NSSF Tanzania

The National Social Security Fund is a fully funded scheme running under defined benefit principles. The scheme is financed through at the rate of 20%.

The page is dedicated to nurturing relationships and creating positive & lasting connections with our members. Our page will talk about all matters pertaining to Social Security, Benefits that member of NSSF are entitled with and it also serves as a platform for members to channel their complains and queries. Welcome to the official National Social Security page, We are here to respond to all your complains and queries.

Photos from NSSF Tanzania's post 29/06/2024

NSSF Tupo SabaSaba Banda namba 13 karibu tukuhudumie

NSSF tunawakaribisha wanachama na wananchi wote kutembelea banda letu namba 13 ili waweze kujipatia huduma mbalimbali tunazozitoa kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), SabaSaba. Karibu Tukuhudumie

Photos from NSSF Tanzania's post 28/06/2024

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF

Na MWANDISHI WETU,
Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuhitimisha Bunge Jijini Dodoma, tarehe 28 Juni, 2024.

Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA. Aidha, Bw. Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujali maslahi ya watanzania.

Pamoja na hayo, Bw. Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.

26/06/2024

RAIS DKT. SAMIA ANAGUSWA NA KUJALI MAISHA YA WAFANYAKAZI
*Amenyanyua kikokotoo, Ndejembi asema huo ni mwanzo tu

22/06/2024

CHETI CHA SHUKRANI

NSSF imeshiriki na kudhamini Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari pamoja na Kikao Kazi Cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali 2024. Mhe. Nape Moses Mnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akimkabidhi cheti Cha shukrani Bw. Sebera Fulgence - Afisa Uhusiano Mkuu wa NSSF.

Photos from NSSF Tanzania's post 22/06/2024

NSSF YAPOKEA GAWIO KUTOKA CRDB IKIWA NI ENEO MOJAWAPO LA UWEKEZAJI

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki katika hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali na Taasisi zake iliyofanyika tarehe 21 Juni, 2024 jijini Dodoma.

Photos from NSSF Tanzania's post 21/06/2024

NSSF YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA ATE, YAZUNGUMZIA MSAMAHA WA TOZO NA MATUMIZI YA TEHAMA

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki mkutano mkuu wa 65 wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE). Mkutano huo ulifunguliwa tarehe 20 Juni 2024 na Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye alimuwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Deogratius Ndejembi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Katambi amesema ni maagizo na maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa taasisi zote za Serikali kushirikiana na taasisi za binafsi katika usimamizi mzuri wa sera, sheria, taratibu, kanuni, mipango na mikakati ya Serikali ili kufikia malengo ya pamoja.

Naye, Meneja Uandikishaji, Ukaguzi na Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi amesema Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi yakiwemo kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

Amesema hivi sasa NSSF imetoa msamaha kwa waajiri wenye malimbikizo ya michango na tozo itokanayo na ucheleweshaji wa michango.

Bw. Sasi amesema kuwa Bodi ya Wadhamini ya NSSF imetoa msamaha wa tozo kwa waajiri wote wa sekta binafsi. Amebainisha kuwa katika msamaha huo waajiri wote ambao wana malimbikizo ya michango watakaolipa malimbikizo yao yote hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2024 watapata msamaha wa tozo kwa asilimia 100.

Kwa waajiri ambao watalipa malimbikizo yote kati ya tarehe 1 Agosti, 2024 hadi 31 Agosti, 2024 watapata msamaha wa tozo kwa asilimia sabini na tano (75) na waajiri wote ambao hawana malimbikizo yoyote ya michango ya wanachama wanayodaiwa na NSSF mpaka kufikia tarehe 31 Mei, 2024 na kuendelea hadi tarehe 31 Julai, 2024 watasamehewa tozo zote wanazodaiwa kwa asilimia mia moja 100.

Bw. Sasi amesema NSSF imepiga hatua kubwa kwenye TEHAMA ambapo waajiri wanaweza kujisajili na kusajili wafanyakazi wao na kuwasilisha michango bila kufika katika ofisi za NSSF kupitia mfumo wa huduma binafsi kwa mwajiri (Employer portal).

“Maendeleo haya ya TEHAMA yamesaidia katika kuongeza ufanisi na kukuza thamani ya NSSF pamoja na kuongeza wanachama," amesema Bw. Sasi.

