Efatha Church Temeke

Efatha Church Temeke

Efatha Church Temeke deals with the mission of healing and deliverance, containing 22 centers, under the Senior regional Pastor Ester Habakuki Hagai

this page is managed by Efatha ministry temeke, under Senior Regional Pastor Cecilia Mtunda Makundi, we intended to show how God fufill HIS promices to HIS people, basing on all the deads and events that are undertaken in all centres of Efatha Temeke, under control of ICT group of Efatha ministry Temeke, page lunchs all the events in image form and Videos, this is inorder to make all tongues, trib

Photos from Efatha Church Temeke's post 08/09/2024

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 8/9/2024 KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA.

MTUMISHI JOSEPH AWINO
SOMO: SAFARI YA UMILIKI

Umiliki ni safari si jambo la mara moja, tumeokolewa na kutoka hatua moja Kwenda nyingine , ni jambo la mtembeo, tunatembea hatua kwa hatua

Wagalatia 4:1-7
1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;

2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,

5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.

7 K**a ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na k**a u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Daniel 2:17-22
Ufahamu unakupa kile unachomiki kudumu, maarifa ni kuhakikisha kile unachomiiki kwa Roho ya maarifa kinaongezeka na kuwa cha thamani.
Umiliki upo ndani ya majira, majira ya Mungu kumiliki yapo ndani ya muda na wakati
Kuzaliwa kupo ndani ya muda, Maisha yapo ndani ya muda na wakati na kufa kupo ndani ya muda na wakatii ndio maana mtu napokufa watu huuliza alizaliwa lini
Tunakombolewa kwasababu wakati wetu wa kumiliki uliisha kuamriwa
Mungu hubadili majira na nyakati kwa majira yake
Zaburi 31

Yoshua 1:15
" hata Bwana atakapowapa ndugu zenu raha, k**a alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Bwana aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua."

Baadhi yetu tunaweza kuwa wakuu tunachelewa kupata umiliki na tunajiuliza maswali lini mimi nitaolewa au nitaoa/ lini mimi nitapata Maisha ambayo si ya kuhangaika/ ni lini kazi ninayofanya itanipa furaha lakini leo Roho mtakatifu yupo hapa ili kujibu maswali yetu. Maswali yote uliyonayo ni ya wakati fulani katika maisha
Swali lolote ulilonalo katika umiliki limefichwa ndani ya muda

MAMBO 5 YATAKAYOKUSAIDIA KATIKA SAFARI YA UMILIKI

1. Liko tumaini jipya katika majira uliyonayo maana MUngu wa majira yote
Isaya 35 Ukiwa uliokuwa ndani yako unakwenda kuondoka unakwenda kufurahi.
Mungu ni Mungu wa majira yote
Ni kazi yako kuondoa tumaini la zamani na kuingiza tumaini jipya
2. Mngoje Bwana kwa utulivu
Acha kelele, acha maneno mengi wewe mngojee Bwana kwa utulivu pasipo na kelele, mngojee katika uwepo wake.

Isaya 40:31
Vipo vilivyoamriwa kwaajili yako, vipo vilivyojuu unatakiwa kuwa na mbawa ili kuvifikia, vipo vingine vinahitaji hatua
Maombolezo 3:25-26
Unapomngoja kwa utulivu yapo mambo yafuatayo yatatokea kwako
i) Utagundua kwanini upo kwenye majira hayo uliyo nayo
Isaya 37:23
Mwanzo 37:28
Luka 4:1-13 shetani anaweza kukuchomeka mahali pale ambapo hapana umiliki wako

3. Mtafute Bwana kwanza
Isaya 55:6
Zaburi 16:11

4. Uwe na Imani binafsi katika Kristo Yesu
Imani iwe ndani yako si kwa mtu, Imani ikuwa kwa mtu basi umepotea mfano haruni alipoona Bwana anchelewa akamtengeneza mungu wake. Imani yako iwe kwako na Yesu wako alie mwanzilishi wa Imani yako
Yakobo 5:7-11
Waebrania 6:11

5. Tafakari wema wake hata k**a nafsi yako imechoka, yeye ni mwema asubuh na mchana, kuna wakati alikulinda na ajali, aliponya Watoto wako

Zaburi 77:1
" Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia."

