Medical Stores Department (MSD)

MSD is annually audited by CAG and has fully-fledged competent internal audit Unit that oversees internal controls effectiveness.

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by the public health services as the Ministry of Health may fr

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 30/08/2024

Watekinolojia wa dawa wa MSD wanashiriki mkutano mkuu wa chama cha wateknolojia wa dawa Tanzania (TAPHATA), unaofanyika mkoani Morogoro kuanzia tar 28 - 30 Agosti 2024.

Akifungua mkutano huo Mfamasia Mkuu wa Serikali Ndg. Daudi Msasi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin O. Mollel amewakumbusha wanataaluma hao kuendelea kuzingatia misingi ya taaluma yao, na kuwataka kuwa mahili katika utekelezaji wa majukumu yao

Msasi ameongeza kuwa Wateknolojia Dawa hao wakifanya kazi kwa kuzingatia misingi ya ufamasia itapelekea kuboreka kwa huduma za afya nchini na kupunguza malalamiko na changamoto nyingine kwenye mfumo wa utoaji huduma za afya nchini.

Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu, inasema "wateknolojia dawa nguzo muhimu katika huduma bora za dawa nchini pamoja tunaweza.

MSD imeruhusu Watekinolojia dawa wake kutoka makao makuu na kwenye kanda zake kushiriki mkutano huo kwa lengo la kujumuika na wenzao ili kubadilishana ujuzi na weledi.

Aidha mkutano huo unawakutanisha watekinolojia dawa mbalimbali nchini kuzungumza na kukumbushana majukumu yanayohusu utoaji huduma katika tasinia hiyo.

.78

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 30/08/2024

Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kitengo chake cha Uhakiki Ubora imeendelea na zoezi lake la ufuatiliaji wa ubora wa bidhaa za afya ambazo imeshazisambaza kwa wateja wake (Post Marketing Surveillance (PMS). Lengo la zoezi hili ni kulinda afya za watumiaji kwani kuna changamoto nyingi kwenye mnyororo wa ugavi wa dawa zinazoweza kuathiri ubora wa bidhaa za afya ikiwemo namna ya usafirishaji, utunzaji na hali ya hewa kwenye maeneo yao.

Kaimu Meneja wa Kitengo cha Uhakiki Ubora Estella Meena amesema zoezi hili linaisaidia MSD kufahamu changamoto ambazo wateja wa MSD wanakutana nazo pale wanapokuwa wanatumia bidhaa za MSD. Meena ameongeza kuwa Utekelezaji wa zoezi hili ni muongozo uliotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na ushauri wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) kuitaka MSD k**a msambazaji wa bidhaa za afya nchini kufuatilia ubora wa bidhaa ambazo tayari zipo kwa wateja wake.

Zoezi hili linafanyika kwa awamu ambapo awamu hii linahusisha Wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Iringa, Mbeya, Dodoma na Tabora ambapo wateja wa Hospitali za Rufaa za Kanda (ZRH), Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospital za Wilaya, Vituo vya Afya, pamoja na Zahanati zilizopo kwenye mikoa hiyo zitatembelewa.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 29/08/2024

Katika muendelezo wa vipindi vya elimu kwa umma, Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tabora Bw.Rashid Omar na Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD Bi. Etty Kusiluka, wameshiriki mahojiano kupitia kipindi cha Darajani, kinachorushwa na kituo cha radio cha Uyui FM cha Mkoani Tabora, kueleza majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na MSD kanda ya Tabora, sambamba na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa fedha uliokwisha (2023/2024)

29/08/2024

Picha
Katika muendelezo wa vipindi vya elimu kwa umma, Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tabora Bw.Rashid Omar na Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD Bi. Etty Kusiluka, wameshiriki mahojiano kupitia kipindi cha Darajani, kinachorushwa na kituo cha radio cha Uyui FM cha Mkoani Tabora, kueleza majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na MSD kanda ya Tabora, sambamba na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa fedha uliokwisha (2023/2024).

