La Familia Movies
fahamu kuhusu filamu, tamthilia, na kadhalika za duniani. Tazama kilicho bora kabisa.
Triumph (2021)
iMDb: 5.8
Genre: Drama
Runtime: 1h 40mins
Rating: PG13
Starring: RJ Mite, Terrence Howard, Jonathon Schaech, Colton Haynes, na wengine
Storyline: hizi ndio zile filamu ambazo unapenda kuangalia na familia ikajifunza kitu kizuri namna ya kuishi na watu wa makundi maalum katika jamii yetu hiiihii kwani na wao ni watu k**a sisi na wanastaili kupewa nafasi katika kila nyanja ikiwemo michezo.
Hapa utafurahia mchezo wa masumbwi miaka hio ya 80 ulivyokuwa muhimu katika kuleta matumaini ya ndoto za mafanikio kwa kijana Mike, ambaye alizaliwa akiwa na mtindio wa ubongo kwa kukosa oksijeni ya kutosha pindi tuu alipozaliwa..
Utakachokifurahia zaidi katika filamu hii ni vile Terrence Howard alivyozinasua zile speeches zake za kimarekani na kuendana vilivyo na maudhui ya humu ndani.
Nimependa pia kumuona, Colton Hayes, huyu alitamba kwenye Arrow k**a sidekick wa Green arrow, jamaa anajua alafu anajua tena...maana ameigiza vizuri sana k**a kaka mwema na rafiki mzuri sana, licha ya utanashati alionao
Maadili humu ndani ni ya kiwango cha juu mno, maana kuanzia lugha, mavazi, na maudhui kwa ujumla ni ya kiwango cha juu,
Ninashauri inapaswa kuangaliea na rika la watu wote na inahamasisha jamii youote ile funiani kuishi vyema na kila mtu, pasipo kumchukulia udhaifu wake wa kimwili au akili.
NB: steringi haumwi wala hana tatizo lolote lile la afya ya akili, usidanganyike, jamaa anajua sana kuigiza yaani😂😂😂😂
Enjoy.
Coming Soon, well, its here!
Long awaiting movie kuhusu biography ya Bob Marley ni hii apaaa
An Affair To Die For (2019)
iMDb: 4.8 (2,140)
Genre: Horror, Thriller
Runtime: 1h 22mins
Stars:
Directed by Victor Garcia
PG-16 (18+)
Synopsis: Mke anamcheat mume, na mume mwingine anamcheat mkewe. utundu utundu na akili nyingi zinapelekea familia zote mbili zijikute kwenye fiasco, msala usio na mwenyewe.
Stori inahusu wanandoa. K**a umeoa na unawaza kumcheat mumeo/mkeo, nakushauri uitazame hii filamu, maana utajifunza mengi zaidi namna gani ujanja wa kucheat unavokuaga jau.
ili kutoharibu spoilers, ni filamu ambayo hutochoka kuiangalia, ingawa ina rates ndogo mno. rangi inavutia na matukio yamerekodiwa kwa ustadi mkubwa kwelikweli, kiasi cha kutoamini k**a imeshutiwa maeneo mawili tuu, jijini Sofia hukoo, nchini Bulgaria.
Binafsi nimeipenda, na k**a una muda wa kupendelea Thriller, hii utaipenda sana. Scene za kutisha sidhani..maana sijaziona hata...au kwa sababu ndio kwenye thriller zenyewe...maana mi kiukweli sizielewagi filamu za kutisha na wala sinaga mpango nazo, kwa kweli..
Enjoy.
True to the Game (2017)
iMDB: 5.1
Genre: Crime, Thriller
Runtime: 1h 48mins
Rating: R
Starring: Columbus Short, Vivica A. Fox, Erica Peeples na wengine
Sroty ya hii movie, well, huenda napenda kuangalia filamu za watu weusi zaidi, nimeipenda sana.
jinsi mlolongo wake ulivyo (screenplay) umefanana mno na TV Movie, na hauchoshi kutazama.
speed ilivyoanzia ndio hivyoivyo inavyokolea na kumalizia, ni moja ya filamu tamu mno nilizoweza kutazama za crime/Drama maana tunajua jinsi filamu za aina hiyo zinavyoumizaga vichwa na kuboa.
connection iliyopo kati ya Columbus Short na Erica Peebles haielezeki, na kamera imewapenda hivyoivyo walivyo
nimekuja kugundua kuwa hata wao waliliona hili ndio maana wakaamua kutengeenza sequels zake, maana ipo ya pili (2020) na ya tatu (2021).
sijaboreka kuitazama wala kusimama, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Vivica Fox was amazing, k**a sio yeye.