Photos from Efatha Church Temeke's post 08/09/2024

Umiliki ni safari si jambo la mara moja, tumeokolewa na kutoka hatua moja Kwenda nyingine , ni jambo la mtembeo, tunatembea hatua kwa hatua.

Wagalatia 4:1-7
1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;

2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.

3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,

5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.

7 K**a ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na k**a u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.

KATIBU:MTUMISHI JOSEPH AWINO

Photos from Efatha Church Temeke's post 08/09/2024

Yohana 4: 24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

08/09/2024

USHUHUDA.

Naitwa Josephine Andrea namshukuru Mungu kwa ajili ya mtoto wangu kwani alipokuwa darasa la saba alipata ugonjwa ikaonekana k**a anadalili za Pumu ya kuzaliwa hivyo anatakiwa kutumia dawa maisha yake yote lakini mimi na mtoto wangu tulikuwa na Imani kuwa haitakuwa hivyo, tuliendelea kumwomba Mungu tarehe 19/8/2024 tulirudi hospitali tena kupima daktari hakuona kitu chochote hivyo napenda kumshukuru Mungu kwa uponyaji

Photos from Efatha Church Temeke's post 08/09/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 08/09/2024.

USHUHUDA.

Naitwa Grace Rashid namshukuru Mungu maana Mungu haangalii mtu bali anaangalia moyo,
Tumezaliwa wengi lakini mimi peke yangu nimeokoka, nilipitia vikwazo vingi sana kwasababu ya kuokoka hadi kuna muda nilikuwa natamani kurudi katika dini yangu lakini Mungu amenipigania katika wokovu,
pia namshukuru Mungu kwaajili ya afya ya mtoto wangu maana alikuwa anaumwa kila tukienda hospitali hawakuti chochote wakati nahangaika familia yangu walisema lolote likitokea ni wewe wao hawahusiki kwasababu nimeamua kuacha dini lakini nikamwambia Mungu nimeamua kuchagua fungu lililo jema, nilipoenda tena hospitali wakasema kuwa mtoto sukari yake imeshuka sana kwahiyo tulilazwa hospitali mimi niliendelea kumsihi Mungu amkumbuke mtoto wang una sasa mtoto wangu ni mzima Mungu amempigania

Photos from Efatha Church Temeke's post 01/09/2024

Yohana 4:7-8 “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” Pasipo pendo usiseme unamjua Mungu, hapana! Kwa maana ni katika pendo tu tuna kile tunachosema tunacho. Pasipo pendo Mungu hayupo, pasipo pendo hakuna ubaba.
Waefeso 3:14-19 “ Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu kwenu. Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani…...”
Biblia inasema “ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, ” apa ina maana kuwa hakuna ubaba pasipo Mungu.
Kuna aina tatu ya ubaba
• Ubaba wa Mbinguni
• Ubaba wa kiroho
• Ubaba wa kimwili
Ubaba huu wote unamilikiwa na Baba mmoja ambaye ni baba wa Mbinguni, kwa maana ubaba wa Mbinguni ndiyo umezaa ubaba wa kiroho na wa kimwili hapa duniani.
1 Wakorinto 4:15-21 “ Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi, nawasihi mnifuate mimi…….”
Ustawi wa Mungu na umiliki wake unaenda katika viwango, Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wote ni mmoja hivyo wanaposhuka hapa duniani kimwili ndipo tunakuwa na baba yako, mama yako na baba wa kiroho, wote wana nguvu juu yako, lakini kumbuka wote wanafanya katika roho.
Baba yako wa kimwili aliyekuzaa anaweza kukubariki k**a amebarikiwa kupitia pendo la Mungu k**a sivyo hakuna kitu utakachopokea, baba wa kiroho anazo nguvu za kukubariki kwa sababu baba yako wa kiroho anayo mamlaka katika Mungu ili kubariki wale wanaomwabudu Mungu lakini siyo watumishi wote ambao wana roho ya ubaba ndani yao; kuwa baba wa kiroho kuna gharama, ni lazima uwe umewekwa wakfu na Mungu na siyo na mwanadamu.
© Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha Mwenge.

