Minister Kelvin Audax

Bwana Yesu alitoa uhai wake kwa Ajili ya kuokoa ulimwengu hivyo kupitia Yeye dhambi zetu zinafutwa k

27/01/2023

I've received 400 reactions to my posts in the past 30 days. Thanks for your support. 🙏🤗🎉

Aniset Butati- Take Over 03/12/2022

Gusa link usikilize
https://youtu.be/75kYv8ndte8

Miongoni mwa nyimbo zinazopatikana katika Ep ya Aniseti Butati ni huu hapa Take Over na ndio uliobeba jina la Ep
Gusa link usikilize

Aniset Butati- Take Over

Lucy Charles- Samson (Official music Video) 16/11/2022

https://youtu.be/dsT44NUYWIE

*Bwana Yesu Kristo asifiwe sana*
Nachukua nafasi hii kukukaribisha kutazama video ya wimbo huu uitwao Samson
Mungu akubariki sana naamini utabarikiwa

https://youtu.be/dsT44NUYWIE

*Kwa video na audio nzuri k**a hii piga number +255744440245*

Lucy Charles- Samson (Official music Video)

25/08/2022

Kuna watu wengi wanaomba lakini hawajibi, wanaishia kuhama makanisa leo yupo huku, kesho kule. Lakini neno linasemaje kwa habari ya kujibiwa

Yakobo 4
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
🔴Mwaomba hampati na sababu mnaomba vibaya, utajiuliza naombaje vibaya je napiga kelele ndio yawezekana unapiga kelele mbele za Mungu maana maombi yake mtu muovu ni sawa na kelele mbele za Mungu maombi ya kuomba matakwa yako ni pasipo kutaka mapenzi ya Mungu ya timie hizo ni sawa na kelele tu.
Kuna namna ya kuomba maombi yaletayo majibu ni lazima ufuate kanuni za maombi yajibiwayo, lakini zaidi ya Yote ni kuwa na Roho wa Mungu ndani yako (Roho mtakatifu) huyo atakufundisha namna nzuri ya kuomba, lakini pia atakusaidia kuomba k**a Biblia isemavuo.

Warumi 8
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu k**a apendavyo Mungu.

🔴Roho utusaidia madhaifu yetu kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, unapokua na Roho anakusaidia kuomba ipasavyo, kwa sababu yeye ni Roho wa Mungu hivyo anajua mapenzi ya Mungu kwetu, nae anatufundisha namna ya kuomba ipasavyo ili yale mapenzi ya Mungu yatimie.
SOMO LA NAMNA YA KUOMBA IPASAVYO LITAKUJIA SIKU SI NYINGI

19/08/2022

MAOMBI YA KUVUNJA MAAGANO NA KUFUTA VIAPO VINAVYOTESA MAISHA YAKO

19/08/2022

TABIA ZA WANA WA MUNGU

18/08/2022

Tabia za wana wa Mungu. Sehemu ya 2

06/06/2022

JE UNAJUA KUWA KUNA WATOTO WAPO KWENYE VITUO VYA YATIMA HAWANA WAZAZI ILA WANA MAHITAJI K**A VILE WATOTO WAKO WALIVYO NA MAHITAJI JE ULISHAWAHI KUTOA SIKU KWENDA KUWATEMBELEA
AU UPO BUSY SANA
JIFUNZE KUGAWANA KILE KIDOGO ULICHO PAMOJA NA WASIO NACHO

26/05/2022

WANAWAKE MUWE NA UPENDO KWA NDUGU WA MUME WAKO!!

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja mume pamoja na mke wake, mume akamwambia mke wake...

"Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoja

Kesho nitawaalika ili tujumuike nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke akasema kwa unyonge "sawa mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda katika mishughuliko yake lakini baada ya masaa kadhaa akarejea nyumban na kumuuliza mke wake.

"Mke wangu umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa wameshafika."

Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Mumewe akamwambia mungu akusamehe mke wang kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja

Na kwa nini hukunambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wangu watakuwa hapa nini unafanya mke wangu."

Mke akamjibu "waache waaje nitawataka radhi, kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Basi mume ikambidi aondoke pale nyumban kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua...
Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake, mamaake dada zake pamoja na kaka zake

Akastuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa leo anatuarika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana sasa vipi yeye ametoka si busara."

Yule mwanamke akastuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?"

Mumewe akamjibu "Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti."

Mke akamwambia "Lete chakula huku chakula kilichokuwepo ni kichache haki tawatosheleza."

Mume akamjibu "Mimi nipo mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo k**a wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu.

21/05/2022

HAYA YOTE UNAYOONA YANAENDELEA DUNIANI SIO KWAMBA MUNGU HAONI MUNGU ANAONA. ILA AMENYAMAZA NA KUACHA KILA MMOJA ACHAGUE KILE ANACHOONA NI CHEMA ILA MWISHO WA YOTE NI HUKUMU

21/05/2022

ULE MLANGO WAKO WA MAFANIKIO ULIOFUNGWA NA MUOVU UNAENDA KUFUNGUKA KWA JINA LA YESU

20/05/2022

USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA ....
Tafadhali soma,
Jina langu ni Memory nilifanya uasherati wakati wa siku zangu za chuo kikuu. K**a matokeo ya hii, nilitoa mimba 4 na ya mwisho iliharibu tumbo langu na karibu nipoteze uhai wangu. Niliona kuzimu wakati wa utoaji mimba yangu ya mwisho na nilifikiri nitakufa. Nilimuahidi Mungu kwamba nitaacha ukahaba ikiwa ataokoa maisha yangu na Mungu asifiwe, alinipa nafasi ya pili. Baada ya kuoa mwaka jana, sikuweza kuchukua mimba kwa sababu sikuwa na tumbo lakini mume wangu hakuniacha. Usiku mmoja, wakati nilikuwa nimelala. Mwanamume alionekana katika ndoto zangu. Alivaa mavazi meupe na akaweka mkono wake juu ya tumbo langu. Nilijua ni Mungu aliyenipa tumbo jipya. Kabla ya mtu huyo kutoweka, kutoka kwa ndoto zangu. Aliniuliza kushiriki ushuhuda huu na kwamba mtu yeyote atakayesoma atapata muujiza wa haraka na mafanikio. Mara tu nilipoamka, nilivua nguo na kufanya mapenzi na mume wangu. Leo, mimi ni mama wa watoto watatu (wavulana 3). Usishangae kwani Yeye ni Mungu wa miujiza isiyowezekana. SASA, NINAPITISHA MUUJIZA WANGU KWA KWAKO K**A NILIVYOAMRIWA: 1. Kwa kila mikono inayomwamini Mungu, utapokea muujiza wa mafanikio.
2. Chochote moyo wako unavyotamani unaweza kuwa, unapodai sala hii kwa imani, "IMEFANYIKA MBINGUNI." Andika "Amina" na SHIRIKI POST HII KWA VIKUNDI 5 TOFAUTI NA UONE KINACHOTOKEA KWA MASAA 24 USIPUUZE HII.

HAKIKISHA UNASHIRIKI HII KWA IMANI

Usifanye utani na hii sala, 🙏
Fuata tu maagizo na uone kinachotokea

20/05/2022

SIMULIZI YA KWELI YA KUSIKITISHA,.