ZIpo baadhi ya scenes za Nudity, chache mno na violence kidogo, so, ni vyema ukatazama kwa wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Enjoy!
You Got Served (2004)
iMDb:3.8
Genre: Drama, Music (Dance)
Runtime: 1h 35mins
Rating: PG-13
Network: Sony (Screen Gems)
Starring: Omarion, Marquest Houston, Meagan Good, Jennifer Freeman, Steve Harvey na Lil Kim, of coz na wengineo.
Story za Kudance na kushake shake zinajulikana, zipo na vibe flani hivii la kipekee. nimeiangalia hii movie late coz sikupataga bahati ya kuishuhudia miaka hio.
Mzigo waliopiga Omarion na Marquest houston sio poa, na kumbe Steve Harvey mambo zake za TV Shows hajaanza leo kutawala jukwaa😂😆
nlipenda alivyomleta yule LAPD Cop kwa mikwara ili alinde dola 5000 za ushindani😂😂
wow, Meagan Good is bae tangu kitambo, ndani humu unaona kabisa alivyokua na njaa ya kutaka kuwa leading character, maana kamfunika kila kitu Jennifer Freeman..
all in all ni filamu nzuri ya kupotezea mida coz editing yake ni ya kawaida sana, maana kuna fade in na faded to blacks kibaaaao aisee😂😂😂😂
sijaona matusi, wala lugha chafu, maadili yamezingatiwa vilivyo kwa kijana wa miaka 12, na kuna sehemu chache mno za watu ku kiss, na ni nzuri kuangalia na madogo.
Enjoy
Encanto (2021)
IMDB: 7.2
Genre: Animation, Comedy, Family, Fantasy and yes! Musical
Runtime: 1h 42 mins
Network: Disney+
Rating: PG
Starring: Stephanie Beatriz, María Cecilia Botero, John Leguizamo na wengine
Story: well, wote tunajua mambo ya Disney. story flani hivii ya watoto, teens na hamu ya kuwa na maajabu.
nimeifurahia filamu hii na haijaniboa hata kidogo kwa sababu story yake inatembea straigh bila longolongo.
Vfx effects na animations za hao waingiza sauti zinavutia mno,
Jared Bush, Byron Howard na Charise Castro Smith wamefanya kazi ngumu na nzuri ya kuandika, kuandaa na kuongoza filamu hii.
naskia wakulungwa walizama Colombia mwaka 2018 k**a watalii ili kutafuta sehemu halisi inayoweza kuendana na story yao/idea.
baada ya kunogewa na kazi nzima iliyoandikwa, Disney wakaamua kuajiri wataalamu wa muziki kutoka Colombia ili waulete uhalisia wa Muziki na utamaduni wa huko tangu hatua za awali za maandalizi ya filamu hii.
ingawa muziki haujatawala sana kwenye hii filamu kuliko filamu zingine za Musical (wakereketwa nadhani mtakubaliana na mimi) ule uhalisia wa kushik**ana na utamaduni wa muziki wa colombia maarufu k**a madrigal umesadifiwa vilivyo, hasa kwenye wimbo wa We dont talk about Bruno-no-no-noo
anyway, enjoy!
Father Stu (2022)
iMDb: 6.5
Genre: Biography, Drama
Runtime: 2h 04mins
Rated R movie
Written & Directed by Rosalind Ross
Starring: Mark Wahlberg, Mel Gibson, Teresa Ruiz, Jacki Weaver na wengine
Story: hii filamu imetoka aprili mwaka huu na nikaaambiwa kua mwamba Mark Wahlberg (na namkubali sana tangu enzi hizo, hadi mambo ya Uncharted, Spencer confidential etc) amenenepa ili tuu aendane uhusika na sroty nzima..nikadokezwa kua jamaa aliongezea mpunga wa ziada ili filamu iwe kali zaidi,...well, noma.
Story ni simple sana, na inavutia kwa uhalisia wake, kisa cha mwanamasumbwi aliyetaka kuwa msanii wa holywood akaishia kubatizwa (kuokoka) na kuwa mkatoliki, na kunoga kulipozidi akaamua kua padre!