Photos from Efatha Church Temeke's post 01/09/2024

SOMO: MWAKA WA KUMILIKI
Sisi ni sura ya Mungu, sisi siyo nyani hivyo tunapaswa kuelewa kuwa sisi ni sura ya Mungu, katika mwaka huu wa kumiliki tunapaswa kukusanya taarifa zote tunazostahili kuwa nazo kuhusu kumiliki ili tuweze kumiliki.
Hauwezi kumiliki k**a mmiliki hajakuruhusu, ili uweze kumiliki, haijalishi utafanya kazi kwa bidii kwa namna gani au unaomba kwa namna gani, lakini k**a mmiliki hajakupa wewe hiyo haki ya kumiliki kamwe hautaweza kumiliki, hata ukijaribu au mtu akikukabidhi mali zake ili zikusaidie, hizo mali hazitadumu na wewe. Unaweza kwenda hata ukakopa fedha kwa sababu unatamani kumiliki, lakini baada ya kukopa na kununua ardhi, ukanunua gari au ukaanzisha biashara utaishia kufilisika tu kwa maana mmiliki hajakuridhia uweze kumiliki, na ndiyo maana unaona watu wengi sana wanatembea na madeni; kwa nini? Kwa sababu hawajapewa kibali cha kumiliki na ndiyo maana watu wengi leo hii ni maskini.
Yesu Kristo akasema, “wale walionacho wanaongezewa na wale wasionacho hata kile kidogo walichonacho watanyang’anywa” hii ndiyo sababu unaweza kuona watu wengi wanategemea watu wengine hawajitegemei, wamiliki ni wachache sana, kwa nini? Kwa sababu mmiliki hajawapa haki ya kumiliki, hivyo tunapaswa kumjua mmiliki ili kwamba tuweze kumiliki.
K**a tukiwa na mahusiano mazuri na mmiliki (MUNGU) lazima atatuhakikishia umiliki wetu.
© Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha Mwenge.

01/09/2024

Ibada siyo hiari bali ni agizo na k**a hausikii msukumo wa wewe kwenda ibadani basi jua kuwa uhusiano wako na Mungu haupo tena, Mungu akurehemu na kukurejesha katika nafasi.
© Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha Mwenge.

01/09/2024

TITLE: THE YEAR OF POSSESSION
We are the image of God, we are not monkeys. In this year of Possession we should collect all the information we deserve to have about Possession so that we can Possess.
You cannot Possess if the Owner does not allow you, no matter how hard you work or how you ask, but if the Owner has not given you the right to own it, you will never be able to own it, even if you try or someone entrusts you with his assets to help you, those assets will not last. You might even go and borrow money because you want to own it, but after borrowing and buying land, buying a car or starting a business, you will end up bankrupt because the owner has not approved you to own it, and that is why you see so many people walking around with debts; why? Because they have not been given permission to own and that is why many people today are poor.
Jesus Christ said, "those who have will be increased and those who do not have even the little they have will be taken away" this is the reason why you can see many people depend on other people they do not rely on themselves. The owners are very few, why? Because the owner has not given them the right to own it, so we have to know the owner so that we can own it.
If we have a good relationship with the owner (GOD) he must guarantee our ownership.
© Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira- Efatha Church

01/09/2024

Worship is not voluntary but an order and if you do not feel the urge to go to worship then know that your relationship with God no longer exists, may God have mercy on you and restore you to a place.
© Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira- Efatha Church