Dada yangu na mimi tulipoteza wazazi wetu katika umri wa miaka 4-5 kwa ajali ya gari,.

Baada ya wazazi wetu kufa mjomba wangu mwovu na mkewe walirithi mali zote za wazazi wangu, tangu tukiwa wachanga na aliahidi kutuchukua.

Siku chache baadaye mambo yalizidi kuwa mbaya .. tuliacha masomo tangu yeye
alipokataa kulipa ada yetu.

Walitudhulumu,. na kuishi nao ilikuwa k**a tupo kuzimu.

Sikuweza kuvumilia kujiona na nateseka mimi na dada yangu, Usiku mmoja tuliamua kutoroka nyumbani na dada yangu kuanza na kwenda kuanza maisha ya mtaani.

Tukawa waombaji barabarani ..tulikuwa tulilala barabarani, Sehemu machafu tena hapana usalama, Wanaume, mvua, mbu, maradhi yalikuwa changamoto kwetu.

Nguo zetu zilionekana mchafu sana.

Maisha hayakuwa sawa kwetu lakini hatukuwa na chaguo.

Kwa bahati nzuri alasiri moja tulikuwa tunaomba barabarani, na kukutana na MWANAMKE mmoja katika gari na kuniuliza swali ambalo ama haki lilinikumbusha mengi na kuniuliza pia, aliuliza, wazazi wako wapo wapi!? na nikamwambia kwa unyenyekevu
hadithi yangu yote

Aliguswa na story yangu na akaniambia nisifadhaike atatusaidia hivi karibuni na kila kitu kitakuwa vizuri tena.

Siku chache baadaye alikuja mtaani na kutupeleka kwake.

Nilifurahi lakini nilikuwa na huzuni kwa sababu yeye ni mgeni kabisa kwetu.

Alituambia hana watoto kwa hivyo anataka kutuchukua ..na kutufanya watoto wake. tulipata msisimko..lakini tukajisemea mwisho mateso yetu yataisha.

Alitupa elimu nzuri na akatutendea vizuri sana.

Sasa DADA yangu ni DAKTARI na mimi ni ENGINEER.

Leo maisha yako pia yanaweza kubadilika kwa kumwamini na kumtegemea MUNGU.

USIWE MVIVU WA KUSEMA AMEN ....,

Ninatangaza kuwa Mungu Mwenyezi atachukua kitu chochote kinachounda aibu katika maisha yako; Majeraha yatapona, machozi yako yatafutwa , na baraka zako zilizoibiwa zitarejeshwe katika folda tofauti tofauti katika jina la MUNGU Mtukufu

AMEN.
Share kwa wingi na wengine iwafikie

20/05/2022

MITEGO YA MAPAMBO YA SHETANI INAYO WAFANYA WANAWAKE KUKOSA KUINGIA MBINGUNI

LADY ADELINE WA UFARANSA.

Onyo la Bwana kwa kila mwanamke mmoja duniani. Nilikuwa nimepiga magoti nikisali wakati ghafla macho yangu ya kiroho yalifunguka. Nilimwona mwanamke katika maono.

Bwana aliniuliza, “Je! Unamwona yule mwanamke? unaona nini? ”

Nikasema, "Bwana naweza kumuona yule mwanamke lakini simjui."

Bwana akasema, “Mtazame kwa uangalifu. Unaona nini? ”

Nikamtazama yule bibi. Anaonekana yuko kwenye sherehe. Alikuwa akiongea na rafiki yake na akicheka lakini hakuna kitu kilinigusa.

Bwana akasema, "Kweli huoni chochote?"

Mara nikagundua kuwa yule mwanamke alikuwa amevaa blauzi ambayo ilikuwa nzuri lakini kuzunguka bega kulikuwa na fursa na kando ya mkono kulikuwa na mashimo mengi madogo yanayofunua ngozi ya mwili wake.

Bwana akasema, “Mwanamke unayemuona ni mtumishi Wangu. nampenda sana kwani anaishi kwa hofu yangu lakini angalia blauzi amevaa. Ananiogopa lakini mavazi yake ni ya wasiwasi.

Bwana aliniuliza, "Je! Ninyi watu mnasema mimi siangalii mwili, ninaangalia tu moyo?"

Nikasema, "Bwana, nilikuwa nikifikiria hivyo."

Bwana akasema, "Je! unawezaje kufikiria hivyo? Je! Hausomi kile Biblia inasema kwamba mwili wako ni hekalu Langu. Unawezaje kukosa hekima wakati tayari nilikwambia kwamba mwili wako ni hekalu Langu? Je! Unawezaje kutarajia mimi kukuacha uharibu hekalu Langu? unawezaje kufikiria mimi nikitazama moyo wako ukipuuza mwili wako ambao ni hekalu Langu? Onywa binti yangu kwa kuwa macho yangu hayatazami mbali hata na watoto Wangu hata kwa sekunde moja na macho yangu yanamwangalia binti yangu huyu ambaye ninakuonyesha. "

niliendelea kumtazama mwanamke huyu wakati sauti ya Bwana iliyosikika ilikuwa ikiongea nami. Kilichonigusa ni wakati Bwana aliposema, "Ninampenda sana."

Nilikuja kuelewa kuwa Bwana anatupenda sisi sote lakini kuna watu anawapenda sana k**a mwanamke huyu.

Bwana alisema, “Nataka binti yangu awe mwepesi. Sipendi uchi wao ufunuliwe. Waambie wabadilishe mavazi yao ipasavyo. ”

Ibilisi alijaribu kunizuia kutoa ujumbe huu lakini tunamshukuru Bwana. kaka na dada yangu mpendwa nilikuwa nimelala na nilihisi uwepo wa nguvu wa Bwana. K**a matokeo, nilifungua macho yangu. Mara nikaona malaika wawili wenye kung'aa wamesimama mbele yangu.

wakati huo sauti ya Bwana ilisema na kusema, "Binti yangu Adeline, katika ufalme Wangu, kutakuwa na wanaume wengi lakini wanawake wachache."

Nikamwambia, "Bwana, unamaanisha nini na kwa nini kutakuwa na wanawake wachache?"

Bwana akasema, "Je! Unataka kujua kwa nini kutakuwa na wanawake wachache katika ufalme Wangu?"

nikasema, "Ndio Bwana, nataka kujua kwanini."

Bwana akasema, "Hivi ndivyo nimekuja kukuonyesha, na chochote nitakachokuonyesha usiwafiche binti zangu ulimwenguni kote. Lazima wasikie. ”

kisha Bwana akaongea na malaika wa nuru na kuwaambia, "Sasa mwambie ni kwanini watakuwa wanawake wachache katika ufalme wa Mbingu."

Malaika waliniambia, “Adeline, mwanamke yeyote ambaye amevaa wigi hataingia katika ufalme wa Mbingu. mwanamke yeyote anayesuka nywele zake kwa nywele bandia hataingia katika ufalme. ”

Nikasema, "Je! Ni hivyo?"

Wakasema, “Ndio. Mwanamke yeyote anayetumia kucha ya bandia kwenye kucha zao hataingia katika ufalme. Mwanamke yeyote anayepaka lipstick hataingia katika ufalme. mwanamke yeyote aliye na kope hataingia. ”

Ndugu nilikuwa na hofu kusikia ukweli huu.