Yes, hii ni story ya kweli ya jamaa mmoja anaitwa Stuart Long, na jamaa alitokewaga kweli na Bikira Maria na Yesu mwenyewe pasipo (stu) kujua!
Anyway, fanya uitafute kisha uangalie uwezo na nia ambayo Mark ameionesha kwenye kazi hii, maana hata mimi ninadhani mwamba amepania kupata oscar ya mwakani, yeye na Mel Gibson.
Kuna lugha chachechache za kihuni ndio maana imekuwa rated R, lakini inafaa kuangalikika na rika zote.
TeresaRuiz kaua, Mel Gibson fundi kacheza kidogo tuu lakini moto wake hauzimiki, jamaa anajua alafu anajua tena. Nikimsifia sana Mark Wahlberg mtasema nampigia debe, fanya kuitafuta kisha uiangalie.
NOTE: Andaa yai, maana..😂😂😂bila subtitles mwanangu, unaeza usitoboe😂😂😂😂
Enjoy!
Tom Clancys: Without Remorse (2021)
iMDb: 5.8
Genre: Action, Thriller
Runtime: 1h 49mins
Rated R movie
Amazon Original Movie
Directed by: Stefano Sollima
Starring: Michael B. Jordan, Jodie Turner-Smith, Jamie Bell, Guy Pearce,Lauren London na wengine
Story: nikuambie tuu kuwa mi ni Shabiki mzuri mno wa Michael B. Jordan na hapa k**a kawaida, hajakosea kitu.
jamaa anajua namna ya kukufanya uendelee kutamani kumuangalia, na alivyocheza pia mwanadada Lauren London, man, nimemmis sana kumuona tena kwenye filamu mwanamama huyu, bado still uzuri wake hauchuji yaani, na ile sumaku kwa kamera, phenomenal.
kwa ufupi tuu nikudokeze kuwa Lauren London ndio yule sista aliyechezaga movie ya ATL (2006) na T.I miaka ileeeh🤩🤩 na ndio chuma kilichomtoa vizuri sana, then pia kwa madea, na hata Series ya Single Ladies, etc
hii movie imepata reviews za chini huko iMDb kwa sababu mbalimbali lakini ujue tuu kuwa penye wajuaji wengi napo ni matatizo tuu..so, yah, tazama kwanza kisha ndio ufuatilie huko
story nzuri inasisimua, na hakuna picha mbaya, inaangalikika na vijana hata watoto wadogo, ila ukubali tuu kuona milipuko na mabunduki kwa sana
enjoy!
The Marksman (2021)
IMDb: 5.6
Genre: Action, Adventure
Runtime: 1h 48mins
PG-13
Directed by: Robert Lorenz
Story: flani hivii ya La familia.
Liam kashaanza kuzeeka, ndio maana hizi filamu zinaanza kumpendeza zaidi, maana jinsi alivyokuwa anamjali na kumlea mtoto ni ile kabisaa hood ya mtoto na mjukuu au kitukuu...najua unaelewa nikisema hivi😂😂
nimependa maafui walivyoigiza na kucheza poa, hasa yule aliyefiwa na mdogo ake, kafanya good mno...mno.
yamekuwa ni maisha halisi ya Dunia ya sasa yenye watu salama na wapole dhidi ya watu wabaya.
k**a una familia, hii ni filamu nzuri ya kutazama na mwanao au watoto wadogo wengi nyumbani, maana hakuna hata kipande kimoja utakachohofia😂😂na nina uhakika madogo hawatoboreka.
Enjoy😇
ARQ (2016)
iMDb: 6.4
Genre: Action, Sci-Fi, Thriller
Runtime: 1h 28mins
TV-MA
Netflix
Written & Directed by: Tony Elliot
Starring: Robbie Amell, Rachael Taylor, Shaun Benson na wengine
story ya hii movie...hivi unajua ushawahi kuangalia movie unahisi unaielewa ila unafikia kipindi hauelewi lakini unan'gan'gania tuu kuangalia?😂😂 ndio hii sasa🤣🤣
kisa flani hivii cha inayofanywa na mashine, the arq.
kadri unavyoiangalia hii filamu zaidi ya mara moja ndio unaielewa vizuri na kujua kuwa kila neno la script na kwenye story lina maana yake.
ila nikuambie kitu...akili nyingi nazo huondoa maarifa...enjoy.