01/09/2024

SHUHUDA
Anaitwa Neema Paulo anamshukuru Mungu alikuja kanisani na Mtume Josephat Elias Mwingira alitamka neno kuwa watumishi wasiogope chochote ndipo alilishika neno hilo na akaamua kutoka nje na jiko lake kwa ajili ya kuchoma vitumbua alianza na kilo 6 za vitumbua. Mwaka 2024 aliahaidi mkuto na alikopa hela kwa ajili ya Bwana kiasi cha shilingi laki 4. Mumewe alimwambia asipeleke kiasi chote hicho ila alitoa kwa ajili ya Bwana na ndipo alimuona Bwana akifanya katika familia yake alinunua boda boda kwa ajili ya mume wake afanyie kazi.
Mtume mkuu alitangaza juu ya Mwaka wa kumilikki na aliamini katika Mwaka huu lazima amiliki, alimuona Mungu katika kazi yake ya vitumbua kwa maana watu walikuwa wanatoka mbali wanakuja kununua kwake vitumbua na vilikuwa vinapewa sifa nzuri.
Alikuja katika mkesha alipata kibali cha kuonana na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na alimueleza juu ya biashara yake, Mtume Mkuu alimkumbatia na Neema aliamini ya kuwa atakuja kumiliki na atakuja kuwa mtu mkubwa alipotoka katika mkesha ule alipokea order kubwa ya vitumbua ambayo hajawahi kuipata tangu aanze kupika vitumbua.
Neema anamshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo yake makuu. Ushauri wake kwa watumishi ni kuwa wasimuache Mungu wa Efatha na watu watoe mkuto maana unalipa.

01/09/2024

SHUHUDA
Anaitwa Steven Lema anamshukuru Mungu kwa amtendo yake, mwaka 2008 alikuja kwa ajili ya kuombewa juu ya mitihani yake. Mtume Josephat Elias Mwingira alitamka neno kuwa watakuwa wakuu na watakuwa kichwa na sio mikia. 2009 matokeo ya darasa la 4 yalitoka na akawa wa kwanza shuleni kwao katika kipindi hicho, steve alikuwa anaongoza katika mitihani yake hadi alipoanza masomo yake ya sekondari alikuwa wa kwanza anaongoza hadi alipomaliza masomo yake ya sekondari.
Steve alianza chuo cha Muhimbili ila katika maisha yake ya chuo akaanza kubadilika na alianza kufanya mambo yasiyompendeza Mungu. Mwaka 2022 alipata mpenzi na ndipo alipoamua kumpeleka kwa wazazi wake kwa ajili ya kujitambulisha na kupeleka mahari, ila katika hatua za kutaka kupeleka mahari steve alipitia vita kubwa ya mahusiano na mpenzi wake.
Mwaka 2023 alikutana na watu ambao walikuwa wanamshuhudia kuhusu habari za Yesu. Steve alikuwa haamini tena kuhusu Mungu ila alisikia sauti ikimwambia aamini na ndipo alipoamini na akakubali kuongozwa sala ya toba na akaanza kuja kanisani Efatha. Steve alipata sehemu ya Kwenda kufanya kazi ila mpaka afanye Interview kwanza ndipo apate hiyo kazi steve alitii na alifanya majaribio hayo lakini hakubahatika kupita katika majaribio hayo.
Mwaka 2024 alikuja kanisani na alisikia Neno kutoka kwa Mtume Mkuu kuhusu kuomba na ndipo alianza kufanya maombi yeye na mkewe katika kipindi hicho chote hakuwa na kazi wala ajira kokote ila hakukata tamaa aliamini atapata kazi.
Steve alipata kazi ambayo tofauti na kile alichosomea ila hakukata tamaa, alifanya kazi hiyo ambayo alikuwa analipwa kiasi kidogo sana cha pesa ila alikuwa anaweka ahadi kiasi kikubwa cha mkuto.
Baada ya muda kupita Steve alipigiwa simu na watu kumpongeza na ndipo alipopigiwa simu katika taasisi ambayo inampa Mungu utukufu. Steve anamshukuru sana Mungu wa Efatha kwa matendo yake makuu.

01/09/2024

SHUHUDA
Anaitwa Sara Julius anamshukuru Mungu ni mzaliwa wa mwezi wa 8 wanamshukuru Mungu kwa kuwawezesha na kuwapa kibali katika mwezi wao. Pia wanawashukuru viongozi wao wote kwa kuwashika mkono kwa maombi na pia wanawashukuru watumishi wote kwa ajili ya maombi waliyoomba kwa ajili ya mwezi wao.