Malaika walisema, "Mwanamke yeyote anayetumia unga wa uso hataingia katika ufalme wa Mbingu kwani unga huu wa uso hubadilisha ngozi ya mwanamke."

ndipo Bwana akasema na kusema, "Nina uchungu na huzuni ndani Yangu kwa sababu binti zangu ambao wananitumikia na wananiogopa wanatumia vitu hivi ambavyo ni vyombo vya adui kwani hawataingia katika ufalme Wangu. Wamevaa wigi na viambatisho. wanatumia kucha na vifaa vya uovu vya adui. Nenda uwaambie binti zangu wanaoniogopa na kutembea katika utakatifu lakini bado wanatumia bidhaa za urembo hawataingia katika ufalme Wangu. ”

Mpendwa wangu sauti ya Bwana ilijawa na huzuni alipozungumza maneno haya.

Bwana alisema, “Nimejawa na huzuni kwa waja Wangu. Wananitumikia kwa kweli na wanatembea katika utakaso lakini wameambatanishwa na midomo hii, wigi, na mapambo. Waambie waachane na vitu hivi. Vinginevyo, hawataingia katika ufalme wa Mbingu. ”

Bwana aliwaambia malaika wa nuru, "Mwambie ni nini kilitokea wakati watumwa na binti zangu wanapokufa na mapambo haya ya ulimwengu."

malaika waliniambia, "Wakati waliokufa katika Kristo walipokufa katika Bwana tunakuja kuwachukua na kuwapeleka kwa ufalme wa mbinguni lakini wanapokuja tunaangalia ikiwa mavazi yao meupe yamehifadhiwa safi. ikiwa nguo zao nyeupe zinaonekana, hatuwachukua wale watakatifu ambao wameshindwa kuweka nguo zao safi. Katika hali hii, pepo na malaika wa Shetani wangekuja kuwak**ata watakatifu hawa na kuwaongoza kwenye uharibifu. hata hivyo wakati wanawake wanaomcha Bwana wakifa vazi lao jeupe huwa hawana doa kila wakati. Ndio maana tunakuja kuwachukua kwa mavazi yao ni meupe k**a theluji lakini mara tu tunapojaribu kuwafikisha kwenye ufalme wa milele malaika wa Shetani wangejitokeza kwa kutarajia. wao hutuambia kila wakati, ‘Huwezi kuwapeleka Mbinguni. Wao ni mali yetu na ufalme wetu. Sio zako. ’Kuna mabishano mengi kati yetu na mashetani zaidi ya kaburi kwa sababu ya roho za binti za Mungu.”

malaika wa nuru waliniambia, "Tunakuja kupata binti za Mungu kwa sababu wanatembea kwa usafi na kumcha Bwana na wameosha mavazi yao ambayo ni meupe k**a theluji na hayana doa lakini pepo wanaendelea kutuambia, 'Hatuna toa nguo nyeupe (hiyo inamaanisha maisha matakatifu ya utakasona kumcha Bwana) lakini angalia kuonekana kwa hawa binti za Mungu kwa kuwa wana vitambulisho vyetu. ’pepo siku zote hutuelekeza juu ya kuonekana kwa wanawake na tunapoangalia roho za hawa binti za Mungu ambazo zimeosha mavazi yao tunaweza kuona kuwa kwenye vichwa vyao wana wigi, viambatisho na kusuka. Wana kope. Wana midomo. Wana unga wa uso. Wana rangi ya kucha. ”

malaika waliniambia, "Isipokuwa binti za Mungu wasipo jitenga na mapambo ya ulimwengu hatuwezi kuwapeleka katika ulimwengu wa mbinguni ambapo hakuna wanawake walio na kiambatisho na kucha za bandia. Mabinti wa Mungu lazima watengane na mapambo mabaya na ubatili. hata k**a wanawake hawa wataogopa Bwana wanapokufa wakishindwa kujitenga na ubatili huu, roho zao zitapambwa na wigi, kope, na kucha na hatuwezi kuwapeleka katika Jiji la Milele na vyombo hivi vya mashetani. licha ya mavazi yao meupe, hakuna mtu atakayeingia Mbinguni na wigi, midomo, na unga wa uso kwani Mbinguni hakuna mtu aliye na nywele bandia na kucha. Hatuwezi kuchukua mtu yeyote aliye na misumari iliyopakwa. binti za Mungu wengi wanakufa na hofu ya Bwana lakini hatuwezi kuwapeleka kwenye ufalme wa dhahabu kwa sababu ya mapambo haya ya adui. Ni adui ambaye anachukua roho zao kwa sababu hatuwezi kuleta vitu hivi Mbinguni. waambie wanawake katika makanisa bidhaa za urembo na mapambo ya ulimwengu yanaonekana kwenye nyuso zao katika maisha ya baadaye. Bwana anapinga kushik**ana na mabadiliko ya rangi ya asili. ”

Bwana alisema, "Ninapinga kushik**ana na kope bandia kucha bandia nywele bandia ninapinga mabadiliko ya rangi yako ya asili. waambie binti zangu wabaki na nywele zao za asili tu. Hawana haja ya viambatisho vya nywele. Hiyo ni kuongeza kwa kile nilichokiumba. Kwa kuwa binti zangu wameambatana na ubatili hawaendi Mbinguni. Vitu hivi ni vitambulisho vya mashetani. Wanabadilisha uumbaji wa asili. waambie waachane na viambatisho na kucha za bandia. Haipaswi rangi ya nywele zao. Watu wanakufa na kuja na viambatisho vya wigi na nywele bandia mbele ya lango la Mbingu. "

Mpendwa nataka ushiriki ujumbe huu hata ikiwa wewe ni mwanaume. Shiriki ujumbe huu na dada na mama zako. Bwana atakukumbuka wakati unashiriki onyo lake na watu Wake. Nisaidi kushare kwa wengine ili wakombolewe🙏

20/05/2022

K**a wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hii inakuhusu sana, hasa kwa wale wanaopenda kukubali kila ombi la urafiki wanalotumiwa. Ni ushuhuda wa kijana Fabio Adjavon mzaliwa wa Ghana akiwa na makazi yake nchini Afrika ya kusini, ambapo kupitia ukurasa wake wa Facebook alitumiwa ombi la urafiki na mtu asiyemjua ambaye kwenye profile picha yake kulikuwa na picha za kutisha, ambapo kijana huyo kabla hajakubali ombi la urafiki na mtu huyo akaamua kuangalia picha zilizoko kwa mtu huyo amuombaye urafiki na kukuta picha za ajabu sana kitendo ambacho kilimpa ugonjwa kwa siku mbili. Yote haya ameyaeleza alipofika kanisani kwa nabii TB Joshua huko Nigeria ambako alifanyiwa maombi na kufunguliwa.

Shetani na mawakala wake wamejaa Facebook na kwenye mitandao ya kijamii, ili kuwamaliza watu, hususani vijana ambao huwa wanakubali urafiki na wasichana warembo au vijana watanashati hata k**a hawajawahi kuonana nao au kuwajua, ila wanavutiwa na sura au muonekano wao na bila kujua ni kwamba wamekubali urafiki na shetani ambaye nia yake ni kuharibu mahusiano, hakuna kuoa wala kuolewa, kutofanikiwa kazini au chochote afanyacho.

