Mwanamke na Uongozi

Mwanamke na Uongozi

A Tanzanian NGO strives to promote Women's full, effective participation and equal opportunities for leadership at all levels of decision making.

04/11/2024

Huu ni mwanzo mpya wa wiki, nafasi ya kufanya mambo makubwa na kufikia malengo yako. Kumbuka, kila hatua unayochukua, hata ndogo, inakusogeza karibu na ndoto zako. Usikate tamaa na jiamini kwamba unaweza kushinda changamoto yoyote inayokujia.

“Kila jua linapochomoza, ni fursa mpya ya kuandika historia yako kwa upya.”

01/11/2024

Happy New Month!

Embracing November with gratitude and purpose. May this month bring growth, resilience, and new opportunities to make a difference. Let’s keep pushing forward and stay inspired.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 31/10/2024

Leo tumewasilisha mada muhimu kuhusu jinsi ya kubeba na kuendeleza ajenda ya kazi yenye staha kwa walimu, tukilenga kuboresha mazingira yao ya kazi na kuongeza thamani ya kazi yao kwa jamii.

Ni jukumu letu kuimarisha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kuwahudumia wanafunzi kwa ufanisi na kwa heshima wanayostahili.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 30/10/2024

Mwanamke na Uongozi tumeshiriki mjadala wa kazi yenye staha kwa walimu wa k**e, tukijadili changamoto wanazokutana nazo na fursa zilizopo kwa kuboresha mazingira ya kazi yao, hasa vijijini.

Pamoja, tunatafuta suluhu zinazolenga kuwawezesha walimu hawa kwa utu, usalama, na msaada unaohitajika ili waweze kutoa elimu bora kwa vizazi vijavyo.

29/10/2024

Empowered girls become powerful leaders. Let’s nurture young girls to take on leadership roles, break barriers, and drive positive change in their communities.

22/10/2024

Katika mwezi huu wa mtoto wa k**e, tunasherehekea nguvu, ndoto, na uthubutu wa kila binti. Tuwape nafasi, elimu, na usaidizi wa kuweza kufikia upeo wa mafanikio yao. Tukumbuke, tunapowekeza kwa wasichana, tunajenga kizazi imara cha viongozi wa kesho.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 16/10/2024
Photos from Mwanamke na Uongozi's post 16/10/2024

Wanawake tuna nguvu ya kubadilisha maisha ya wanawake na wasichana wengine wanaopitia changamoto mbalimbali.

Tunaamini katika jitihada za pamoja, ambazo tunaweza kuwapa msaada wanaohitaji ili waweze kushinda vikwazo na kufikia ndoto zao. Tuwape matumaini, msaada, na fursa, kwa sababu kila mwanamke anastahili nafasi ya kujitambua na kufanikiwa.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 15/10/2024

Wana mtandao wa Anza na Ulichonacho tukipokea somo namba ya kujilinda na kujikinga na Ugonjwa wa kansa ni pamoja na kufanya vipimo vya mara kwa mara ili kuweza kupata kujitibia mapema.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 15/10/2024

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere. Wanamtandao wa Anza na Ulichonacho tuliweza kuwatembelea wagonjwa waliopo katika hospital ya Ocean Road. Katika matembezi haya tuliweza kuwapa sadaka ya mahitaji iliyokuwa imeandaliwa na wana mtandao hawa.

14/10/2024

“Njia pekee ambayo Uongozi unaweza kutunzwa k**a Uongozi na watu ni pale ambapo Viongozi wanapokuwa na sababu ya kuogopa hukumu kutoka kwa watu”

13/10/2024

“Lengo la maendeleo ni binadamu, na hitaji kuu la binadamu ni utu. Uchaguzi wa maendeleo ni uchaguzi wa vitendo.”

13/10/2024

“Maendeleo lazima yahusishe watu wenyewe na kujitegemea katika maendeleo ya jamii ni muhimu.”Mwl Julius Nyerere

Katika Nukuu hii inaonyesha jukumu la watu binafsi katika kuchangia maendeleo ya jamii zao kupitia juhudi za kujitolea.

Ewe mdau wetu karibu katika mtandao wetu wa Hisani na ni mtandao huru ambao unalenga katika kujitolea kwa chochote ulichonacho na kusaidia wengine.

13/10/2024

Katika kuenzi kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Timu ya Wanamtandao wa Anza na Ulichonacho watasherekea kuadhimisha maadhimisho haya na Wanawake wenye maradhi ya Kansa katika Hospital ya Ocean Road.