Photos from Efatha Church Temeke's post 01/09/2024
Photos from Efatha Church Temeke's post 01/09/2024

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE TAREHE- 1/9/2024

Zaburi 23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”

© Mchungaji Julius Cheyo- Kanisa la Efatha Mwenge.

01/09/2024
Photos from Efatha Church Temeke's post 25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 25/8/2024 KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA.

MCHUNGAJI KIONGOZI: ESTER HAGAI HABAKUKI
SOMO: NEEMA YA MUNGU

Neema ni kustahilishwa pale ambapo hukustaili hata kidogo, ni kibali unachokipata ikiwa huna sifa kabisa ya kupata.
Neema inatusaidiaje kuingia kwenye umiliki wako? ni kukuleta hapo ulipo yaani upo Efatha, umempokea Yesu, awe Bwana na mwokozi wa maisha yako na unaishi nae
Neema itakusaidia nini?

2 Wakorintho 9:8
"Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema"

Neema inakusaidia kuzaa neema nyingine, neema ya kwanza ni kukutoa kule ulipo kuwa. Kila kitu unachokitaka lazima iwepo neema ya kukusogeza

NEEMA ITAWEZAJE UFANYA KAZI/ UFANYE NINI ILI NEEMA YA KWANZA IWEZE KUFANYA KAZI

1. Imani
Itamfanya Mungu ajue kile alichokupa awali kinafanya kazi
2. Toba
Tunaomba toba ni kwa kila unachokutana nacho hata k**a hakikuhusu wewe omba toba
3. Shukrani
Mwambie Bwana Yesu asante maana sistahili hata kidogo maana kwa kadiri unavyoshukuru unakuwa unakiri kuwa neema yako inafanya kazi, unakuwa unamwambia Mungu neema ile iongezeke tena
4. Utii
Kumbukumbu la torati 28 Mungu anaweza kumtumia mtu yoyote kukuletea sauti
5. Matoleo
kwasababu neema ni zawadi, kwa kutoa Zaidi Bwana hufanya zaidi

NEEMA IKIONGEZEA INAFANYA NINI?
1. Kwa kadiri inavyoongezeka inaondoa kujisifu
2 Wakokorinto 3:18
2. Unakuwa mtu wa ibada
3. Bwana mwenyewe analinda milki yako
4. Inakupa kuzidi na kuongezeka katika utukufu
5. Unapata zawadi za umiliki sawasawa na neema inavyozidi
MAOMBI
Bwana hajawahi kumshusha mtu kazi, hawezi kushusha frequency zaibada,mwambie Bwana wewe hufanya sisi tupande si kushuka, maishaa uliyoyatoa kwa Yesu haikuwa yakushushe bali yakupandishe, sadaka zako na muda wako uliotoa hukuta ili ushuke bali upande

Chochote kinachoinuka kwangu kiwe siri au ubaya iwe zurii au baya halitashusha uthamani wangu, nimegonga muhuri kwenye maombi yangu.

25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.
MCHUNGAJI KIONGOZI ESTER HAGAI HABAKUKI.

Neema inakusaidia kuzaa neema nyingine, neema ya kwanza ni kukutoa kule ulipo kuwa. Kila kitu unachokitaka lazima iwepo neema ya kukusogeza

NEEMA ITAWEZAJE UFANYA KAZI/ UFANYE NINI ILI NEEMA YA KWANZA IWEZE KUFANYA KAZI
1. Imani
Itamfanya Mungu ajue kile alichokupa awali kinafanya kazi
2. Toba
Tunaomba toba ni kwa kila unachokutana nacho hata k**a hakikuhusu wewe omba toba
3. Shukrani
Mwambie Bwana Yesu asante maana sistahili hata kidogo maana kwa kadiri unavyoshukuru unakuwa unakiri kuwa neema yako inafanya kazi, unakuwa unamwambia Mungu neema ile iongezeke tena
4. Utii
Kumbukumbu la torati 28 Mungu anaweza kumtumia mtu yoyote kukuletea sauti
5. Matoleo
kwasababu neema ni zawadi, kwa kutoa Zaidi Bwana hufanya zaidi

Photos from Efatha Church Temeke's post 25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.
Zaburi 9:1-2 "Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu."