28/08/2024

Picha
Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tabora Bw.Rashid Omary na Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD Bi. Etty Kusiluka, leo wameshiki kipindi maalum cha Elimu kwa Umma, kwa kueleza majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na MSD kanda ya Tabora, sambamba na mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa fedha uliokwisha.

Kipindi hicho cha elimu kwa umma kimerushwa mbashara kupitia kipindi cha Meza Huru, kinachorushwa na redio ya kijamiii ya Voice of Tabora ( VOT FM) ya Mkoani Tabora.

28/08/2024

Pongezi kutoka MSD

22/08/2024

Kwa miaka 30 sasa, tunajivunia kuwafikia watanzania kote nchini, iwe mijini, vijijini, visiwani, mabondeni, milimani, tunawafikia, kwani dhamira yetu ni moja tu, nayo ni maisha.

Tuambie wiki hii umekutana na magari au gari yetu sehemu gani?

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 21/08/2024

MSD imekabidhiwa tuzo ya shukrani na Hospitali ya Temeke kwa kutambua maboresho ya huduma zake ikiwemo huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo na upatikanaji wa dawa muhimu uliofikia asilimia 98.

Akikabidhi tuzo hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dkt. Joseph Kimaro amesema wanaishukuru MSD kuendelea kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati hasa mashine 10 za kusafisha damu (Dialysis).
"Mashine tumeshazifunga na tumeanza huduma kuanzia mwezi wa 6 mwaka huu. Kwa sasa tuna wagonjwa 18 wanapata huduma hapa kwa bei nafuu ya shilingi 150,000 kwa wale wanaolipa papo kwa papo." Amesema Dkt.Kimaro

Dkt. Kimaro ameongeza kuwa, pamoja na huduma ya kusafisha figo MSD imeiwezesha huduma ya upatikanaji dawa muhimu kufikia asilimia 98% na kupunguza malalamiko kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma hospitalini hapo.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya MSD Dar es salaam Bi. Betia Kaema amesema kumekuwa na maboresho makubwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Bi Kaema aliongeza kuwa Huduma ya Kusafisha figo ni moja ya kipaumbele cha MSD. Kwa Miaka miwili nyuma tumekuwa tukihudumia hospital tano na sasa tumeiwezesha Hospitali hii ya Temeke. lengo letu ni kuhakikisha wateja wetu wote wanaweza kutoa huduma hii kwa bei za chini ili kuwawezesha watanzania kupata huduma hii kwa bei wanazoweza kuzimudu.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 20/08/2024

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Mhe. Elibariki Kingu amesema wameridhishwa na utendaji wa MSD ukilinganisha na hapo nyuma, na kuiomba serikali kukamilisha sehemu ya mtaji wa MSD iliyobakia kuiwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Pamoja na kuipongeza Menejimenti ya MSD kwa maboresho ya kiutendaji,Mwenyekiti huyo
ameiagiza MSD kuendelea kuhakikisha mifumo ya kiutendaji ya Wizara ya Afya na ile ya MSD inasomana ili kuongeza uwazi katika mnyororo mzima wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.

Mhe. Kingu ametoa maelekezo hayo mbele ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Menejimenti ya Bohari ya Dawa kilichofanyika katika kumbi za Bunge, jijini Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema upo umuhimu wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na pamba, hivyo kampuni Tanzu ya MEDIPHAM ya MSD iharakishe uanzishwaji wa kiwanda hicho mkoani Simiyu.

Katika wasilisho lake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema utimizaji wa mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya umeimarika kutoka asilimia 75 mwaka 2022/23 kufikia asilimia 86 kwa mwaka 2023/24. Ameongeza kuwa MSD imefanikiwa kusambaza bidhaa za afya kwa muda uliopangwa kwa wastani wa asilimia 93.

20/08/2024

Waswahili husema maisha ni safari, na wakaenda mbali na kusema safari ni hatua! Vivyo hivyo utumishi ni safari, na kwa hakika hatua tumezipiga, kwani ni mbali tumetoka.

