Tuombe Na Yesu Kristo

NJOO UJIFUNZE KUMJUA MUNGU NA KRISTO WAKE, MAPENZI YAKE, AMRI ZAKE NA SHERIA ZAKE, UTOKE VIFUNGONI UKAMUABUDU PASIPO MASHAKA NAWE UTAJIBIWA KILA UMUOMBAPO.

05/08/2024

Ukisikia mkristo anamzungumzia Yesu jua anazungumzia ile Sanamu au yule muigizaji wa hile movie yao

02/08/2024

Usijidanganye kuwa una Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hayupo ulimwenguni kwa sasa, hizo ulizonazo ni roho chafu za mpinga kristo

14/07/2024

NENO LA MUNGU NI TORATI NA MANABII

BIBLIA AGANO LA KALE NA JIPYA NI MAPOKEO YA KIDINI
Mungu hakuwahi ligawa neno lake katika mgawanyo huu.

13/07/2024

Mwenye swali lolote kuhusu ufalme wa mbinguni namkaribisha aulize

30/06/2024

K**a umewahi kujifunza chochote katika ukurasa huu, basi MSHUKURU MUNGU SANA MAANA UKURASA HUU NDIYO NJIA PEKEE IENDAYO UZIMANI. Yeye ajifunzaye katika ukurasa huu ajifunza lile neno sahii lililotoka kwa Bwana kwa ajili ya watu wake ulimwenguni katika nyakati hizi.
Ni kweli mafundisho mengine yanaumiza na kuvunja moyo kutokana na mienendo yetu tulionayo leo hii, lakini hatuna jinsi, mkuu wa ulimwengu huu kwa sasa Ibilisi alishatuaminisha kuwa hayo tuyapendayo (UONGO) ndio yanayotufaa ili tukaangamie nae siku ya hukumu kwenye ziwa la moto 🔥🔥🔥

UNA HERI WEWE ULIYEBAHATIKA KUUONA UKURASA HUU NA KUJIFUNZA NA KUYASHIKA MAONYO YALIYOPO KATIKA UKURASA HUU BILA KUGEUKA NYUMA.
NJOO JIFUNZE BURE, NIMEPEWA BURE NAWAPA BURE BILA SADAKA WALA MATOLEO YOYOTE.

JINA LA BWANA LIBARIKIWE MILELE NA MILELE ...

21/06/2024

Natumaini siku si nyingi mtanielewa NINAPOSEMA UKRISTO NA UISLAM NA MADHEHEBU YAKE YOTE HAVIKUTOKA KWA MUNGU BALI NDIO NJIA PANA IENDAYO UPOTEVUNI Maana imeandikwa:

📖 Mathayo 7:20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Wherefore by their fruits ye shall know them.

14/02/2024

Yesu alitundikwa msalabani akiwa UCHI! Je ni busara kwako leo hii kuchorwa mfano wa tukio hilo usoni mwako?
Je Yeye anakutazamaje? Na unahisi Mungu anajisikiaje anapokutazama na ukimdhiaki mwanae??

18/01/2024

HAKA KASANAMU VIFUANI MWAO KAMEWATAJIRISHA WENGI ULIMWENGUNI. NA HII NDIYO MAANA HALISI YA MANENO HAYA;

📖 Mathayo (Mat) 4:8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
Mathayo (Mat) 4:9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

😁😁😁 Yesu alilishinda hili jaribu ila walimwengu wameshindwa, KAANGALIE JIRANI YAKO ANAVYOKULA BATA KWA JASHO LAKO. AKIKUDANGANYA KATUMWA NA MUNGU

08/01/2024

HUU NDIO UFALME WA SITA ULMWENGUNI. UFALME MBAYA NA MUOVU KUPITA FALME ZOTE TANGU KUUMBWA KWA ULIMWENGU.

📖Mathayo (Mat) 24:21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

Ufalme unaotesa na kuangamiza wanadamu KATIKA HALI YA SALAMA.
Ufalme unaomkufuru Mungu wa mbinguni kwa sanamu ya msalaba na uvunjaji wa sheria za Mungu. Huu ndio UFALME WA 6 DUNIANI uliopewa hesabu ya 666. Ndio ufalme wenye mamlaka mbili (pembe mbili mfano wa mwana kondoo), yaani UKRISTO NA UISLAM.
Ufalme ulioamua kumtawala ulimwengu kwa kutumia neno la Mungu lililogeuzwa geuzwa, ukijifanya umetumwa na Mungu

Usiseme hukujua, hata uwe mkristo au muislamu wa dhehebu gani. Mti muovu hauwezi zaa tunda jema. Kimbia moto unakungoja maana umeshaipokea chapa yake (namaanisha wewe tayari ni mfuasi wa hizi dini na madhehebu yake.

