Universal Human Development - Uhuden

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Universal Human Development - Uhuden, Non-Governmental Organization (NGO), Zanaki Street, Dar es Salaam.

Universal Human Development (UHUDEN), is a Non-Government organization established under section 12 (1) of the NGO Act No. 24 of 2002, of the United Republic of Tanzania.

I am Here to Network! 11/08/2023

I am Here to Network! Learning from one another is a great way to move forward together

Juma’s Substack | Juma Killaghai | Substack 10/08/2023

Juma’s Substack | Juma Killaghai | Substack My personal Substack. Click to read Juma’s Substack, by Juma Killaghai, a Substack publication. Launched 4 minutes ago.

11/08/2022

Umaskini na utajiri ni dhana mbili ambazo zinategemea jinsi akili zetu zilivyoandaliwa. Nchi tajiri ni tajiri kwa sababu sehemu kubwa ya watu wao ni matajiri na nchi maskini ni maskini kwa sababu sehemu kubwa ya wananchi wao ni maskini. Tofauti ya tajiri na maskini iko katika jinsi wanavyofikiri.

Wanaofikiri inavyotakiwa wanakuwa matajiri na wanaofikiri kinyume na inavyotakiwa wanakuwa maskini.

PITCH VIDEO FOR PRINCE ZAYED SUSTAINABLE PRIZE 01/07/2022

UHUDEN's program area spans many sectors. One of the most important sector is the sector of health and wellness. Non Communicable Diseases (NCDs) are causing a serious health problem. Each year 41 million people are killed by NCDs around the globe. The world economy also loses about 2.1 trillion dollars because of poor productivity. At UHEDEN we think this problem needs to be handled differently. Focusing on drugs and other medical procedures is not working. A better approach is to educate the people on how they can avoid NCDs

PITCH VIDEO FOR PRINCE ZAYED SUSTAINABLE PRIZE The video articulates the problem we want to solve, the solution we are proposing, the impact of our solution and why we think we should win the prize,

02/06/2022

Why we think Non Communicable Diseases are a big problem and what needs to be done to lessen the problem

29/04/2022

TABIA ZETU NI K**A KIWANDA CHA KUZALISHA UMASKINI!

Kuna tabia ukizikumbatia basi jiandae kuwa ndani ya mduara wa umaskini usio na mwisho.

Miongoni mwa tabia hizo ni:

1. Kuwa na matumizi makubwa kuliko mapato, hususan yale matumizi yanayohusu vitu ambavyo havina ulazima.

Kutumia pesa ambayo ungeweza kuigeuza kuwa mtaji kununua vitu ambavyo wala huvihitaji, ni kukaribisha umaskini usio na sababu.

Moja ya hatua za awali kabisa katika kujiondolea umaskini ni kujizuia kufanya manunuzi ya vitu ambavyo hatuvihitaji.

2. Kutojifunza mbinu mbalimbali za kuwa na pato zaidi ya moja..

Watu wengi tunaishi kwa pato moja halali ambalo aghalabu halitoshelezi mahitaji yetu.

Kwa sababu ya kutowekeza muda kujifunza mbinu za kupata mapato ya ziada ambayo ni halali au tunaishi maisha yenye dhiki kubwa, au tunafidia pale palipopungua kwa wizi au rushwa. Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa watumishi wa umma na hata wale wa sekta binafsi.

Ufumbuzi wa tatizo hili ni kutenga mbinu kujifunza mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kujiongezea pato la halali.

3. Kuendekeza ubinafsi..

Moja ya mambo ya kushangaza sana ni tofauti kubwa kati ya tabia za matajiri na tabia za maskini kuhusiana na suala zima la kujinyanyua kiuchumi.

Matajiri ndio wanaoona thamani ya kushirikiana kuliko maskini. Dhana ya masoko ya hisa na mitaji kimsingi iliasisiwa na matajiri kwa sababu hiyo. Hapa matajiri wanawashirikisha wananchi wa kawaida kuweka mkono wao kwenye shughuli za kibiashara zinazofanywa na matajiri hao.