Photos from NSSF Tanzania's post 21/06/2024

NSSF YAANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU KATIKA NYUMBA ZAKE

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanza zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu walioshindwa kutekeleza matakwa ya mkataba wa ununuzi wa nyumba katika miradi yake ya Dar es Salaam. Zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu hao lilifanyika tarehe 18 Juni 2024 katika mradi wa nyumba za Kijichi, Temeke.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja Miliki wa NSSF, Geofrey Timoth amesema zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu walioshindwa kulipa madeni yao ya muda mrefu katika nyumba za NSSF ni endelevu katika miradi yote.

Timoth amesema kuwa NSSF ilitoa notisi ya siku 30 na baadaye ilitoa siku 14 ya kuwataka wadaiwa hao kulipa madeni yao lakini hawakulipa, hivyo baada ya kujiridhisha na kufanya tathimini, NSSF ilifanya maamuzi ya kuwatoa wadaiwa sugu katika nyumba zake ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kununua nyumba hizo kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Dionisia Kamugisha, ametoa wito kwa wananchi wa mtaa huo walionunua nyumba za NSSF kulipa madeni yao wanayodaiwa ili kuepuka adha ya kuondolewa katika nyumba hizo.

Photos from NSSF Tanzania's post 21/06/2024

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA: NSSF YAENDELEA KUBORESHA MIFUMO YA RASILIMALI WATU NA UTAWALA

Na MWANDISHI WETU,

Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa wananchi kuwa wafuatiliaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika simu zao za kiganjani ili kujipatia huduma nyingi za kijamii zinazotolewa na Serikali.

Mhe. Simbachawene amesema hayo tarehe 19 Juni 2024, wakati akifungua Maadhimisho ya Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16, mwaka huu, katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Naye, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Ekwabi Mujungu, amesema Mfuko unashiriki katika Wiki ya Utumishi wa Umma yenye kauli mbiu isemayo "Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma uliojikita kwa Umma wa Afrika ya Karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi; Ni Safari ya Mafunzo na Mabadiliko ya Kiteknolojia".

Bw. Mujungu amesema NSSF ni sehemu ya mabadiliko hayo ya kiteknolojia kwa kuhuisha shughuli za kiutendaji kupitia mifumo ya kidijitali ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watumishi ndani ya ofisi na wateja wanaowahudumia.

Amesema Wiki ya Utumishi wa Umma ni fursa kwa NSSF kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kupitia majukumu yake ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

"Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la NSSF ili waweze kufahamu huduma tunazotoa, vilevile kwa wajasiriamali waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya baadaye," amesema Bw. Mujungu.

Amesema akiwa Msimamizi wa rasilimali watu, wanaendelea kuboresha mifumo ya rasilimali watu na utawala ili kuendelea kutoa huduma bora kwa watumishi ndani ya NSSF.

20/06/2024

TAARIFA KWA UMMA: MSAMAHA KWA WAAJIRI WENYE MALIMBIKIZO YA MICHANGO NA TOZO ITOKANAYO NA UCHELEWESHAJI WA MICHANGO

20/06/2024

Salamu za Pongezi

Photos from NSSF Tanzania's post 18/06/2024

MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KARIBU TUKUHUDUMIE

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) upo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo, NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, uwekezaji (fursa za nyumba na viwanja). Pia, elimu kuhusu huduma za NSSF kidijitali pamoja na dawati la kutatua changamoto kuhusu mafao, michango na huduma mbalimbali za NSSF.

17/06/2024

Eid Al Adha Mubarak

Photos from NSSF Tanzania's post 16/06/2024

Amesisitiza kuwa, waliokuwepo kwenye mpango wa matumizi ya ardhi ambao ni takribani 145 walishaongea na NSSF na tayari walishakubaliana.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Milki wa NSSF, Bw. Geofrey Timoth amesema katika kutekeleza maelekezo hayo ya Waziri wa Ardhi, NSSF inatarajia kuondoa nyumba zote ambazo zipo kwenye barabara na miundo mbinu ya maji pamoja na kuhakiki watu wachache ambao wanadai walikuwepo tokea mwaka 2021/22.

Bw. Timoth amesema zoezi hilo ni muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliyotoa wiki iliyopita.

Amebainisha namna ambavyo NSSF wanaenda kutekeleza maelekezo ya Waziri wa Ardhi ni kuwa bàadhi ya maendelezo yaliyofanywa ambayo waliyabaini mwaka 2021 na 2022 wamekubaliana kuwa watakaa na wahusika kwa sababu yapo kwenye mpango wa ardhi.