06/01/2024

Mrumi alimgombanisha mwanadamu na Mungu ili aweze kumtawala. Akayavuruga maandiko na kuingiza mapokeo yake ili Mungu asiwatazame wanadamu kabisa wala kuwasikiliza waombapo.
Leo unafanya ibada kwa mwongozo wa muovu unadhani Mungu atakusikiliza?
Ebu tafakari, k**a lengo la kumuweka Yesu msalabani ilikuwa ni kumdhalilisha, wewe unayesali mbele ya msalaba Yesu anakutazamaje

28/12/2023

UKITAKA KUJUA UKWELI UNAUMIZA NI PALE MKRISTO NA MUISLAMU WANAPOAMBIWA HIZO NI DINI POTOFU.
Maandiko matakatifu katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 13 yanataja dini mbili kubwa zilizo kinyume na Mungu ulimwenguni.
Ya kwanza ni dini ya wayahudi,
mnyama mwenyewe vichwa saba ya ni dini iliyomiliki katika nyakati za falme saba tofauti zilizotawala ulimwengu. Ukinza na ufalme wa Ashuru, Babeli, Medi, Ajemi, Yunani na Rumi (uliopo mpaka sasa ambao ni wa sita) na wa saba haujaja bado maana huo ndio wa mwisho baada ya huo dunia itachomwa.
Ya pili ni dini ya Ukristo na Uislam
Mnyama mwenye pembe mbili (yaani mamlaka mbili) mfano wa mwana kondoo (yaani zinazondesha shughuli zake kwa kuiga alichofanya mwanakondoo wa Mungu Yesu Kristo)
Ukristo uliamuru wafuasi wake watengeneze sanamu ya tukio la kifo cha Yesu msalabani. Tukio ambalo liliifanya dini ya wayahudi ambayo ilikuwa karibu kufa kwa upanga wa neno la Bwana Yesu Kristo na walipomuua dini ikaishi tena. Kwa waliosoma kitabu cha ufunuo sura ya 13 wananielewa. (Siwezi nukuu haya hapa ili kufupisha chapisho ila k**a unanifatilia ukiwa na biblia karibu utanielewa. SANAMU HIYO NI SANAMU YA MSALABA (Iwe ni kwa kuichonga, kuichora, ama kusubu)

Lengo la dini ya Ukristo na badae uislam kupatikana lilikuwa ni kumtawala mwanadamu bila kutumia nguvu za kijeshi. Ikumbukwe mtawala wa ulimwengu huu kwa sasa yani ufalme wa sita ulimwenguni (uliopewa alama ya 666) Rumi ama ukristo na uislam kwa sasa Yesu Kristo alikukuta isipokuwa wakati huo ulikuwa unatawala kisiasa chini ya Kaisari. Baada ya kuhama kutoka katika siasa na kuwa dini ukawa chini ya mababa wa kiroho, mfano papa kwa kirumi, baba askofu, mitume nk.
Kwa kifupi hizi dini ndizo nabii Daniel alizitabiri k**a chukizo la uharbifu (Dan 9:27) na Bwana Yesu katika

📖 Mathayo (Mat) 24:15
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),

Kwamba ni dini zitakazoingia katika hekalu takatifu (Yerusalem) na kulinajisi hekalu na kupelekea hekalu hilo kuvunjwa kabisa lisionekane jiwe juu ya jiwe.

Fatilia zaidi mafundisho haya na uyasome kwa mapana zaidi ndani ya ukurasa huu katika post zilizotangulia umfahamu Mungu wa kweli anahitaji nini ili uweze kuuingia ufalme wake. Jina la Bwana lihimidiwe daima, Amen.

24/12/2023

Siku za kuliangamiza sanamu la dini kuu ulimwenguni inaloutesa na kuupotosha ulimwengu zimekaribia.

📖 Ufunuo wa Yohana (Rev) 13:14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia SANAMU yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. And deceiveth them that dwell on the earth by the means of those miracles which he had power to do in the sight of the beast; saying to them that dwell on the earth, that they should make an image to the beast, which had the wound by a sword, and did live.

01/12/2023

Muabudu Mungu KATIKA ROHO NA KWELI ukiwa huru, bila gharama mahali popote duniani

27/11/2023

USIOGOPE KARIBU UJIFUNZE

Usitafute saana kunifahamu mimi, TAFUTA SANA kuufahamu vyema na kuushika ujumbe wa Mungu niliouleta kwako, mimi ni mtanzania k**a wewetu sina jipya usilolijua zaidi ya hili neno la Bwana. KUMBUKA, SIHITAJI CHOCHOTE KUTOKA KWAKO. Jifunze bure, uliza swali bure, ujibiwe bure. NIMEPEWA BURE NIKULETEE BURE, HATA GHARAMA ZA KUKUFIKISHIA WEWE UJUMBE HUU BWANA ANANILIPA YEYE. Tafadhali tembelea ukurasa huu ujifunze mengi kuhusu njia ya kweli ya uzima wa milele bure.

19/11/2023

Njia pana iendayo upotevuni.

30/10/2023

Isaya (Isa) 43:19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Behold, I will do a new thing; now it shall spring forth; shall ye not know it? I will even make a way in the wilderness, and rivers in the desert.

21/09/2023

Mtu yeyote anayetembelea ukurasa huu wa Tuombe Na Yesu Kristo kwa nia njema ya kujifunza, hakika ana sehemu yake katika ufalme wa Mungu aliye hai Yeye aliyenituma nikufikishie ujumbe wake uliomo katika ukurasa huu.