Tafadhali ungana nasi kwa kutoa chochote ulichonacho k**a Sadaka ya kuwapatia wagonjwa hawa.

Wasiliana nasi kupitia nambari 0659174229.

Anza na Ulichonancho, Badilisha Maisha ya Wengine

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 11/10/2024

Bado tunaendelea kusherekea Siku ya Mtoto wa K**e Duniani, tukizingatia kuwa ukombozi wa mtoto wa k**e ni jukumu la jamii nzima. Mtoto wa k**e ana nafasi muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na hivyo ni lazima kila mmoja wetu—wanajamii, viongozi, na wadau mbalimbali—kujitolea kuhakikisha haki zao za msingi zinaheshimiwa na kutekelezwa. Haki hizi zinajumuisha upatikanaji wa elimu bora, usalama, afya, na fursa sawa katika uongozi na ajira.

Tunatoa wito kwa jamii nzima kuzingatia kwamba kumwezesha mtoto wa k**e ni kuijenga jamii yenye usawa, haki, na maendeleo endelevu. Ni wakati wa kuondoa vizuizi vya kitamaduni, kijamii, na kiuchumi vinavyomzuia mtoto wa k**e kufikia uwezo wake kamili. Kwa pamoja, tunaweza kujenga mustakabali bora zaidi kwa watoto wa k**e, na hatimaye kwa jamii nzima.

11/10/2024

Kheri ya Siku ya Mtoto wa K**e Duniani.

Leo tunasherehekea ujasiri, uthubutu na ndoto za kila mtoto wa k**e. Tuendelee kuunga mkono haki zao, kuwapa nafasi ya kujifunza, kuongoza, na kung’aa kwa uwezo wao wote.

10/10/2024

Leo tunashetekea siku ya Afya ya Akili Duniani.

Afya ya akili ni muhimu k**a afya ya mwili. Leo tunakumbuka kuwa kila mmoja wetu ana haki ya kujisikia vizuri kiakili. Tupendane, tusaidiane, na tuwe na huruma. Kila hatua ndogo tunayochukua kuelekea afya bora ya akili ina umuhimu.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 09/10/2024

Bado changamoto ni nyingi sana, hususan mitazamo hasi kuhusu Uongozi na nafasi za maamuzi kwa wasichana. Hali hii inawanyima wasichana fursa za kushiriki kikamilifu au kujumuishwa katika mikakati ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa. Zaidi ya hayo, masuala ya afya ya uzazi yanaendelea kuwa changamoto. Wazazi na walezi wengi bado hawajakuwa na uwazi wa kuzungumza na watoto wao kuhusu njia bora za kujilinda na kujihakikishia usalama wa afya zao ili kufikia ndoto zao. Badala ya kuzuia changamoto hizo mapema kwa kutoa elimu, jamii inasubiri hadi tatizo litokee ndipo hatua zinachukuliwa, na mara nyingi watoto wanalaumiwa badala ya kupewa msaada wa kujikwamua na changamoto hizo.

Ni muhimu kwa jamii kubadilisha mtazamo huu na kuwekeza katika kuwaelimisha watoto wa k**e mapema, kuwapa nafasi za maamuzi, na kuwaongoza kuelekea mustakabali mzuri kwa jamii na Taifa letu kwa ujumla.

Cc

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 09/10/2024

Mwanamke na Uongozi tulihudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Uzinduzi wa Mradi iliyoandaliwa na Msichana Initiative , ambapo tulijadili changamoto zinazowakabili watoto wa k**e katika maeneo muhimu.

Ripoti ilibainisha jinsi masuala k**a afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia, ukosefu wa nafasi za maamuzi na uongozi, afya ya akili, ndoa za utotoni, na mimba za utotoni yanavyoathiri maisha ya watoto wa k**e. Changamoto hizi zimekuwa kikwazo kwa wasichana kutimiza ndoto zao na kujiendeleza kielimu na kiuchumi. Kupitia ripoti hii, imeonekana wazi kuwa kuna umuhimu wa juhudi za pamoja katika kuwasaidia wasichana hawa kupata haki zao na nafasi bora za maendeleo.

Cc

08/10/2024

Katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa K**e Duniani, ambayo yanafanyika kila mwaka tarehe 11 Oktoba, Mwanamke na Uongozi tunasisitiza zaidi umuhimu wa kulinda haki na utu wa watoto wa k**e, hasa wasichana wenye ulemavu. Siku hii ni fursa ya kuikumbusha jamii kuhusu changamoto wanazokutana nazo watoto wa k**e na umuhimu wa kuhakikisha kuwa kila msichana anapata fursa sawa za elimu, afya, na ushiriki wa kijamii, bila ubaguzi wa kijinsia au ulemavu.

