Occupational Safety and Health Authority - OSHA
OSHA ni Wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu).
Taasisi hii ina wajibu wa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vilivyopo katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusabisha magonjwa na ajali. Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi ( OSHA) ilianzishwa inchini mwaka 2001 chini ya Sheria Na. 30 ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997 k**a sehemu ya Mpango wa Maboresho katika utoaji wa Huduma za Serikali kwa wananchi. Makusudi ya kuanzishwa kwa OS
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda akiwa na wakuu wa taasisi za Umma na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa kwa washiriki wa mkutano kwenye Hotel ya Gran Melia, Mkutano huo wa ulifunguliwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 28 jijini Arusha, mkutano huo ambao umeandaliwa na Msajili wa Hazina, umeongozwa na kauli mbiu isemayo"Mikakati ya Taasisi na Mashirika kuwekeza Nje ya Tanzania" umewakutanisha Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma na Wenyeviti wa Bodi.
Mtendaji Mkuu Bi khadija Mwenda akiwa na baadhi ya Viongozi wa TUGHE Taifa pamoja na Mkurugenzi mkuu wa ATE Bi Suzane Doran Ndomba kwenye Semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya TUGHE, semina inayofanyika jijini Arusha
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi khadija Mwenda akiwa na Watumishi na Viongozi wa TUGHE tawi la OSHA kwenye Semina ya Waajiri na Viongozi wa TUGHE, Semina inayofanyika jijini Arusha, ambapo OSHA imetoa mada iliyowasilishwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA kuhusu dhana ya Usalama na Afya mahali Pa kazi. Aidha picha na 2 na 3 ni baadhi ya watumishi wakifuatilia mawasilisho hayo.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda wa Kwanza Kulia akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa TUGHE Cde Hery Mkunda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ATE Bi. Suzane Doran Ndomba kwenye hafla ya ufunguzi wa Semina ya waajiri na wafanyakazi nchini inayofanyika jijini Arusha.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Chama cha Waajiri nchini ATE Bi. Suzane Doran Ndomba kwenye ufinguzi Semina ya Waajiri na Wafanyakazi nchini inayofanyika jijini Arusha
OSHA YAWAKUMBUSHA WAAJIRI, WAFANYAKAZI UMUHIMU WA USALAMA NA
AFYA KAZINI
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umeelezea umuhimu
wa kulinda uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika rasilimali watu
kuanzia kipindi watu wanapozaliwa, kulelewa, kupata elimu na kuajiriwa au
kujiajiri katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Umuhimu huo umeelezwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija
Mwenda, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu masuala ya Usalama na
Afya kazini katika semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) inayofanyika Jijini
Arusha kuanzia Agosti 26 hadi 29, 2024.
Kiongozi huyo Mkuu wa Taasisi ya OSHA amesema hadi kufikia hatua ya mtu
kuwa na ujuzi fulani na kuajiriwa ama kujiajiri, serikali inakuwa imewekeza
kwa kiwango kikubwa ikiwemo kugharamia huduma za afya tangu utotoni
pamoja na kumpatia elimu ya kumwezesha kupambana na mazingira yake.
“Serikali yetu inawekeza fedha nyingi katika kuwahudumia watu wake tangu
akina mama wanapokuwa wajawazito, wanapojifungua na kulea Watoto wao
ikiwemo kuwapatia elimu katika ngazi tofauti,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa
OSHA na kuongeza:
“Kwa mantiki hiyo serikali inategemea kupata faida ya uwekezaji uliofanyika
katika watu wake (return on investment) kupitia watu hao kushiriki katika
shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kipindi kirefu. Jambo ambalo
litawezekana tu endapo wafanyakazi katika sehemu za kazi watalindwa dhidi
ya vihatarishi vya magonjwa, ajali na vifo vinavyoweza kutokea katika
sehemu za kazi.”