18/09/2023

Dakika zako 10 katika ukurasa wako Tuombe Na Yesu Kristo nizaidi ya miaka yako 10 ukiwa katika nyua za kanisa au msikiti

25/02/2023

Usidanganyike, k**a wewe ni mkristo wa dhehebu lolote au muislamu wa dhehebu lolote , tambua kuwa hii chapa umeshaipokea.
👉 CHAPA USONI maana yake wewe ni mfuasi wa kawaida
👉 CHAPA MKONONI maana yake wewe ni mtenda kazi (Mtumishi au kiongozi katika dini hizi au madhehebu yake)

😥 Inasikitisha kuona mtu anapuuza ujumbe huu. Ila ana heri yule asikiaye maneno haya ambayo ROHO WA MUNGU AWAAMBIA MATAIFA.

Mamlaka ya Rumi ilianzisha hizi dini k**a mbinu ya kuutawala ulimwengu kwa urahisi bila kutumia nguvu za kijeshi baada ya kuona jinsi watu walivyotii kwa dini ya wayahudi hasa kwa kutegemea torati na manabii. Wakaamua kuanzisha ukristo na baadae uislam kwa wale ambao hawakuukubali ukrsto lakini sheria zikawa ni zile zile torati na manabii na wakikazania zaidi SADAKA maana lengo lao ni kumiliki utajiri mkubwa.

Jiulize. K**A DINI HIZI ZIMETOKA KWA MUNGU IWEJE WAO WAWE NI WA KUPOKEA TUU NA SIO KUSADIA JAMII? SHULE NA HOSPITALI ZAO MASIKINI HATHAMINIWI!

Jifunze mengi zaidi katika mafundisho yaliyomo katika ukurasa huu juu ya UFALME WA MUNGU na jinsi mamlaka ya giza inavyozitumia dini hizi mbili kuuangamiza ulimwengu k**a ilivyoandikwa katika torati na manabii . Mafundisho haya yanezingatia zaidi neno la Mungu kuliko mawazo ya binadamu. Karibu sana

28/01/2023

UWEZI KULIPOKEA NENO LA MUNGU BILA KUYAFAHAMU HAYA.
Kwa kuwa kulipokea neno la Mungu ni sawa na kujikomboa katika utumwa wa Shetani, huwesi kulielewa neno la Mungu pasipo kumuabgusha yeye aliyekuteka. K**a Bwana anacyosema;

📖Mathayo 12:29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.

Hii ndiyo SABABU BWANA AKATUPA FUNDISHO HILI KWANZA ILI TUMTAMBUE ALIYETUFUNGA, TUKUBALI WENYEWE MIOYONI MWETU KUMKATAA NDIPO TUWEZE KULIPOKEA NENO LA UZIMA. FUNDISHO HILI NI MSINGI WA IMANI YETU NA MNYORORO WA KUMFUNGA IBILISI ASIRUDI KUTUDANGANYA TENA.
BOFYA HAPA KULIPITIA FUNDISHO HILO👇👇👇

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=295345737557819&substory_index=0&id=271334453292281&mibextid=Nif5oz

21/01/2023

JE NA WEWE NI MMOJA WA WASIOLIFAHAMU HILI KUHUSU UKRISTO NA UISLAM?

Mtu mmoja mwenye nia ya kujifunza ameniuliza swali hili hapo pichani kuhusu Ufunuo13. Nami nikaona ni vyema niwashirkishe wote wasiofahamu neno hili muhimu.

Ufunuo 13 yote inazungumzia dini mbili. Dini ya kwanza ni dini ya wayahudi (Mnyama mwenye vichwa saba) yaani dini iliyodumu katika vipindi saba vya falme saba zilizoandikiwa kutawala ulimwengu ambapo falme tano zimeshapita, mmoja upo na mmoja haujaja bado. (1. Ufalme wa Ashuru 2. Ufalme wa babeli 3. Ufalme wa wamedi, 4. Ufalme wa uajemi 5. Ufalme wa wayunani. Hizi zimeshapita. 6. Ni ufalme wa warumi (roman empire) unaotawala mpaka sasa kwa kutumia dini ya ukristo na uislam na mfalme wao akiwa ni papa. Ufalme wa saba haujaja bado. Huu utakuja baada ya ile miaka 1000 ya utawala wa Kristo.

MNYAMA MWENYE PEMBE MBILI MFANO WA MWANA-KONDOO ni dini iliyoanzishwa na mamlaka ya kirumi kwa mfano wa imani aliyoileta Bwana Yesu Kristo lakiniinanena k**a Joka , yaani INADANGANYA!. Dini hii ina pembe mbili yaani mamlaka mbili, wakristo na waislamu. Dini hii iliyoanzishwa na ufalme wa 6 ulimwenguni imepewa hesabu ya 666 yaani vipindi vitatu katika maandiko vyenye nyakati 6 sita. Yaani kitasa cha kwanza mpaka cha sita, baragumu ya kwanza mpaka ya sina na muhuri wakwanza mpaka wa sita kwa kuzingatia mpangilio wake katika maandiko.
KWA KIFUPI
Mnyama mwenye pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo ni dini ya ukristo na uislam. Ukiwa mfuasi wa dini hizi na madhehebu yake yote ulimwenguni FAHAMU KUWA UMEIPOKEA CHAPA YA MNYAMA HUYO NA HUNA SEHEMU KATIKA UFALME WA MUNGU MAANA DINI HII INADANGANYA. Haijalishi wewe ni ndogo au kubwa, masikini au tajiri.

