HakiElimu
Nearby non profit organizations
Tabata Segerea
Floor
Dar es Salam 00255
38524
Temeke
Kisutu Hananasif
Kigamboni
Gongo la Mboto, Dar es Salam
Mikocheni, Dar es Salam
Our non-profit organisation strives for an open, just and democratic society with quality education.
Kwa mujibu wa tathimini iliyofanywa na Marafiki wa Elimu wa Wilaya ya Ukerewe katika Shule 15 za Msingi na Shule 5 za Sekondari , kwa ujumla wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum wanawaruhusu watoto wao kwenda shule kupata elimu
๐๐๐๐ฆ๐ ๐ฒ๐๐๐ง๐๐๐ฅ๐๐ ๐ค๐ฎ๐ฐ๐๐๐ง๐ ๐ฎ๐ค๐ข๐ ๐๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐๐ง๐๐๐ฎ๐ง๐ณ๐ข ๐ง๐๐ก๐ข๐ง๐ข ๐๐๐ง๐ณ๐๐ง๐ข๐
Leo HakiElimu pamoja na taasisi za elimu zilizopo ndani na nje ya nchi wamezindua mradi wa kuboresha mafunzo ya walimu kwa kutumia teknolojia ya Uhalisia Pepe yaani Virtual Reality (VR) ambao unatarajiwa tunaleta mapinduzi katika elimu hapa nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo Mkuu wa Programu wa HakiElimu, Boniventura Godrey ameeleza faida za mradi huu katika elimu
๐ฃ๏ธ "Ni wakati muafaka kukumbatia teknolojia ya Uhalisia Pepe na suluhisho nyingine za kiteknolojia ili kukuza ubunifu, fikra yakinifu, na kushughulikia pengo la ujuzi nchini."
๐ง "Uhalisia Pepe hauko tu kwa burudani; ina uwezo wa kubadilisha masomo magumu kuwa rahisi kuelewa, kuleta dhana zisizo za wazi kwenye maisha, na kuongeza ushiriki wa wanafunzi."
Naye mwakilishi kutoka Ubalozi kutoka Ubalozi wa Finland nchini Tanzania, Sanna-Liisa Taivalmaa ameelezea nia ya Serikali ambao ndio wafadhili wa mradi huu ambao unatarajiwa kufanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka miwili.
๐ "Tumejizatiti kuhakikisha kwamba ubunifu wa kidijitali unafikiwa na wote na unaathiri wanafunzi kwa njia yenye manufaa."
Teija Lehtonen kutoka Chuo Kikuu cha HAMK kilichopo Finland anaelezea majukumu yao ya msingi katika mradi huu.
๐ "Chuo chetu kitatoa mafunzo ya pedagogia ya VR kwa taasisi za elimu nchini Tanzania na kitasaidia kupima athari za mradi huu kwenye jamii."
Jussi Kajala, mwanzilishi mwenza wa 3D Bear ambao ni washirika watekelezaji wakuu katika mradi huu kwa upande wake amefafanua dhana nzima ya mafunzo haya ambayo yanatarajiwa kutolewa katika vyuo vya walimu Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
๐ "VR na AR ni maneno ya kiufundi, lakini kwa urahisi maneno haya yana maana ya uigaji wa hali halisi, ambayo husaidia katika mazoezi ya ujuzi kwa ufanisi na wepesi pia niwatoe hofu, ๐ ๏ธ Zana zetu zinapatikana kwa urahisi na hazihitaji teknolojia ya hali ya juu."
Uzinduzi huu umehudhuriwa na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo VETA, Save the Children, Association of Tanzania Employers, UNIDO, West Evan, FDC, HAMK University na 3D Bear.
โช๏ธ Ufuatiliaji uliofanywa na Marafiki wa Elimu katika Shule 20 zilizopo Wilaya ya Mpwapwa umeonesha kuna shule ambazo zinazopokea kiwango kidogo cha fedha ya ruzuku ya chakula kwa watoto wenye ulemavu, huku shule nyingine zikipokea kiwango kikubwa zaidi ya kile kilichoainishwa kwenye mwongozo.
โช๏ธ Je Mwalimu Mkuu unafahamu kila mwezi mwanafunzi mmoja anastahili kupokea ruzuku ya shilingi ngapi kwa ajili ya chakula?
โช๏ธTunawatakia kila la kheri watahiniwa 1,230,780 katika mitihani ya kumaliza darasa la saba na kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2024.