Hivyo, Mtendaji Mkuu wa OSHA ametoa wito kwa waajiri na wafanyakazi
kuhakikisha kwamba katika sehemu zao za kazi kunakuwa na mifumo
madhubuti ya usalama na afya ikiwa ni Pamoja na kuzingatia taratibu zote
muhimu za usalama na afya k**a inavyoelekezwa na wataalam kutoka
katika Ofisi yake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUGHE, Bw. Joel Kaminyoge, ameeleza
jinsi wanavyoshirikiana na OSHA katika kutoa elimu ya masuala ya usalama na afya kwa waajiri na wafanyakazi nchini hususan wanachama
wa TUGHE.
Mkufunzi wa OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu dhana nzima ya usalama na afya kazini kwa ustawi wa afya ya mfanyakazi katika kongamano la Wahandisi Wanawake linalofanyika Ukumbi wa JNICC Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahandisi Wanawake kutoka Taasisi ya OSHA wakifuatilia kwa karibu matukio na mada mbalimbali katika kongamano la Wahandisi Wanawake linalofanyika Ukumbi wa JNICC Dar es Salaam.
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umeshiriki Kongamano la 9 na Maonesho ya Wahandisi Wanawake (TAWECE) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wataalam wake ambao ni wahandisi wanawake wamehudhuria kongamano hilo kwa lengo la kuendelea kubadilishana uzoefu na wahandisi wenzao kutoka sekta mbalimbali za umma na binafsi.
Aidha, OSHA imewasilisha mada kuhusiana na dhana nzima ya usalama na afya kazini kwa ustawi wa afya ya mfanyakzi katika shughuli mbalimbali za wahandisi pamoja na kushiriki maonesho yanayofanyika sambamba na kongamano hilo kwa minajili ya kuendelea kulishirikisha kundi hilo muhimu la wahandisi taratibu muhimu za usalama na afya mahali pa kazi hususan katika shughuli za kihandisi.
OSHA imefadhili kongamano hilo la siku mbili (Agosti 21 na 22) kutokana na mahusiano mazuri baina yake na Taasisi ya Wahandisi Nchini katika kulinda nguvukazi inayotumika katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo viwanda na miradi ya ujenzi.
Siku ya Kinadamu duniani, Humanitarian day, OSHA imeshiriki kwenye maadhimisho hayo yaliofanyika Jijini Dar es salaam Agosti 19
MATUKIO KATIKA PICHA
Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ambapo OSHA ilifanya wasilisho kuhusu utendaji wake.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akifanya wasilisho kuhusu utendaji wa OSHA katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa wakifuatilia wasilisho la Naibu Waziri, Mhe. Katambi katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi, akifanya wasilisho mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu maboresho ya kanuni za Igonomia na Mazingira ya Kazi ambayo Kamati hiyo ilielekeza yafanyike.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Kushoto) akifuatilia wasilisho la Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi, kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Kamati hiyo yaliyotolewa Oktoba 2023.
KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NDOGO YAIPONGEZA OSHA KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umewasilisha maboresho ambayo yamefanyika katika kanuni mbili za usalama na afya mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.
Maboresho hayo ambayo yamefanyika katika kanuni za Igonomia na Mazingira ya Kazi yalishauriwa kufanyika na Kamati hiyo katika kikao chake cha Oktoba 26, 2023 baada ya OSHA kuwasilisha kanuni hizo mpya mbele ya Kamati hiyo.
Wasilisho hilo limefanywa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi, ambaye alimwakilisha Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete. Katambi ameambatana na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa na Watendaji wengine wa Wizara na Taasisi ya OSHA.
Mhe. Katambi ameiambia Kamati kuwa mapendekezo yote yaliyotolewa ikiwemo kujumuisha tafsiri ya neno Mamlaka pamoja kuondoa maudhui yanayojirudia katika kanuni hizo yameshughulikiwa ipasavyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) pamoja na Taasisi ya OSHA kwa kupokea na kutekeleza maagizo ya Kamati yake.