"Kwa hiyo tutakaa na wahusika na tutawaambia ni nini cha kufanya ili waendelee kuwa na amani kwenye maeneo husika," amebainisha Timoth.

Ameendelea kubainisha kuwa maeneo ambayo yaliendelezwa nje ya mwaka 2021/22 yataenda kuondolewa kwa sababu NSSF ina mpango wa kuyaendeleza pamoja na utaratibu wa kuzuia uvamizi kwenye maeneo mengine.

Photos from NSSF Tanzania's post 16/06/2024

NSSF yarudisha kwa jamii na kusaidia vifaa vya kuboresha huduma za afya

Na MWANDISHI WETU,

Kilimanjaro. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kutekeleza jukumu lake lingine la kurudisha kwa jamii kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mazingira ya utoaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Kituri, Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.

Baadhi ya vifaa hivyo ni meza, viti, makabati na mabenchi kwa ajili ya wagonjwa ambapo NSSF kupitia sera yake ya uchangiaji na udhamini (CSR), imekuwa ikiiunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maeneo ya afya, elimu, michezo na maeneo mengine ya kijamii kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania kwa ujumla. NSSF imekuwa ikifanya hivyo kwa kurudisha kwenye jamii kupitia sekta ya afya, elimu pamoja na huduma za kijamii.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja wa NSSF Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Audrey Claudius amemkabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kituri Mhe. Athuman Ramadhan Karavile, kwa ajili ya Zahanati hiyo ya Kituri.

Msaada huo umetolewa mwishoni mwa wiki hii huko Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Photos from NSSF Tanzania's post 16/06/2024

NSSF ILIVYOSHIRIKI NA KUTOA HUDUMA MAONESHO YA MBEYA CITY EXPO 2024

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki na kutoa Huduma katika Maonesho ya Biashara ya Mbeya City Expo 2024 yaliyofanyika kuanzia tarehe 23-30 Mei, katika viwanja vya Uhindini.

Maonesho hayo yaliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya kwa kushirikiana na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA). Lengo la maonesho hayo lilikuwa ni kupanua wigo wa uzalishaji bidhaa na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja, Mkoa na Taifa kwa ujumla pamoja na upatikanaji wa teknolojia mpya za uzalishaji bidhaa kupitia majukwaa mbalimbali.

Kupitia maonesho hayo NSSF imeweza kuhudumia wanachama kwa kuwaunganisha na huduma mbalimbali za kidijitali ikiwemo NSSF Taarifa ambayo inawawezesha wanachama kupata taarifa binafsi, michango na madai yao bila kulazimika kufika katika Ofisi za NSSF.

Pia, NSSF imetoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa makundi mbalimbali pamoja na wafanya biashara, wakulima na wafanyakazi kutoka sekta rasmi.

10/06/2024

MIRADI YA VIWANJA VISIGA NA KILUVYA

Photos from NSSF Tanzania's post 09/06/2024

NSSF YAZIDI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZAKE KIDIJITALI

*Ni kupitia mfumo wa NSSF Taarifa mwanachama anaweza kupata taarifa zake kiganjani popote alipo

Na MWANDISHI WETU,
Tanga. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF), ulishiriki katika Maonesho ya 11 ya Biashara na Utalii yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga, na kutumia fursa hiyo kutoa elimu na huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii huku ukiwataka wanachama wake kutumia huduma ya NSSF Taarifa ili kupata taarifa zao mbalimbali kiganjani zikiwemo za michango popote walipo bila ya kulazimika kufika ofisi za NSSF.

Hayo yamesemwa na Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga, Bw.Abubakari Mshangama. Amesema NSSF Taarifa ni mfumo rafiki na rahisi unaowawezesha wanachama kupata taarifa binafsi, michango na madai yao.

Bw. Mshangama amesema huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS), programu ya simu ya kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.

“Tupo hapa kwenye maonesho haya kimkakati kwa kutoa elimu kuhusu huduma zetu mbalimbali, pia kuitangaza programu hii ya kidijitali zaidi ambayo inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma kwa njia ya ujumbe mfupi,” amesema Bw. Mshangama.

Aidha, amesema kupitia maonesho hayo NSSF inaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii hususan katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kutangaza fursa za uwekezaji za nyumba, viwanja pamoja na elimu kuhusu mafao.

Awali, akizungumza mara baada ya kutembelea banda la NSSF, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe. Zainab Abdallah amewataka wafanya kazi waliopo katika sekta rasmi na wajasiriamali kujiunga na NSSF ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa.