Katika Shule 20 zilizotembelewa na Marafiki wa Elimu wa Wilaya ya Ukerewe, hakuna hata moja iliyo na uzio unaoweza kuzuia mtu asiingie shuleni kwa utaratibu, hii inaweza kusababisha changamoto ya ulinzi na usalama wa watoto wenye mahitaji maalum hususani kwa baadhi ya watu wenye fikra na imani potovu juu ya makundi haya.
Jumla ya washiriki 26 (Walimu 20 na Maafisa Elimu 6) kutoka Halmashauri 3 za Mpwapwa, Kilosa na Korogwe, wameendelea kunufaika na mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa AMUCTA-Tabora. Mafunzo haya yanalenga kuimarisha Uwajibikaji katika Elimu Jumuishi.
Dr. Ildephonce Mk**a, Mhadhiri, Elimu Jumuishi โ AMUCTA, akiongoza mafunzo kwa walimu na maafisa elimu wa Elimu Jumuishi yaliyofanyika katika ukumbi wa AMUCTA mkoani Tabora, alibainisha mambo muhimu ya kutiliwa mkazo ili kuwa na ufanisi katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2022-2026.
Amebainisha kuwa ili Elimu Jumuishi iwe na ufanisi ni lazima iwe na sifa zifuatazo;
1. Ifik**e (Accessibility) 2. Ushirikishwaji (Participation) 3. Ujifunzaji (Learning).
Mk**a amesema sifa tajwa hapo juu zinategemea uwepo na ushiriki wa โmafiga matatuโ (Key players) ya Elimu Jumuishi ambayo ni Mazingira, Walimu na Wazazi. Akipungua yeyote kati ya hawa, Elimu Jumuishi haiwezi kuwa na ufanisi.
Kwa upande mwingine Fraterinus Mutatembwa, Mhadhiri Elimu Jumuishi kutoka AMUCTA amesema, โIli mwalimu awe na ufanisi katika ufundishaji wake katika darasa Jumuishi ni lazima awatambue watoto au wanafunzi wake kulingana na uwezo na changamoto zao za ujifunzaji. Hii itamsaidia kuandaa somo lake ikiwemo mbinu sahihi atakazozitumia kufundishia na zitakazowafaa wanafunzi wote katika darasa Jumuishi sambamba na maandalizi ya dhana za ujifunzajiโ
Miongoni mwa mambo yaliyobainika mwanzoni mwa mafunzo haya ni pamoja na baadhi ya washiriki kutokuwa na uelewa wowote kuhusiana na Elimu Jumuishi ingawa wao ndio watekelezaji wakubwa wa Elimu Jumuishi. Hali hii imeibua maswali mengi na baadhi ya washiriki wameomba mafunzo haya yatolewe kwa walimu wengi zaidi ili kuleta ufanisi katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi.
Hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya utekaji na uuaji wa watoto katika maeneo mbalimbali jambo limeleta hofu kubwa hasa kwa wazazi na walezi. Suala hili limeibua mjadala mkubwa sana ambao unaendelea mpaka sasa.
Suala la ulinzi na usalama wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi, jamii na serikali kwa ujumla. Jamii inatakiwa iwe bega kwa bega katika kufanikisha wajibu huu kwa kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa ikiwemo haki ya kuishi, sambamba na kuchukua hatua pale ambapo watoto wanaonekana kunyimwa haki zao.
Ambatana nasi katika dakika 4 kusikia jamii na HakiElimu wanasemaje kuhusu matukio haya. Tafakari, Chukua Hatua.............
๐๐๐ซ๐๐๐ข๐ค๐ข ๐ฐ๐ ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐๐ข๐ญ๐ ๐ฐ๐๐ข๐๐ฎ๐ ๐๐๐ข๐ฏ๐ฎ ๐ง๐ ๐๐๐ข๐๐ก๐ข ๐ณ๐ ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐ฎ๐ฆ๐ฎ๐ข๐ฌ๐ก๐ข
Marafiki wa Elimu Geita wamewasilisha tathimini ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi kwa mwaka 2022- 2026 uliofanyika katika shule 25 (15 msingi na 10 za Sekondari) zilizopo katika Halmashauri ya Mji Geita katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu mkoani Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa hiyo Rafiki wa Elimu, Nurath H. Swalehe ametaja mambo mazuri na changamoto za utekelezaji wa elimu jumuishi katika shule hizo.