Aidha, ameahidi Kamati yake kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi chini yake katika kuwahudumia Watanzania kupitia ushauri na maelekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha utendaji wa Serikali.
Wakati huo huo, OSHA imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na kufanya wasilisho kuhusu utendaji wa Taasisi hiyo ambapo Mtendaji Mkuu, Bi. Khadija Mwenda, ameieleza Kamati hiyo umuhimu wa kulinda nguvukazi ya Taifa kupitia uimarishaji wa mifumo ya usalama na afya katika sehemu za kazi.
“Hadi inapofika hatua ya mtu kuajiriwa k**a mfanyakazi serikali inakuwa imewekeza rasilimali nyingi sana kwake kuanzia anapozaliwa, kukua, kusoma hadi kuajiriwa hivyo inakuwa ni hasara kubwa kwa Taifa endapo mfanyakazi huyu atapata ulemavu au kupoteza maisha kabla ya kutoa mchango wake wa kutosha katika uzalishaji,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa OSHA
Tunachokifanya OSHA ni kushauri na kusimamia maeneo ya kazi kuweka mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya magonjwa pamoja na kulinda mitaji ya wawekezaji ili kuleta tija katika uzalishaji pamoja na kulinda ustawi wa wafanyakazi.”
Akihitimisha mjadala wa wajumbe wa Kamati hiyo ya Bajeti baada ya wasilisho la OSHA, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Oran Njeza, amesema Kamati yake itaendelea kutoa ushauri unaolenga kuboresha utendaji wa Serikali ikiwemo Taasisi ya OSHA.
OSHA YATOA MAFUNZO KWA UMOJA WA WANAHABARI NCHINI
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetoa mafunzo kwa wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Nchini (JOWUTA) kwa lengo kuwajengea uelewa wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.
Mfunzo hayo yamefanyika leo (Agosti 16) katika Ofisi za OSHA zilizopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam yakiwa yamejumuisha washiriki takribani 100 kutoka katika Vyombo vya Habari vya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akifungua mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema mafuzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taasisi ambao miongoni mwa malengo yake makuu ni kuongeza uelewa wa wadau mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama na afya kazini.
“Miongoni mwa changamoto za usimamizi wa masuala ya usalama na afya kazini ni pamoja na uelewa mdogo wa masuala husika miongoni mwa wadau wetu na wananchi kwa ujumla. Hivyo, ili kushughulikia changamoto hiyo tumeona ni muhimu tukawa na utaratibu maalum wa kuwafikia wadau wetu kwa njia ya mafunzo,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa OSHA na kuongeza:
“Mwezi Aprili tulikutana na wahariri na sasa tumeona ni wakati mwafaka kukutana nanyi ikiwa ni mwendelezo wa kuyafikia makundi mbalimbali ya wadau wetu. Kimsingi kwakuwafikia wanahabari tunaamini kwamba tutapata tija kubwa kwani mbali na kuwawezesha kupata uelewa wa jinsi ya kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia kanuni bora za usalama na afya, mtatusadia sana kutoa elimu kwa wananchi kupitia kalamu zenu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JOWUTA, Bw. Musa Juma, ameishukuru Taasisi ya OSHA kwa kuona umuhimu wa kulifikia kundi la wanahabari ambao nao wanakabiliwa vihatarishi vya usalama na afya katika kazi zao k**a wafanyakazi wengine.
Mafunzo hayo ya waandishi wa habari yalihusisha mada mbalimbali zikiwemo; Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Utambuzi na udhibiti wa vihatarishi vya usalama na afya mahali pa kazi pamoja na utoaji wa huduma ya kwanza mahali pa kazi.