👉Nimefafanua kwa upana zaidi kwenye fundisho lenye kichwa cha habari; MPINGA KRISTO AMESHAKUWEPO NA NYAKATI ZAKE ZIPO UKINGONI.
Karibu tena twendelee kujifunza pamoja.

11/01/2023

CHUKIZO LA UHARIBIFU (Mt 24:15)
*********************
👉Hili ndio yule mnyama mwenye pembe mbili mfano wa mwana kondoo ANENAYE K**A JOKA (Ufunuo 13:11)
👉Yaani DINI MOJA yenye mamlaka mbili. DINI YA MATAIFA yenye matawi mawili; Ukristo na Uislam.
DINI ILIYOLINAJISI HEKALU LA MUNGU.
HII NDIYO DINI ILIYOPEWA HESABU YA 666.
Karibu tujifunze pamoja.

16/10/2022

K**a ulikuwa unamlilia Mungu akuoneshe njia ya kweli na ya kumfikia Yeye, ukurasa huu ndio mahali sahii unaweza kujifunza njia zake.
Elimu hii ni bure!!! Tembelea ukurasa huu kila mara ujifunze njia ya kweli.
Hatuhitaji sadaka yako wala matoleo ya aina yoyote!!! Elimu hii ya Mungu ni bure!

23/09/2022

MAFUNDISHO YA UKURASA HUU NI MAFUNDISHO MAALUM KWA WATEULE WA MUNGU. "WATU WACHACHE WALIOANDIKWA MAJINA YAO KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE TANGU KUUMBWA ULIMWENGU HUU."
WATU WA DINI HAWAWEZI KUYAELEWA KAMWE!!
MTUKUZE MUNGU K**A UNAYAELEWA MAANA HUU NDIO UFUNGUO WA MLANGO WA UZIMA WAKO

13/09/2022

ACHA KUMSEMA MUNGU VIBAYA.

Watu wa dini wamezoea kumsema Mungu wetu vibaya kupitia kauli zao hasa pale yanapotoke matukio mabaya.

Mfano mzuri ni pale mtu anapofariki. Viongozi wa dini na madhehebu hupenda kusema; "Tulimpenda ila Mungu kampenda zaidi."
Ebu tafakari kidogo, Mungu akimpenda mtu ndio amuue?
Ni wangapi ambao Mungu aliwapenda katika maandiko akawaua?
Na k**a Mungu akikupenda anakuua, kuna faida gani sisi kutafuta Yeye?
Kwa lugha rahisi, kauli hii inamaanisha kumpenda Mungu ni kupenda kifo.

KAULI ZA NAMNA HII NI ZA SHETANI, ambaye hutumia dini na viongozi wa dini hizi kumtukana Mungu. Mungu akikupenda utaishi maisha marefu na ya furaha.
Kumbuka imeandikwa;
📖Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

UPENDO WA MUNGU WETU NI KUTUPA MAISHA MAREFU NA YENYE FURAHA bali shetani yupo kutuua.

24/08/2022

Je waufahamu
MTO WA MAJI YA UZIMA NA MTO WA MAJI YA MAUTI!?

Dini ya wayahudi kwa nguvu za Shetani, ilishirikiana na utawala wa mamlaka ya kirumi kumuua mwana wa Mungu Yesu Kristo na baadaye kuwaangamiza wafuasi wa Kristo wote na kazi zao. Kisha Ibilisi shetani, kwa kupitia mamlaka ya Kirumi akaanzisha Ukristo na baadaye akaleta Uislam.

Dini hizi mbili kwa pamoja katika maandiko zimetajwa k**a "MAJI K**A MTO!" (Ufunuo 12:15), mto uliotoka katika kinywa cha shetani ili kummeza mwanamke (mwanamke kati Ufunuo 12 umaanisha neno la Mungu, ama nguvu ya Mungu duniani AU MTO WA MAJI YA UZIMA.) Mto huu wa uongo(Mauti) uliletwa kwa ajili ya kumuua mwanadamu kiroho. Uliletwa kumtenga mwanadamu na Mungu aliye hai. MTO HUU UJIFANANISHA NA MTO WA MAJI YA UZIMA MAANA MTO WA MAJI YA UZIMA Mungu aliondoa. Leo hii watu wote ulimwenguni wamekunywa maji ya mto huu wa mauti wakidhani wanakunywa maji ya uzima k**a wadanganywavyo na watendakazi wa Ibilisi. Yaani viongozi wa dini hizi na madhehebu yake.