Ndani ya miaka 30 ya utumishi wa MSD, tumeboresha sana eneo miundombinu ya usafirishaji, kila kijiji, kata, mtaa, mji, wilaya, mkoa tunaufikia, iwe jua au mvua, majini au nchi kavu hakika tuko kila sehemu.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 16/08/2024

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary Silaa, akizungumza na watumishi wa MSD Kanda ya Kagera hivi karibuni, mara baada ya kutembelea Kanda hiyo kwa lengo la kujadili masuala mbali yanayohusu Kanda hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwapongeza kwa kutimiza malengo yao waliyojiwekea kwa mwaka wa fedha ulioisha.2023/2024.

Katika hatua nyingine Bi. Silaa alipokea mkakati wa Kanda hiyo kujenga Makao Makuu yake wilayani Chato mkoani Geita, ikiwa ni hatua inayotazamiwa kuongeza, upatikanaji wa bidhaa, na ufanisi katika utekelezai wa majukumu ya Kanda hiyo.

16/08/2024
14/08/2024

Kongole sana Mhe. , kwa kuteuliwa kwako kuongoza k**ati ya Afya na Masuala ya UKIMWI, ni ahadi yetu kukupatia ushirikiano katika kipindi chote cha uongozi wako, ili kwa pamoja tujenge taifa letu.

14/08/2024

Hakika ni Miaka 30, ya kulihudumia taifa na kuokoa maisha ya watanzania.
@30

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 13/08/2024

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere amekutana na Mtendaji Mkuu wa SADC Mheshimiwa Elias Mpedi Magosi na kujadiliana naye namna ya kutekeleza Mpango wa pamoja wa Ununuzi wa Pamoja wa bidhaa za afya kwa nchi wanachama wa SADC.

Mazungumzo hayo yalifanyika kando ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC unaoendelea mjini Harare, Zimbabwe.

Pamoja na mambo mengine walijadili jiu ya kuweka mikakati ya pamoja ya jinsi ya kutekeleza Mpango wa Ununuzi wa Pamoja wa bidhaa za Afya wa SADC (SPPS), ili kunufaisha nchi wanachama kupata bidhaa za Afya zenye ubora kwa gharama nafuu.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mtendaji wa SADC anayeshughulikia masuala ya Mtangamano wa kikanda Bi. Angele Makombo N'tumba pamoja na viongozi wandamizi kutoka Sekretarieti ya SADC

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 11/08/2024

Watumishi 36 wa MSD kutoka Kanda zake 10, wameshiriki mafunzo maalum ya siku 4 ya kuendesha mitambo, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao, katika chuo cha bandari, kilichoko jijini Tanga.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 10/08/2024

Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya MSD, chini ya uongozi wa mwenyekiti wa bodi hiyo Bi. Rosemary Silaa, wakipokea zawadi kutoka kwa Menejimenti ya MSD, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika kuiongoza na kuisimamia vizuri MSD, katika kutekeleza majukumu yake.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 09/08/2024

MSD Kanda ya Dodoma, yawatambua na kuwatunuku vyeti na tuzo watumishi wa Kanda hiyo, kufuatia judi na mchango wao katika kufanikisha malengo ya Kanda hiyo kwa Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024.

Akizungumza wakati kukàbidhi tuzo na vyèti hivyo kwaniaba ya Menejimenti ya MSD, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mboyi Wishega, ameupongeza uongozi wa Kanda hiyo kwa hatùa hiyo ya kutambua na kuthamini mchango wa watumishi wake katika kufanikisha malengo waliyojiwekea k**a Kanda, na kusisitiza kuwa hatua hiyo muhimu na mfano kuigwa na viongozi wengine .

Ameongeza kuwa zoezi hilo la utambuzi kwa watumishi hao, litachochea hamasa ya kazi na kuwa chachu ya kuongeza ubunifu na juhudi zaidi katika kufikia malengo katika mwaka mpya wa fedha unaoendelea 2024/2025.