“Niendelee kuwahimiza wafanyakazi na waajiri wajue kwamba ni takwa la kisheria wahakikishe wanawasajili wafanyakazi NSSF ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali,” amesema.

Photos from NSSF Tanzania's post 06/06/2024

WAZIRI SILAA AZUIA UTAPELI ENEO LA NSSF

*Ni baada ya NSSF kuweka mtego wa kuwak**ata matapeli hao

*Walitaka ‘kumpiga’ Mama milioni nane, wakaishia mikononi mwa polisi

Na MWANDISHI WETU,
Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Jerry Silaa amempa siku 14 Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha amewaondoa watu wote waliovamia ardhi inayomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtaa wa Malela, Kata ya Toangoma Dar es Salaam.

Mhe. Silaa amesema hayo tarehe 5 Juni 2024 katika Mtaa wa Malela Toangoma mara baada ya kuwak**ata watuhumiwa sugu wanne wanaodaiwa kuwatapeli wananchi na kuwauzia ardhi, baada ya NSSF kuweka mtego uliofanikisha kutiwa nguvuni kwa watuhumiwa hao.

Amesema kuanzia sasa anapiga marufuku Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kujihusisha na mauzo ya ardhi pamoja na nyaraka za Serikali za mitaa kutumika kuuzia viwanja na kuwa hivi sasa Wizara ya Ardhi inafanya marekebisho ya GN ya mwaka 2021, inayotoa nyaraka zinazotumika katika mauzo ya ardhi ambapo wanatarajia kutoa nyaraka mpya za kuuza maeneo nchini.

“Watu wa Serikali za Mitaa wakae mbali na shughuli za ardhi kwa hili watatusamehe nipo makini sana na masuala ya ardhi pamoja na utapeli wa ardhi unaoendelea,” amesema Mhe. Silaa.

Aidha, amewaagiza Polisi kuwak**ata watuhumiwa hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria huku akimuagiza Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO) kufanya operesheni maalumu katika eneo hilo ili kuwak**ata watuhumiwa wengine na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Nataka niwapongeze wenzetu wa NSSF kwa kufanikisha kuk**atwa kwa watuhumiwa hawa ambao wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuuza maeneo ya NSSF na kuwadhulumu wananchi,” amesema Mhe. Silaa.

Naye, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malela, Oswin Mkinga amewashukuru NSSF kwa kuweka mtego uliofanikisha kuk**atwa kwa watuhumiwa hao na kuwa maeneo hayo yanamilikiwa na NSSF na ni sehemu ya mradi wa viwanja 20,000 vya Toangoma ambavyo vilinunuliwa kwa utaratibu wa fidia mwaka 2000.

Amesema kuanzia mwaka 2000 mpaka 2023 utaratibu uliratibiwa na Wizara ya Ardhi kwa maana ya kuvipima na kuanza kuviuza, ambapo kuanzia mwaka 2019 alipoingia kwenye uongozi wa mtaa huo aliukuta uvamizi wa viwanja hivyo, lakini moja ya jitihada walizozifanya ni kutoa elimu kwa wananchi kuwa maeneo hayo ni mali ya NSSF na yanauzwa kwa utaratibu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Miliki wa NSSF, Geofrey Timothy amemshukuru Mhe. Silaa kwa ushirikiano wake. Amesema walipewa taarifa kuwa eneo hilo kuna matapeli wanashiriki kuuza maeneo ya Mfuko na hivyo waliweka mtego uliofanikisha kuk**atwa kwa matapeli hao.

“Ujumbe huu naomba ufike kwa wote waliovamia maeneo ya NSSF na pia ninawahakikishia wanachama wa NSSF kuwa maeneo yao yapo salama kwa sababu tuna utayari wa kutosha wa kuyafanya yawe salama,” amesema Timothy.

Mmoja ya waliotapeliwa kwa kuuziwa ardhi katika eneo hilo, Bi. Asha Ally Seif ameipongeza NSSF kwa kufanikisha kuk**atwa kwa watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kumtafuta bibi na kudai hilo ni eneo lake jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Photos from NSSF Tanzania's post 05/06/2024

NSSF YAWANOA WATUMISHI WAKE ILI KUZIDI KUIFIKIA SEKTA ISIYO RASMI

Na MWANDISHI WETU,
Dodoma. Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kupitia kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi wamejengewa uelewa kuhusu Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Isiyo Rasmi (NISS) ambao ni mahususi kwa ajili ya wanachama waliojiajiri kupitia sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote.