Lakini nikutoe mashaka na wasi wasi, k**a ilivyoandikwa katika;

📖Ufunuo wa Yohana 12:16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake."

NCHI ilimsaidia mwanamke, maana yake WATU WA MATAIFA , mimi na wewe tutafunua vinywa vyetu kuitangaza kweli ya Mungu kwa upya na dini hizi na madhehebu yake vitatoweka ulimwenguni na nguvu ya Mungu iliyofichwa (Mto wa maji ya uzima) itarejeshwa ulimwenguni tena k**a ilivyokuwa nyakati za Kristo. Na agano jipya la Mungu kwa wana wa Israeli litatimizwa.

Karibu tena na tena katika ukurasa huu wa Tuombe na Yesu Kristo tujifunze pamoja tukafunge mto huu wa maji ya mauti ili Mungu aturejeshee mto wa maji ya uzima watoto wetu na vizazi vijavyo vikaokolewe na mto huu upelekao watu kuzimu.
Yapo mafundisho mengi katika ukurasa huu ambayo yatajibu maswali yako mengi juu ya kinachoendelea ulimwenguni kwa sasa na jinsi ya kuiokoa nafsi yako na vizazi vyako vijavyo.

BWANA alimwambia Samweli,

📖1 Samweli 3:11 Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.

Na mi nakuhabarisha kuwa Bwana ameshatenda neno jipya! (AMEIFUNUA SIRI KUU ! Ameiweka wazi NGUVU YA IBILISI ALIYOKUWA AKIITUMIA KUWAANGAMIZA WENGI! Yaani Ukristo na uislam na madhehebu yake yote ndiyo hile njia pana iendayo upotevuni!! Basi USIIFUATE!! USIYANYWE HAYO MAJI YALETAYO MAUTI YA MILELE, ACHA SASA!!

24/07/2022

WOKOVU ALIOULETA BWANA YESU KRISTO.

Nukuu;

Mathayo 10:34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
Mathayo 10:35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
Mathayo 10:36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
Mathayo 10:37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

Habari za leo rafiki yangu na mfatiliaji wa mafundisho katika ukurasa wetu pendwa wa Tuombe na Yesu Kristo. Leo nimekuletea jambo muhimu sana la kujifunza katika kuuendea ufalme wa mbinguni. Mara nyingi tumesikia neno wokovu likitajwa katika makanisa na hata majumbani mwa watu k**a imani fulani ya kumuokoa mwanadamu. Watu walioamini katika imani hiyo huongozwa sala fulani na baada ya hapo huaminishwa kwamba ameokoka na taabu za ulimwengu zimekoma kwake! Wote tunafahamu kuwa mtu "akiokoka" haimaanishi kwamba yeye sio mkristo tena bali ni mkristo wa dhehebu la "kilokole" k**a walivyo walutherani, Wasabato, waanglikana na madhehebu mengine. Maana yake ni kwamba "kuokoka hakubadili kitu mbele za Mungu, bado mtu anakuwa chini ya mwanvuli wa ukristo, dini ambayo ilianzishwa na wanadamu.

WOKOVU HALISI WA BWANA YESU KRISTO!

Hapo mwanzo nimetanguliza nukuu ya maneno aliyoyasema Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mtu yeyote mwenye nia ya kuwa mfuasi wake imempasa kuwa tayari kufarakana na watu anaowapenda na watu muhimu, watu wa nyumbani mwake. Je upo tayari kuona unafarakana na mpenzi wako, mtu umpendaye sanaa! Kwa ajili ya Bwana Yesu?
Jibu unalo moyoni ILA KUWA MAKINI! Wapo waliofarakana na ndugu zao ama wapenzi wao kwa ajili ya dini na madhehebu ya wanadamu wakidanganywa kuwa hiyo ndio njia ya Kristo! Utapata hasara bure!

WOKOVU ALIOULETA BWANA YESU ni huu! Kukufahamisha wewe mteule habari hii njema, ya kwamba UKRISTO na UISLAM na madhehebu yake yote ndiyo ile njia pana iendayo upotevuni USIIFUATE! TOKA HUMO! Usiangalie watu watakuonaje! Watakuchukuliaje! Achana na ibada zao zilizojaa ahadi za uongo! Achana na sanamu zao za misalaba ya kusubu, kuchora na kuchonga! Toka humo! K**A WANAFUNZI WA YESU WALIVYOTOKA KATIKA MASINAGOGI YA DINI YA KIYAHUDI! NA WEWE TOKA KATIKA MAKANISA NA MISIKITI LEO HII UKAMUABUDU MUNGU WA KWELI MOYONI MWAKO.

Japo watu wako watakuchukia, wewe vumilia maana BWANA anasema;

📖Mathayo 10:22 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Na hapo ndipo ukivumilia mpaka mwisho UTAOKOKA.

Ebu tutazame Ufunuo 7.