Kuweza kuwa na mtaji wa kutosheleza mahitaji muhimu ya uzalishaji na kukua kibiashara siyo jambo jepesi. Kupitia masoko ya mitaji na hisa matajiri hutumia mauzo ya hisa (vipande vya karatasi vilivyopewa thamani fulani) kukusanya mtaji mkubwa wa kufanya shughuli zao ziende kwa ulaini.

Katika kuwashirikisha watu wa kawaida matajiri wanazidi kujiongezea utajiri, huku maskini katika ubinafsi wao, wakizidi kujiongezea umaskini!

Katika dunia ambayo mantiki inafanya kazi, ilitakiwa iwe kinyume chake. Maskini wako wengi. Wingi wao ni nguvu ambayo ikitumika vizuri inaweza kuleta matokeo ya kustaajabisha.

Hebu tutazame mfano huu. Mchezo wa 'merry go round', maarufu kwa jina la 'mchezo' au upatu huku kwetu, unatufunza jinsi ambavyo watu wa chini wanaweza kutumia nguvu ya wingi wao, kupindua meza dhidi ya umaskini wao.

Kwa mfano, mkiwa watu 100 na mkakubaliana kuchangishana, mathalani shilingi 5,000 kwa siku, kila mmoja wenu atakuwa na utajiri wa shilingi 500,000.00 ndani ya siku mia moja tu!

Ndani ya miezi 10 kila mwana mchezo atakuwa na uwezo wa kumiliki shilingi 1,500,000.00, au kundi lote kwa pamoja kumiliki shilingi 150,000,000.00!

Hawa jamaa wakiamua kuwekeza kwenye kilimo kuna uwezekano mkubwa kwamba ndani ya miaka 3 - 5 wanauaga kabisa umaskini!

Huu ni mfano tu. Ziko aina nyingi za kushirikiana zinazoweza kusaidia sana kuondoa umaskini kwenye jamii.

Moja ya hizo njia ni ile ya kila tajiri kumiliki taasisi ya hiari (foundation) ya kusaidia watu wenye sifa kutekeleza ndoto zao za kiuchumi.

Kulundika pesa benki huku zikipoteza thamani kidogo kidogo kila siku kutokana na mfumuko wa bei huko nje ya kuta za benki, siyo njia nzuri ya matumizi ya hizo pesa.

Pesa inatakiwa izunguke; itumike kuzalisha pesa nyingine zaidi. Kila mwaka kila tajiri anayemiliki foundation akichukua sehemu ya faida aliyopata kwenye biashara na vitega uchumi vyake, na kuitia kwenye foundation yake ili iwafikie watu wengine wenye sifa, siyo tu kwamba atakuwa amefanya kitendo chenye thawabu kubwa kwa Mungu, lakini pia atakuwa amefanya kitendo kikubwa sana cha kuijenga nchi!

Hebu fikiria kila mwaka Mo Dewji, Said Bakhresa, Rostum Aziz, na wengine kila mmoja atoe bilioni 2 na kuitumbukiza kwenye kibubu cha foundation yake. Wakipatikana matajiri kumi maana yake ni kwamba kila mwaka kuna bilioni 20 za kuwasaidia Watanzania wanaopigania ndoto zao za kiuchumi.

K**a kibubu cha pamoja kitatoa shilingi milioni 5 tu kuwekeza kwa kila atakayefikia vigezo, hapo tunaongelea wanufaika 4,000 kwa mwaka.

Ikiwa robo tu ya hawa ndio watakaofanikiwa kuwa na biashara endelevu, bado nchi itakuwa imenufaika kwa kiasi kikubwa kupitia ajira zitakazotengenezwa pamoja na kodi itakayolipwa.