01/06/2024

TUNAPINGA RUSHWA

01/06/2024

Karibu Tukuhudumie, Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni

Photos from NSSF Tanzania's post 30/05/2024

NSSF YAWANOA WASTAAFU WATARAJIWA MKOA MWANZA

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetoa elimu kwa wastaafu watarajiwa wa Mkoa wa Mwanza ambao ni wanachama wa NSSF kuhusu namna bora ya kufanya maandalizi ya kustaafu, mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko huo ambapo umewahakikishia kuwa umejipanga kuwahudumia kupitia pensheni ya uzee. Elimu hiyo imetolewa Mei 28, 2024 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Mwanza, ambapo mgeni rasmi katika semina hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mheshimiwa Mtanda alitumia fursa hiyo kuipongeza NSSF kwa kuendelea kutoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kwani elimu hiyo itawasaidia kuishi maisha bila ya wasiwasi, huku akiwasihi wastaafu watarajiwa kuweka mipango mizuri ya matumizi ya fedha watakazolipwa na NSSF.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NSSF, Bw. Robert Kadege aliwahakikishia wastaafu watarajiwa kuwa NSSF ipo imara na itaendelea kulipa pensheni ya uzee kila mwezi na kwa wakati. Bw.Kadege alitumia fursa hiyo pia kuwaasa waajiri wa sekta binafsi kuhakikisha wanatekeleza vema wajibu wao wa kusajili wafanyakazi na kuwasilisha michango kwa wakati.

Nao baadhi ya wastaaafu watarajiwa ambao ni wanachama wa NSSF, wameishukuru NSSF kwa kutoa elimu hiyo kwa wakati sahihi kwani imewasaidia kuwaondolea hofu ya maisha ya baada ya kustaafu na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi

Photos from NSSF Tanzania's post 30/05/2024

KATIBU MKUU ATEMBELEA NSSF
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Bi. Mary Maganga amekutana na Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Ofisi za NSSF, Dar es Salaam, ambapo amepongeza kazi kubwa inayofanywa na NSSF katika kutekeleza majukumu yake ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

Photos from NSSF Tanzania's post 23/05/2024

NSSF YAWAHAKIKISHIA WASTAAFU WATARAJIWA KUWA IKO IMARA NA INAENDELEA KULIPA MAFAO KWA WAKATI BILA USUMBUFU

*Yasema imejikita zaidi kutoa huduma kidijitali

Na MWANDISHI WETU,
Mbeya. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kuwanoa wastaafu watarajiwa kwa kuwapa mafunzo ya kujiandaa kustaafu huku ukiwahakikishia kuwa utaendelea kulipa mafao yaliyoainishwa kwenye sheria kwa wakati bila ya usumbufu wowote.

Hayo yalisemwa na Bw. Robert Kadege, Meneja Huduma kwa Wateja wakati akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, amewahakikishia wastaafu wake kuwa NSSF iko imara na itaendelea kuwalipa wastaafu pensheni zao kila ifikapo tarehe 20 hadi 24 ya kila mwezi.

Bw. Kadege amesema hayo tarehe 22 Mei, 2024 jijini Mbeya ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo yaliyoandaliwa na NSSF kwa wastaafu watarajiwa wa mkoa huo ambao wamepatiwa elimu kuhusu namna bora ya kufanya maandalizi ya kustaafu, mafao mbalimbali yanayotolewa, fomula na jinsi ya kuendesha shughuli za kiuchumi ambazo wastaafu wanapaswa kuzifanya pamoja na elimu kuhusu afya.

“Naomba niwape salamu za Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba ambaye ameniambia niwahakikishie kuwa Mfuko wetu uko imara na endelevu na kuwa unaendelea kulipa mafao yaliyoainishwa kwenye sheria hivyo msiwe na wasiwasi wowote,” amesema Bw. Kadege.

Naye, Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Bw. Deus Jandwa amewashukuru washiriki wa semina hiyo kwa mwitikio mkubwa wa kuhudhuria mafunzo hayo ambapo amewahakikishia kuwa NSSF imejikita kutoa huduma zake kidijitali zaidi kupitia PORTAL ambayo kwa upande wa waajiri (Employer Portal) inawarahisishia kuwasilisha michango ya wanachama wao kwa wakati na vilevile kwa upande wa wanachama (Member Portal) wanaweza kufuatilia taarifa zao popote walipo bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.