Safety (2020)
iMDb: 6.9
Genre: Biography, Drama, Sport
Runtime: 2h na 2mins
PG
Network: Disney
Directed By: Reginald Hudling
Stars: Jay Reeves, Thaddeus J. Mixson, Corrine Fox, and others
Story: mzigo wa disney wa kimyakimya, na una moto wake wa kipekee wa kimyakimya, wa kisa cha kweli, cha jamaa alieenda college, na akaishi na mdogo wake mambo yalipomuwia magumu..kiasi cha kubambwa na kocha wake wa michezo.
Nimependa utulivu wa waigizaji wote, matumizi madogo ya miziki na makelele ya sound effects, mavazi ya wahusika wote wa ray na fahmarr yanaonesha dhahiri umasikini wanaoupitia, yaani...
Ni masaa mawili ambayo hautayajutia, ila k**a ukiiangalia mchana au usiku mwingi ni lazima usinzie😂😂
Haters wengi wanalalamikia kuwa hii filamu imekaaa kishabiki mno, hao wa Clemenson, na hakuna cha ziada😂😂
Anywwy, Enjoy
Dating & New York (2021)
iMDb: 5.1
Genre: Comedy, (Romance)
Runtime: 1h 31mins
PG 13: (16+)
Written & Directed by: Jonah Feingold
Stars: Eva Victor, Jerry Ferarra, Catherine Cohen na wengine
Story: hii ni lovestory ya wapenzi waliokutana kwenye match app, na kujitungia visheria vya kipuuzi vya kuwa na mahusiano pasipo kufanya mapenzi wala kushikana mikono, kisa wapo singo, so, wawe single wenye furaha.😂😂
Yah, tunajua wote mwisho wa siku nini kinafuata.
Nimefurahia jinsi alivyoigiza, anajua sana, ingawa jamaa yetu kuna muda amekuwa k**a sloppy flani hivii..siez mlaumu coz ye ni comedian..😄😄
Hii ni filamu ambayo hata teens wanaeza angalia, hasa wa sasa coz utajifunza perks za mwanzo kabisa za mahusiano, na kujua maana halisi ya neno 'ghosting'
anajua sana kuchekesha, hata k**a haumuelewi, utakubali tuu baadae, jokes zake za kisayansi nimezikubali sana, so funny🤣🤣
Ni filamu flani hivii ya kuchangamsha macho..so..yah
Enjoy.
Charm City Kings (2020)
IMDB: 6.7
Genre: Drama
Runtime: 2h 5mins
Directed by: Angel Manuel Soto
Starring: Jahi Di'Allo Winston, Meek Mill na wengine
PG Rating: Rated R movie (16+)
Network: Warner Max
Story: maboss wakiwa Jada pinkett smith na Will Smith, hakunaga kazi mbovu hapaa.
Nilipomalizia kuangalia na kusikia wimbo wa dmx ule wa Ruff Ryder anthem ndio sasa nikaelewa vizuri lengo la kufanyika kwa movie hii mwaka husika.
K**a unapenda filamu za wamarekani weusi zikiwaasa maafili na namna wanavyopambana na vurugu za kutoka, hii ni filamu nzuri sana kwako.
Na k**a unapenda bikes🚴♂️🏍 utaenjoy sanaa...tena sana...maana kuna freestyles zile zenyewe, like a pro rider.
Kuna kitu kuhusu huyu kid anayeigiza, nilimuona kwenye kazi moja ya netflix mwaka juzi hivii, namuona tena hapa....well, next time nitamgusia kwa undani.
Story ipo lit, kafanya unyama wa maana kwenye kuigiza, so real yaani..
Anyway, wenyewe wameilalamikia kuwa dogo ameigiza soft sana kuliko wenyeji wa baltimore walivyo, but, hey, who cares anyway..
Enjoy
From straight A's to # # # (2017)
IMDb: 5.2
Genre: Biography, Drama
Runtime: 1h 27mins
Directed by: Vanessa Parise
Starring: Halley Pullos, Sasha Clements, Jessica Lu na wengine.
PG Rating: 18+
Story ya hii film ni ya kiduanzi sana. ina idea mpya sana kwenye jamii nyingi za hapa duniani, kuwa mdada ameutazama feminism kwa dhana tofauti na ya kipekee mno, mno.
Kwa ufupi, mdada maarufu k**a belle knox aliamua kuigiza filamu za kikubwa ili alipe ada ya chuo mwaka wake wa kwanza.