Bi Nurath amesema "Watoto wanajumuishwa katika shughuli zote za ujifunzaji shuleni bila kubagua aina ya ulemavu na hali zao walizo nazo pia shule zinazingatia usawa wa kijinsia katika mgawanyo wa kazi"
Kwa upande wa changamoto Bi Nurath amesema "Ufuatiliaji huu umebaini kuwa pamoja na baadhi ya wazazi kujitokeza katika uandikishwaji wa watoto wenye mahitaji maalum, bado idadi kubwa ya watoto hao wamekuwa wakiacha shule kutokana na sababu mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka mitatu jumla ya wanafunzi walioacha shule ni 162 kati ya wanafunzi 3,255 walioandikishwa katika shule tulizotathimini."
Kwa upande wa Halmashauri ya Mji Geita, Afisa Elimu Maalum divisheni ya Msingi Geita Mji Bi Mary Venanace ametaja jitihada mbalimbali ambazo wamezichukua ikiwemo kupita mtaa kwa mtaa kuwatambua na kuwaandikisha watoto wenye mahitaji maalum na ujenzi wa miundo mbinu inayozingatia mahitaji ya watoto wenye uhitaji.
Afisa Elimu Maalum divisheni ya Sekondari Bi Amina Mobeye amesema walimu wote wa Sekondari wana uwezo wa kufundisha madarasa ya elimu jumuishi isipokuwa siyo wote wenye uwezo wa kufundisha elimu maalum.
Kiongozi wa Marafiki wa Elimu Geita, Ndugu Ayubu Bwanamadi amelishukuru Shirika la HakiElimu kwa kuwapatia mafunzo ambayo yamewawezesha kufanya tathimini hiyo na kushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuwapa kibali cha kufanya tathimini hiyo ambayo ana imani ripoti hii itachochea jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo kuongeza uwajibaki na ushirikiano katika kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi.
๐๐๐ค๐ข๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ง๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ฐ๐๐ฎ๐ง๐ ๐๐ง๐ข๐ฌ๐ก๐ ๐ง๐ ๐ฎ๐ฏ๐ฎ ๐ค๐ฎ๐๐จ๐ซ๐๐ฌ๐ก๐ ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐ฎ๐ฆ๐ฎ๐ข๐ฌ๐ก๐ข
Shirika la HakiElimu limeingia makubaliano ya mahusiano na AMUCTA (Archbishop Mihayo University College of Tabora) ambayo yanalenga kuimarisha uwajibikaji katika Elimu Jumuishi hapa nchini.
Makubaliano hayo ya ushirikiano ndani ya kipindi cha mwaka mmoja yanahusisha huduma za kuwajengea uwezo walimu na maafisa elimu katika Elimu Jumuishi, Ushauri kwa walimu (Teachers Mentorship Programs), pamoja na uchambuzi na uchechemuzi katika eneo la Elimu Jumuishi.
Zoezi la utiaji saini limefanyika katika ofisi za AMUCTA mkoani Tabora, na kushuhudiwa na Dr. John Kalage, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Prof. Mary Kitula, Deputy Principal for Academic Affairs (DPAA) -AMUCTA sambamba na viongozi na maafisa waandamizi kutoka pande zote mbili za makubaliano.
๐๐๐ค๐ข๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐ง๐๐๐จ๐ซ๐๐ฌ๐ก๐ ๐๐ฐ๐๐ณ๐จ ๐ฐ๐ ๐๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ค๐ฎ๐ญ๐๐ค๐๐ฅ๐๐ณ๐ ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐๐ก๐ข๐ซ๐ข๐ค๐ข๐ฌ๐ก๐ข
Shirika la HakiElimu kwa ushirikiano na chuo cha AMUCTA-Tabora, kupitia mradi wa Kuimarisha Uwajibikaji kwa Elimu Jumuishi, wameanza mafunzo kwa walimu 20 na maafisa elimu 6 kutoka halmashauri 3 (Kilosa, Mpwapwa na Korogwe).
Mafunzo haya yanalenga mosi, kuwajengea uwezo walimu katika kuwatambua watoto/ wanafunzi wenye uhitaji maalumu walioko shuleni na wale walio nje ya shule na pili kuwafundisha na kuwapa ujuzi wa kufundisha madarasa ya Elimu Jumuishi.
Wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu Dr. John Kalage amesema shirika la HakiElimu kupitia mradi wa Kuimarisha Uwajibikaji unaofadhiliwa na Taasisi ya CBM (Christoffel-Blindenmission) wana nia ya dhati katika kuwawezesha walimu kuweza kuwatambua na kuwafundisha wanafunzi kulingana na mahitaji yao. Aidha amewashukuru walimu na maafisa wa Elimu Jumuishi kwa kuhudhuria mafunzo hayo
Akifungua mafunzo Upendo Rweyemamu, Afisa Elimu, mkoa wa Tabora amebainisha jitihada zinazochukuliwa na serikali ili kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi 2022-2026 ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi maeneo mbalimbali nchini sambamba na kuandaa wataalamu wa kutekeleza mpango huo, jambo lililopelekea kuongezeka kwa uandikishwaji wa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule mbalimbali.
Rweyemamu amesema "Idadi kubwa ya watoto waliokuwa wanafichwa sasa imepungua na matokeo ya haya tumeona kuna idadi kubwa ya watoto wenye mahitaji maalumu wanaoandikishwa shuleniโ
Licha ya kuwepo kwa mafanikio haya, bado Afisa Elimu wa mkoa amebainisha changamoto kadhaa. Ameeleza kuwa si walimu wote wanao ujuzi wa kuwafundisha watoto wenye mahitaji maalumu na si wote wana ujuzi au uwezo wa kuwatambua wanafunzi au Watoto wenye mahitaji maalumu. Hivyo amewashukuru HakiElimu kwa kuyaandaa mafunzo hayo mkoni Tabora.
Ameongeza kuwa kupitia mafunzo hayo walimu na maafisa wa Elimu Jumuishi watajua nini maana Elimu Jumuishi na kwa namna gani wataweza kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu. โMatarajio yangu ni kwamba baada ya mafunzo haya walimu ya maafisa elimu mlioko hapa mtafanya vizuri zaidi katika kufanikisha mpango mkakati wa kitaifa wa Elimu Jumuishi,โ
Marafiki wa Elimu wilayani Mpwapwa chini ya uratibu wa shirika la HakiElimu wamefanya uwasilishaji wa ripoti ya ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2022-2026. Ufuatiliaji huu ulilenga kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa Mkakati wa Elimu Jumuishi katika wilaya ya Mpwapwa kuanzia mwaka 2022 hadi 2024 katika ngazi ya shule na kwamba ulifanyika katika shule 15 za msingi na shule 5 za sekondari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa uwasilishaji wa ripoti hii, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ndugu Oberty Mwalyego amesema kipindi cha nyuma ilikuwa ni kawaida kusikia watoto wenye ulemavu wakifichwa majumbani na kunyimwa haki yao ya kupata elimu, ila kwasasa hali hiyo imebadilika sana na kwamba sasa watoto wenye ulemavu wanaandikishwa kwa wingi katika wilaya ya Mpwapwa na kutolea mfano wa uandikishaji katika shule ya Msingi Chazungwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Marafiki Elimu Mpwapwa ndugu Steven Noel akiwasilisha matokeo hayo alisema wamebaini ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kati ya kipindi cha mwaka 2022 na mwaka 2024.
Akitoa ushuhuda wa namna ambavyo alipata fursa ya elimu, ndugu Kandido Mnemele mwakilishi wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Mpwapwa (SHIVYAWAPWA) anasema โโNakumbuka siku moja nilikuwa nacheza na rafiki zangu ambao walikuwa wamevaa sare za shule na Mwalimu alishangaa kwanini mimi sikuwa nimevaa sare, yule akasimama na kuniuliza kwanini nilikuwa sijaandikishwa shuleni na akanitaka kesho yake niende shuleni kuandikishwaโโ
Ushuhuda wa Pandido unaonesha namna ambavyo Walimu wanayo nafasi adhimu ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu na wao wapate fursa ya elimu k**a watoto wengine โโhii confidence mnayoniona nayo leo ni kwasababu Walimu walinionesha upendo, ni muhimu kuwa na watu ambao watatembea kwenye jamii na kuwatambua watoto wenye ulemavu na kuwaandikisha, mimi pia nilitambuliwa hivyoโโ.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ndugu Oberty Mwalyego ametoa wito kwa wadau wa elimu kuhakikisha kuwa watoto wote wenye ulemavu wanaoandishwa shuleni wanaendelea kujifunza katika mazingira wezeshi ili wafikie malengo yao ya kielimu lakini pia kuzifikia ndoto zao.