Sura hii inazungumzia kipindi hiki cha dhiki tunachopitia ulimwenguni. Kipindi cha utawala wa tawi la mwisho la ukristo na uislam. Kipindi cha manabii wa uongo au kwa lugha rahisi "ulokole!"
Katika hii sura tunaona wana wa Israeli 144000 wakiokolewa pamoja na watu wengine kutoka mataifa na kabila mbali mbali wasiojulikana idadi yao wakiwa tayari WAMEOKOKA KUTOKA KATIKA UKRISTO NA UISLAM NA MADHEHEBU YAKE. (Yule mnyama mwenye pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo; Ufunuo13 )

📖Ufunuo wa Yohana 7:9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

Hao ni kina sisi, mimi na wewe tuliotoka katika ukristo na uislam na madhehebu yake na KUTUBU DHAMBI ZETU na kuamua kumfata Yesu daima maishani mwetu na kumtumikia mioyoni mwetu milele pasipo kugeuka nyuma.

Bwana atatufuta machozi ya taabu
Zetu zote tunazopitia katika nyakati hizi. Hizi si ahadi zangu bali za Bwana!

📖Ufunuo wa Yohana 7:14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
Ufunuo wa Yohana 7:15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
Ufunuo wa Yohana 7:16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.
Ufunuo wa Yohana 7:17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Basi rafiki yangu, KUOKOKA NI KUTOKA KATIKA KAMBA ZA DINI YA UKRISTO NA UISLAM NA MADHEHEBU YAKE na kuwa mtu huru na kumfuata Bwana Yesu Kristo na kumuabudu Mungu wa mbinguni katika roho na kweli. Na saa yetu ndio sasa.

📖Yohana 4:23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu.
Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

NIKUKUMBUSHE TU; Ibada yako leo ikawe ya siri. Omba kwa siri moyoni mwako maana huko ndipo Mungu anapopatikana.

📖Mathayo 6:5 Tena msalipo, msiwe k**a wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
Mathayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE!

12/07/2022

MWENYE NGUVU KARIBU KWENYE UFALME WA MBINGUNI.

Imeandikwa;
📖Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Habari yako rafiki unayesoma makala hii. Natumaini sio mara yako ya kwanza kutembelea ukurasa huu na k**a ni mara yako ya kwanza basi usiache ku-LIKE UKURASA WETU ILI UWE UNAPATA MAFUNDISHO YETU KWA URAHISI PALE TUNAPOCHAPISHA FUNDISHO JIPYA. Huduma zetu ni bure na hatuhitaji sadaka wala tozo za aina yoyote; HUDUMA ZETU KWA HABARI YA UFALME WA MBINGUNI NI BURE.

Basi baada ya utangulizi huo naomba tugeukie fundisho letu la leo. Katika hiyo Math 11: 12 niliyoanza nayo hapo juu, ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo wengi huyasoma lakini wasijue maana yake hata sasa.

Bwana anasema "Tangu siku za Yohana Mbatizaji UFALME WA MBINGUNI UNAPATIKANA KWA NGUVU!

Na WENYE NGUVU WANAUTEKA!

NI WAKINA NANI HAO WENYE NGUVU?

NI NGUVU GANI WALIZO NAZO?

WAMEPATA WAPI HIZO NGUVU?

JE WEWE NI MMOJA WAO?

Hakika wewe ni mmoja wapo ondoa shaka maana ukifahamu siri ya maneno haya ya Bwana Yesu huna kizuizi tena kuuingia ufalme wake.
NENO LA MUNGU LIMEANDIKWA KWA MAFUMBO ili wale ambao hawajakusudiwa kuuingia ufalme wake wasielewe. Si ajabu hata leo nikifumbua fumbo hili, ukawaona au kuwasikia watu wakinipinga na kunipuuza. Ila kwa TAARIFA YAO, HAPATAKUWA NA MSAADA MWINGINE WA KUUINGIA UFALME WA MBINGUNI ISIPOKUWA KWA MAFUNDISHO YA UKURASA HUU, MAANA NI MANENO YA BWANA MWENYEWE! Inajulikana wazi kuwa neno la nabii Isaya ndilo linalowatesa lakini wewe unayesoma sasa usiushupaze Moyo wako maana utaiangamiza nafsi yako.

📖Mathayo 13:14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

KWANZA TUZITAZAME NGUVU ZINAZOHITAJIKA KUUTEKA UFALME WA MBINGUNI
Nguvu kuu inayohitajika ni nguvu ya IMANI.
K**a leo tunavyowaona watu wakiweka imani zao katika sanamu za msalaba, mwezi na nyota nk. Na ukiwakosoa wanakuwa wakali ndivyo hivyo leo hii mtu akiweka nguvu zake katika kuamini njia hii ya kweli nifundishayo leo basi AMESHAUTEKA UFALME WA MBINGUNI HUYO! Wakati wa Yesu na Yohana mbatizaji, habari njema ya ufalme wa mbinguni waliyoihubiri ilipingwa sana na wafuasi wa dini ya kiyahudi na dini za watu wa mataifa zilizokuwepo wakati huo. LAKINI LEO VITA NI KUBWA ZAIDI KWETU WA
HASA SISI WATU WA MATAIFA kwa sababu ya dini ya ukristo na uislam na madhehebu yake yanayotawala ulimwengu. (Watu wa nataifa ni sisi ambao sio wa uzao wa Israeli. NB. Hakuna uisraeli wa kiroho k**a wengi wadanganywavyo. Mungu umtazama kila mwanadamu kwa asili yake na mbinguni tutaingia hivyo hivyo kwa asili zetu.)