20/05/2022

Soma shuhuda hii upone na usimame kwenye nafsi yako vizuri

Jinsi Ibilisi Anavyozuia Maombi Yako

Ndugu msomaji wa blog hii, kati ya makala au masomo ambayo nimeyaandika humu, hili ni somo na ushuhuda mmojawapo wenye nguvu sana ambao, kila mwana wa Mungu atakayeusoma, atapata msukumo wa rohoni usio wa kawaida. Haya ni mafunuo yenye nguvu mno ambayo, hakika yatakuinua kwa kiwango cha juu sana nawe utamshukuru Mungu. Nilipouona ushuhuda huu kwenye mtandao, moyo wangu ulianza kuwaka niweze kuutafsiri harakaharaka na kuuweka kwenye blog hii ili yamkini uweze kuwafikia wapendwa wengi iwezekanavyo.

Huu ni ushuhuda ulioandikwa na Mchungaji John Mulinde wa Uganda kutokana na kile alichosikia kutoka kwa mhusika mwenyewe. Mhusika huyo, mchungaji hajamtaja, lakini alikuwa ni kijana ambaye alimtumikia shetani tangu angali tumboni mwa mama yake. Baadaye, kwa neema ya Bwana kijana huyo aliokolewa, ndipo akaanza kueleza siri hizi za ufalme wa giza na ufalme wa nuru.

Mamilioni ya Wakristo duaniani tunamwomba Mungu wetu kwa ajili ya mahitaji mbalimbali tuliyonayo. Lakini liko swali moja kubwa linalojirudiarudia ndani ya mioyo yetu karibu kila siku. Tunajiuliza, “Nimeomba sana na kwa muda mrefu. Mbona Mungu hajibu…?” Tunabaki bila majibu, tunavunjika moyo, na tunaanza kudhani labda sisi ni wenye dhambi sana ndio maana hatujibiwi.

Ukiifahamu siri iliyomo kwenye ushuhuda huu, utatiwa nguvu sana za rohoni; maana maarifa ndiyo yanayotufanya tuwe na nguvu za Mungu. Tunaenenda kiimani kwa kadiri ya kiwango cha maarifa au ufahamu uliomo ndani yetu. Tukijua sana, tunaweza sana; tukijua kidogo, tunaweza kidogo.

Karibu ujipatie maarifa ambayo Bwana wetu ameruhusu yatufikie. Nami na hakika utamfurahia Bwana kwa kukupigisha hatua nyingine ya imani. Utafanya vema k**a ukiweza kuwapatia na wengine somo hili la muhimu sana kwa ajili ya mwili wa Kristo.

******************

Yafuatayo ni maelezo ya Mchungaji John Mulinde:

Napenda nikushirikishe ushuhuda wa kijana mmoja ambaye aliokoka; kijana ambaye alikuwa akimtumikia ibilisi. Na mtu yule alipotoa ushuhuda wake, ulinitia changamoto kubwa sana. Sikutaka kuamini. Ilinibidi nifunge kwa muda wa siku kumi mbele za Bwana, huku nikimuuliza, “Bwana, hivi mambo haya ni kweli?” Na ilikuwa ni katika wakati huo ndipo Bwana alipoanza kunifundisha kile kinachotokea kwenye ulimwengu wa roho pale tunapoomba.

Kijana huyu alizaliwa baada ya wazazi wake kuwa wamejiweka wakfu wao wenyewe kwa lusifa. Wakati bado akiwa tumboni, walifanya matambiko mengi na kumweka wakfu awe mtumishi wa lusifa. Alipozaliwa na kufikisha miaka minne, tayari alianza kutumia nguvu zake za kiroho. Hata wazazi wake walianza kumwogopa! Akiwa na miaka sita, baba yake alimkabidhi kwa wachawi ili akapatiwe mafunzo. Na akiwa na miaka kumi, alikuwa akifanya mambo makubwa katika ufalme wa ibilisi. Alikuwa akiogopwa hata na wachawi wa kawaida.

Alikuwa bado ni kijana mdogo, lakini mambo aliyokuwa anafanya yalikuwa ni mabaya mno. Alikua hadi kufikia miaka ya ishirini akiwa na damu nyingi ya watu mikononi mwake. Aliua watu kila alipotaka. Alikuwa na uwezo wa kutoka nje ya mwili wake kupitia taamuli ya kinjozi (transcendental meditation), yaani kitendo cha kutuliza mawazo na mwili k**a wafanyayo Wahindukatika yoga. Tazama mfano HAPA. Katika huko kutaamuli, angeweza hata kunyanyuka kimwili kutoka ardhini pale alipokaa na kuelea hewani (levitate). Tazama mfano HAPA. Wakati mwingine aliweza kutoka nje ya mwili; akauacha mwili wake na kwenda nje huko na kule kufanya mambo mbalimbali (astro-travelling). Na kijana huyu alitumiwa na shetani kuharibu makanisa mengi; na kuwaharibu wachungaji wengi.

Siku moja, alipangiwa kwenda kuharibu kanisa moja ambalo lilikuwa na maombi ya kutosha. Kulitokea na migawanyiko mingi kanisani na kuchanganyikiwa kwingi. Alianza kufanya kazi kwenye kanisa hili; lakini mchungaji wa kanisa lile aliitisha mfungo wa kanisa zima. Kanisa lilipoanza kufunga, watu walitubu sana na kufanya mapatano mengi. Na watu wakawa kitu kimoja, na wakaanza kuomba kwa ajili ya kazi ya Bwana katikati yao. Na wakaendelea kufanya maombezi na kumlilia Mungu ili awarehemu na kuingilia kati maishani mwao. Na kadiri siku zilivyoendelea, bwana huyu alikuwa akija tena na tena akiwa na mapepo kinyume na kanisa hili. Lakini lilitoka neno la kinabii likiwaambia Wakristo wasimame pamoja na kufanya vita dhidi ya nguvu za giza ambazo zilikuwa zinashambulia kanisa lile.

Siku moja, kijana huyu aliuacha tena mwili wake chumbani kwake na akatoka nje. Aliongoza jeshi kubwa la mapepo moja kwa moja hadi kwenye kanisa lile ili kwenda kufanya vita vya kiroho.

Sasa, ufuatao ni ushuhuda wake.

Roho yake ilikuwa inapaa hewani juu ya kanisa lile na kujaribu kulishambulia, lakini kulikuwa na kifuniko cha nuru juu ya kanisa hilo. Wakati waliendelea na mapambano, ghafla, kulikuja jeshi la malaika ambalo liliwashambulia na kukawa na mapambano makali pale hewani. Hatimaye, mapepo yalikimbia, lakini yeye alik**atwa na wale malaika.