Tunaamini kwamba kila msichana ana uwezo wa kufikia ndoto zake endapo atapewa mazingira salama na yenye usawa, yanayomlinda dhidi ya aina zote za ubaguzi, unyanyasaji, na unyimaji wa fursa. Kwa wasichana wenye ulemavu, changamoto hizi mara nyingi huwa kubwa zaidi kutokana na ukosefu wa huduma stahiki na mazingira yasiyokuwa jumuishi. Ni muhimu kwa jamii kutambua haki zao na kuhakikisha kuwa wanapata huduma wanazohitaji ili waweze kufikia malengo yao.


**eDuniani

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 07/10/2024

Pichani ni Wafadhili wetu kutoka Women First İnternational Fund wakiwa na wanufaika wetu wa Mradi wa The chance for a new Beginning, ewe mdau wetu tunapenda kukumbusha kwamba mradi huu ulikuwa unalenga kuwasaidia wasichana zaidi ya 20 katika kuwapa mafunzo ya ujuzi mbalimbali ambao utawasaidia wao kuutumia na kujikwamua kiuchumi

Mafunzo haya yalikuwa ni ya Miezi 6, tunafurahi kuona wasichana hawa wamerudisha tabasamu lao na matumaini mapya kuwa inawezekana endapo umepewa nafasi ya kuanza upya tena.

Ndugu wadau wetu, washirika wetu, wafuasi wetu na wanajamii kwa ujumla, tuendelee kuwashika mkono wasichana wanaopitia changamoto mbalimbali kwani wana uwezo wa kufanya makubwa endapo tukiwapa nafasi nyingine ya kujifunza tena.



…………………………………………………………………………………
From the picture above, are our donors from Women First International Fund along with our beneficiaries from the ‘The Chance for a New Beginning’ project. To our stakeholders, we would like to remind you that this project aimed to assist more than 20 girls by providing them with various skills training that would help them utilize these skills to improve their economic situation.

This training lasted for 6 months, and we are happy to see these girls regain their smiles and have renewed hope that it is possible if given the opportunity to start afresh.

To our stakeholders, partners, followers, and the community at large, let us continue to support girls who are facing various challenges, as they have the potential to achieve great things if given another opportunity to learn.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 07/10/2024

Leo, tulipata Ugeni wa kumkaribisha mfadhili wetu kutoka Women First International Fund Ilikuwa ni fursa ya kipekee kwa timu yetu na wanufaika wetu wa Mradi wa ‘The Chance for a New Beginning’. Wafadhili wetu waliweza kuzungumza moja kwa moja na wafanyakazi wetu pamoja na walengwa yaani wanufaika wa mradi huu na kupata ufahamu wa moja kwa moja juu ya changamoto na mafanikio ya kazi yetu.

Katika Mabadilishano haya yaliwapa fursa ya kushuhudia maendeleo yanayofanyika na kuelewa changamoto zinazokabili jamii yetu.Ujio wa wageni wetu hawa haujaimarisha tu ushirikiano wetu bali pia ulihamasisha timu yetu kuendelea na jitihada za kuleta mabadiliko chanya ndani ya Taasisi na hata Nje ya Taasisi. Tunawashukuru sana wafadhili wetu huyu ambao wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufikia malengo yetu ya pamoja.

………………………………………………………………………………
Today, we had the privilege of hosting our donor from the Women First International Fund It was a remarkable opportunity for our team and beneficiaries, particularly those involved in our ‘The Chance for a New Beginning’ initiative. During the visit, our donor interacted directly with our dedicated staff and beneficiaries, gaining firsthand insight into the transformative impact of our work.

This exchange allowed them to witness the progress being made and understand the challenges faced by our community. The meeting not only strengthened our partnership but also inspired our team to continue our efforts towards positive change. We are grateful for the donor’s support and the encouragement they provided to our beneficiaries, reaffirming the importance of collaboration in achieving our shared goals.

06/10/2024

Jana ilikuwa siku ya Walimu Duniani.

Mwanamke na Uongozi tunatambua na kuthamini michango chanya inayofanywa na Walimu wote Nchini ikiwa ni pamoja na kuchagiza katika Maendeleo ya Elimu kwa Jamii yetu.