Je, unataka kuona mtoto wako akiwa na furaha, akijifunza, na akiwa na marafiki wengi? Elimu jumuishi ndiyo jibu!
โช๏ธJe ukiwa k**a mzazi au mlezi , ukiacha michango ya fedha unayotoa ili kumwezesha mtoto wako kupata elimu, je ni shughuli zipi nyingine zipi zinazohusu elimu ya mwanao ambazo unashiriki? Tafakari, Chukua, Hatua ..........
- Utafiti wa makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto nchini Tanzania uliofanywa na ulibaini kuwa ingawa Madawati ya Jinsia na Ulinzi wa Watoto yanapaswa kufanya shughuli za msingi katika jamii kutokana na majukumu yao, lakini hakuna hata moja lenye bajeti. Kwa kiasi kikubwa, wanalazimika kusubiri kuripotiwa kwa matukio yaliyotokea.
- Ukosefu wa bajeti unapunguza uwezo wao wa kufanya shughuli za uenezaji wa habari na uelekevu wa jamii kuzuia unyanyasaji wa watoto.
- Tafakari Chukua Hatua...............................
- Hoja ya nguvu wiki iliyopita kupitia jukwaa letu la Facebook ilitolewa na mdau wa elimu aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani Mmbaga katika mada ya Lugha ya Kufundishia.
- Mtunzi Dedan Runoba anatumbuiza na shairi lake la Elimu Jumuishi Haki ya Mtoto , beti zingine zitaendelea kesho
- Ushiriki Wako Unaweza Kubadilisha Mustakabali wa Watoto Wetu.
- Tafakari Chukua Hatua......................
- Mtunzi Dedan Runoba anamalizia na shairi lake la Elimu Jumuishi, Haki ya Mtoto. Je nawe ungependa kushiriki jukwaani na kazi yako ya sanaa tuwasiliane inbox.
- Ushiriki Wako Unaweza Kubadilisha Mustakabali wa Watoto Wetu.
Elimu kwa Wote: Kwa pamoja tunaweza kuzifanya ndoto zao zitimie! Tafakari Chukua Hatua......
Siku ya pili ya # imetawaliwa na ufunguzi rasmi wa mkutano wa kimataifa wa elimu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umefunguliwa na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango.
Mkutano huo unahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri wa Elimu na wawakilishi kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki, Wadau wa Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wadau wa Sekta ya Elimu.
Katika hotuba yake Makamu wa Rais, Dkt Mpango amesema kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanapaswa kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu ili kukidhi mahitaji ya utoaji elimu bora.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ambayo yanalenga kuongeza ubora wa elimu pamoja na kuandaa rasilimali watu yenye ujuzi itakayoendana na mahitaji ya dunia ya sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu na Mwenyekiti wa Bodi wa RELI Afrika, Dkt. John Kalage katika hotuba yake amesisitiza kuwa mkutano huu unatoa wito kuwa pamoja tunaweza kujenga mustakabali bora kwa watoto wote kwa kuimarisha mifumo ya elimu katika Afrika Mashariki na kuhakikisha kila mtoto anafurahia haki yake ya kupata elimu bora.
โช๏ธ Leo tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Vijana tunawatakia kila la heri vijana wote nchini na ujumbe wetu ni Vijana ni Taifa la Leo ushiriki wao kikamilifu kwenye michakato ya kidemokrasia utalifanya taifa letu kuwa na maendeleo endelevu katika karne hii ya 21.
โช๏ธ Elimu ni Haki, Siyo Upendeleo. Hakikisha Hakuna Mtoto Anayeachwa Nyuma. Tafakari Chukua Hatua..................
โช๏ธ Kuna methali isemayo "Ukilima pantosha, utavuna pankwisha". Je methali hii ina maana gani kwa wanafunzi walioko masomoni?
โช๏ธ Tunawatakia kila kheri wakulima wote nchini tunaposherehekea sikukuu ya nane nane.
โช๏ธ Hoja ya nguvu wiki hii inatoka kwa mdau wetu kupitia mtandao wa Twitter anayetambulika k**a Abasi Mzigua
โช๏ธ Mwalimu Dedan Runoba kutoka Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora anatuambia katika kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapata haki ya kupata elimu, Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alisititiza Elimu Bure kwa wote, Shule Maalum, Mafunzo Maalum ya Walimu na Jamii inayojumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum.