Ndiyo, alik**atwa na malaika! Alijiona akiwa ameshikiliwa na malaika sita. Na wakamleta kwa kumpitisha kwenye paa hadi kwenye madhabahu ya kanisa. Akawa yuko pale huku watu wanaendelea kuomba. Walikuwa wamezama kwenye maombi, wakifanya vita vya kiroho; wakifunga na kuvunja, na kutupa nje. Mchungaji alikuwa kwenye madhabahu akiongoza maombi hayo na vita. Roho wa Bwana akaongea na mchungaji, akisema, “Nira imevunjika, na mhusika yuko hapa mbele yako. Msaidie kwa kumfungua.“

Mchungaji alipofungua macho yake, alimwona yule kijana akiwa ameanguka pale hajitambui. Mwili wake ulikuwa pamoja naye! Kijana yule anasema kuwa haelewi ni kwa vipi mwili wake uliungana naye; maana alikuwa ameuacha nyumbani. Lakini ndio alikuwa pale; hajui ni kwa vipi aliingia, isipokuwa tu malaika walimpitishia kwenye paa.

Sasa, mambo haya ni magumu kuamini, lakini mchungaji alinyamazisha kanisa na kuwaambia kile ambacho Bwana alimwambia. Kisha akamwuliza yule kijana, “Wewe ni nani?” Kijana yule alikuwa anatetemeka wakati mapepo yalipoanza kumtoka.

Kwa hiyo, waliomba kwa ajili ya kufunguliwa kwake, na hatimaye baadaye alianza kusema ushuhuda wake. Hivi sasa kijana huyu ameshaingia kwa Bwana na ni mwinjilisti, akihubiri Injili. Anatumiwa sana na Bwana kuwaweka huru watu wengine.

Usiku mmoja, mimi (John Mulinde) nilienda kwenye chakula cha usiku mahali fulani. Sababu hasa ya kwenda pale ni kwa vile kuna mtu alinieleza habari za huyo kijana; na nilikuwa na shauku kubwa sana ya kumwona, na kuona k**a kweli hadithi yake ina ukweli wowote. Kwa hiyo, nilipofika, nilikaa mezani. Na jioni ile, kijana huyu alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda wake. Alizungumza juu ya mambo mengi sana. Mara nyingine alilia kutokana na mambo aliyoyafanya. Alipomaliza kusema, alitoa ombi.

Kulikuwako na wachungaji wengi pale kwenye ukumbi. Alisema, “Ninawaomba ninyi, wachungaji. Tafadhalini, wafundisheni watu namna ya kuomba.” Watu ambao hawaombi, wanaweza kuchukuliwa na chochote, katika chochote na ibilisi; na ziko hata njia za adui za kutumia maisha yao na maombi yao. Adui anajua hata namna ya kutumia kwa faida yake maombi ya watu wasiojua kuomba. “Wafundisheni watu namna ya kutumia silaha za kiroho ambazo Mungu amezitoa.“

Kisha alieleza jinsi ambavyo alikuwa akiongoza mapambano kwenye anga. Alikuwa akienda pamoja na maajenti wengine wa shetani na mapepo mengi hadi angani. Ilikuwa k**a zamu. Inabidi kwenda kutekeleza zamu yako. Kwa hiyo, ni mara nyingi tu alikuwa na muda wa kwenda kwenye anga ili kufanya vita. Na akasema kuwa kule angani, kwenye ulimwengu wa roho, k**a anga limefunikwa na blangeti la giza, blangeti hilo linakuwa ni nene sana; na ni k**a jiwe. Na linakuwa limefunika eneo lote. Na mapepo haya yanaweza kwenda juu yake na chini yake. Na yakiwa huko, yanaweza kuathiri matukio yanayoendelea duniani.

Pale mapepo wachafu pamoja na maajenti wa shetani wa kibinadamu wanapomaliza zamu yao, wanashuka duniani kwenye maeneo ya kimaagano, iwe ni kwenye maji au ardhini, ili kuweza kurejesha upya nguvu zao, maana zinakuwa zimepungua kutokana na kufanya kazi angani wakati wa zamu yao. Na wanarejeshaje nguvu zao? Ni kupitia kafara ambazo watu wanatoa kwenye madhabahu hizi. Kafara zinaweza kuwa ni uchawi wa wazi, damu za aina zote, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba, vita, na utoaji wa kafara za wanadamu na wanyama. Zinaweza pia kuwa ni kafara za uzinzi, pale ambapo watu wanafanya uzinzi na uashetati wa kila aina. Na matendo haya maovu yanaleta nguvu kwenye ulimwengu wa giza. Na ziko aina nyingi za kafara.

Kijana huyo alisema kuwa, maajenti wa shetani wanapokuwa juu kwenye anga, na Wakristo wakaanza kuomba hapa duniani, maombi ya Wakristo huonekana kwa namna tatu. Maombi yote huonekana k**a moshi ambao unapaa kuelekea mbinguni.

Baadhi ya maombi huonekana k**a moshi, na yanaenda juu kiasi na kupotelea hewani. Maombi ya aina hii hutoka kwa watu ambao wana dhambi maishani mwao na hawako tayari kushughulika nazo. Maombi yao ni dhaifu sana, kiasi kwamba yanapeperushwa na kupotelea angani.

nyingine ya maombi nayo ni k**a moshi ambao unainuka juu hadi unapofikia kwenye ule mwamba, lakini hayana nguvu ya kupenya mwamba huo. Kwa kawaida, hawa ni watu ambao hujaribu kujitakasa, lakini hawana imani juu ya kile ambacho wanakifanya pale wanapoomba, yaani wanaomba lakini moyoni hawana ujasiri kwamba kile wanachokiomba watakipokea. Mara nyingi huwa wanapuuzia mambo mengine ya muhimu yanayotakiwa wakati mtu anapoomba.

Aina ya tatu ya maombi ni k**a moshi ambao umejaa moto. Yanapokuwa yanapaa, yanakuwa ni ya moto sana kiasi kwamba yanapoufikia ule mwamba, unaanza kuyeyuka k**a nta. Yanapenya mwamba huo na kuendelea hadi juu.

Mara nyingi watu wanapoanza kuomba, maombi yao huonekana k**a aina ya kwanza ya maombi. Lakini kadiri wanavyoendelea kuzama, yanageuka na kuwa ya aina ya pili. Na wakiendelea zaidi, ghafla yanalipuka moto. Na maombi hayo yanakuwa yana nguvu sana kiasi kwamba yanapenya kabisa ule mwamba.

Mara nyingi maajenti wa uovu hubaini kwamba kuna maombi yanabadilika na kuelekea kwenye kuwa moto. Kisha huwasiliana na viumbe vingine vilivyoko duniani na kuwaambia, “Mvurugieni mtu huyo maombi! Mfanyeni aache kuomba! Mwondoeni kwenye maombi!“

Mara nyingi Wakristo hushindwa na mbinu hizi. Wanakuwa wanaomba kwa nguvu; wanatubu; wanaruhusu Neno kukagua nafsi zao; imani inaanza kujengeka. Maombi yao yanaanza kuwa na shabaha zaidi. Kisha ibilisi anaona kuwa maombi yao yanaanza kukusanya nguvu. Ndipo vurugu zinaanza ili kuharibu maombi hayo. Mara simu inalia. Wakati mwingine, katikati ya maombi ambapo mtu alikuwa amezama kabisa, , simu inaweza kulia na unawaza kuwa, ngoja niende nikaipokee kisha nitarudi kuendelea na maombi.