25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.

USHUHUDA

Anaitwa Steven Gabriel anamshukuru Mungu maana alikuwa mtu wa kuja kanisani na kuondoka pasipo ubatizo, siku ya jana ailibatizwa na kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na mradhi lakini tangu amebatizwa siku ya jumamosi 24/8/2024 ameponywa sasa anajiskia mwepesi yale yaliyokuwa yanamsumbua siyasikii tena

25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.

USHUHUDA

Naitwa Maria Shirima namshukuru Mungu maana mtoto wake alikuwa na shida ya ngozi tangu amezaliwa hadi ikafikia hatua ya kupangiwa mavazi ya kuvaa na kula aina ya vyakula hali hii hakuipenda. Siku moja Mtume na Nabii alitangaza wote wenye matatizo yaliyoshindikana hospitali waguse madhabahu yeye Maria akagusa na kwanzia wakati ule mtoto wake akaanza kupokea uponyaji na saa hii mtoto amepona kabisa

25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.

USHUHUDA

Anaitwa Natalia Mpota alikuwa na shida ya mgongo alikuwa hawezi kusimama kwa muda mrefu na alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu bila kupumzika njiani hali hii ilidumu kwa miaka miwili siku ya ijumaa kulikuwa na mkesha wa ukombozi baada za kufanyiwa maombi aliweza kusimama kwa muda mrefu na sasa naweza kutembea mwendo mrefu bila kupumzika Sifa na utukufu tunamrudishia Mungu wa mbinguni.

Photos from Efatha Church Temeke's post 25/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 25/08/2024.

SOMO LA UFUNGUZI

ASKOFU: DESDERIA KIPENGELE
Zaburi 103:1-10
1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.

2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.

3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,

4 Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,

5 Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa k**a tai;

6 Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.

7 Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake.

8 Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

9 Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele.

10 Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.

23/08/2024

HAPPY BIRTHDAY OUR BELOVED MOTHER

Indeed you are a Kingdom Icon and Our Mother in Faith, Mama Eliakunda Mwingira.

We thank God for His Faithfulness in your life and for making you to see another beautiful Year. We pray for Multiplied Grace, Multiplied Glory with Multiplied Impact on the earth.

May the Oil on your head remain ever fresh and may you keep walking stronger in Jesus Name. We pray that your joy will continually be filled. Thank you for the role you play in the Church and to our Spiritual Father Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira and for being such a Blessing in our Lives.

We Love You and We Celebrate you Mama.

Photos from Efatha Church Temeke's post 19/08/2024

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA MBAGALA TAREHE 18/08/2024.

MCHUNGAJI KIONGOZI: ESTER HAGAI HABAKUKI

UMOJA KATIKA KRISTO YESU

Umoja asili yake ni Mbinguni, umoja ulianzia katika
Mwanzo 1:26

“ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kw asura yetu;wakatawale samakiwa baharini, na ndege wa angani na Wanyama; na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Neno linaposema kuwa tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu maana yake kulikuwa na kikao wakakaa na kuadhimia, maana yake hapa hakuwa mmoja walikuwa wengi, wakati ambao Mungu alikuwa anamtengeneza mwanadamu hakumtengeneza kwa namna ya uchache wala kwa namna ya ubinafsi bali walikuwa katika kikao walikaa na kukubaliana kwahiyo siku mwanadamu anaumbwa aliwekewa roho ya umoja ambapo hapo kulikuwa na Mungu, Baba, Mwana na Roho.
Wakati wa uumbaji wa mwanadamu walimweka sawasawa na wao walivyo yaani mwanadamu nayo ni mwili, nafsi na Roho. Tunaposema Mungu maana yake kuna utatu mtakatifu na mwanadamu hawezi kuwa mwanadamu pasipo utatu wa mwili, nafsi na Roho.
Kwanini umoja ni nguvu kwasababu kuna utatu mtakatifu na Mungu ni nguvu yaani Mungu anapokaa nguvu zake huonekana.
K**a hakuna umoja Mungu hawezi kuja
Yohana 17:11-20
Saa ambapo mwanadamu alipokosea ile nguvu aliyoumbwa nayo iliondoka
1.umoja wa mwadamu na Mungu
2.umoja wa mwanadamu na mwadamu
Wanadamu wasipokaa katika umoja watachukiana
Yohana 17:20-23
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
21 Wote wawe na umoja; k**a wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja k**a sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao k**a ulivyonipenda mimi.