Aidha, Meneja Malipo ya Pensheni wa NSSF, Bi. Nancy Mwangamila amewaeleza wastaafu watarajiwa umuhimu wa kuandaa taarifa zao za uanachama, michango na kuwataka kwenda kuzihakiki k**a zipo sawa ili wakati wa kufungua madai ya kustaafu kusijitokeze changamoto yoyote kuhusiana na taarifa hizo ili waweze kulipwa kwa wakati.

Meneja Huduma za Matibabu wa NSSF, Bi. Aisha Marine naye amesema huduma ya afya inatolewa kwa wanachama ambao wapo kwenye ajira na wanachangiwa michango yao kwa wakati bila kukosa pia kwa wastaafu wanaweza kupata huduma hiyo kwa kuchangia asilimia sita ya mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa hiari yao kwa kuandika barua ya kuomba kukatwa asilimia hiyo ambayo itakatwa kwa muda wa miezi mitatu ndipo watakuwa wamefikia kigezo cha kupata huduma ya matibabu. Pia alitoa elimu ya namna bora ya kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Awali, Bi. Lydia Kimario, Afisa Mkuu Mafao ametoa mada kuhusu namna kukokotoa mafao na jinsi gani wanaweza kujiandaa kabla ya kustaafu.

Mzee Merthob Kapinga (76), amesema alistaafu utumishi mwaka 2008 na tokea kipindi hicho amekuwa akipokea pensheni yake kila inapofikia tarehe 22 ya kila mwezi. “NSSF inataka wanachama wake wasipate shida, nawashukuru sana kwani wanatusaidia na wanatujali wazee wastaafu,” amesema Mzee Kapinga.

Photos from NSSF Tanzania's post 22/05/2024

NSSF YAWAJENGEA UWEZO WASTAAFU, YAWAHIMIZA KUTUMIA MIFUMO YA TEHAMA KUPATA TAARIFA ZAO MBALIMBALI

Na MWANDISHI WETU,
Mbeya. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendesha mafunzo kwa wastaafu watarajiwa zaidi ya 200 na kuwaeleza umuhimu wa kufuatilia taarifa zao mbalimbali kupitia mifumo ya TEHAMA ambayo inawawezesha waajiri na wanachama kupata taarifa zao popote walipo bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.

NSSF imetengeneza PORTAL ambayo kwa upande wa waajiri (Employer Portal) inawarahisishia kuwasilisha michango ya wanachama wao kwa wakati na vilevile kwa upande wa wanachama (Member Portal) wanaweza kufuatilia taarifa zao popote walipo bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.

Mafunzo hayo yamefunguliwa tarehe 21 Mei, 2024 jijini Mbeya na
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Bw. Emmanuel Kayuni, ambaye ameitaka NSSF kuendelea kutoa elimu hiyo hata kwa wafanyakazi wanaoanza kuajiriwa ili waweze kujipanga mapema na kustaafu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja wa Huduma kwa Wateja, Bw. Robert Kadege amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wastaafu watarajiwa ili waweze kuelewa mambo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali ambayo inarahisisha huduma kwa wanachama.

Bw. Kadege ametoa wito kwa waajiri wa sekta binafsi kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa wakati kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ( Employer Portal) ili kuwaondolea usumbufu wanachama pindi wanapostaafu kwa mujibu wa sheria.

Naye, Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Bw. Deus Jandwa amehimiza wafanyakazi kutumia mifumo ya TEHAMA na kuhakikisha michango yao inawasilishwa kila mwezi kidijitali katika ofisi za NSSF

''Sasa hivi mifumo yetu imerahisishwa, unaweza ukaingia kwenye mifumo ya NSSF kwa kutumia simu yako ukaangalia michango k**a mwajiri anakuletea au la na k**a michango haiwasilishwi basi mfanyakazi anatakiwa kutoa taarifa NSSF ili tuchukue hatua kwa muhusika,'' amesema Bw. Jandwa.

Bi. Subira Lugala mmoja wa wastaafu watarajiwa ametoa wito kwa wafanyakazi ambao hawajajiunga na NSSF kujiunga ili waweze kustaafu kwa staha pindi wakati utakapofika.

Naye, Dkt. Maundi Keneth amesema semina hiyo imewatoa hofu na kujiandaa wanapoelekea kustaafu.