Mbinu zingine za kuvuruga maombi nazo zinaweza kutumika; hata k**a ni kukugusa mwili wako na kuleta maumivu mahali fulani. Hata pia kukufanya ujisikie njaa ambapo utajisikia kwenda jikoni kutengeneza japo chakula kidogo. Ilimradi tu wakiweza kukufanya utoke mahali pale, wanakuwa wameshakushinda. Wachungaji, ni lazima muwafundishe watu jinsi ya kuomba. Tengeni muda, si tu kwa ajili ya maombi ya juujuu. Mara moja kwa siku, Wakristo wanatakiwa kuwa na muda wa kujielekeza kwa moyo wote kwa Mungu, bila kuwapo kwa kitu chochote cha kuwaharibia umakini wao.

Na k**a watu waking’ang’ana kabisa kwa njia hii ya maombi na kuruhusu kupata mwongozo wa kiroho, kisha wakawa wanaendelea na kuendelea, lazima kitu kitatokea rohoni. Moto utalipuka na kugusa ule mwamba na kuuyeyusha! Kuyeyuka kunapoanza, ni moto sana kiasi kwamba hakuna pepo ambaye anaweza kustahimili. Wala hakuna roho ya mwanadamu inayoweza kustahimili pia. Wote wanakimbia.

K**a mtu atajitoa kuomba kwa bidii na kwa kumaanisha namna hiyo, hatimaye kutafuata kufunguka kwa ulimwengu wa roho. Na mara hili linapotokea, matatizo yote haya katika maombi yanafikia mwisho! [Yaani ule ugumu na ule uzito unakwishilia mbali!] Yule ambaye anakuwa anaomba duniani anakuwa sasa anajisikia kuwa maombi ni kitu kilaini kabisa, cha kuburudisha, na chenye nguvu.

Na nimegundua kuwa wakati huo, huwa tunapoteza kabisa hisia za muda na mambo mengine. Si kwamba tunakosa mpangilio; la hasha! Mungu anakuwa anashughulika na muda wetu. Lakini inakuwa ni k**a unaachilia kila kitu, na unaunganishwa moja kwa moja na Mungu. Maombi yako yanapopenya, kunakuwa hakuna kizuizi tena kuanzia hapo; na mtu anayeomba anaweza kuendelea kwa muda mrefu k**a apendavyo. Hakuna kabisa kizuizi.

Na mara anapomaliza kuomba, lile tundu linabakia wazi.

Kijana huyu pia alisema kuwa, watu wa namna hii wanapomaliza kuomba na kuondoka mahali hapo, lile tundu linakuwa linaondoka pamoja nao. Wanakuwa hawaenendi tena chini ya lile blangeti la jiwe. Wanakuwa wanaenenda chini ya mbingu zilizo wazi. Na akasema kwamba, katika hali hiyo, ibilisi hawezi kufanya kile anachokitaka kwao. Na uwepo wa Mungu unakuwa k**a nguzo kutoka mbinguni ikiwa iko juu ya maisha yao. Wanalindwa; na kunakuwa na nguvu kubwa sana ndani ya hiyo nguzo kiasi kwamba kadiri wanavyotembea huku na kule, uwepo huo unakuwa unagusa hata watu wengine. Nguzo hiyo inakuwa inatambua kile ambacho adui amefanya kwa watu wengine. Na pale watakatifu hao wanapozungumza na watu wengine, na wale watu wakawa wamesimama nao, wanaingia ndani ya nguzo hiyo. Na mradi tu wakiwa ndani ya ile nguzo, vifungo vyote vya adui vinadhoofika.

Kwa hiyo, watu hawa wenye mpenyo huu wa kiroho wanapowashuhudia wenye dhambi habari za Yesu Kristo, upinzani wa wenye dhambi unakuwa wa chini. Ni rahisi kuwaleta wenye dhambi kwa Kristo. Wanapoomba kwa ajili ya wagonjwa, au kwa ajili ya mambo mengine, maombi yao yanakuwa na nguvu sana.

Na k**a kuna sehemu ambako maombi ya namna hii huombwa mara kwa mara, uwepo wa Mungu unakuja mahali pale na hauondoki. Hivyo, hata watu wasiomjua Mungu wanapokuja kwenye sehemu k**a hizo, ghafla vifungo vyao vinakatika.

Na k**a atatokea mtu wa kusema nao kwa uvumilivu na kwa upendo, wanaweza kugeuka haraka sana; si kwa nguvu au kwa uwezo, bali ni kwa Roho wa Mungu, ambaye anakuwa yuko pale. Na k**a hakuna mtu atakayewajali watu hawa, wanakuja kwenye uwepo wake na kujisikia hatia, wanaanza kujadili k**a wakubali au la. Pale watakapoondoka, vifungo vinakuwa na nguvu zaidi kwao. Na ibilisi anajihadi kwa kila njia kutowaruhusu kurudi tena kwenye sehemu k**a hizo.

Je, shetani anakaa kimya tu baada ya mtu kupata mpenyo?

Kijana huyu alisema kuwa, ibilisi anawachukia sana watu wa namna hiyo, yaani wale waliopata mpenyo wa maombi.

Sasa unaweza kupiga picha, sote tulikuwa tumekaa chini tunamwangalia kijana huyu akieleza ushuhuda wake. Alikuwa anatueleza mambo ambayo yeye mwenyewe alikuwa akiyafanya na aliyoyashuhudia kwa macho yake. Alitueleza kile ambacho walifanya kwa watu ambao walipata mpenyo katika maombi. Alisema kuwa waliwaweka akilini sana watu k**a hao. Kisha waliwafuatilia sana na kujifunza kuhusu wao ili kuwajua vizuri. Walitafuta kila kitu kuwahusu. Hivyo, walifahamu udhaifu wao wote, na ikitokea mtu akawashinda kwenye maombi na kupenya, wanawasiliana na wengine kwenye ulimwengu wa giza na kusema, “Mumlenge mtu huyu kwenye eneo hili na hili. Udhaifu wake uko hapa na hapa.”

Kwa kuwa mtu wa aina hii anapotoka nje ya kifuniko cha maombi, roho ya maombi inakuwa juu yake, uwepo wa Mungu upo juu yake, roho yake inakuwa iko juu, na furaha ya Bwana ndiyo nguvu zake; anapokuwa anaenda, adui anajaribu kila njia kuleta yale mambo ambayo yatamvuruga ili asielekeze macho yake kwa Bwana.

K**a, kwa mfano, imeshajulikana kuwa udhaifu wake uko kwenye eneo la hasira, basi adui atasababisha watu watende mambo ambayo yatamfanya akasirike. Na k**a hayuko makini kumsikiliza Roho Mtakatifu, na akaingiwa na hasira, basi ataondoa macho yake kwa Bwana. Na anapokuwa na hasira hivyo, ghadhabu zinamjaa. Baadaye anapokuja kujirudi, anakuwa anataka kutupilia mbali hali hiyo na kuendelea na furaha ya Bwana, lakini anajikuta hajisikii tena ile furaha k**a mwanzo. Anajitahidi kujisikia vizuri tena; lakini haiwezekani tena. Kwa nini? Alipojiachilia kwenye kishawishi cha hasira, mapepo walifanya bidii zote katika muda huo kufunga lile tundu kule juu. Na mara waliporudishia lile jiwe, uwepo wa Bwana unakuwa umekatika, yaani ile nguzo iliyokuwa inatokea mbinguni na kumfunika inakuwa haimfikii tena!