Pasipo kuwa na umoja maana yake hakuna kukamilika.

Umoja unazaa matunda ndani ya kanisa,
Ni hatari sana k**a ndoa zinavunjika sana kanisani kwasabbau kuna nguvu ya kanisa inakuwa inapotea kwasababu ndoa ni ya Mungu mwenyewe.

Kwanini Umoja

1. Ndipo ufalme unatenda kazi, ni tabia ya kifalme kufanya kazi kwa pamoja. Kazi ya Yesu kuja ni kutuelezea habari za ufalme wa Mungu
2. Alikuja kurudisha umoja kati yake na sisi
3. Alihitaji aache kanisa linatembea pamoja
4. Ili turudi katika umiliki wetu, huwezi kumiliki k**a huna nguvu ya kubeba
5. Ilikuwa na sehemu ya kuifunza kuwa sisi tumetoka pamoja, Yesu alikuja kutufundisha kuwa sisi ni wamoja

Utawezaje kuwa na umoja.

1. Jiweke mwenyewe katika umoja, jiambie mwenyewe kuwa siwezi kufanya kazi pasipo mwili, Roho na nafsi ili kuhakisha ulinzi wako mwenyewe
2. Jiambie kwamba utatu unatakiwa kukaa ndani yako. Utatu Mtakatifu lazima ukae na utatu wa mwili
3. Amini kuwa wewe ni umoja, watu wanakutegemea sana yan hawawezi kufanya maamuzi pasipo wewe
4. Mpende na kumuheshimu kila unayemwona mbele yako maana hujui ni kikao gani kimefanyika na huyo mtu kuhusu wewe.

Photos from Efatha Church Temeke's post 18/08/2024

Utawezaje kuwa na umoja
1. Jiweke mwenyewe katika umoja, jiambie mwenyewe kuwa siwezi kufanya kazi pasipo mwili, Roho na nafsi ili kuhakisha ulinzi wako mwenyewe
2. Jiambie kwamba utatu unatakiwa kukaa ndani yako. Utatu Mtakatifu lazima ukae na utatu wa mwili
3. Amini kuwa wewe ni umoja, watu wanakutegemea sana yan hawawezi kufanya maamuzi pasipo wewe
4. Mpende na kumuheshimu kila unayemwona mbele yako maana hujui ni kikao gani kimefanyika na huyo mtu kuhusu wewe.

Kiongozi Ester H. Hagai

Photos from Efatha Church Temeke's post 18/08/2024

Yohana 17:11-20 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja k**a sisi tulivyo.
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, k**a mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.Wao si wa ulimwengu, k**a mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. K**a vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.

Pasipo kuwa na umoja maana yake hakuna kukamilika
Umoja unazaa matunda ndani ya kanisa,
Ni hatari sana k**a ndoa zinavunjika sana kanisani kwasabbau kuna nguvu ya kanisa inakuwa inapotea kwasababu ndoa ni ya Mungu mwenyewe

KWANINI KUWA NA UMOJA
1. Ndipo ufalme unatenda kazi, ni tabia ya kifalme kufanya kazi kwa pamoja. Kazi ya Yesu kuja ni kutuelezea habari za ufalme wa Mungu
2. Alikuja kurudisha umoja kati yake na sisi
3. Alihitaji aache kanisa linatembea pamoja
4. Ili turudi katika umiliki wetu, huwezi kumiliki k**a huna nguvu ya kubeba
5. Ilikuwa na sehemu ya kuifunza kuwa sisi tumetoka pamoja, Yesu alikuja kutufundisha kuwa sisi ni wamoja

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Our Story

this page is managed by Efatha ministry temeke, under Senior Regional Pastor Cecilia Mtunda Makundi, we intended to show how God fufill HIS promices to HIS people, basing on all the deads and events that are undertaken in all centres of Efatha Temeke, under control of ICT group of Efatha ministry Temeke, page lunchs all the events in image form and Videos, this is inorder to make all tongues, tribes, and nations to be disciples of The LORD Jesus christ of Nazareth, son of living God, as it is the vision given to the Apostle and Prophet JOSEPHAT ELIUS MWINGIRA, The anointed one.

