Apostle Shemeji Melayeki - Global Family Gatherings Church

GlobalFamilyGatherings

11/09/2024

Shida ya watu wengi ni kwamba wanahisi wana akili kuliko waandishi wa Biblia.
Yaani unasoma mstari… unanyanyua kichwa unaipa tafsiri inayokuja kichwani mwako. Halafu unasema nimefunuliwa XYZ.
Jambo la kwanza kabisa ni kujua kuwa Biblia haiwezi kumaanisha leo kitu ambacho mwandishi hakumaanisha wakati huo kikiandikwa. Badala ya kusema “NIONAVYO MIMI” jiulize “MWANDISHI ALIMAANISHA NINI HAPA?” utagundua Biblia inaweza kujitafsiri yenyewe.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

11/09/2024

Unasoma Biblia vibaya. Unawaambia watu “Mungu amesema, nawapenda wale wanipendao nao wanitafutao kwa bidii wataniona”… unamwambia, ni wapi Mungu amesema hivyo anakimbilia Mithali. Unamwambia anza mstari wa kwanza… unaona amenywea😂 unaambiwa “ACHA KUDOKOA MISTARI” Unajifanya huelewi. Haya sasa.
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

11/09/2024

Kunyofoa mistari kwenye maandiko nje ya muktadha Ni ugonjwa mbaya Sana.

Unalitesa kanisa la MUNGU.

Ndio chanzo kikuu na kikubwa Cha mafundisho potofu.
—Global Family Gatherings
God's standards.

09/09/2024

MARA NYINGI TUNAHISI WATU WANAELEWA WANACHOTAKIWA KUFANYA.... KWA HIYO TUNAACHA KUWAELEZA WANACHOTAKIWA KUFANYA..

Unajua namna ya kujiandaa kwenda KANISANI?

Somo zima liko hapa...

https://youtube.com/live/T7bIOOLAdHM?feature=share

"God's Standards"

09/09/2024

Vyote vipo hapa!..

07/09/2024

Speak the truth, if it offends people... speak it again.

Iseme kweli, k**a watu wakikwazika... iseme tena.

—Global Family Gatherings
"God's Standards"

07/09/2024

Kuna watu wanataka useme ukweli... ila hawataki useme kwa ujasiri... hawajui kwamba ukweli hausemwi namna nyingine ila kwa ujasiri.. mtu anayetaka uiseme kweli bila kuikazia kwa ujasiri anataka useme ile isiyo kweli. Kweli nusu siyo kweli. Yesu aliwashangaza kwa yale aliyoyafundisha na namna alivyofundisha. ALIFUNDISHA K**A MTU MWENYE MAMLAKA.. na si k**a Mafarisayo.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

07/09/2024

Inachekesha kwamba watu wengi wakiomba Mungu kwa ajili ya mtoto.. wanajua wanachotakiwa kufanya baada ya maombi..

Lakini watu hao hao wanaweza kuomba UJASIRI kwa ajili ya KUHUBIRI INJILI na wasiende kuhubiri Injili.

MAOMBI YANAKUSHUGHULISHA.
Hatua unayochukua baada ya kuomba inaonyesha kwamba ulipokea wakati unaomba.

—Global Family Gatherings
"God's Standards"

06/09/2024

Ni kweli inachukua muda kukua kiroho.
Lakini si MUDA tu pekee.
Ni muda unaotumia kuwekeza kwenye KUJIFUNZA, KUOMBA na KUFANYA yakupasayo.
Usikae kwenye kichaka cha Muda wakati huombi, husomi na kwenye makusanyiko huendi.
Miaka 10 ijayo utakuwa umeongeza miaka 10 na UJINGA utakuwa UMEZEEKA pia.
Plan to grow spiritually
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

06/09/2024

Fikiria kwamba wewe ni mchungaji.. Jumapili unaenda kanisani unakuta mabenchi tu.. kila mtu ana sababu ya kutokusanyika. Hebu fikiria halafu vaa viatu vyao. K**a ambavyo ungefurahi kuona wanafunzi wako wanahudhuria makusanyiko yote basi usimfanyie mchungaji wako kitu ambacho usingependa kufanyiwa ukiwa mchungaji maana kuna uwezekano hata wewe ukawa kiongozi wa kiroho baadaye. Hata hivyo kuhudhuria makusanyiko unajengwa wewe. Kuheshimu mambo ya Mungu ni ibada. Ni ukuaji wa kiroho.
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