Mafumbo haya tunayoyafumbua leo hii ni nguvu kubwa na ya kutosha kumuumbua shetani aliyejificha katika ukristo na uislam.
Unaposikia watu watavishwa mataji k**a ilivyondikwa; ni wale wataofanikiwa kutoka katika dini hizi mbili na madhehebu yake ambazo zimetajwa k**a Chukizo la uharibifu;

📖Mathayo 24:15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),

📖Danieli 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

📖Ufunuo wa Yohana 13:11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena k**a joka.

Naomba kwa leo niishie hapo ila tambua kwa wakati wa Yohana Mbatizaji na Bwana wetu Yesu Kristo watu walihitaji nguvu ya imani ili kutoka katika dini ya kiyahudi na madhehebu yake lakini kwa sasa hali ni mbaya sana! TUNAPAMBANA KUUSHINDA UKRISTO NA UISLAM NA MADHEHEBU YAKE! Si jambo rahisi! Watu hawa wanatumia neno la mungu na wafuasi wao ni wengi na tulio wengi tunapenda kufata mkumbo pasipo kukumbuka kuwa njia ya upotevu ni pana sana na inafuatwa na wengi.

📖Mathayo 7:13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Mathayo 7:14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

MUNGU ANATUHITAJI MIMI NA WEWE TUKAWE MASHUJAA WAKE KUURUDISHA UFALME WAKE DUNIA. LEO HII TAIFA LETU LINAKWENDA KUWA TAIFA TEULE MBELE ZA BWANA K**A ILIVYOKUWA ISRAELI. Maana ameileta habari hii njema KWETU baada ya Israeli kuikataa.

📖Mathayo 21:42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
Mathayo 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.

Kufunuliwa kwa mambo haya maana yake ni kwamba zama za ukristo na uislam na madhehebu yake zipo ukingoni na ufalme wa mbinguni ambao Yohana Mbatizaji na Bwana Yesu walitabiri kukaribia kwake BASI TAMBUA WAKATI HUO NDIO SASA NA MIMI NA WEWE NI WATU TUNAOHITAJIKA KUIENEZA HABARI HII ILI WENGI WAFUNGUKE MACHO YAO NA MASIKIO WATOKE HUMO.

LEO TUPO WACHACHE LAKINI TUKIWAJULISHA WENGINE, ULIMWENGU MZIMA UTAELEWA NA IBILISI NA MAMLAKA YAKE ITATOWEKA KABISA ULIMWENGUNI K**A ILIVYOANDIKWA;

📖Mathayo 13:31 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;
Mathayo 13:32 nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake. (NYUNI maana yake ndege wa angani.)

Mathayo 13:33 Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.

Basi wakati ujao nitawafahamisha nini kitafata baada ya dini ya ukristo na uislam na madhehebu yake kutoweka ulimwenguni.
Endelea kujifunza nami, jina la Bwana lihimidiwe amina!.

02/07/2022

Twendelee kujifunza pamoja katika ukurasa wetu pendwa bila kukata tamaa maana Bwana yupo pamoja nasi daima.
Nitaendelea kuwaletea mafundisho mengine lakini kwanza tuyapitie haya ambayo ni ya msingi.
Mungu awe pamoja nawe, akufungue macho yako na masikio, na akuondolee ugumu wa moyo upate kulipokea na kuliishi neno lake, Amina.

18/04/2022

JE ULIWAHI KUJIULIZA :
KWA NINI WATOTO WADOGO WANATESEKA WAKATI BWANA ALISEMA "WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU?"

Kabla ya yote naomba nikusalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai, amina. Pia naomba nichukue nafasi hii kukukaribisha katika ukurasa huu maalum kwa ajili ya wateule wa Mungu aliyetuumba kwa ajili ya kuzifunua siri ambazo alizificha kwa ajili yao.
Kumbuka si kila mtu amekusudiwa kuuingia ufalme wake, kwa hiyo pambania uzima wako wa milele bila kutazama nyuma wala pembeni au jirani yako atakuonaje, maana siku ya hukumu utasimama mwenyewe hata k**a kosa mlilifanya mkiwa mia nne elfu.

Leo hii ulimwengu unapitia wakati mgumu ambao haujawahi kutokea,. Ni wakati ambao shetani na watumishi wake wanawatesa watu wa kila rika na kila hali bila huruma. UKISOMA MAANDIKO, katika injili Bwana Yesu anasema watoto wadogo waachwe waende kwake maana hao ni mfano wa watu watakaourithi ufalme wa milele, SASA KWA NINI HAO HAO WATOTO walio mfano wa wateule watakaorithi ufalme wa Mungu leo wanateseka kwa maradhi, njaa, vipigo na mateso ya kila namna?

📖Mathayo 19:14 Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.

