Afro Farmers Care Foundation

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afro Farmers Care Foundation, Non-Governmental Organization (NGO), Ubungo, Dar es Salaam.

14/04/2018

Can Intensive Home-Site Farming Change the Face of Farming of Tanzania and other developing Countries!?

Photos from Afro Farmers Care Foundation's post 04/12/2017

Rain season is here again. Work has begun at the farm. Those who labour in sorrow, reap with joy. Suffering in many cases is self choice. All the best to other farmer.

Photos from Lagran Group Tanzania's post 25/10/2017
03/10/2017
02/10/2017
02/10/2017

Agriculture and Rural development holds the key to mitigate the problem of migration n hunger, provided the confidence of our farming and Rural community is restored and they are made to think that they are the real game changers, without their efforts zero hunger will be a distant dream. They need technological support, infrastructure Development, access to better educational n health Care system.

Agriculture and rural development are vital to addressing the root causes of migration.

19/09/2017

MBOGA KILIMO

Photos from Mkulima Young's post 19/09/2017
31/08/2017
Timeline photos 03/08/2017

Zipo tafiti mbalimbali zinazoeleza kuwa tunda hili huleta nafuu kwa wagonjwa wa saratani (cancer). Ni tunda lenye ladha nzuri linalopendwa na watu wa rika zote. Ni moja ya mazao ambayo wakulima wengi hawalipi kipaumbele k**a zao linaloweza kuleta kipato kizuri. Je, umeshaiona fursa ya kulima zao hili? Anza leo, tajirika kesho

Photos from Afro Farmers Care Foundation's post 03/08/2017

Mazao ya aina mbalimbali yenye tija ya kibiashara. Mkulima makini ni yule anayejikita kwenye kilimo chenye tija bila kufuata mkumbo. Tafakari zao la kulima kabla. Zijue changamoto zake. Jua soko lilipo. Na mwisho kabisa tumia mwanya wa kilimo kujikwamua kimaisha. Kilimo ni utajiri uliojificha chini ya ardhi. Anza leo, tajirika kesho.

Photos from Afro Farmers Care Foundation's post 16/06/2017

SHAMBA DARASA, MOROGORO

01/06/2017

Habari ndugu msomaji wetu wa makala za kilimo, Natumaini tunaendelea vizuri na mapambano ya kila siku. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vitu vya msingi kwanza, na natumaini ukimaliza mfululizo wa makala hizi utakua mkulima hodari wa nyanya. Kila kitu lazima kiwe na msingi imara, karibu tujifunze wote:

Utangulizi:
• Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia k**a zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa k**a zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni k**a; Malawi, Zambia na Botswana.
Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.

Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.

Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.

Mazingira

• Hali ya Hewa:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu k**a vile Baka jani chelewa n.k.)

• Udongo:
Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.

Aina za Nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)

Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida
Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.

Kuandaa Kitalu cha Nyanya

Mambo muhimu ya kuzingatia:
Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
Eneo la kitalu k**a ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
• Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.

Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya

Aina ya matuta:
matuta ya makingo (sunken seed bed)
matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
matuta ya kawaida (flat seed beds)

Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].
Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.

Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu

1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);
matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
Matuta haya hayatuamishi maji k**a mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.

Hasara:
o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo k**a hayakutengenezwa vizuri.

2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):
Faida:
matuta haya ni rahisi kutengeneza
hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
nyevu mdogo unaopatikana ardhini
ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
huzuia mmomonyoka wa ardhi

Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
mvua nyingi.

3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):

Faida:
ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
na kusambazwa mbegu huoteshwa
ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu

Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.

Kusia Mbegu
Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.

Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi k**a vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini

Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni
Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.

Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
Rules)
Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishik**ane vizuri na udongo.
Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.

Maandalizi ya Shamba la Nyanya
Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. K**a ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.

Jinsi ya kupanda miche:
Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani
Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.
Asante sana:

Timeline photos 10/05/2017
Photos from Kinasoru East Africa Tanzania Ltd's post 02/05/2017
Timeline photos 19/04/2017

Oceans are an important source of food. They host 80% of the planet’s biodiversity, and are the largest ecosystem on Earth.

Timeline photos 14/04/2017

Biodiversity is essential for food security and nutrition.

Photos from Afro Farmers Care Foundation's post 30/03/2017
Making climate-smart agriculture the norm | CIAT Blog 30/03/2017

Making climate-smart agriculture the norm | CIAT Blog “Climate-smart agriculture requires a carefully tailored package of interventions, developed in unison with farmers”

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Ubungo
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 12:00

Other Non-Governmental Organizations (NGOs) in Dar es Salaam (show all)
TAMASHA VIJANA TAMASHA VIJANA
Sinza Lufungira, Mbogo Street, House No. 12
Dar Es Salaam

TAMASHA-vijana translates to “Celebrate Youth!” something that we are passionate about

Art in Tanzania Art in Tanzania
Umoja Road Block 2Q, Madale Village
Dar Es Salaam, 23333

Art in Tanzania - a self-sustainable NGO helping communities in Tanzania.

Lalji Foundation Lalji Foundation
Morani House
Dar Es Salaam

The Lalji Foundations pledges to give back to the community and improve lives.

Education For Disabled Tanzania Education For Disabled Tanzania
NSSF Road St, Bagamoyo Road
Dar Es Salaam, 14121

We are a non-profit organization, our main goal is to change lives of youths, children and those in

Stop TB Tanzania Stop TB Tanzania
Mikocheni
Dar Es Salaam

Tanzania joining other countries to start STOP TB chapter in Tanzania aiming to comply with Moscow de

Vijana Na Ujana Vijana Na Ujana
Dar Es Salaam

Universal Human Development - Uhuden Universal Human Development - Uhuden
Zanaki Street
Dar Es Salaam, 11105

Universal Human Development (UHUDEN), is a Non-Government organization established under section 12

yowedfoundation2019 yowedfoundation2019
Mbezi Luis Mwisho, Makao Makuu
Dar Es Salaam

Nantambelele niokoe foundation Nantambelele niokoe foundation
CHANIKA
Dar Es Salaam

� DENY CHILD ABUSE � RIGHTS AND EQUALITY TO ALL CHILDREN � DISABILITY IS NOT A CHALLENGE FOR A CHILD

Romme love justice Romme love justice
Sam Nujoma/Lufungira Road
Dar Es Salaam

ROMME Love Justice Tanzania, an anti Human Trafficking organisation is a member of TANAHUT.

Youth On Top Youth On Top
6 Guinea Road, Osterbay
Dar Es Salaam

We prepare, inspire and empower the youth in achieving their full potential thereby living a successful and productive life there upon become agents of change

Zeal for Care Organization Zeal for Care Organization
Majumba Sita
Dar Es Salaam

helping people with great needy