Tunaendelea kuwapongeza kwa juhudi zao na maarifa katika ufanyaji kazi wao, k**a tunavyojua Ualimu ni wito na hakika tuna kila sababu za kuwapongeza katika kazi hii. Licha ya Changamoto zao za kikazi ambazo zinapelekea wakati mwingine kufanya kazi katika Mazingira Magumu lakini Walimu hawa bado wanaendelea kufanya kazi kwa wito ili kuhakikisha tunajenga mazingira rafiki kwa ajili ya vizazi vyetu vilivyopo na hata kizazi cha baadae.

Photos from Mwanamke na Uongozi's post 04/10/2024

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa 2024, tuhakikishe sauti zetu zinasikika. Ushiriki wa kila mmoja wetu ni muhimu kwa kujenga jamii yenye usawa na haki.

Vijana, Wanaume na Wanawake sote ni haki yetu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mtaa 2024.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Videos (show all)

Happy Friday from our team to yours! As we wrap up another productive week, we want to take a moment to appreciate all t...
Katika kuenzi kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Timu ya Wanamtandao wa Anza na Ulichona...
Mwanamke na Uongozi kushirikiana na @iriglobal tulifanikiwa kuandaa Mafunzo ya Uongozi na Kampeni UVCCM Mkoani Tanga.Kat...
Happy Weekend from our team to yours😍Muda wetu mwingi tunautumia kucheza na kufurahia pamoja💥💥Wewe je🤷‍♀️#WeekendVibes#T...
Anza na Ulichonacho ni mtandao wa wanawake takribani 80 ambao wana kazi au shughuli zinazowaingizia kipato. Mtandao huo ...
Challenge Accepted to our Team…..
Leo tunasherekea siku ya hedhi DunianiTimu ya Mwanamke na Uongozi tumefanya igizo fupi kuonyesha ni kwa namna gani wasic...
“The Chance For A New Beginning “Ni mradi uliofadhiliwa na @womenfirstfund  na katika  mradi huu unalenga  kuwasaidia ma...
MnU team participated in our P-Plus program, which took place in Dodoma. We advocated for the Dodoma City Council to inc...
Katika kuendelea kusherekea miaka 7 toka kuanzishwa kwa Taasisi yetu, tumeweza kuwafikia wanawake na wasichana katika se...

Telephone

Website

Address

Sinza A
Dar Es Salaam
Other Non-Governmental Organizations (NGOs) in Dar es Salaam (show all)
Art in Tanzania Art in Tanzania
Umoja Road Block 2Q, Madale Village
Dar Es Salaam, 23333

Art in Tanzania - a self-sustainable NGO helping communities in Tanzania.

Lalji Foundation Lalji Foundation
Morani House
Dar Es Salaam

The Lalji Foundations pledges to give back to the community and improve lives.

Education For Disabled Tanzania Education For Disabled Tanzania
NSSF Road St, Bagamoyo Road
Dar Es Salaam, 14121

We are a non-profit organization, our main goal is to change lives of youths, children and those in

Stop TB Tanzania Stop TB Tanzania
Mikocheni
Dar Es Salaam

Tanzania joining other countries to start STOP TB chapter in Tanzania aiming to comply with Moscow de

Vijana Na Ujana Vijana Na Ujana
Dar Es Salaam

Universal Human Development - Uhuden Universal Human Development - Uhuden
Zanaki Street
Dar Es Salaam, 11105

Universal Human Development (UHUDEN), is a Non-Government organization established under section 12 (1) of the NGO Act No. 24 of 2002, of the United Republic of Tanzania.

yowedfoundation2019 yowedfoundation2019
Mbezi Luis Mwisho, Makao Makuu
Dar Es Salaam

Nantambelele niokoe foundation Nantambelele niokoe foundation
CHANIKA
Dar Es Salaam

� DENY CHILD ABUSE � RIGHTS AND EQUALITY TO ALL Children �

Romme love justice Romme love justice
Sam Nujoma/Lufungira Road
Dar Es Salaam

ROMME Love Justice Tanzania, an anti Human Trafficking organisation is a member of TANAHUT.

Zeal for Care Organization Zeal for Care Organization
Majumba Sita
Dar Es Salaam

helping people with great needy

Problem Solver Mission Problem Solver Mission
Dar. . Es. . Salaam
Dar Es Salaam

Ni Shirika Linalo Wasaidia Watu Kupata Wanachokitaka. Lina shughulika na Utatuzi wa Matatizo ya Kiroho, Kifedha, Kiafya na Mahusiano yaliyoshindikana.

Da Tabu Foundation Da Tabu Foundation
P. O. BOX 20950
Dar Es Salaam, 12113

social activists who fight against violence and sexual violence and provide education to the community "Wanaharakati wa kijamii Tunaopambana kupinga ukatili na unyanyasaji wa kiji...