Wote tunafahamu watoto wadogo hawajui kitu, sasa dhambi ziwapasazo mateso wamezitoa wapi?
Wakati mwingine unaweza ukajiuliza kwa nini huyu mtoto alizaliwa, maana anateseka tangu kuzaliwa, hata raha ya kuishi hajawahi kuiona.

JIBU NI HILI.

HIKI NI KIZAZI CHA WATU WAMCHUKIAO MUNGU.

Soma vizuri kwa utulivu andiko hili, ikibidi lirudie hata mara mbili au zaidi, kisha twendelee.

📖Kumbukumbu la Torati 5:8 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.
Kumbukumbu la Torati 5:9 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha WANICHUKIAO,

Kwa wale waliowahi kusoma mafundisho yaliyotangulia katika ukurasa huu watakuwa wameanza kuelewa. Tangu Bwana Yesu na wafuasi wake walipouawa na dini ya Uyahudi kupata nguvu tena na baadae kuzaliwa dini ya Ukristo na Uislamu ulimwenguni, Mungu alianza kuuadhibu ulimwengu kwa kuwa walimchukia mwanae na kuabudu Sanamu za Msalaba, Mwezi na Nyota, na nyingine zilizo chini ya hizo.

Kwa hiyo k**a Mungu alivyoahidi KUPATILIZA uovu kwa vizazi, leo hii watoto wachanga wanateseka kwa makosa ya vizazi vilivyotanguli.
Na kwa nyakati hizi za MWISHO WA UTAWALA WA MAMLAKA YA GIZA, mateso yamekuwa mengi na mazito kwa wanadamu ili wawakimbilie kwa wingi manabii na makristo wa uongo waliopewa kufanya kazi nyakati hizi kila kona ulimwenguni kuhakikisha kila mwanadamu anakuwa mfuasi wao.

NINI KIFANYIKE?
HAKUNA CHA KUFANYA ZAIDI YA KUTAFUTA KUMJUA MUNGU WA KWELI NA KUTUBU ILI AKUONDOLEE CHUKI ILIYOPO KATI YAKO NA YEYE, AKUREHEMU, NA UZAO WAKO UTAKUWA SALAMA MILELE. Maana ameahidi;

📖Kumbukumbu la Torati 5:10
" nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu."

Tembelea zaidi ukurasa huu upitie mafundisho mbali mbali yaliyotangulia ujifunze mengi kuhusu nyakati tulizopo na njia sahii ya kuundea uzima wa milele. Jina la Bwana libarikiwe milele na milele Amina.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Telephone

Website

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00
Other Religious Centers in Dar es Salaam (show all)
Neema Gospel Choir Neema Gospel Choir
Dar Es Salaam, 2550766777288

🌍Gospel Music Choir - WORSHIP & PRAISE🎤 🏆Award Winning - Best Gospel Music Group East Africa 2021

Moravian Kipunguni B Moravian Kipunguni B
Kipunguni B
Dar Es Salaam

HUBIRI KWELII ,SIMAMIA KWELI, FUNDISHA NA KUITENDA KWELI

amos.marko.37 amos.marko.37
Dar Es Salaam

WOKOVU NI SASA KWA WANAOTAMBUA NYAKATI

Sheikh Hamza Rajab Abuu Seif Sheikh Hamza Rajab Abuu Seif
Dar Es Salaam

karibu katika Mawaidha na Darsa mbalimbali

Kagimbo Kagimbo Kagimbo Kagimbo
Dar Es Salaam, KGB198900

Family matters

Lemonde d'aujourd'hui Lemonde d'aujourd'hui
Numérl Whatsapp:+255625(07254
Dar Es Salaam

Huu Ndio Uislamu Huu Ndio Uislamu
Dar Es Salaam

Huu Ndio Uislam - Hii ni Mobile App ambayo inamrahisihia muislamu kufahamu dini yake kwa urahisi, kusoma vitabu mbalimbali, kusikiliza na kutazama video za masheikh mbalimbali.

Mungu nijibu Mungu nijibu
Erick Mbazendore
Dar Es Salaam, 222444

Wokovu upo kwa YESU pekee Wokovu upo kwa YESU pekee
0754890965
Dar Es Salaam

Tujifunze kwa pamoja jinsi gani Mungu anakuthamini wewe mwanadamu, hata akadiriki kumtoa mwanawe wa pekee Yesu ili aje akutoe katika dhambi na mateso ya shetani. Ni upendo wa ajabu...

Kinondoni Revival Choir Kinondoni Revival Choir
Kinondoni
Dar Es Salaam

Kinondoni Revival Choir is choir ministrering in KR Church, Kinondoni Assemblies of God.

Pastor Monday Adonu Pastor Monday Adonu
Dar Es Salaam

assurance deliverance prayer call and be bless +2348129729572 or+255679697220

Minister Kelvin Audax Minister Kelvin Audax
Dar Es Salaam, 14110

Bwana Yesu alitoa uhai wake kwa Ajili ya kuokoa ulimwengu hivyo kupitia Yeye dhambi zetu zinafutwa k