Mtu huyo hataacha kuwa mwana wa Mungu. Lakini ule upako wa ziada uliokuwa unaandamana naye maishani; ule uwepo uliokuwa ukitenda mambo bila yeye kutumia nguvu zozote, unakuwa umekatika! Maana pepo wachafu wanatafuta uliko udhaifu wako.

K**a udhaifu wa mtu ni kwenye masuala ya mapenzi, adui ataandaa watu, matukio, na mambo ambayo yatainua hisia za mtu huyo za tamaa ya kimapenzi. Na k**a mtu huyo atazikubalia hizo tamaa na kufungua akili yake kuyapokea mambo hayo, na kuyalea nafsini mwake, pale anapomaliza kila kitu na kutaka kurejea tena kwenye hali ya upako ili asonge mbele, anakuta kwamba ule uwepo haupo tena. Labda unasema, “Hii si vizuri kabisa.” Kumbuka tu Biblia inasemaje, “ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu. Vaeni dirii ya haki.” Mara nyingi hatuoni haja ya silaha hizi za kivita. Lakini kumbuka Yesu alivyotuambia juu ya namna ya kuomba “Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.”

Kila mara unapopata mpenyo katika maombi, unapofika mwisho, kumbuka kuwa wewe bado ni kiumbe mwanadamu aliye dhaifu. Kumbuka kuwa haujakamilishwa bado. Mwombe Bwana, useme, “Bwana, nimefurahia wasaa huu wa maombi, lakini nitakapotoka nje kwenye dunia, usiniongoze kwenye majaribu. Usiruhusu niangukie kwenye mtego wa ibilisi. Najua kuwa adui anatega mitego kule nje. Sijui ni mitego ya namna gani. Na ninajua kuwa bado mimi ni dhaifu katika baadhi ya maeneo. K**a nikiingia kwenye hali fulanifulani, nitaanguka. Unilinde, Bwana. Unapoona ninaelekea kule ambako kuna mitego niliyotegewa, nifanye nielekee upande mwingine. Uingilie kati, Ee, Bwana. Usiche niende tu kwa nguvu zangu na uwezo wangu. Niokoe na yule mwovu.”

Mungu anaweza kufanya hivyo. Lakini, k**a kuna kitu kibaya kitatokea, ambacho kitakufanya uondoe macho yako kwa Kristo, wewe sema tu, “Asante Yesu.” Ndiyo sababu Mtume Paulo aliandika, “Mshukuruni Mungu kwa kila jambo.” Baadhi ya mambo si mazuri. Yanaumiza, na tunashangaa kwa nini Mungu anayaruhusu yatufikie. Lakini k**a tu tungejua kwa njia hiyo anatuokoa na mambo yapi, tungemshukuru. Tukijifunza kumwamini Bwana, tutamshukuru kwa kila jambo.

Yule kijana aliendelea kusema kuwa, unapopata mpenyo katika maombi, majibu yako ni lazima yatakuja. Alisema kuwa jibu mara zote huja, lakini mara nyingi, huwa halifiki kwa mtu aliyeliomba. Kwa nini? Ni kwa sababu ya mapambano yaliyoko kwenye anga. Pia, majibu yanaweza kuzuiliwa iwapo viumbe waovu wa rohoni watafanikiwa kurejesha ule mwamba na kuziba tundu ambalo mwombaji alifanikiwa kulitoboa kwa njia ya maombi yake.

Kisha aliongea jambo ambalo kwa kweli lilitikisa imani yangu. Binafsi ilinibidi niingie kwenye mfungo wa siku kumi, ili kumwuliza Bwana k**a hilo alilosema lilikuwa na ukweli wowote. Basi sikiliza haya: Kijana huyu alisema kuwa, kila Mkristo anaye malaika ambaye anamtumikia Mkristo huyo. Nasi tunafahamu kuwa Biblia inasema kuwa malaika ni roho wanaotutumikia. (Waebrania 1:14). Alisema kuwa watu wanapoomba, majibu huletwa kwa mikono ya malaika. Malaika huleta majibu, k**a ambavyo tunasoma kwenye kitabu cha Danieli. Kisha alisema jambo ambalo ni gumu sana. Alisema kwamba, k**a yule anayeomba anafahamu silaha za kiroho na amejivika silaha hizo, majibu nayo huja kwa kupitia malaika ambaye, naye amejivika kikamilifu kwa silaha hizohizo.

Lakini, k**a anayeomba hajali silaha za kiroho, basi malaika nao wanakuja bila silaha hizo. Wakristo ambao hawajali kile ambacho kinaingia mawazoni mwao; hawashindani kuangusha mawazo yasiyofaa; malaika wao huja bila chapeo. Silaha zozote utakazoacha kuzitilia maanani duniani, malaika anayekutumikia naye anakuwa hanazo. Kwa maneno mengine, silaha zetu za kiroho hazitulindi miili yetu, bali zinalinda vitu vile vya kiroho tunavyofanikiwa kuvipata kutoka kwa Bwana.

Malaika anapokuwa anakuja, mapepo wanamtazama na kumkagua na kubaini maeneo ambayo hajajifunika; na hayo ndiyo maeneo ambayo watashambulia. K**a hana chapeo kichwani, basi watashambulia kichwani. K**a hana dirii, watashambulia kifuani. K**a hana viatu, watajaribu kutengeneza moto ili kumwunguza miguuni.

Sasa, najua kuwa hili ni gumu kuamini; mimi narudia tu kile ambacho kijana huyu alisema. Kisha tulimwuliza, “Je, malaika wanaweza kuungua moto?” Na unajua alisema nini? Kumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa roho. Hizi ni roho kwa roho zinapambana. Mapambano ni makali sana, na pale wanapomshinda malaika wa Mungu, jambo la kwanza wanalokimbilia ni lile jibu alilobeba; na wanalichukua hilo. Na hizi zinakuwa ni zawadi ambazo hutolewa kwa watu kupitia imani za siri, au uchawi.

Kumbuka kile ambacho Biblia inasema kupitia kitabu cha Yakobo. Vipawa vyote vyema hutoka kwa Mungu (Yakobo 1:17). Kwa hiyo, shetani anapata wapi vitu vizuri anavyowapatia watu? Baadhi ya watu ambao hawawezi kupata watoto, huenda kwa wachawi na waabudu shetani, na wanapata mimba! Mtoto anakuwa ametoka wapi? Je, shetani ni muumbaji? HAPANA! Anaiba kutoka kwa watu ambao hawaombi maombi yao hadi mwisho.

Katika Biblia, Yesu alisema, “Ombeni bila kukoma.” Pia alisema, “atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? ” Je, Yesu atakukuta bado unangojea? Au utakata tamaa na kumwacha adui aibe kile ambacho umekuwa ukikiombea?

Na hawaridhiki tu na kuiba jibu la maombi. Wanataka pia kumweka malaika kifungoni. Na wanaanza kupambana naye. Wakati mwingine wanafanikiwa kumk**ata na kumfunga malaika. Inapotokea hivyo, Mkristo anakuwa k**a chakula chao duniani. Wanaweza kumfanyia chochote maana hana ulinzi tena kwenye ulimwengu wa roho.