06/09/2024

Mungu anakuhudumia wewe kupitia viongozi wako wa kiroho. Kuwaheshimu ni kukaa katika mpango wa Mungu hasa wale wanaojitaabisha usiku na mchana kuhakikisha ya kwamba unakua kiroho kwa mafundisho, maombi na maelekezo. Uwathamini watu hawa. Mungu ameweka ukuaji wetu wa kiroho mikononi mwa watu wengine. Usipowatii na kuwaheshimu hautakua kiroho. MUNGU HUTUMIA WATU kujenga watu.
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

06/09/2024

Mwenendo usiofaa huzifanya nguvu za Mungu zisiweze kukusaidia. Hebu fikiria Mungu anakupa watu wa kukusaidia lakini unahakikisha unawavuruga na hatimaye wanaondoka kwa sababu ya tabia yako mbaya. Utashangaa unakwama kumbe wewe ndiye sababu wala si Mungu hakusaidii. Mungu hawezi kuendelea kuwaleta watu ili uwavuruge. Omba kwa ajili ya ukuaji wako wa kiroho. Ona nguvu za Mungu zikikusaidia kuvuka. Nuia kubadilika.
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

06/09/2024

Ukuaji katika mambo ya rohoni unahitaji gharama. Yaani unaweza kufikiri unaelewa kwa sababu umesikiliza video 2 au 3 za Apostle Shemeji Melayeki kisha ukatoa "boko" moja matata mpaka watu wanashangaa ulichosema umeelewa ni kipi. Moto wa kuchomea mahindi ili yaive vizuri ni moto wa taratibu. Ukifanya papara unajikuta umejipakapaka kweli ila haina mizizi. Amua kuweka jitihada za dhati za kukaa chini na kujifunza. Tulia ujifunze kitu kimoja baada ya kingine, jiulize maswali na huku ukiuliza mwalimu wako. Tena ni muhimu sana kujifunza systematically chini ya mtu mmoja. Hatua kwa hatua. Unajifunza hivyo?
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

06/09/2024

Kristo anakaa ndani yangu… ukuaji wangu ni ili niweze kumdhihirisha Yeye katika kila eneo. Habari njema ni kwamba Yeye hutenda kazi hiyo ndani yangu. Ushirikiano wangu ni kutomzuia Yeye kuwa wazi ndani yangu kwa kufahamu mimi ni nani ndani yake. Mwisho wa siku.. NIJIONE NDANI YAKE k**a Yeye ANAVYOJIONA NDANI YANGU. Namjifunza Yeye ili nimfananie Yeye katika mwenendo wangu maana hakika ASILI YAKE NINAYO. Haleluya🎉🎉
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

05/09/2024

Yaani wakati mwingine inakubidi USOME TU BIBLIA. Soma tu bila kuhangaika kutafuta mafunuo. Soma tu kuelewa habari nzima. Ni muhimu sana. Jifunze kusoma k**a vile hakuna mistari. Soma k**a vile hakuna sura. Fuatilia tu "story" hadi mwisho. Elewa hiyo story.. NJIA YA AWALI KABISA YA KUPONA UGONJWA WA "KUNYOFOA MISTARI" NJE YA MUKTADHA NA KUTOA TAFSIRI ZA UONGO. Let's build..
–Global Family Gatherings
"God's Standards"

05/09/2024

Aliyeweka sura na mistari kwenye Biblia alikuwa na nia nzuri "KUTUSAIDIA WAKATI WA KUNUKUU"

Shida ni kwamba watu wengi wanafikiri mstari wa Biblia unajitosheleza wenyewe.
Jifunze kusoma Biblia k**a vile haina sura na mistari.
Soma nyaraka k**a unasoma barua ya kawaida. Elewa mtiririko. Acha kukomaa na mstari.
Na kutafuta "UFUNUO" kwenye mistari. MAPOTOFU MENGI YANAANZIA HAPO.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

05/09/2024

Kuna tofauti kati ya kufanya "Bible Study" na kunukuunukuu mistari kuhalalisha unachotaka kumaanisha.
Kwa mtindo wa kunukuunukuu mistari hata ukitaka kuwa mchawi unapata mstari wa kusimamia.. siyo hilo tu..hata ukitaka kuiba, kuwa mlevi, kuoa wake wengi, kutembea na hausigeli, kuua, kuoa kahaba, kutembea uchi, kuwa mchoyo, na mengine mengi.
Kweli ni kweli kuanzia Mwanzo mpaka UFUNUO.. Shauri lote la Mungu ni matokeo ya UCHAMBUZI WA MAANDIKO siyo KUNUKUU mistari.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

05/09/2024

Bible study is not a careless study.