Jamani tuigeni kwa wenzetu. Kwa mfano, Wamarekani wangekuwa k**a sisi, leo mtu k**a Mark Zuckerberg, tajiri namba 10 duniani, ambaye utajiri wake unafikia dola bilioni 89.9, huenda bado angekuwa anahangaika kutafuta namna ya kuifanya kampuni yake changa ya Facebook idumu na kukua, huku wenye pesa zao wakiwa wamezikumbatia bila hata kujua kiasi walicho nacho!

Zuckerberg kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake kadhaa wa chuo kikuu cha Harvard walianzisha mtandao wa Facemash mwaka 2003, uliokuwa unawalenga wanafunzi wa Harvard pekee. Hata hivyo mtandao huo ulifungiwa na chuo hicho baada ya muda wa siku mbili tu, kwa madai ya kukiuka utaratibu.

Wakati mtandao huo unafungiwa tayari ulishasajili zaidi ya wanachama 450 na hivyo kutoa taswira juu ya kukubalika kwa wazo lililouanzisha.

Mwezi Januari 2004 Zuckerberg alisajili mtandao mwingine kwa jina la Facebook. Huu mtandao mpya ulifungua milango kwa wanafunzi wa vyuo vingine vya Marekani na ilipofika mwezi Juni 2004 tayari ulikuwa na wanachama wanaofikia 250,000 kutoka zaidi ya vyuo 34 vya Marekani.

Mwaka 2005 kampuni ya Facebook ilifungua milango kwa wanafunzi wa vyuo vyote duniani; na mwaka 2006 ikaruhusu watu wote waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 13 duniani kujiunga. Hivi sasa mtandao wa Facebook una wanachama wanaozidi bilioni 2.9 duniani kote!

Wamarekani ni watu waliojijengea utamaduni imara wa kushikana mkono pale fursa inapoonekana. Mwaka huo wa 2004, tajiri muasisi wa kampuni ya Paypal, Peter Thiel, aliona fursa iliyokuwemo ndani ya Facebook. Aliamua kuwa mwekezaji wa kwanza mkubwa kwa kutoa dola laki tano na kununua umiliki wa 10% ya kampuni. Mwaka 2012 Thiel aliamua kuuza sehemu kubwa ya hisa zake za Facebook. Mauzo ya hizo hisa yalimpa kiasi cha dola milioni 400!

Leo, miaka 18 baada ya Zuckerberg kupewa dola laki tano, Zuckerberg ni jina kubwa duniani. Huwezi kumiliki dola bilioni 89.9 halafu dunia isikujue.

Watanzania tubadilikeni. Tujifunze kushirikiana kwa dhati ili tuondekane na umaskini. Siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Juhudi za kundi kubwa la watu kwa pamoja zina ufanisi mkubwa zaidi ukilinganisha na juhudi za kila mtu peke yake, kivyake vyake.

25+ Best Free Online Education Sites (2022 List) 24/04/2022

HAKUNA MAENDELEO YA KWELI BILA ELIMU!

Wanafalsafa wanasema elimu ni ufunguo wa maisha. Hawajakosea! Ni ukweli mtupu.

Tatizo ni kwamba elimu ina gharama. Kuna wengi wanaitamani lakini hawawezi kumudu gharama.

Hata hivyo kuna taasisi nyingi zinazotoa elimu bure kabisa kwa njia ya mtandao, ikiwemo vyuo vikuu.

Link ifuatayo inataja taasisi bora kabisa zaidi ya 25 duniani ambazo zinatoa elimu bure kwa njia ya mtandao.

https://www.guru99.com/free-online-education-sites.html

25+ Best Free Online Education Sites (2022 List) Sites For Free Online Education helps you to learn courses at your comfortable place. The courses of these websites are offered by top universities. You can learn a specific subject without much inves

Here Are The Top 7 Websites For Free Online Education 24/04/2022

HAKUNA MAENDELEO YA KWELI BILA ELIMU!

Wanafalsafa wanasema elimu ni ufunguo wa maisha. Hawajakosea! Ni ukweli mtupu.