Kwaupande wake Meneja wa Kanda hiyo Bi. Mwanashehe Jumaa, amesema amewiwa kutambua mchango wa watumishi hao, kwani juhùdi na ŵeledi wao, ndio nguzo kuu katika kuhakikisha huduma za bidhaa za afya zinafika wananchi kwa wakati.

Amesisitiza kwamba utambuzi huo wa tuzo na vyeti, umehusisha kada na maeneo yote ya utendaji kamà vile mauzo, ulinzi na usalama, usambazaji pamoja na huduma kwa wateja.

Akizungumza kwaniaba ya Watumishi hao, Mwenyekiti wa wafanyakazi tawi la Kanda hiyo (TUGHE), ameushukuru uongozi wa Kanda hiyo, kwa kutambua mcĥango wao katika kufikia malengo, huku akisema tukio hilo limeleta hamasa na kuchochea umoja na mshik**ano miongoni mwa watumishi, hivyo kuleta chachu ya kufanya vizuri zaidi kwa mwaka mpya unaoendelea sasa.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 08/08/2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, yaeleza kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kuzalisha Mipira ya Mikono cha MSD, kilichoko idofi, Makambako Mkoani Njombe.

Hayo yameelezwa hii leo agosti 7, 2024 na Mwenyekiti wa k**ati hiyo Mhe.Christina Mnzava, wakati k**ati hiyo ilipotembelea mradi huo kwa lengo la kukagua na kupokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Mhe. Mnzava kwaniaba ya k**ati hiyo, amepongeza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na MSD, katika kuendeleza mradi huo, ambayo umetoa ajira kwa wananchi wa eneo hilo.

Aidha, k**ati hiyo imeitaka MSD kuhakikisha inakuja na mpango na mkakati madhubuti wa kufunga mashine za viwanda vingine vya Dawa, zilizoko eneo hilo, ili kutimiza adhima ya serikali ya kuletwa kwa mashine hizo.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meneja Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji wa MSD Hassan Ally, ameeleza kwamba Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha glavu milioni 80 kwa mwaka, ukilinganisha na mahitaji ya nchi ya milioni 58 kwa mwaka, ambayo hugharimu takribani bilioni 16.7.

Ameongeza kwamba hadi kufikia Juni 2024, uwekezaji Kiwandani hapo umefikia jumla ya bilioni 12.4, ambazo ni gharama za uwekezaji na Uendeshaji kwa mwaka wa kwanza.

Aidha amesisitiza kwamba katika kipindi cha miezi 5 kiwanda hicho kimezalisha jumla ya gloves milioni 4, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.14, ambazo zimeanza kuingia sokoni mwezi Agosti 2024.

Naye Naibu waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel, ameipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa inaoendelea kuufanya kwenye sekta ya Afya, ikiwemo uanzishwaji wa viwanda.

Aidha, amebainisha maendeleo yaliyopatikana ndani ya kipindi kifupi cha utawala wake, huku akisisitiza kwamba serikali itaendelea kuhakikisha miradi yote inatekelezwa.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 07/08/2024

Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rosemary Silaa umetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ghala jipya la kisasa la MSD, unaendelea katika eneo la kizota jijini Dodoma.

Akizumgumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Silaa ameipongeza Menejimenti ya MSD kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo, huku akimtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi huo, kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, ameeleza jinsi mradi huo utakavyosaidia katika uhifadhi wa bidhaa za afya, sambamba na kupunguza gharama za uhifadhi, pamoja na uendeshaji kwani utapunguza umbali wa kufuata bidhaa za afya, kwa Kanda zilizoko pembezoni mwa Dodoma, badala ya kufuata bidhaa hizo Jijini Dar es Salaam

Aidha amebainisha kuwa mradi huo, utasaidia upatikanaji wa bidhaa za afya kwa wakati kwa wananchi, kufuatia uwepo wa ghala hilo kubwa la kimkakati makao makuu ya nchi, Dodoma.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 28/07/2024

Baadhi ya Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakiwa kwenye picha mbalimbali, ɓaada hii Leo kushiriki mbio za Dodoma Marathon 2024, zilizokuwa na lengo la kuchangia kuboresha huduma ya mama na mtoto.