Dogo ni smart na ana akili sana, ila amejipa double character na kujisomesha kwa njia mbadala, kitu ambacho wengine wamekiona k**a sio sawa kijamii.
Filamu nzima ina mtazamo chanya wa dunia ya sasa ya nchi zilizoendelea, na kuleta hoja mpya.
Huko mtajua wenyewe, ila sista ameigiza poa sana kwenye upande wake.
Hii filamu imekosolewa saana kwa kutofuata story halisi na imeleta hoja mpya, so, chochote walichofanya waandaaji kukufanya uuone pia mtazamo wao kwa njia chanya, ni wao..watajiju.
Nimeiweka hapa coz ninajua ni tatizo la jamii k**a sio sasa, basi linakuja.
So, enjoy, huku ukijua kuwa tahadhari ni muhimu..
Status Update (2018)
IMDB: 5.8
Genre: Comedy,Fantasy, Romance
Runtime 1h 45mins
Directed by Scott Speer
Rating PG-13
Starring: Ross Lynch, Olivia Holt, Courtney Eaton, Harvey Guillen na wengine kibaaao
Story: High school Movie
Wote tunajua movies za high school zilivyo, musical, drama za hapa na pale, ila ninatoa pongezi kwa comedies zilizopo humu, nimecheka mpaka nimehisi mbavu kuuma🤕😂😂
Story ya kifala sana, eti jamaa amepata app ambayo inaitwa YOUniverse, ukipost chochote kile, kinakua..🤣🤣
Na jamaa lilivyo jinga, linapost tuu, mpaka simu ilipombomokea na kuvunjika kioo🤣🤣
K**a unaelewa 'zee zee zee' hata kiduchu, hii movie utacheka mpaka ujikojolee, maana vituko vilivyo mbele ndio vikali zaidi ya vile vya mwanzoni😂😂
Anyway, wasiopenda mambo ya kishuleshule wataona miyeyusho ila nimeenjoy kila sekunde ya mapenzi, comedy na hio fantasy nzima ya kupata wishes kwa kutumia app.
Enjoy!
The 15:17 to Paris (2018)
IMDB: 5.3
Genre: Biography, Drama, Thriller
Runtime: 1h 34mins
PG-13
Directed by: Clint Eastwood
Starring: humjui hata mmoja..so..yah😒
Story ya hii filamu ina ukweli asilimia mia. Inahusu jambo lililotokeaga kwenye treni ya umeme ikitokea Amsterdam na kuelekea Ufaransa, na gaidi mmoja alipanda akiwa na nia ya kuua abiria wote.
Sasa, kwa kuwa filamu haina ufundi mwingi, ze dairekta aliamua kuita wahusika wakuu (Anthony Sadler, Alek Skarlatos na Spenser Stone) waliofanya ushujaa kwenye shambulio hilo. Unaambiwa kiukweliukweli, aliyemdondosha yule gaidi pale ni Raia wa Ufaransa, ila aliipiga chini tuzo ya heshima kutoka kwa serikali ya Ufaransa kwa kuhofia migongano kati yake na jamii ya uislamu ya Nchini ufaransa, so kaomba tuu aendelee kuwa k**a mtu asiyejulikana, na kuwapa wamarekani wengine waliomsaidia kujizolea maujiko yote
Hii inasemekana kuwa ndio filamu mbovu zaidi katika zile filamu za mwamba Clint Eastwood, kitu ambacho nimeona si cha kweli.
Katika biography films zote nilizowahi kuangalia (ingawa ni chache) hii nimeona na kuuelewa utofauti wake.
Kwanza ni filamu fupi kuliko zote za zee dairektaa, pia Uhalisia wa kuigizwa upo so natural, no drama at all, so original, na hii ni kwa sababu wameigiza wahusika wakuu, kwa namna rahisi mno...ingawa script imeandikwa kishamba sana, sijajua kwanini.
Its true, kwa filamu ambayo story yake ni inafaa kuwa dakika tano au kumi hivii, tunapaswa kumpongeza kwa dhati ze dairekta kwa kwenda kuumua story sehemu zingine, ingawa inaweza kuhamisha wazo kuu.
Ndugu mwandishi humu ndio kazingua kutuchanganyia madesa ya dini, siasa, jamii na makorokocho mengine bila kuwa na umakini wa kutosha.