Tatizo ni kwamba elimu ina gharama. Kuna wengi wanaitamani lakini hawawezi kumudu gharama.

Hata hivyo kuna taasisi nyingi zinazotoa elimu bure kabisa kwa njia ya mtandao, ikiwemo vyuo vikuu.

Link ifuatayo inataja tovuti 7 bora kabisa duniani ambazo zinatoa elimu bure kwa njia ya mtandao.

https://www.forbes.com/sites/zackfriedman/2019/05/29/free-online-education/?sh=1086cc2e342b

Here Are The Top 7 Websites For Free Online Education Here's how to get access to top-rated, online courses - for free.

9 Top Universities Offering Free Online Courses 24/04/2022

HAKUNA MAENDELEO YA KWELI BILA ELIMU!

Wanafalsafa wanasema elimu ni ufunguo wa maisha. Hawajakosea! Ni ukweli mtupu.

Tatizo ni kwamba elimu ina gharama. Kuna wengi wanaitamani lakini hawawezi kumudu gharama.

Hata hivyo kuna taasisi nyingi zinazotoa elimu bure kabisa kwa njia ya mtandao, ikiwemo vyuo vikuu.

Link ifuatayo inataja vyuo vikuu 9 bora kabisa duniani ambavyo vinasomesha baadhi ya course bure kabisa.
https://www.topuniversities.com/student-info/distance-learning/9-top-universities-offering-free-online-courses

9 Top Universities Offering Free Online Courses Find out how to access free online courses from Harvard University, MIT and many more.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Why we think Non Communicable Diseases are a big problem and what needs to be done to lessen the problem

Address

Zanaki Street
Dar Es Salaam
11105

Opening Hours

Monday 09:00 - 05:00
Tuesday 09:00 - 05:00

Other Non-Governmental Organizations (NGOs) in Dar es Salaam (show all)
Art in Tanzania Art in Tanzania
Umoja Road Block 2Q, Madale Village
Dar Es Salaam, 23333

Art in Tanzania - a self-sustainable NGO helping communities in Tanzania.

Lalji Foundation Lalji Foundation
Morani House
Dar Es Salaam

The Lalji Foundations pledges to give back to the community and improve lives.

Education For Disabled Tanzania Education For Disabled Tanzania
NSSF Road St, Bagamoyo Road
Dar Es Salaam, 14121

We are a non-profit organization, our main goal is to change lives of youths, children and those in

Stop TB Tanzania Stop TB Tanzania
Mikocheni
Dar Es Salaam

Tanzania joining other countries to start STOP TB chapter in Tanzania aiming to comply with Moscow de

Vijana Na Ujana Vijana Na Ujana
Dar Es Salaam

yowedfoundation2019 yowedfoundation2019
Mbezi Luis Mwisho, Makao Makuu
Dar Es Salaam

Nantambelele niokoe foundation Nantambelele niokoe foundation
CHANIKA
Dar Es Salaam

� DENY CHILD ABUSE � RIGHTS AND EQUALITY TO ALL Children �

Romme love justice Romme love justice
Sam Nujoma/Lufungira Road
Dar Es Salaam

ROMME Love Justice Tanzania, an anti Human Trafficking organisation is a member of TANAHUT.

Zeal for Care Organization Zeal for Care Organization
Majumba Sita
Dar Es Salaam

helping people with great needy

Da Tabu Foundation Da Tabu Foundation
P. O. BOX 20950
Dar Es Salaam, 12113

social activists who fight against violence and sexual violence and provide education to the community "Wanaharakati wa kijamii Tunaopambana kupinga ukatili na unyanyasaji wa kiji...

Mwangaza Tanzania Mwangaza Tanzania
Dar Es Salaam

Women Mean Business Women Mean Business
Pieta Lane, Masaki
Dar Es Salaam

Women Mean Business program aims to equip start-up women-owned SMEs by enhancing their business development skills and impacting entrepreneurial values.