Photos from NSSF Tanzania's post 18/05/2024

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MRADI WA UWEKEZAJI WA JENGO LA HOTELI YA NYOTA TANO WA NSSF

Aeleza matarajio ya Serikali ya awamu ya sita ni kuona miradi ya kimkakati ukiwemo hoteli ya nyota tano jijini Mwanza unakamilika

Na MWANDISHI WETU,
Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amesema ni azma ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona miradi ya kimkakati ukiwemo hoteli ya nyota tano inayojengwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Mwanza inakamilika.

Mhe. Mtanda amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya kimkakati.

“Nawapongeza NSSF kwa kazi nzuri na ubunifu mkubwa wa miradi ya kimkakati wanayoitekeleza sehemu mbalimbali nchini, nawaomba waendelee kuongeza kasi ya utekelezaji ili ile azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona miradi mbalimbali ya kimkakati inakamilika k**a ilivyokusudiwa.

Mhe.Mtanda amesema mradi wa NSSF wa hoteli ya nyota tano wa jijini Mwanza, utakapokamilika utaongeza thamani katika jiji hilo, amewahakikishia Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa NSSF kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuanza kutumika k**a ilivyokusudiwa.

Awali, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Mapesi Maagi amesema uwekezaji wa mradi huo ni moja kati ya majukumu manne ya Mfuko ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

Bw. Maagi amesema uwekezaji wa hoteli hiyo utakapokamilika utachochea maendeleo ya Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwa kuinua shughuli za kiuchumi hususan utalii hasa ukizingatia kuwa Mkoa wa Mwanza umepakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo karibu na mkoa huo.

Naye, Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Bw. Emmanuel Kahensa amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufanya ziara hiyo ya kikazi katika mradi huo wa hoteli ya nyota tano.

Akitoa taarifa, Mhandisi Helmes Pantaleo ambaye ni Meneja Miradi wa NSSF ameelezea utekelezaji wa mradi na changamoto zote ambazo zilikuwa ni kikwazo zimetatuliwa. Mhandisi Pantaleo amesema utekelezaji unaendelea ambapo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na kuanza kazi mwezi Machi 2025.

Photos from NSSF Tanzania's post 18/05/2024

NSSF YAENDELEZA KASI UTOAJI ELIMU YA HIFADHI YA JAMII MWANZA

Yaitaka jamii kutambua kuwa NSSF ni rafiki wa maisha yao ya sasa na ya baadaye

Wajasiriamali katika Mwalo wa Magomeni Kirumba Mwanza wachangamkia fursa wajiunga na kujiwekea akiba

Na MWANDISHI WETU,
Mwanza. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kufungua fursa kwa wajasiriamali na wavuvi wa Mwalo wa soko la Magomeni, jijini Mwanza ambao wamepatiwa elimu ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya kujiwekea akiba kwa kujiunga na NSSF kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Akizungumza tarehe 17 Mei 2024 wakati akitoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasiriamali na wavuvi wa Mwalo huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya amewataka wajasiriamali na wavuvi wa soko hilo kuchangamkia fursa ya elimu ya hifadhi ya jamii waliyopatiwa kwa kujiunga na kujiwekea akiba kwani NSSF ni rafiki wa maisha hivyo wasikubali kuishi bila ya rafiki huyo kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Bw. Mziya ametoa elimu hiyo ikiwa ni kuelekea kilele cha Malkia wa Nguvu, Kanda ya Ziwa ambapo Mfuko ni moja ya wadau kupitia kampeni ya ‘WEKA TUWEKE’ ya Clouds Media yenye fursa kwa makundi mbalimbali ambayo ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, wavuvi, wakulima, mama lishe, wafugaji na wajasiriamali wengine wote.
“Mtu anapopatwa na majanga mbalimbali rafiki mwema wa maisha yake ya sasa na ya baadaye ni NSSF, hivyo napenda kutoa wito kwa wajasiriamali, wavuvi, wakulima, mama lishe, wafugaji kuchangamkia fursa hii kwa kujiunga na NSSF ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na Mfuko likiwemo la matibabu na pensheni ya uzee,” amesema Bw. Mziya

Amesema taratibu za kujiunga na NSSF ni rahisi sana na kujiandikisha ni bure ambapo baada ya mwanachama kujaza fomu yake atapatiwa kitambulisho chenye namba ya uanachama na hapo hapo ataweza kujichangia kila mwezi shilingi 30,000 ambayo itamuwezesha kunufaika na mafao yote yanayotolewa na
Mfuko.