โช๏ธ Je wewe unachangia vipi kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata elimu bora? Tafakari Chukua Hatua ...
Utafiti wa makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto nchini Tanzania uliofanywa na umeibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo, shule zipo mbali na makazi na shule shikizi hazijajengwa bado, hivyo ni changamoto kwa watoto wadogo wenye ulemavu kuandikishwa shuleni. Hii, pamoja na ukosefu wa usafiri na kutokuwapo kwa mabweni, kunafanya iwe vigumu kwa watoto wadogo kuhudhuria shule mara kwa mara. Hii pia ilihusiana na kiwango kikubwa cha watoto wadogo wenye ulemavu kuacha shule.
โช๏ธ "Je! Mimi, Wewe na Serikali tunawajibikaje kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi ili kuhakikisha watoto wote wanajifunza ipasavyo?" Tafakari Chukua Hatua
โช๏ธ "Je! Mimi, Wewe na Serikali tunawajibikaje kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi ili kuhakikisha watoto wote wanajifunza ipasavyo?"
โช๏ธ Leo tumezindua kampeni inayolenga kuhamasisha uwajibikaji na uwazi katika utoaji wa elimu jumuishi.
โช๏ธ "Je!, Mimi, Wewe na Serikali tunawajibikaje kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi ili kuhakikisha watoto wote wanajifunza ipasavyo?"
Bado siku 1 yaani Kesho fuatilia ukurasa huu kufahamu kuna kipi kipya
Bi Maria Lyeme ni mdau wa Elimu kutoka mkoa wa Singida. Kisa chake kuhusu uwajibikaji ili kuwawezesha watoto wa k**e kufikia ndoto zao,kinapamba ukurasa wetu siku ya leo. Tuambie na wewe kisa chako. Tafakari Chukua Hatua...
Click here to claim your Sponsored Listing.
An Open, Just,Democratic Society with Quality Education for all.
HakiElimu was founded in 2001 by a group of 13 Tanzanians who had formed a clear and longstanding commitment to transform public education for all children, having noted that education in Tanzania was in a mess, and that the many attempts to reform it had appeared to go nowhere.
It seemed clear to this group that the local education had not improved much because technocratic solutions were being applied to essentially political problems, and that the volumes of technically sound documents produced by policy reform officials were not quite relevant because they were not taking into account the politics of institutional change in Tanzania.
With this in mind, the founders of HakiElimu sought to create an organisation to enable the ordinary citizens to actively get involved and make a difference in the education sector. They believed that education would improve when ordinary citizens became involved and create meaningful public participation in education governance. Therefore, we could say that HakiElimu is an experiment to see whether schools can be governed in an inclusive, open and democratic fashion; and whether the poor can access the relevant information and influence policy and practice.
Videos (show all)
Contact the organization
Website
Address
Upanga
Dar Es Salaam
Opening Hours
Monday | 08:00 - 16:30 |
Tuesday | 08:00 - 16:30 |
Wednesday | 08:00 - 16:30 |
Thursday | 08:00 - 16:30 |
Friday | 08:00 - 14:00 |
Umoja Road Block 2Q, Madale Village
Dar Es Salaam, 23333
Art in Tanzania - a self-sustainable NGO helping communities in Tanzania.
Morani House
Dar Es Salaam
The Lalji Foundations pledges to give back to the community and improve lives.
NSSF Road St, Bagamoyo Road
Dar Es Salaam, 14121
We are a non-profit organization, our main goal is to change lives of youths, children and those in
Mikocheni
Dar Es Salaam
Tanzania joining other countries to start STOP TB chapter in Tanzania aiming to comply with Moscow de
Zanaki Street
Dar Es Salaam, 11105
Universal Human Development (UHUDEN), is a Non-Government organization established under section 12 (1) of the NGO Act No. 24 of 2002, of the United Republic of Tanzania.
CHANIKA
Dar Es Salaam
๏ฟฝ DENY CHILD ABUSE ๏ฟฝ RIGHTS AND EQUALITY TO ALL Children ๏ฟฝ
Sam Nujoma/Lufungira Road
Dar Es Salaam
ROMME Love Justice Tanzania, an anti Human Trafficking organisation is a member of TANAHUT.
P. O. BOX 20950
Dar Es Salaam, 12113
social activists who fight against violence and sexual violence and provide education to the community "Wanaharakati wa kijamii Tunaopambana kupinga ukatili na unyanyasaji wa kiji...