikasimama akabonyeza bonyeza Tena kwenye computer yake Kisha akaniruhusu kupita.
ITAENDELEA...
WhatsApp me 0788967317
Madam president 2
Ni baada ya wiki mbili kupita siku hiyo nikiwa ofisini napanga vitu baadhi , nilipokea ujumbe kuwa nahitajika kwa mkurugenzi,
Basi nilirudishia mlango Kisha nikatoka kupanda ngazi, njiani nilipishana na jamaa ambaye sura yake haikuwa ngeni Sana hata Hivyo sikumjali Sana,
Ndipo nikafika kwa katibu muhtasi ambaye alitabasamu tu na kunielekeza nipite..
Nilifungua mlango Kisha nikaingia ndani na kupigwa na butwaa,
Mbele yangu Janet alikua amekaa na mkurugenzi wakiongea Mambo kadha wa kadha,
Basi niliwasalimia Kisha nikakaa kwenye kiti..
"Ndio Afisa huyu Ni madam Janet kutoka Ofisi ya Raisi,
Ni mgeni wako!" Aliongea huku akimtazama Janet,
"Hello Allan, nadhani Ni Mara ya pili kuonana hongera kwa uteuzi nadhani Mara ya mwisho tulionana kule Segera sekondari"
Alianza Janet huku dimpo zake zikionekana,
"Ah tunajua Hali ya mkoa wa Pwani wanafunzi hawana muamko Sana na elimu, kwahiyo K**a Ofisi tukaona tuje na program fulani hivi ambayo itasaidia watoto kupenda shule na ndipo Sasa tukaona kupitia maafisa michezo wa Wilaya mnaweza kuja na wazo zuri ambalo linaweza kuwa Chachu sambamba na Hilo ,kwa wiki moja hii tutambelea shule zote za sekondari katika Wilaya hii kuongea machache na walimu wa michezo kwahiyo sasa kajiandae tuanze safari,"
Alisema Janet K**a Mwalimu anayeongea na mwanafunzi wake,
"Afisa, kajiandae saa 6 kamili ziara itaanza wewe ndio mwenyeji, na pia Ni wakati wako kujua baadhi ya zile shule ambazo hamjafika, usijali ofisi italipa allowance zote kajiandae bhana"
Bwana shija ambaye tulipenda kumuita Broo aliongea Basi nilitoka nje na nikachukua boda boda Hadi kwangu,
Nilimwambia mke wangu Hali ilivyokua,
"Kwahiyo Kuna siku Nitakuwa narudi usiku Sana ama nisirudi kabisa, but Ni wiki moja tu d"
Nilisema baada ya kuchukua begi langu na nguo kadhaa,
Nilifika na kupanda kwenye Gari na K**a nilivyotabiri msafara haukuwa na watu wengi Sana,
"Nimekwisha"
Niliwaza Gari ikiondoka tulikaa na Janet Siti moja ya nyuma kabisa huku kila mmoja akiwa anasubiri mwenzake aanze kuongea...
"Hatimaye tumeonana Allan"
Alianza Janet akitabasamu,
"Yeah Asante Sana kwa kunipa Shavu aisee"
Nami nilisema,
"Shavu gani Tena" aliuliza Janet huku akishikilia vizuri mkono wake wakati landcruiser ikichanja mbuga,
"Ningezeeka kule kwenye chaki aisee"
Nilisema nikicheka,
"Hahaha umejuaje K**a Ni Mimi?"
Aliuliza
"Ah who else? Ni wewe tu bhana " nilisema,
"Hata hivyo kasome bado Kuna nafasi nyingi kwa ajili yako"
Alisema Janet
"Okay dereva Kuna iyo njia hapo pinda kulia tuingie hapo Kuna shule tunaweza kuanza nayo"
"Ah shule gani Tena hebu achana na izo mishe Mimi nimekuja kukutembelea mpenzi wangu tule Bata kwa wiki moja hii, huko tunaweza kutuma maafisa elimu kata" alisema Janet Sasa nilitamani kuruka dirishani,
Wakati mwingine nilitamani kucheka,.
"Whaaaat?"
Nilihamaki,
"Yes, baby,!, Kumbuka nilichokuambia nakupenda Allan kila siku nilijaribu kukutafuta kila sehemu mpaka pale nilipokukuta Segera , believe me nilitaka upate cheo kikubwa zaidi lakini bado Kuna vigezo haukutimiza"
Alisema Janet kauli ambayo ilitoka kabisa ndani ya moyo wake,
"Asante Janet kwa kunipenda lakini......"
alinikatisha.