Nilimwuliza kijana huyo, “Una maana kuwa malaika anaweza kushikiliwa katika ulimwengu wa giza?” Sasa alikuwa anaeleza uzoefu wake, na akasema, hawatamshikilia malaika kwa muda mrefu kwa sababu ya Wakristo wengine ambao wanaomba mahali pengine. Jeshi la ziada litatumwa, na malaika atakuwa huru. Na k**a yule Mkristo anayehusika hajaomba hadi kwenye mpenyo, basi atabakia mateka. Ndipo shetani atatuma malaika wake na malaika wa nuru kwa mtu huyu, na hapo ndipo uongo na udanganyifu unapotokea; maono ya uongo na unabii wa uongo. Uongozi wa uongo, na kufanya kila aina ya maamuzi mabaya. Na mara nyingi, mtu wa namna hii anaweza kupata mashambulizi na vifungo vya kila aina.

Niliondoka kwenye kile chakula cha jioni huku na mawazo mengi sana. Nikasema, “Bwana, sitaki hata kujaribu kuamini jambo hili.” Linaondoa ujasiri na usalama wangu wote! Nilipoenda kumlingana Bwana, ilikuwa ni kwa siku kumi; na Bwana alifanya mambo mawili. Kwanza, si tu kwamba alithibitisha mambo hayo niliyoyasikia kutoka kwa yule kijana, bali pia alifungua akili zangu zaidi ili kuona mambo mengine mengi zaidi ya yale ambayo niliyasikia. Pili, aliniongoza kuona kile ambacho tunatakiwa kukifanya wakati mambo haya yanapotokea ili tuweze kuwa washindi.

Alinipa mambo matatu:

Moja: namna ya kutumia silaha za vita vyetu vya kiroho. Biblia inaziita silaha za Mungu. Si silaha zetu. Tunapozitumia, tunamruhusu Mungu kupigana kwa niaba yetu.

Mbili: tambua uhusiano wa roho zinazotutumikia, yaani malaika, na maisha yetu ya kiroho. Na ni lazima kuwa makini sana na kile kinachotokea mioyoni mwetu; k**a mwongozo wa kile ambacho kinatakiwa kutokea rohoni kutuhusu sisi.

Tatu: ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hatakiwi kuja k**a mtumishi wetu, kututumikia na kutuletea vitu mbalimbali. Hakimbiikimbii kwa Baba kumweleza kile ambacho tunataka. Hiyo ni kazi ya malaika. Lakini Yeye husimama pamoja nasi. Anafanya nini? Anatuongoza, anatufundisha, anatutangulia, anatusaidia kuomba inavyotakiwa. Na mambo haya yanapotokea kwenye ulimwengu wa roho, anatuambia. Wakati mwingine anakuamsha usiku na kukwambia, “Omba.” Wewe unasema, “Hapana! Muda wangu haujafika.” Na anasema, “Omba sasa!” Kwa nini inakuwa hivyo? Ni kwa sababu Yeye anaona kila kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Wakati mwingine anasema, “Kesho ni kufunga.” Wewe unasema, “Hapana, nitaanza Jumatatu!”

Lakini kumbuka kuwa Yeye anaelewa kile kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho. Ni lazima tujifunze kuwa makini na Roho Mtakatifu. Anatuongoza kwenye njia za haki. Wapendwa, tuishie hapa. Labda wakati mwingine tutaongea jinsi ambavyo tunaweza kuomba hadi kupata mpenyo, maana sasa tunajua mapambano yaliyoko rohoni na jinsi ya kupenya; na namna tunavyoweza kudumu tukiwa na mpenyo tuliopata. Na mara tunapojifunza hili, linakuwa ni jambo la furaha sana. Tukumbuke tu jambo moja: vita si vyetu, bali ni vya Bwana! Haleluya!

Hebu tusimame. Mwangalie mwenzio machoni na utafakari ni mara ngapi amekosa kile ambacho Mungu alikiandaa kwa ajili yake. Lakini shikaneni mikono k**a inawezekana; watu wawili au watatu, kisha tu muambiane, “Hakuna haja ya kushindwa tena! Tunaweza kushinda! Iko nguvu ya kutosha kushinda! Yesu tayari ameshafanya kazi yote.” Muombeane ninyi kwa ninyi ili Bwana aweze kutusaidia kushinda. Hatutakiwi kushindwa. Iko neema ya kutosha; nguvu ya kutosha kuleta ushindi!

Asante Yesu.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

MAOMBI YA KUVUNJA MAAGANO NA KUFUTA VIAPO VINAVYOTESA MAISHA YAKO
TABIA ZA WANA WA MUNGU
Tabia za wana wa Mungu. Sehemu ya 2

Website

Address


Dar Es Salaam
14110
Other Religious Centers in Dar es Salaam (show all)
Neema Gospel Choir Neema Gospel Choir
Dar Es Salaam, 2550766777288

🌍Gospel Music Choir - WORSHIP & PRAISE🎤 🏆Award Winning - Best Gospel Music Group East Africa 2021

Moravian Kipunguni B Moravian Kipunguni B
Kipunguni B
Dar Es Salaam

HUBIRI KWELII ,SIMAMIA KWELI, FUNDISHA NA KUITENDA KWELI

amos.marko.37 amos.marko.37
Dar Es Salaam

WOKOVU NI SASA KWA WANAOTAMBUA NYAKATI

Sheikh Hamza Rajab Abuu Seif Sheikh Hamza Rajab Abuu Seif
Dar Es Salaam

karibu katika Mawaidha na Darsa mbalimbali

Kagimbo Kagimbo Kagimbo Kagimbo
Dar Es Salaam, KGB198900

Family matters

Lemonde d'aujourd'hui Lemonde d'aujourd'hui
Numérl Whatsapp:+255625(07254
Dar Es Salaam

Huu Ndio Uislamu Huu Ndio Uislamu
Dar Es Salaam

Huu Ndio Uislam - Hii ni Mobile App ambayo inamrahisihia muislamu kufahamu dini yake kwa urahisi, kusoma vitabu mbalimbali, kusikiliza na kutazama video za masheikh mbalimbali.

Mungu nijibu Mungu nijibu
Erick Mbazendore
Dar Es Salaam, 222444

Wokovu upo kwa YESU pekee Wokovu upo kwa YESU pekee
0754890965
Dar Es Salaam

Tujifunze kwa pamoja jinsi gani Mungu anakuthamini wewe mwanadamu, hata akadiriki kumtoa mwanawe wa pekee Yesu ili aje akutoe katika dhambi na mateso ya shetani. Ni upendo wa ajabu...

Kinondoni Revival Choir Kinondoni Revival Choir
Kinondoni
Dar Es Salaam

Kinondoni Revival Choir is choir ministrering in KR Church, Kinondoni Assemblies of God.

Pastor Monday Adonu Pastor Monday Adonu
Dar Es Salaam

assurance deliverance prayer call and be bless +2348129729572 or+255679697220

FPCT Mlimani FPCT Mlimani
Mawasiliano
Dar Es Salaam