Videos (show all)

THE ANNUAL GATHERING 2024 - PRECIOUS CENTRE KIBAHAApostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, extends a warm invitation...
Shuhuda ni mojawapo ya matokeo ya kutembelewa na Bwana. Tunatangaza kuwa shuhuda kama hizi zikawe ni za kudumu kwa jina ...
Acha Bwana akatende na kwako maana Yesu aliyemtendea huyu mama, ni yeye yule jana na leo na hata milele! Huyu Yesu tunay...
Barikiwa na ushuhuda huu mfupi — Acha ushuhuda huu ukawe BARAKA na UNABII kwako & ukaifanye IMANI yako ijengeke zaidi kw...
KANISANI LA EFATHA LIMEKUANDALIA MKUTANO MKUBWA WA INJILI ENEO LA MBAGALA VIWANJA VYA ZHAKHEM TEMEKE NA MTUME NA NABII J...
IBADA YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU YA KWANZA TAREHE 1/5/2024, KANISA LA EFATHA MBAGALA DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Mwana wa Mungu, ni siku MOJA (1) tu imebaki katika kuelekea KUSANYIKO kuu la SIFA la WANA wa MUNGU, Umejiandaaje?Biblia ...
Kuelekea KUSANYIKO hili kubwa la SIFA la Wana wa Mungu katika mji mtakatifu wa Precious Center Kibaha.Umejiandaaje kuwep...

Address


Mbagala
Dar Es Salaam
P.OBOX41587
Other Dar es Salaam government services (show all)
U.S. Embassy Tanzania U.S. Embassy Tanzania
686 Old Bagamoyo Road, Msasani
Dar Es Salaam

The U.S. Mission to the United Republic of Tanzania. Terms of Use: https://www.state.gov/tou

Waterbuck Safaris Waterbuck Safaris
55 Ali Hassan Mwinyi Road, East Upanga
Dar Es Salaam, 3272

We offer Wildlife Safaris to all National parks of Tanzania, Tailor-made safaris, Camping safaris, H

bibowildnet.africa bibowildnet.africa
Bahari Beach
Dar Es Salaam, 14122

bibowildnet.africa �It is based on wild issues �wild photographing �Promoting afican tourism especially Tanzania � #Visitzanzibar � #Visittanzanianationalparks � #tanzaniaunforgett...

Godfrey Godfrey
Masakahgodfrey389@gmail. Com
Dar Es Salaam, MASAKA

MUONA MBALI "360" MUONA MBALI "360"
Kinondoni
Dar Es Salaam

TWENDE NA MAMA "360"

Maneno ya Ahlubait a.s" Maneno ya Ahlubait a.s"
Dovya B
Dar Es Salaam

Maneno, Nasaha, Hekima na Mafunzo ya Mtume Mohamad {s.a.w.w} pamoja na kizazi chake kitukufu {Ahlubait a.s}

Tourism Tz Tourism Tz
Mikicheni
Dar Es Salaam

Visit Tanzania for Tourism

Mkuulo Mkuulo
Kilolo
Dar Es Salaam, 25632

ExtRa DisCovery ExtRa DisCovery
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam, 16102

best wishes filled an empty heart. bad wishes filled the dieing heart. stay awaken😳

Vggggg Vggggg
Dfdfdf
Dar Es Salaam, 11000

Hugulole Hugulole
Dar
Dar Es Salaam, 156870

hi

Kuhani Musa Kuhani Musa
Mbezi Temboni
Dar Es Salaam