"Usiseme kitu, usiseme chochote usiseme kitu naomba usiseme kitu "
Alisema Janet
"Eeh Mungu nisaidie dhidi ya hiki kiumbe, natokaje hapa"
"John twende pale new Ambassador hotel"
Aliongea Janet ,
Dereva alikata Kona na kuelekea kwenye hotel hiyo kubwa Sana ambayo ilikua Ni kituo Cha vigogo kwa mkoa mzima wa Pwani, kwa haraka wageni katika hii hotel walipata huduma zote ambazo wangepata katika hotel kubwa kubwa za kule Jijini Dar,
Kwa unyongea nilishuka na kuelekea hapo Hotelini K**a vile mbuzi anayekwenda machinjoni,
"Balaa gani Hili Tena"
Nilijisemea nikipiga hatua kumfuata Janet
"Karibu Sana Allan, wewe John unaweza kutafuta meza yako tuu"
Alisema Janet huku akinivutia kiti niweze kukaa,
Ilikua K**a saa 7 kasoro hivi Hivyo tuliagiza chakula na kuanza kula,
"Yaani Nina hamu na wewe balaa miaka yote hiyo nilikua nakuwaza wewe tu mpenzi niambie Sasa maisha yako yakoje"
Alianza Janet,
"Ah tunamshukuru Mungu Mambo yako vizuri kabisa things goes on"
Nilisema huku nikipiga msosi lakini mawazo yangu yalikua maili kadhaa huko,
Nilimuwaza mke wangu pamoja na mtoto wangu ambao maskini hawakujua kinachoendelea huku,
hauko sawa Allan, huonyeshi kufurahia , huonyeshi kujali yaani Ni K**a hauko hapa,..
Niambie kitu gani unacho wewe,"
Janet Sasa aliacha kula Kisha akanitazama,
Nilitamani kumwambia kuwa tayari nimeoa na nina mtoto ,
Ila sauti nyingine ikaniambia huo Ni uoga,.
"Acha ujinga Allan piga chombo hiyo"
Sauti nyingine bila shaka ilitoka kwa Shetani ilininong'oneza
"Hapana ujue wakati natoka sikufunga ofisi yaani hapa nawaza kweli aisee" nilisema huku nikiwa nakaa sawa...
"Ooh hivyo tu na kumbe nimesahau huna Simu Afisa, okay subir"
Alisema Kisha akatoa Simu yake ya mkononi Aina ya Motorola ya kufunua hivi akabonyeza bonyeza namba Kisha akaweka sikioni,
"Ndio mkurugenzi, Niko na Afisa Michezo hapa , tunaelekea huko vijijini na kutokana na mizunguuko ya wiki hii naomba mkaimishe mtu ofisi yake kwa muda"
Alisema Kisha akazima Simu yake hiyo kwa kuifunika,
"Haya kingine?, Hakuna, Basi Endelea kula" alisema Janet akiwa anatabasamu
"Naamini tuna mengi ya kuongea Allan, let's go"
Alisema Kisha akanyanyuka,
Aliongea na Dereva wake Kisha John akaniaga akasepa zake,
Tulipanda juu ghorofani ambapo kulikua na chumba kizuri sana chenye sebule kubwa,
Nilivua koti langu Kisha nikakaa sebuleni, wakati huo Janet alipitiliza bafuni kuoga Kisha akatoka akiwa amejifunga Taulo
"Vipi huogi?"
"Aah nakuja we oga kwanza bhana"
Nilisema huku nikimaliza kuomba Sala za mwisho...
"Potelea pote,"
Nilisema Kisha nikaenda bafuni kuoga.
****************
Siku tatu tulibaki pale Hotelini Ni Mara chache tu John alikuja kuleta taarifa mbali mbali tu Janet,
Mapenzi yalikolea kwani hatukuelewa K**a Ni mchana au usiku, ilikua Ni kulala na kulala na kufanya mapenzi tu, ..
Simulizi hii imekamilika yote mpaka mwisho ina episode 18 tu njoo inbox au WhatsApp number 0788967317
Simulizi na Riwaya Za Saul David bril
Click here to claim your Sponsored Listing.
Videos (show all)
Category
Contact the establishment
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
Get ready for a bunch of excitements from the trends of the Spencer Show and Spencer Minja at large!
Fredyluttah98@gmail. Com
Dar Es Salaam, 1133
I'm Minister,Mc,Canceller, Public Speaker, and teach Music generally
Dar Es Salaam
FOR BEST CARTOON tuma sms inbox hutegenezwa kwa dkk 10 Kwa Bei nafuu ya mtanzania �