“Lengo la NSSF ni kutoa pensheni lakini kuna maisha ya kujenga pensheni na maisha ya kula pensheni. Katika maisha ya kujenga pensheni unajiwekea kidogo kidogo na wakati unajenga pensheni unapata na mafao mengine k**a matibabu na mafao ya uzazi kwa kina mama na kwa wale ambao watachangia mpaka kufikisha umri wa kustaafu watakuwa wanakula pensheni,” amesema Bw. Mziya.

Naye. Bi. Rehema Chuma, Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi ameendelea kutoa wito kwa wananchi waliopo kwenye makundi mbalimbali ya sekta isiyo rasmi kujiunga na kuchangia NSSF ili waweze kujenga kesho yao iliyokuwa njema. Amesema baadhi ya wanachama waliojiandikisha walipatiwa vitambulisho vyao hapo hapo.

18/05/2024

SEKTA ISIYO RASMI WATAKIWA KUJIWEKEA AKIBA KUPITIA NSSF

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya asema NSSF ina madirisha mawili ya kujiunga na NSSF moja ni la walioajiriwa kwa mujibu wa sheria na lingine ni wale ambao hawajaajiriwa wakiwemo wanafunzi. Mziya ameendelea kwa kusema wajasiriamali ambao hawajajiunga tunaendelea kuwapatia elimu kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

RAIS DKT. SAMIA ANAGUSWA NA KUJALI MAISHA YA WAFANYAKAZI*Amenyanyua kikokotoo, Ndejembi asema huo ni mwanzo tu#amenyanyu...
MIRADI YA VIWANJA VISIGA NA KILUVYA
WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUWEKA AKIBA KUPITIA NSSFMkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Oma...
SEKTA ISIYO RASMI WATAKIWA KUJIWEKEA AKIBA KUPITIA NSSF Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bw. Omary Mziya asema NSSF ina...
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Mshomba amemshukuru Mhe. Deogratius Ndejembi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, V...
NDEJEMBI ATOA ONYO KWA WAAJIRI WASIOWASILISHA MICHANGO YA WAFANYAKAZI WAO NSSFSerikali imesema haitawavumilia waajiri wo...
MAONESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI (OSHA)
MAONESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI (OSHA)
MAONESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI (OSHA)
MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. AMOS MAKALLA AIKARIBISHA NSSF KUWEKEZA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA
MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. AMOS MAKALLA AIKARIBISHA NSSF KUWEKEZA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA
MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. AMOS MAKALLA AIKARIBISHA NSSF KUWEKEZA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA

Telephone

Address


Dar Es Salaam
1322

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Other Dar es Salaam government services (show all)
U.S. Embassy Tanzania U.S. Embassy Tanzania
686 Old Bagamoyo Road, Msasani
Dar Es Salaam

The U.S. Mission to the United Republic of Tanzania. Terms of Use: https://www.state.gov/tou

Waterbuck Safaris Waterbuck Safaris
55 Ali Hassan Mwinyi Road, East Upanga
Dar Es Salaam, 3272

We offer Wildlife Safaris to all National parks of Tanzania, Tailor-made safaris, Camping safaris, H

Travel Hype Adventures Travel Hype Adventures
Dar Es Salaam, 255

Tour operators based in Dar es Salaam and Arusha, offering safaris to all Tanzania destinations

bibowildnet.africa bibowildnet.africa
Bahari Beach
Dar Es Salaam, 14122

bibowildnet.africa �It is based on wild issues �wild photographing �Promoting afican tourism especially Tanzania � #Visitzanzibar � #Visittanzanianationalparks � #tanzaniaunforgett...

Godfrey Godfrey
Masakahgodfrey389@gmail. Com
Dar Es Salaam, MASAKA

MUONA MBALI "360" MUONA MBALI "360"
Kinondoni
Dar Es Salaam

TWENDE NA MAMA "360"

Maneno ya Ahlubait a.s" Maneno ya Ahlubait a.s"
Dovya B
Dar Es Salaam

Maneno, Nasaha, Hekima na Mafunzo ya Mtume Mohamad {s.a.w.w} pamoja na kizazi chake kitukufu {Ahlubait a.s}

Tourism Tz Tourism Tz
Mikicheni
Dar Es Salaam

Visit Tanzania for Tourism

Mkuulo Mkuulo
Kilolo
Dar Es Salaam, 25632

ExtRa DisCovery ExtRa DisCovery
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam, 16102

best wishes filled an empty heart. bad wishes filled the dieing heart. stay awaken😳

Vggggg Vggggg
Dfdfdf
Dar Es Salaam, 11000

Hugulole Hugulole
Dar
Dar Es Salaam, 156870

hi