Pamoja na mafunzo darasani ya nadharia, wanafunzi wetu hupewa fursa ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kujionea uhalisia wa kile kinachofundishwa darasani, hapa ni wanafunzi wa mafunzo ya Risk assesment yanayoendelea jijini Dar es salaam, wakiwa katika moja ya mafunzo kwa vitendo jijini Dar es salaam, mafunzo haya ya usalama na afya mahali Pa kazi hutolewa na OSHA pekee kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya www.osha.go.tz kujua mafunzo tunayotoa.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwan Kikwete akipata maelezo ya namna ya matumizi ya vifaa vya ukaguzi kwenye banda la OSHA, kwenye maadhimisho ya Siku Vijana Kimataifa iliyofanyika Agosti 12, 2024 Jijini Dodoma, maadhimisho hayo ambayo yamehudhuriwa na Vijana wapatao 3000 yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, kauli mbiu ya mwaka huu ni Vijana na matumizi ya Fursa za kidijitali kwa maendeleo endelevu.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda Akiwa na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Wilaya ya Kilosa, kwenye halfa ya Uzinduzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi Wilayani Kilosa mkoani Morogoro, Uzinduzi uliofanywa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Heri ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane.
Bado tupo Viwanja vya Nane nane Nzuguni Dodoma na John Mwakangale Dodoma, bado hujachelewa karibu tukuhudumie, upate elimu, ushauri kuhusiana na msauala ya Usalama na Afya sehemu yako ya kazi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akitembelea Banda la OSHA kwenye Maonesho ya Nane nane Viwanja vya Nzugu Mkoani Dodoma
Je una maswali au ushauri, karibu tutakusikiza na kukuhudumia, Tupo Nane Nane Mbeya Viwanja vya John Mwakangale na Nzuguni Dodoma, bado hujachelewa tembelea mabanda yetu kupata mengi zaidi.
Njoo upate elimu sahihi ya Matumizi ya PPE ili kujikinga na vihatarishi sehemu ya kazi.
Njoo jifunze kuweka mifumo ya Usalama na Afya katika eneo lako la kazi. Maonesho ya Wakulima Nane nane Nzuguni Dodoma na John Mwakangale Mbeya
Njoo upate elimu ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi
Karibu usajili eneo lako la kazi, Viwanja vya Nane Nane Dodoma na Mbeya.
Karibu tukuhudumie, upate elimu ya Usalama na Afya, tupo Viwanja vya Nane nane Nzuguni Dodoma na Viwanja vya John Mwakangale Mbeya.
Baadhi ya Wananchi wakiendelea kupata elimu kuhusu masuala ya Usalama na Afya mahali pa Kazi kwenye Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, ambapo Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) inashiriki kwenye Maonesho ya Nane nane Mkoani Mbeya na Dodoma
Click here to claim your Sponsored Listing.
Videos (show all)
Contact the organization
Telephone
Website
Address
Ikungi Street
Dar Es Salaam
Opening Hours
Monday | 08:00 - 15:30 |
Tuesday | 09:00 - 15:30 |
Wednesday | 08:00 - 15:30 |
Thursday | 08:00 - 15:30 |
Friday | 09:00 - 17:00 |
686 Old Bagamoyo Road, Msasani
Dar Es Salaam
The U.S. Mission to the United Republic of Tanzania. Terms of Use: https://www.state.gov/tou
55 Ali Hassan Mwinyi Road, East Upanga
Dar Es Salaam, 3272
We offer Wildlife Safaris to all National parks of Tanzania, Tailor-made safaris, Camping safaris, H
Dar Es Salaam, 255
Tour operators based in Dar es Salaam and Arusha, offering safaris to all Tanzania destinations
Bahari Beach
Dar Es Salaam, 14122
bibowildnet.africa �It is based on wild issues �wild photographing �Promoting afican tourism especially Tanzania � #Visitzanzibar � #Visittanzanianationalparks � #tanzaniaunforgett...
Dovya B
Dar Es Salaam
Maneno, Nasaha, Hekima na Mafunzo ya Mtume Mohamad {s.a.w.w} pamoja na kizazi chake kitukufu {Ahlubait a.s}
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam, 16102
best wishes filled an empty heart. bad wishes filled the dieing heart. stay awaken😳