Mbio hizo zimefanyika hii leo tarehe 28, mkoani Dodoma na kuhusisha watu na taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

16/07/2024

Karibuni tuwahudumie amana_hospitality .meruhospital

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 14/07/2024

Watumishi wa MSD Kanda ya Dodoma, wamejumuika pamoja hapo jana 13/07/2024, kwa lengo la kutathimini utendaji wao kwa mwaka wa Fedha ulioisha 2023/2024 na sambamba na kuukaribisha mwaka mpya wa Fedha, ikiwa ni pamoja na kujiwekea malengo mapya.

Watumishi hao mbali na kujadiliana kuhusu utekelezaji wa majukumu yao, walishiriki pia katika michezo mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuwaleta pamoja na kuboresha mahusiano baina yao.

Michezo hiyo ni pamoja mpira wa miguu, mpira wa Pete, karata, pool table, riadha, draft pamoja na mchezo wa kuongelea.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Bi. Mwanashehe Jumaa amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa weledi, na kuhakikisha wanaongeza ubunifu na umahiri Ili waweze kufikia malengo waliojiwekea kwa mwaka mpya wa Fedha 2024/2025.

Aidha Bi. Mwanashehe Jumaa ametumia fursa hiyo pia kuwapongeza watumishi wa Kanda hiyo kwa utendaji kazi mahiri kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/24.

Nao watumishi wa Kanda hiyo, wameupongeza uongozi wa Kanda hiyo kwa wazo hilo, wakisisitiza limewajenga kwani imekuwa nadra kukutana na kujadiliana nje ya Ofisi, kutokana na wingi wa majukumu.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 10/07/2024

Meneja wa MSD Kanda ya Kagera, Bw. Kalendero Masatu, akikabidhi tuzo maalum kwa baadhi ya wateja wake wanaohudumiwa na kanda hiyo, kwa utendaji na ushirikiano wao katika kuiwezesha kanda hiyo kutekeleza majukumu yake vyema.

1. Halmashauri ya Kyerwa imepokea tuzo maalum kufutia juhudi zake za ulipaji wa madeni.

2. Halmashauri ya Mbogwe imepokea tuzo maalum kwa juhudi zake za kuwasilisha Maoteo/mahitaji yake kwa wakati, kulingana na kalenda ya usambazaji wa bidhaa za afya.

3. Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imepokea tuzo maalum kwa jitihada zake, katika kutumia vyanzo vyake vingine vya mapato kununua bidhaa Bohari ya Dawa (MSD).

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 06/07/2024

MSD Kanda ya Iringa imeshiriki kwenye Tamasha la Ruaha Marathon mwaka 2024. Tamasha hilo lililofunguliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa limefanyika kwenye Mbuga ya Wanyama ya Ruaha (Ruaha National Park) leo tarehe 6 Julai, 2024 mkoani Iringa.

Wafanyakazi wote wa kanda ya Iringa wameshiriki kwenye Tamasha hilo ambapo wafanyakazi wameshiriki kwenye mbio za urefu wa Kilometa 5, 10, 21 na 42.

Akizungumza baada ya kushiriki Tamasha hilo Kaimu Meneja wa Kanda ya Iringa Robert Lugembe amesema menejimenti ya MSD inatambua umuhimu wa mazoezi kwa watumishi wake, hasa katika kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza, ndio maana imeruhusu wafanyakazi kushiriki kwenye mbio hizo.

Lugembe ameongeza kuwa pamoja na kushiriki michezo wafanyakazi hao wamepata fursa wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo kwenye mbuga hiyo ya Ruaha. Lakini pia ziara hizi za pamoja zinawakutanisha wafanyakazi wote na kujenga uelewano wa pamoja wa kiutendaji katika kufikia malengo ya taasisi kwa ujumla, alisema Bw. Lugembe

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 05/07/2024

Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wanaosomea Udaktari mwaka wa nne (MD4) wakiwa kwenye matukio mbalimbali walipotembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea namna taasisi hiyo, inavyotekeleza majukumu yake.