The first thing you learn is to PAY Attention to DETAILS.

—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

04/09/2024

Huwezi kumwandaa daktari kwa kurukaruka na kukimbiambia.. Maprofesa hawaji kufundisha na vibrations. Wanakuja wako "calm" wametulia. Hawana haraka. Wanakwenda hatua kwa hatua. Jiwe baada ya jiwe. Mpaka siku unakabidhiwa leseni ya udaktari unaingia kazini na ujasiri.No half backed believers.Kaa chini ujifunze systematically.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

04/09/2024

Ukiona kila wakati unatamani kusikia kitu kipya... muda si mrefu utaanza kupoteza ramani. Ukomavu ni pale ambapo una uwezo wa kuelezea jambo lile lile moja kwa njia nyingi. K**a unanifuatilia utagundua sioni aibu kurudiarudia jambo moja hata mara 1000. Hii ndiyo kanuni ya kujenga imani ya mtu.Ukishaanza kuchoka KUHESABIWA haki kwa imani unataka kusikia mambo amazing... You will be amazed kweli kweli.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

04/09/2024

Watu wengi wanaokuwa kiroho hawafundishwi "the so called deep revelations" wako pale pale.. wanasikia.. Haki kwa imani, msamaha wa dhambi, maombi, karama za Roho, mwenendo wa mwamini, UINJILISTI, uanafunzi, uzima wa MILELE.. upendo. Usiyadharau maji yaliyotulia.. kina chake kitakuja kukuumbua.
Take Time Again Learn! Learn!.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

04/09/2024

INAHITAJI muda wa kutosha kusikiliza walio mahiri katika kuchambua maandiko Matakatifu (Mwanzo mpaka Malaki) ili uweze kupata "pattern" ya uchambuzi huo.
Ukisikiliza "sermon" moja halafu unaanza kwenda kupambana na Zaburi utakayokutana nayo hutaamini.😀 Take Time. No hurry!. Unawahi wapi? Kaa kwanza na notes za mwalimu wako. Rudiarudia. Fundisha yale aliyokufundisha. Rudiarudia sanaaa
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

03/09/2024

K**a ambavyo Mungu anasamehe; Mwamini ana stamina hiyo hiyo kwenye roho yake.

Roho wa Kristo ndiye aliyekuzaa katika ufufuo wa Yesu siku ile ulipoamini.

Wewe ni mwana wa Mungu.. unaweza KUSAMEHE hata ukiwa na sababu ya kulaumu

Kwa SABABU una nguvu k**a Baba yako. Ni asili yako.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

03/09/2024

Mungu kusamehe ni swala la fadhili zake za milele na rehema zisizokoma. Mungu anasamehe kwa ajili ya jina lake. Mungu anafurahishwa na rehema. Ndio maana ikifika swala la kusamehe… aisee HIYO NI TABIA YA MUNGU SIYO PRAYER POINT YAKO. Unapokea kwa kuamini kuwa Mungu ameshughulika na dhambi zako katika Kristo ili usiwe na hatia mbele zake. Umeamini? Au bado unamshawishi?
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

03/09/2024

Watu wengi sana wana “struggle” kusamehe. Eti Mungu naye ana struggle kusamehe?
Watu wengi wanashindwa kujizuia kuwa na hasira! Eti Mungu naye ana struggle na hasira😂 sasa nani wa kumsaidia mwingine? 😂 Unawaambia watu “Watu dhaifu hawawezi kusamehe” na wakati huo huo unamhubiri mungu asiyeweza kusamehe. You need brain surgery. 🔪
—Global Family Gatherings
“God’s Standards”

02/09/2024

Nakutakia wiki njema sana mwana wa Mungu. Nenda ukafanikiwe katika mambo yako.. Uone uhalisia wa nguvu za Mungu ndani yako kwa sababu una Roho wa Mungu wewe siyo mwili wa nyama tu ni roho iliyohuishwa kwa Roho Mtakatifu.. tembea katika uhakika na nguvu za Mungu zilizokuokoa.
You're supernatural, do more supernatural things this week!.
Global Family Gatherings
"God's Standards"

02/09/2024

God LOVED us when we were unLIKEable.