Msiseme namsifia sana ze dairekta, ila mjue tuu kuwa kibabu kina miaka 91 sasa na kashabeba Oscars tatu na vituzo vingine zaidi ya 157, akishindana kwenye nafasi zaidi ya 280 hukoo..
So, hata akikosea, huna haki ya kumkosoa, coz makosa yake ni burudani tosha kwa wengine hasa wanaojua..enjoy!
Red Notice (2021)
IMDB: 6.3 (watu 222,689)
Genre: Action, Comedy
Runtime: 1h 58mins
Starring: Dwayne Johnson, Ryan Reynolds, Gal Gadot, na wengine.
PG Rating: PG-13
Network: Netflix
Story: kiufupi, hii ndio movie iliotazamwa kuliko zote kwa wenye Netflix zao, na kiufupi tuu, director ndugu
Ambaye pia ameandaa na kuandika mzigo wote huo ametisha kweli kuwachezesha hao vinara watatu kwa sasa.
Ndio maana hii movie imegombaniwa sana, tena saana na makampuni makuvwa ya filamu huko holywood, alafu kidedea akaja kuibuka universal, ambaye kamuuzia Netflix😂😂
Anyway, leo siongelei story, maana najua utaiona tuu, utake usitake..
Washkaji wamekula dola milioni 20 kila mmoja hapo juu, kizembe tuu yaani...
Enjoy..
The Virtuoso (2021)
IMDB: 4.5
Genre: Action, Thriller
Runtime: 1h 50mins
Starring: Anson Mount, Abbie Cornish na Anthony Hopkins
PG rating: R rated
Story: Katika kazi alizotengeneza prodyuza hii ni mojawapo ya kazi kali na niliyoipenda, yah, coz ameandika mwenyewe na kuongoza pia mwenyewe, ndio maana ametupa ladha moja ya kishkaji sana na ya ukweli mno, mno.
katisha sana, kaigiza vizuri sana hadi mi mwenyewe nimepagawa🤩🤩 anajua😍😍
Story nzuri kweli, ingawa ilivyoanza anza inawachuja watu wengi kwa mikwara yake ya ki-sniper😄😄
Nasubiria kwa hamu sequel yake, sijajua la produza anafikiria nini, ila natamani sana, tena sana kumuona akifanya yake mwakani, mbele ya fundi ambaye ulimwengu mzima unajua kuwa jamaa hakosei hata iweje.
Mi binafsi naunga mkono hoja, sijajua unaonaje? Iendelee au isiendelee?
Oh yah, furahia story ya mapenz kidogo😂😂 action kidogo🙂🙃 Msisimko kidogo😄😄 na kuboreka kidogo😂😂 k**a wewe sio kauzu🤣🤣🤣
Enjoy. Wastue na wana wa-follow tuongezeke..
Dirty Little Saint (2019)
IMDB: 5.7
Genre: Drama, Romance
Runtime: 1h44mins
Starring: Jordan Lane Spice, David A. Gregory, na Luke Guldan, Matt Magnusson na wengine
Network: Passionflix
PG Rating: R rated
Story: Filamu nzuri sana k**a unaishi katika mapenzi, kuna mengi ya kujifunza na kuyafahamu, ku-enjoy.
Waigizaji ni wa kawaida sana, na wamejitahidi kuigiza kiuhalisia kabisaa kuendana na maisha halisi (real life) na ni lazima utafurahia kuiangalia, kuliko zile movies feki za holywood zenye fantasy nyingi.
Kila kilichofanyiwa kazi humu ni maisha halisi kwenye jamii za watu wote, ndio maana utaona sometimes waigizaji k**a wamekuwa sloppy hivii, huenda wamefanya kwa makusudi au ni maalum uwezo wao umeishia hapo, na imependeza sana, tena sana.
Binafsi nimefurahia kila dakika niliyoangalia, ingawa sexy scenes zimekuwa a bit sloppy, (chache lakini).
Enjoy.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Videos (show all)
Contact the establishment
Telephone
Website
Address
2, Tanya, Yombo Dovya
Dar Es Salaam
Opening Hours
Monday | 09:00 - 21:30 |
Tuesday | 09:00 - 21:30 |
Wednesday | 09:00 - 21:30 |
Thursday | 09:00 - 21:30 |
Friday | 09:00 - 21:30 |
Saturday | 09:00 - 21:30 |
Sunday | 09:00 - 19:30 |