Apostle Shemeji Melayeki - Global Family Gatherings Church, Dar es Salaam Videos

Videos by Apostle Shemeji Melayeki - Global Family Gatherings Church in Dar es Salaam. GlobalFamilyGatherings

Other Apostle Shemeji Melayeki - Global Family Gatherings Church videos

Moyo wa Baba!

KUNUKUUNUKUU BIBLIA..

all our books!..
Vyote vipo hapa!.. #share

Kristo anakaa ndani yangu… ukuaji wangu ni ili niweze kumdhihirisha Yeye katika kila eneo. Habari njema ni kwamba Yeye hutenda kazi hiyo ndani yangu. Ushirikiano wangu ni kutomzuia Yeye kuwa wazi ndani yangu kwa kufahamu mimi ni nani ndani yake. Mwisho wa siku.. NIJIONE NDANI YAKE kama Yeye ANAVYOJIONA NDANI YANGU. Namjifunza Yeye ili nimfananie Yeye katika mwenendo wangu maana hakika ASILI YAKE NINAYO. Haleluya🎉🎉 —Global Family Gatherings "God's Standards"

Mungu kusamehe ni swala la fadhili zake za milele na rehema zisizokoma. Mungu anasamehe kwa ajili ya jina lake. Mungu anafurahishwa na rehema. Ndio maana ikifika swala la kusamehe… aisee HIYO NI TABIA YA MUNGU SIYO PRAYER POINT YAKO. Unapokea kwa kuamini kuwa Mungu ameshughulika na dhambi zako katika Kristo ili usiwe na hatia mbele zake. Umeamini? Au bado unamshawishi? —Global Family Gatherings “God’s Standards”

Watu wengi sana wana “struggle” kusamehe. Eti Mungu naye ana struggle kusamehe? Watu wengi wanashindwa kujizuia kuwa na hasira! Eti Mungu naye ana struggle na hasira😂 sasa nani wa kumsaidia mwingine? 😂 Unawaambia watu “Watu dhaifu hawawezi kusamehe” na wakati huo huo unamhubiri mungu asiyeweza kusamehe. You need brain surgery. 🔪 —Global Family Gatherings “God’s Standards”

Uwekezaji mkubwa ambao Mungu amewahi kufanya si kuumba sayari, viumbe na watu wote waliowahi kuishi duniani na watakaokuja ila KIUMBE KIPYA.. Hapa ndipo utajiri wote wa Mungu ulipokaa, hapa ndipo wema wote wa Mungu ulivyomiminwa, hapa ndipo urithi wote wa Mungu ulipowekwa.. Kazi ya Mungu isiyo na makosa ni UKOMBOZI siyo misiba. Kazi pekee ambayo Mungu aliapa kwa nafsi yake kwamba hakika ataitimiza na akaitimiza ni KUWAOKOA WANADAMU NA DHAMBI ZAO. HII NI KAZI ISIYOCHUJA, HII NI KAZI YA MILELE —Global Family Gatherings “God’s Standards”

WAPENI WATU VITU NANYI MTAPEWA... Luka 6:38 Yesu alikuwa anamaanisha nini? Video: https://youtu.be/rLTJyfjx8t0 "God's Standards"

Thank you Jesus. Tuna ujasiri mbele zake milele. Ibada isiyo na mawaa. Isiyo na hofu... isiyo na hukumu.. kwa sababu dhabihu bora imeshatolewa, ibada imekamilika milele.. kuhani mkuu Yesu Kristo ametoa dhabihu na ameketi.. hasimami kila siku kama Haruni na wenzake. Damu imetutakasa milele. Sisi ni waabuduo halisi... waliotakaswa MILELE kwa dhabihu moja bora yenye nguvu ya milele.. —Global Family Gatherings "God's Standards"

Nakala zipo!..

NAMNA MBAYA KABISA YA KUSOMA BIBLIA!.. Namna tulivyojifunza kusoma Biblia hovyo hovyo!..

Bachelor of Arts in Confusion of Understanding Unknown god that can not be understood!!.. 🤣🤣 UNAHITAJI DARASA!..

BELIEVERS' CAMP MEETING TANZANIA 🇹🇿
Registration is ON.. Tumia namba 0683507807

Dalili ya kwanza kuwa umejipanga kwenda kudanganywa kanisani ni KWENDA bila BIBLIA au kwenda na Biblia ambayo huwa unafungua pale mhubiri anaposema "TUFUNGUE KITABU FULANI" Biblia inayokaa kabatini na kufunguliwa Siku ya Makusanyiko tu haitakusaidia. Ni vyema kujiwekea utaratibu wa kujifunza Biblia mwenyewe au kupitia mambo uliyofundishwa kwenye kusanyiko kama ndivyo yalivyoandikwa. Ukiona kuna kitu hukielewei muulize aliyekufundisha au uliza kwenye Makusanyiko madogo na waamini wengine.. Faida ya kuwa serious na mafundisho ni nyingi... Kwanza itakusaidia wewe mwenyewe lakini pia itamsaidia Mwalimu wako ajue kwamba WANAOKUJA KUMSIKILIZA SIYO MAZEZETA.. Yeye pia ataongeza bidii katika kujifunza na kujiandaa kufundisha. Lakini ukija bila Biblia, umejiandaa kuja kushangilia unabii wa nabii na swaga za mtume au suti ya Mchungaji..utashangaa utakapoambiwa "MAANDIKO YANASEMA KWENYE KITABU CHA ELIYA 2:5 UKITOA SADAKA INAYOUMA MUNGU ANAJIBU KWA MOTO" Na utasema "AMEEEEN" AT LAST, MUNGU ANATUPENDA NA HATUWEZI KUUPOKEA UPENDO WAKE KAMA TUSIPOJIFUNZA KWA UMAKINI WA KUTOSHA UFUNUOWA UPENDO WAKE KATIKA MWANAWE YESU KRISTO. Shalom! Ap Shemeji Melayeki...