It was our weaknesses that attracted CHRIST to DEATH.
He died for US not because we were PERFECT BUT... because we needed a PERFECT SAVIOUR who provided a perfect SACRIFICE for remission of ALL our sins FOREVER.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

02/09/2024

How do I know that God loves me?
✍️He has forgiven all my sins.
What's the evidence?
✍️He has given me His Spirit. He lives in me.
This means at His own cost He has cleansed me to become "the most holy place" where "the most Holy God" can dwell. All has been done by the the most powerful sacrifice of Jesus Christ. Oh what a wonderful love. I'M LOVED!
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

31/08/2024

WAPENI WATU VITU NANYI MTAPEWA... Luka 6:38

Yesu alikuwa anamaanisha nini?

Video: PART 1 👉👉 https://youtu.be/rLTJyfjx8t0
Video: PART 2 👉👉 https://youtu.be/xY6qDAkhybo?si=hAfcSQDMs8sMqrSy

"God's Standards"

30/08/2024

Yesu hakutenda dhambi, isipokuwa DHAMBI ZETU ZILIWEKWA JUU YAKE. Hakufanya kosa lolote isipokuwa alikufa nafasi yetu.

Hatukustahili HAKI ITOKAYO KWA MUNGU..ila tumehesabiwa haki BURE.

K**a ambavyo Kristo alifanyika dhambi, na sisi tumefanyika HAKI (watakatifu, wasio na waa) kupitia kufa na hatimaye kufufuka kwake.
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Moyo wa Baba!
KUNUKUUNUKUU BIBLIA..
all our books!..
Kristo anakaa ndani yangu… ukuaji wangu ni ili niweze kumdhihirisha Yeye katika kila eneo. Habari njema ni kwamba Yeye h...
Mungu kusamehe ni swala la fadhili zake za milele na rehema zisizokoma. Mungu anasamehe kwa ajili ya jina lake. Mungu an...
Watu wengi sana wana “struggle” kusamehe. Eti Mungu naye ana struggle kusamehe? Watu wengi wanashindwa kujizuia kuwa na ...

Category

Telephone

Address


Dar Es Salaam
Other Public Figures in Dar es Salaam (show all)
Akhenaton Family Akhenaton Family
P. O. Box, KGN, Dsm
Dar Es Salaam, 36402

...the new breed!

MUSTAFA HASSANALI MUSTAFA HASSANALI
Dar Es Salaam

Pan African Designer, Mustafa Hassanali has showcased in 33 cities in 23 Countries & named One of Af

Ramsey's official tz Othman Ramsey's official tz Othman
Kauli Moja 1 Camp
Dar Es Salaam, 0000

Blog

ipende_ngozi_yako ipende_ngozi_yako
Dar Es Salaam

Tunauza vipodozi asili za ngozi na nywele

Michael Clement Michael Clement
Dar Es Salaam

#never give up never surrender

CayteAkaro Talents Owner CayteAkaro Talents Owner
Ilala
Dar Es Salaam, 0000

Her Own🎂 31.12. LL.B Jurist ⚖️👩‍⚖️🇹🇿 #HairBraiding #Massage #HennaTattoos #ApplicationForVisa #InNungwi-Zanzibar #GoodPrice

Sady King Sady King
Dar Es Salaam

Dee Ommy Dee Ommy
Dar Es Salaam

Dee ommy

Mo Dewiji Mo Dewiji
Posta
Dar Es Salaam, 255

Oficial Man Plate Oficial Man Plate
Dar Es Salaam

Emerging entrepreneur from Tabora Tanzania @Power brand Shop ||Chief Executive Officer (CEO) .

Fatty_the_killer Fatty_the_killer
Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

mtu anaekupenda kwa dhati lazima akuhurumie maana mapenzi ya dhati na HURUMA huishi pamoja

Pst Brian Mwimba Pst Brian Mwimba
Dar Es Salaam, 828282