Ziara hiyo iliyohusisha wanafunzi takribani 50 imelenga kuwapa wanafunzi hao elimu kwa vitendo, juu ya masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Photos from Medical Stores Department (MSD)'s post 05/07/2024

Katika hatua za kuboresha Afya za Watumishi wa MSD na kuleta umoja miongoni mwao, MSD Kanda ya Kilimanjaro imefanya bonanza lililoshirikisha watumishi wote wa kanda hiyo.

Bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu mchanganyiko Wanawake na wanaume, karata, kukimbia na mayai, kukimbia na gunia nk.

Meneja wa Kanda ya MSD Kilimanjaro Rehema Shelukindo amesema michezo hii inaendelea kuleta pamoja watumishi na pia mabonanza k**a haya yataendelea kufanyika kwa wafanyakazi wa kanda hii.

Want your practice to be the top-listed Clinic in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Endelea kufuatilia simulizi hii adhimu, juu ya mabadiliko ya mfumo wa uagizaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutole...
Je wafahamu historia ya mnyororo wa usambazaji wa bidhaa za afya nchini ulianza lini? Fuatilia historia hii adhimu kutok...
Wahenga waliwahi kusema "jungu kuu halikosi ukoko", na wengine wakaenda mbali na kusema hakuna kijiji kisichokuwa na waz...
#Idofi tuko vizuri#KazinaIendelee #Yajayoyanafurahisha
#Idofi kumenoga#KazinaIendelee
#Idofi kumenoga#KazinaIendelee
Fuatilia mikakati ya MSD kuhusu ujenzi wa maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya, ili kukidhi mahitaji ya wateja kwa walau...
#Mauzo ya MSD yaongezeka maradufu! Na je vipi kuhusu ujenzi wa maghala ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi bidhaa ? Mkurugen...
Mkurugenzi Mkuu wa MSD aeleza jinsi MSD ilivyofanikiwa kuboresha usambazaji wa bidhaa za afya nchini, sambamba na uanzis...

Address


Off, Nyerere Road, Keko Mwanga
Dar Es Salaam
9081

Other Dar es Salaam clinics (show all)
Premier Care Clinic Ltd. Premier Care Clinic Ltd.
259 Ali Hassan Mwiyni Road, P. O. Box
Dar Es Salaam, 220

Clinic, Diagnostics-Lab-Ultrasound, Pharmacy

Know your health and have medical service with Dr. Tosiri Know your health and have medical service with Dr. Tosiri
2284
Dar Es Salaam

Pose comments and/or questions to Dr. Tosiri involving Urologic health matters.

Mwamini Hemed Mwamini Hemed
Dar Es Salaam

Mwamini Hemed

African Cure Tanzania African Cure Tanzania
Samora Towers, Floor C3, Room No. 217
Dar Es Salaam

Afya leo Afya leo
Dar Es Salaam

Tambua thamani ya Afya yako katika kufikia malengo yako.

Afya kwanza Afya kwanza
Ilala
Dar Es Salaam

Afya ya uzazi ushauri Na Tiba Afya ya uzazi ushauri Na Tiba
Banana Ukonga
Dar Es Salaam

JENGA AFYA YAKO SASA JENGA AFYA YAKO SASA
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

EMANUELY MSHAURI WA AFYA NA MTOA HUDUMA WA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA AFYA;!?MFANO TEZ DUME BILA UPASUAJI BAWASIRI UTI PID 0672518275

Simactz Simactz
Kijitonyama (Near Sinza Maalum School)
Dar Es Salaam

We connect student with internationally accredited university, we deal with medical tourism and High

Matamu Matamu
Ubungo
Dar Es Salaam, 11000

doxa

AFYA YA JAMII AFYA YA JAMII
Dar Es Salaam

Dr mzee kasambura Dr mzee kasambura
Dale Estate
Dar Es Salaam